Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Historia huwa na mtindo wa kujirudia!!!!!!!!!!!!!!!! Huwezi kutenganisha ubalozi na ujasusi!!!!!!!!!! Kuna msanii fulani amepata .......kuna mchezaji maarufu.........kuna miss fulani maarufu...........Tanzania ni zaidi ya uijuayo!!!!!!!!!!!

Nearly 600 Russian diplomats expelled from Western ...​

TASS
https://tass.com › politics

Forty-five diplomats were expelled from Poland, 40 - from Germany, 35 - from Slovakia, also 35 - from France, 33 - from Slovenia, 30 - from ...

Russia expels dozens of diplomats from France, Italy and ...​

Al Jazeera
https://www.aljazeera.com › news › russia-expels-doze...

18 May 2022 — Moscow has kicked out diplomats from France, Italy and Spain in retaliation for the expulsion of Russian diplomats from European countries ...
 
17

Moscow.

Siku kadhaa baada ya Oleg kuwasili nchini mwake , alihitajika kufika makao makuu ya kitengo ,kwenye idara ya FCD. Kipindi hiki idara ilikuwa inaongozwa na Victor Grushko kipisi Cha mtu mfupi hivi mwenye misimamo mikali raia wa Ukraine. Alifika bwana Oleg, na kueleza mbele ya kamati kwamba ana mpango wa kutaka kuoa baada ya kumtaliki bibiye Yelena. Kutoka kuwa deputy wa balozi alirudishwa mpaka kuwa staff wa kawaida hapo kwenye idara yake. Ingawaje c.v kazini ilikuwa inambeba , alipunguzwa cheo kwa Kasi sana. Kiuhalisia alikuwa senior lakini hapo ofisini hakuwa na kazi maalumu.
Hatimaye michakato ya talaka ilikamilika na maafisa wa kisoviet wakaamuru talaka itoke. Na kweli bibiye na Oleg walitengana rasmi ,huku mwanadada huyu alipandishwa cheo Hadi captain na kupelekwa kwenye balozi za nje ya Russia kama KGB agent. Kiuhalisia career ya Yelena haikuwa damaged kwa namna yoyote ukilinganisha na ya bwana Oleg.
Miezi michache baada ya Oleg kurudi ndani ya Russia, baba yake mzazi Anton lavrentyevich alikufa akiwa na umri wa miaka 82. Na alizikwa na maafisa wachache sana wa KGB. Oleg alitoa risala fupi kama shukran kwa mzee wake kwa kuitumikia kitengo na taifa kwa uzalendo wa Hali ya juu.
Baada ya muda Oleg aliamua kumuoa Leila wiki chache baadaye January 1979. Mama mtu Olga alifurahishwa kwa kijana wake kuamua kuoa Tena . Na hatimaye waliishi kwenye apartment Moja iliyopo mtaa wa 220 Leninsky prospekt kwenye ghorofa ya nane ambalo ni jengo lililokuwa linamilikiwa na shirika la nyumba la KGB. Na baadaye mkewe alipata ujauzito.
Kazi Yake kubwa kwa Sasa Baada ya Oleg kuamua kuoa ilikuwa ni kuandika historia ya kitengo hususan za idara yake ya FCD na kuhifadhi kwenye masjala . Na kamwe Oleg hakutaka kufanya jaribio lolote la kutaka kuvujisha Siri kwa M16.
Ikumbukwe Baada ya tukio la kukamatwa kwa mwanamama Gunvor galtung haavik aliyepewa jina la GRETA, KGB walihisi Kuna msaliti miongoni mwao. Viongozi wakuu wa KGB waliiitisha mkutano wa dharura kujadili hilo swala la kuwepo kwa msaliti miongoni mwao.
Hili swala lilimtisha bwana Oleg , maana yeye ndio alikuwa anajua Nini kinaendelea ndani ya nafsi yake. Hili swala la mapandikizi wa KGB kugundulika na kunaswa kiurahisi liliwachachafya sana wa Russia .
Oleg kila aliyempoint kama jasusi kwenye nchi za Scandinavia alinaswa .
Kwa mfano bergling aliyekuwa afisa police na mfanyakazi wa SAPO shirika la ujasusi la sweeden alinaswa 1979 mjini tel Aviv na Shin bet baada ya kusadikiwa kuwafanyia kazi KGB kuanzia mwaka 1971 na akiwa kama mwangalizi wa UN nchini Lebanon. Inasadikiwa sweeden ilipata hasara ya euro milioni 29 kutokana na Siri zake kuvujishwa . Alihukumiwa kifungo Cha maisha jela. Hili swala la kumnasa msaliti , KGB hawakualiacha lipite hivi hivi waliapa kulifanyia kazi kimya kimya.
Katika shirika hili la kijasusi , kulikuwa na utaratibu wa ongezeko la ten percent ya mshahara kwa afisa yoyote atakayefaulu kozi za lugha ya kigeni hususan kingereza endapo atafaulu.
Oleg hakuacha hii fursa impite. Kozi hii ilitakiwa ikamilike miaka minne , lakini Oleg ndani ya miaka miwili aliikamilisha. Laiti maafisa wenzake wangekuwa makini ,wangemtilia wasiwasi bwana Oleg Kutokana na haraka aliyokuwa nayo katika kujifunza lugha hiyo.
Baada ya kujifunza lugha hii Oleg alijikita katika kutafsiri ripoti mbalimbali za kijasusi .
Hatimaye mwaka 1980 mwezi April mkewe Oleg Leila alipata mtoto wao wa kwanza wa kike aliyeitwa Maria. Oleg alimwalika bwana Mikhail lyubimov ambaye alikuwa amesharudi kutoka Denmark kikazi na kuwa na cheo ndani ya FCD ,kwa ajili ya hafla fupi ya kumkaribisha mtoto wake mpya.
Hilo likapita,lakini huyu bwana Mikhail a.k.a the smiley Mikey alifukuzwa kazi ndani ya KGB, sababu zikiwa ni za kinidhamu na kimaadili. Ishu ilikuwa ni Kutoka kimapenzi na mke wa afisa mwenzake pasipo kuwajulisha wakubwa wa KGB. Nafasi yake ikachukuliwa Victor Grushko kama naibu . Na nafsi ya ukuu wa hii idara kabisa akapewa bwana Gennadi titov maarufu kama crocodile balozi mstaafu nchini sweeden. Idara ya ujasusi kwa nchi za Scandinavia na Britain ndani ya KGB ikawa inasimamiwa na Nikolai gribin aliyekuwa ni mfanyakazi wa chini ya Oleg Gordievsky kipindi akiwa Copenhagen 1976 . Teuzi zilikuwa zinampita tu yeye ndani ya kitengo [emoji2].
Mwaka 1981 Oleg alipasi mthihani wa mwisho wa kingereza . Na Sasa akawa Yuko fluent kwenye lugha Hiyo, na mwezi wa Tisa mkwa huo huo alipata mtoto wa pili aliyeitwa Ana.
Kutokana na kupasi lugha ya malkia alianza kuhudhuria vikao muhimu vya kitengo na pia kuandaa report za kila mwaka za idara. Huku akiwaza ni namna gani atapata tena access ya taarifa nyeti na za Siri za kitengoni na Kremlin.
Ndani ya makao makuu ya M16 pia walikuwa wanajiuliza Nini kimempata SUNBEAM ,lakini walipata taarifa za Oleg kupitia kwa makachero wa PET wa Denmark kwamba Oleg Kwa Sasa ameoa na ana watoto wawili wa kike.

