cariha
JF-Expert Member
- Apr 9, 2015
- 22,077
- 46,549
Ndio hivo Mungu atusaidie aiseeHapa unaweza kushangaa mwanasiasa alikuwa hohe hahe, akishapata madaraka tu anakuwa tajiri wa kutisha kumbe biashara kuuza siri za nchi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio hivo Mungu atusaidie aiseeHapa unaweza kushangaa mwanasiasa alikuwa hohe hahe, akishapata madaraka tu anakuwa tajiri wa kutisha kumbe biashara kuuza siri za nchi.
Futa app ya JF hiyo mpya download hii hapa ya zamani utainjoy https://www.apkmonk.com/app/com.quoord.jamiiforums.activity/Nasikitika picha hazifunguki, na wasiwasi hata wanasiasa wa nchi hii huuza taarifa na wengine hutumika aisee in the name of haki sijui za kisiasa, ka huyo mwanamama katibu wa wizara anauza taarifa si hatari hii
ThanksFuta app ya JF hiyo mpya download hii hapa ya zamani utainjoy https://www.apkmonk.com/app/com.quoord.jamiiforums.activity/
Ahsante mkuu..umetusaidia wengiFuta app ya JF hiyo mpya download hii hapa ya zamani utainjoy https://www.apkmonk.com/app/com.quoord.jamiiforums.activity/
Hopefully nikikamilisha nitaweka na references za kutosha for further reading.Hadithi nzuri sana yenye mvuto wa aina yake, na kwa ushahidi wa picha inaonekana wazi sio hadithi ya kutunga bali ni ya kweli.
Hongera mleta mada endelea kupata hamasa ya kutuletea hadithi hii mpaka mwisho wake.
Shusha vitu mkuu weekend ndefuView attachment 2604932
Huyu ndio Michael foot au codename agent BOOT
Kiongozi wa chama Cha labour party alliyechuana na margareth thatcher katika kinyang'anyiro Cha uchaguzi mkuu wa P.M wa uingereza mwaka 1984.
Huyu bwana alikuwa kwenye payroll ya KGB kwa miaka mingi.
Asante sana ndugu [emoji120]Hopefully nikikamilisha nitaweka na references za kutosha for further reading.
[emoji106][emoji106]17
Moscow.
Siku kadhaa baada ya Oleg kuwasili nchini mwake , alihitajika kufika makao makuu ya kitengo ,kwenye idara ya FCD. Kipindi hiki idara ilikuwa inaongozwa na Victor Grushko kipisi Cha mtu mfupi hivi mwenye misimamo mikali raia wa Ukraine. Alifika bwana Oleg, na kueleza mbele ya kamati kwamba ana mpango wa kutaka kuoa baada ya kumtaliki bibiye Yelena. Kutoka kuwa deputy wa balozi alirudishwa mpaka kuwa staff wa kawaida hapo kwenye idara yake. Ingawaje c.v kazini ilikuwa inambeba , alipunguzwa cheo kwa Kasi sana. Kiuhalisia alikuwa senior lakini hapo ofisini hakuwa na kazi maalumu.
Hatimaye michakato ya talaka ilikamilika na maafisa wa kisoviet wakaamuru talaka itoke. Na kweli bibiye na Oleg walitengana rasmi ,huku mwanadada huyu alipandishwa cheo Hadi captain na kupelekwa kwenye balozi za nje ya Russia kama KGB agent. Kiuhalisia career ya Yelena haikuwa damaged kwa namna yoyote ukilinganisha na ya bwana Oleg.
Miezi michache baada ya Oleg kurudi ndani ya Russia, baba yake mzazi Anton lavrentyevich alikufa akiwa na umri wa miaka 82. Na alizikwa na maafisa wachache sana wa KGB. Oleg alitoa risala fupi kama shukran kwa mzee wake kwa kuitumikia kitengo na taifa kwa uzalendo wa Hali ya juu.
Baada ya muda Oleg aliamua kumuoa Leila wiki chache baadaye January 1979. Mama mtu Olga alifurahishwa kwa kijana wake kuamua kuoa Tena . Na hatimaye waliishi kwenye apartment Moja iliyopo mtaa wa 220 Leninsky prospekt kwenye ghorofa ya nane ambalo ni jengo lililokuwa linamilikiwa na shirika la nyumba la KGB. Na baadaye mkewe alipata ujauzito.
Kazi Yake kubwa kwa Sasa Baada ya Oleg kuamua kuoa ilikuwa ni kuandika historia ya kitengo hususan za idara yake ya FCD na kuhifadhi kwenye masjala . Na kamwe Oleg hakutaka kufanya jaribio lolote la kutaka kuvujisha Siri kwa M16.
Ikumbukwe Baada ya tukio la kukamatwa kwa mwanamama Gunvor galtung haavik aliyepewa jina la GRETA, KGB walihisi Kuna msaliti miongoni mwao. Viongozi wakuu wa KGB waliiitisha mkutano wa dharura kujadili hilo swala la kuwepo kwa msaliti miongoni mwao.
Hili swala lilimtisha bwana Oleg , maana yeye ndio alikuwa anajua Nini kinaendelea ndani ya nafsi yake. Hili swala la mapandikizi wa KGB kugundulika na kunaswa kiurahisi liliwachachafya sana wa Russia .