Kwa upande wa Russia , KGB walianza harakati za mpya za kutaka kuanzisha harakati za kijasusi nchini uingereza. Hii ni kwa mujibu wa boss mpya wa third department Bwana Gennadi titov ambaye ni balozi mstaafu. Baada ya tukio la kufukuzwa kwa majasusi zaidi ya 100 nchini uingereza mwaka 1971, tokea hapo Russia hawakuwa na pandikizi kwa ajili ya kupata infos za kutosha za huko London za kijasusi. Na alihitajika afisa ambaye alikuwa anajua lugha ya malkia kwa ufasaha. Ingawaje kulikuwa na maafisa wa KGB illegal nchini uingereza, Russia walihitaji KGB ambaye angefanya kazi official chini ya diplomatic cover. Kwa mfano yalitumwa maombi kadhaa ya afisa mmoja kufanya kazi ubalozi wa uingereza lakini alikataliwa kutokana na kutiliwa wasiwasi na M15.
KGB walihitaji mtu aliyekidhi vigezo kufanya kazi nchini uingereza. Oleg kupitia vyanzo vyake vya taarifa aliamini anakidhi vigezo. Shida ikaja kwa wakuu wa idara ndani ya kitengo. Genadi titov alitaka aweke mtu wake kwenye hiyo post mpya ya kikazi nchini uingereza. Naye Nikolai gribin alipendekeza hii post ingemfaa Oleg. Baada ya mnyukano na msuguano mkali bwana titov alilegea .
Hatimaye visa application ilitumwa nchini uingereza ya bwana Oleg Kwa ajili ya kuchakatwa.
Zilikuwa ni habari njema sana kwa makachero wa M16.
 
View attachment 2604645
IMG_20230430_122223_288.jpg

Maria na Ana , watoto wa mzee Oleg Gordievsky aliozaa na mkewe Leila
 
Hadithi nzuri sana yenye mvuto wa aina yake, na kwa ushahidi wa picha inaonekana wazi sio hadithi ya kutunga bali ni ya kweli.

Hongera mleta mada endelea kupata hamasa ya kutuletea hadithi hii mpaka mwisho wake.
Hopefully nikikamilisha nitaweka na references za kutosha for further reading.
 
18

Mwanamama Veronica price , pamoja na maafisa wa ngazi za juu wa M16 waliipitia form ya application ya SUNBEAM na hatimaye waliona Sasa huyu bwana akiwa nchini mwao itakuwa ni jambo la heri sana kwao. Lakini swala la ku approve visa application ya Oleg halikuwa jambo jepesi hata kidogo. Hii ni kwa sababu Oleg tayari alishakuwa suspect na mashirika mengi ya ulaya magharibi ikiwemo PET na wao M16. Afisa yoyote wa Russia aliyekuwa ana uhusiano na KGB hakupaswa kuingia ndani ya uingereza endapo . Kimbembe kikawa ni wizara ya mambo ya nje ya uingereza. Kwani lazima wizara hii ingejua rekodi zote za Oleg hususan kufanya kazi nchi za Scandinavia na ingezusha maswali mengi sana. Lakini ni maafisa wachache wa ngazi za juu wa M16 walitaka huyu bwana apewe ruhusa kuingia nchini humo. Swala likawa ni kwamba ofisi ya uhamiaji ingetoa visa ila ni kwamba ingezusha wasiwasi ikiwa bwana Oleg atapewa idhibati ya kuingia uingereza. M16 baada ya kuona kikwazo ni ofisi za uhamiaji za uingereza ni kikwazo wakaamua kucheza Dili na PET . M16 waliwaambia wenzao PET endapo ofisi ya wizara ya mambo ya nje ya uingereza ikitaka enquiries kuhusiana na SUNBEAM kufanya kazi nchi hizo za Scandinavia wao waseme kwamba alifanya na hakuwa suspect wa KGB kama ilivyojulikana mwanzo . Kwa kifupi PET na M16 Walikuwa wanafanya mchezo wa kufoji taarifa za Oleg Ili visa yake ipasishwe na aweze kuingia uingereza. Taratibu zilikamilka na hatimaye diplomatic visa passport ya Oleg ndani ya siku 22 ikawa tayari imekamamilika badala ya siku 30. Kiuhalisia mamlaka za uhamiaji za uingereza zilikuwa Zina doubt sana ila ndio hivyo , majasusi ni majasusi tu.[emoji1]. Hata maafisa wa Russia kwenye ofisi ya wizara ya mambo ya nje walishangazwa na ku DOUBT visa ya Oleg kuwa approved haraka sana baada ya yeye kwenda kuipokea kwenye ofisi za uhamiaji .
Mamlaka za urusi zilikuwa slow kiasi kwamba Oleg ilimpasa asubiri miezi 3 zaidi mbele kabla ya kupewa ruhusa rasmi kutoka nje ya Russia.
Hili swala lilizua mjadala kwa Oleg binafsi na kwa uingereza hususan M16. Ni kwamba KGB walikuwa wanakagua background ya bwana Oleg na historia yake kwa ujumla. Hii kazi ilikuwa inafanywa na kitengo Cha internal investigation wing . Muda mwingi aliotumia kuusubiri alikuwa anaperuzi ma file mbalimbali ya KGB.