Oleg kila aliyempoint kama jasusi kwenye nchi za Scandinavia alinaswa .
Kwa mfano bergling aliyekuwa afisa police na mfanyakazi wa SAPO shirika la ujasusi la sweeden alinaswa 1979 mjini tel Aviv na Shin bet baada ya kusadikiwa kuwafanyia kazi KGB kuanzia mwaka 1971 na akiwa kama mwangalizi wa UN nchini Lebanon. Inasadikiwa sweeden ilipata hasara ya euro milioni 29 kutokana na Siri zake kuvujishwa . Alihukumiwa kifungo Cha maisha jela. Hili swala la kumnasa msaliti , KGB hawakualiacha lipite hivi hivi waliapa kulifanyia kazi kimya kimya.
Katika shirika hili la kijasusi , kulikuwa na utaratibu wa ongezeko la ten percent ya mshahara kwa afisa yoyote atakayefaulu kozi za lugha ya kigeni hususan kingereza endapo atafaulu.
Oleg hakuacha hii fursa impite. Kozi hii ilitakiwa ikamilike miaka minne , lakini Oleg ndani ya miaka miwili aliikamilisha. Laiti maafisa wenzake wangekuwa makini ,wangemtilia wasiwasi bwana Oleg Kutokana na haraka aliyokuwa nayo katika kujifunza lugha hiyo.
Baada ya kujifunza lugha hii Oleg alijikita katika kutafsiri ripoti mbalimbali za kijasusi .
Hatimaye mwaka 1980 mwezi April mkewe Oleg Leila alipata mtoto wao wa kwanza wa kike aliyeitwa Maria. Oleg alimwalika bwana Mikhail lyubimov ambaye alikuwa amesharudi kutoka Denmark kikazi na kuwa na cheo ndani ya FCD ,kwa ajili ya hafla fupi ya kumkaribisha mtoto wake mpya.
Hilo likapita,lakini huyu bwana Mikhail a.k.a the smiley Mikey alifukuzwa kazi ndani ya KGB, sababu zikiwa ni za kinidhamu na kimaadili. Ishu ilikuwa ni Kutoka kimapenzi na mke wa afisa mwenzake pasipo kuwajulisha wakubwa wa KGB. Nafasi yake ikachukuliwa Victor Grushko kama naibu . Na nafsi ya ukuu wa hii idara kabisa akapewa bwana Gennadi titov maarufu kama crocodile balozi mstaafu nchini sweeden. Idara ya ujasusi kwa nchi za Scandinavia na Britain ndani ya KGB ikawa inasimamiwa na Nikolai gribin aliyekuwa ni mfanyakazi wa chini ya Oleg Gordievsky kipindi akiwa Copenhagen 1976 . Teuzi zilikuwa zinampita tu yeye ndani ya kitengo [emoji2].
Mwaka 1981 Oleg alipasi mthihani wa mwisho wa kingereza . Na Sasa akawa Yuko fluent kwenye lugha Hiyo, na mwezi wa Tisa mkwa huo huo alipata mtoto wa pili aliyeitwa Ana.
Kutokana na kupasi lugha ya malkia alianza kuhudhuria vikao muhimu vya kitengo na pia kuandaa report za kila mwaka za idara. Huku akiwaza ni namna gani atapata tena access ya taarifa nyeti na za Siri za kitengoni na Kremlin.
Ndani ya makao makuu ya M16 pia walikuwa wanajiuliza Nini kimempata SUNBEAM ,lakini walipata taarifa za Oleg kupitia kwa makachero wa PET wa Denmark kwamba Oleg Kwa Sasa ameoa na ana watoto wawili wa kike.
Kwa upande wa Russia , KGB walianza harakati za mpya za kutaka kuanzisha harakati za kijasusi nchini uingereza. Hii ni kwa mujibu wa boss mpya wa third department Bwana Gennadi titov ambaye ni balozi mstaafu. Baada ya tukio la kufukuzwa kwa majasusi zaidi ya 100 nchini uingereza mwaka 1971, tokea hapo Russia hawakuwa na pandikizi kwa ajili ya kupata infos za kutosha za huko London za kijasusi. Na alihitajika afisa ambaye alikuwa anajua lugha ya malkia kwa ufasaha. Ingawaje kulikuwa na maafisa wa KGB illegal nchini uingereza, Russia walihitaji KGB ambaye angefanya kazi official chini ya diplomatic cover. Kwa mfano yalitumwa maombi kadhaa ya afisa mmoja kufanya kazi ubalozi wa uingereza lakini alikataliwa kutokana na kutiliwa wasiwasi na M15.
KGB walihitaji mtu aliyekidhi vigezo kufanya kazi nchini uingereza. Oleg kupitia vyanzo vyake vya taarifa aliamini anakidhi vigezo. Shida ikaja kwa wakuu wa idara ndani ya kitengo. Genadi titov alitaka aweke mtu wake kwenye hiyo post mpya ya kikazi nchini uingereza. Naye Nikolai gribin alipendekeza hii post ingemfaa Oleg. Baada ya mnyukano na msuguano mkali bwana titov alilegea .
Hatimaye visa application ilitumwa nchini uingereza ya bwana Oleg Kwa ajili ya kuchakatwa.
Zilikuwa ni habari njema sana kwa makachero wa M16.