Wanasema kwenye headquarters za KGB mfumo wa kutunza mafaili yenye Siri ulikuwa ni complex sana . Ni kwamba kila afisa hapo kitengoni alikuwa na sefu yake ya kuhifadhia ma file kutokana na kila idara . Na baada ya kila afisa kufunga sefu yake funguo zote zilikuwa zinawekwa kwenye boksi special la mbao .kila ufunguo ulikuwa na individual stamp ya kumtambulisha afisa na idara husika . Ni kwamba boksi hili lenye funguo lilipelekwa kwenye ofisi kuu inayosimamia idara mbalimbali na Kisha boksi lile linafungiwa kwenye ofisi kuu ya FCD . Hivyo usalama wa mafaili ya Siri ulikuwa ni kipaumbele . Hivyo Oleg katika harakati za kupekua pekua mafaili alikutana na taarifa za bwana Jack Jones . Huyu alikuwa ni kiongozi wa chama Cha wafanyakazi nchini uingereza na baadaye kiongozi wa chama Cha communist party nchini uingereza . Huyu bwana kwa mujibu wa report za faili lake alikuwa anaiuzia KGB taarifa za kamati kuu za chama na serikali kuanzia 1964 Hadi 1969.
Mwingine Oleg aliyemgundua kwenye mafaili hayo ni bwana bob Edwards mbunge wa chama Cha mrengo wa kushoto Cha labour ambaye alikuwa na uhusiano na Russia miaka ya 1920s na Aliwahi Kukutana na Stalin .na alikuwa kwenye payroll ya KGB akiwauzia informations.
Mtu mwingine aliyekuwa pia ni agent wa KGB alikuwa ni mbunge mstaafu na katibu mkuu wa chama Cha labour party ambaye alikuwa na mahusiano ya Siri na KGB. Ilisemekana alikuwa anapokea fedha kutoka kwa KGB ku support chama chake kama payment ya kuwauzia taarifa za Siri urusi. Na wote hao ambao Oleg aliwagundua walikuwa ni left wingers yaani wale wanaoamini mrengo wa kushoto au pro-soviet.
Pia Oleg aliweza kupata file Moja lenye kurasa 300 hivi zito likamvutia likiwa limepewa jina la BOOT.
Ukurasa wake wa kwanza ulianza kwa maneno haya " I , senior operational officer major Petrov, Ivan Alexeyevich, herewith open a file on the agent Michael Foot, citizen of the United kingdom, giving him pseudonym Boot".
Ni kwamba huyu Michael foot alikuwa ni mbunge mstaafu wa chama Cha labour , mwandishi na pia mpinzani wa Margaret thatcher katika kinyang'anyiro Cha uchaguzi mkuu Cha uwaziri mkuu wakati huo. Naye huyu bwana alikuwa kwenye payroll ya KGB na alikuwa anatumiwa na huyo Petrov . Kiongozi mkuu wa chama Cha upinzani Cha labour . Huyu Foot alikuwa ni mwanasiasa machachari sana. Kwa mfano uchaguzi wa 1979 nchini uingereza James Callaghan baada ya kubwagwa na margareth thatcher akashinda kiti Cha u PM ,alijiuzulu kwenye chama Cha labour na nafasi yake akaichukua huyu Michael foot mwezi November 1980. Kura za maoni zilionyesha chama Cha labour kilikuwa mbele kwa asilimia 10 nyuma ya chama Cha conservative kilichokuwa kinaongozwa na margareth thatcher. Na uchaguzi uliotarajiwa kufanyika mwaka 1984 ulionyesha kwamba Michael foot angekuwa prime minister wa U.k.ila alianguka. Repoti zilikuja kuonyesha baadaye kwamba Laiti angeshinda huyu bwana ingekuwa ni kashfa kubwa kwa P.M wa uingereza kuwa agent wa KGB.
Pia taarifa za huyu bwana zilionyesha alikuwa anapokea fedha kati ya euro 100 Hadi 2000 na hakuwahi julikana ni payment za Nini miaka ya 1960s .

Hizi taarifa zote bwana oleg aliweza kuzihifadhi kwa MATUMIZI YAKE YA BAADAYE.[emoji28][emoji28].
 
IMG_20230429_203853_882.jpg

Huyu ndio Michael foot au codename agent BOOT
Kiongozi wa chama Cha labour party alliyechuana na margareth thatcher katika kinyang'anyiro Cha uchaguzi mkuu wa P.M wa uingereza mwaka 1984.
Huyu bwana alikuwa kwenye payroll ya KGB kwa miaka mingi.
 
17

Moscow.

Siku kadhaa baada ya Oleg kuwasili nchini mwake , alihitajika kufika makao makuu ya kitengo ,kwenye idara ya FCD. Kipindi hiki idara ilikuwa inaongozwa na Victor Grushko kipisi Cha mtu mfupi hivi mwenye misimamo mikali raia wa Ukraine. Alifika bwana Oleg, na kueleza mbele ya kamati kwamba ana mpango wa kutaka kuoa baada ya kumtaliki bibiye Yelena. Kutoka kuwa deputy wa balozi alirudishwa mpaka kuwa staff wa kawaida hapo kwenye idara yake. Ingawaje c.v kazini ilikuwa inambeba , alipunguzwa cheo kwa Kasi sana. Kiuhalisia alikuwa senior lakini hapo ofisini hakuwa na kazi maalumu.
Hatimaye michakato ya talaka ilikamilika na maafisa wa kisoviet wakaamuru talaka itoke. Na kweli bibiye na Oleg walitengana rasmi ,huku mwanadada huyu alipandishwa cheo Hadi captain na kupelekwa kwenye balozi za nje ya Russia kama KGB agent. Kiuhalisia career ya Yelena haikuwa damaged kwa namna yoyote ukilinganisha na ya bwana Oleg.
Miezi michache baada ya Oleg kurudi ndani ya Russia, baba yake mzazi Anton lavrentyevich alikufa akiwa na umri wa miaka 82. Na alizikwa na maafisa wachache sana wa KGB. Oleg alitoa risala fupi kama shukran kwa mzee wake kwa kuitumikia kitengo na taifa kwa uzalendo wa Hali ya juu.
Baada ya muda Oleg aliamua kumuoa Leila wiki chache baadaye January 1979. Mama mtu Olga alifurahishwa kwa kijana wake kuamua kuoa Tena . Na hatimaye waliishi kwenye apartment Moja iliyopo mtaa wa 220 Leninsky prospekt kwenye ghorofa ya nane ambalo ni jengo lililokuwa linamilikiwa na shirika la nyumba la KGB. Na baadaye mkewe alipata ujauzito.
Kazi Yake kubwa kwa Sasa Baada ya Oleg kuamua kuoa ilikuwa ni kuandika historia ya kitengo hususan za idara yake ya FCD na kuhifadhi kwenye masjala . Na kamwe Oleg hakutaka kufanya jaribio lolote la kutaka kuvujisha Siri kwa M16.
Ikumbukwe Baada ya tukio la kukamatwa kwa mwanamama Gunvor galtung haavik aliyepewa jina la GRETA, KGB walihisi Kuna msaliti miongoni mwao. Viongozi wakuu wa KGB waliiitisha mkutano wa dharura kujadili hilo swala la kuwepo kwa msaliti miongoni mwao.
Hili swala lilimtisha bwana Oleg , maana yeye ndio alikuwa anajua Nini kinaendelea ndani ya nafsi yake. Hili swala la mapandikizi wa KGB kugundulika na kunaswa kiurahisi liliwachachafya sana wa Russia .
Oleg kila aliyempoint kama jasusi kwenye nchi za Scandinavia alinaswa .
Kwa mfano bergling aliyekuwa afisa police na mfanyakazi wa SAPO shirika la ujasusi la sweeden alinaswa 1979 mjini tel Aviv na Shin bet baada ya kusadikiwa kuwafanyia kazi KGB kuanzia mwaka 1971 na akiwa kama mwangalizi wa UN nchini Lebanon. Inasadikiwa sweeden ilipata hasara ya euro milioni 29 kutokana na Siri zake kuvujishwa . Alihukumiwa kifungo Cha maisha jela. Hili swala la kumnasa msaliti , KGB hawakualiacha lipite hivi hivi waliapa kulifanyia kazi kimya kimya.
Katika shirika hili la kijasusi , kulikuwa na utaratibu wa ongezeko la ten percent ya mshahara kwa afisa yoyote atakayefaulu kozi za lugha ya kigeni hususan kingereza endapo atafaulu.
Oleg hakuacha hii fursa impite. Kozi hii ilitakiwa ikamilike miaka minne , lakini Oleg ndani ya miaka miwili aliikamilisha. Laiti maafisa wenzake wangekuwa makini ,wangemtilia wasiwasi bwana Oleg Kutokana na haraka aliyokuwa nayo katika kujifunza lugha hiyo.
Baada ya kujifunza lugha hii Oleg alijikita katika kutafsiri ripoti mbalimbali za kijasusi .
Hatimaye mwaka 1980 mwezi April mkewe Oleg Leila alipata mtoto wao wa kwanza wa kike aliyeitwa Maria. Oleg alimwalika bwana Mikhail lyubimov ambaye alikuwa amesharudi kutoka Denmark kikazi na kuwa na cheo ndani ya FCD ,kwa ajili ya hafla fupi ya kumkaribisha mtoto wake mpya.
Hilo likapita,lakini huyu bwana Mikhail a.k.a the smiley Mikey alifukuzwa kazi ndani ya KGB, sababu zikiwa ni za kinidhamu na kimaadili. Ishu ilikuwa ni Kutoka kimapenzi na mke wa afisa mwenzake pasipo kuwajulisha wakubwa wa KGB. Nafasi yake ikachukuliwa Victor Grushko kama naibu . Na nafsi ya ukuu wa hii idara kabisa akapewa bwana Gennadi titov maarufu kama crocodile balozi mstaafu nchini sweeden. Idara ya ujasusi kwa nchi za Scandinavia na Britain ndani ya KGB ikawa inasimamiwa na Nikolai gribin aliyekuwa ni mfanyakazi wa chini ya Oleg Gordievsky kipindi akiwa Copenhagen 1976 . Teuzi zilikuwa zinampita tu yeye ndani ya kitengo [emoji2].
Mwaka 1981 Oleg alipasi mthihani wa mwisho wa kingereza . Na Sasa akawa Yuko fluent kwenye lugha Hiyo, na mwezi wa Tisa mkwa huo huo alipata mtoto wa pili aliyeitwa Ana.
Kutokana na kupasi lugha ya malkia alianza kuhudhuria vikao muhimu vya kitengo na pia kuandaa report za kila mwaka za idara. Huku akiwaza ni namna gani atapata tena access ya taarifa nyeti na za Siri za kitengoni na Kremlin.
Ndani ya makao makuu ya M16 pia walikuwa wanajiuliza Nini kimempata SUNBEAM ,lakini walipata taarifa za Oleg kupitia kwa makachero wa PET wa Denmark kwamba Oleg Kwa Sasa ameoa na ana watoto wawili wa kike.

Kwa upande wa Russia , KGB walianza harakati za mpya za kutaka kuanzisha harakati za kijasusi nchini uingereza. Hii ni kwa mujibu wa boss mpya wa third department Bwana Gennadi titov ambaye ni balozi mstaafu. Baada ya tukio la kufukuzwa kwa majasusi zaidi ya 100 nchini uingereza mwaka 1971, tokea hapo Russia hawakuwa na pandikizi kwa ajili ya kupata infos za kutosha za huko London za kijasusi. Na alihitajika afisa ambaye alikuwa anajua lugha ya malkia kwa ufasaha. Ingawaje kulikuwa na maafisa wa KGB illegal nchini uingereza, Russia walihitaji KGB ambaye angefanya kazi official chini ya diplomatic cover. Kwa mfano yalitumwa maombi kadhaa ya afisa mmoja kufanya kazi ubalozi wa uingereza lakini alikataliwa kutokana na kutiliwa wasiwasi na M15.
KGB walihitaji mtu aliyekidhi vigezo kufanya kazi nchini uingereza. Oleg kupitia vyanzo vyake vya taarifa aliamini anakidhi vigezo. Shida ikaja kwa wakuu wa idara ndani ya kitengo. Genadi titov alitaka aweke mtu wake kwenye hiyo post mpya ya kikazi nchini uingereza. Naye Nikolai gribin alipendekeza hii post ingemfaa Oleg. Baada ya mnyukano na msuguano mkali bwana titov alilegea .
Hatimaye visa application ilitumwa nchini uingereza ya bwana Oleg Kwa ajili ya kuchakatwa.
Zilikuwa ni habari njema sana kwa makachero wa M16.
[emoji106][emoji106]
 
Back
Top Bottom