Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Siku wakiona umuhimu wa hizo idara watajikita huko
[emoji28][emoji28] Sasa hivi wameridhika Hawa wakuu wa hizo idara wawekeze kimafunzo na kubadili mambo kulingana na kipindi hichi tulicho na mabadiliko sio mtu unakuwa mkurugenzi Hadi unaondoka Haina jipya Kwa idara Hadi analetwa mwingine wakati sikuhizi miaka miwili tu inatosha kufanya mabadiliko mkuu wasiwe stagnant kubadilika woooi
 
Tena hii amani non-existent, hamna amani isipokuwa woga , amani katika ukosefu wa furaha ni amani gani.

Mimi wanapo sema hapa kwetu ni kisiwa cha amani nashindwa kuwaelewa, labda wangesema kisiwa cha ujinga.
 
Dah!picha hazifunguki kwangu,naishia kusoma maelezo tu..
 
Tena hii amani non-existent, hamna amani isipokuwa woga , amani katika ukosefu wa furaha ni amani gani.

Mimi wanapo sema hapa kwetu ni kisiwa cha amani nashindwa kuwaelewa, labda wangesema kisiwa cha ujinga.
[emoji28][emoji28][emoji28]misemo hyo ya watu kujificha kukwepa majukumu
 
28



Baada ya CIA kupata clue kwamba possiblity ya Oleg ndiye source wa M16 kama kawaida Yao waka mute Kama hamna kilichokuwa kinaendelea.
.....
Back in London , kwenye ubalozi wa Soviet hapo bwana Oleg alikuwa anasubiri neno lolote kutoka Moscow kwa bashasha kuhusiana na kupandishwa cheo. Hii ni kutokana na mchango wake katika ujasusi na zaidi ku play a key role katika kufanikisha ziara ya Gorbachev nchini uingereza.Alikuwa na possiblity kubwa ya kuwa balozi rasmi au rezident kwa kirusi. Lakini kama kawaida wakubwa huko Moscow kitengoni wakawa wanavuta muda kujidhihirisha kabla ya kutoa tamko rasmi la uteuzi.
Lakini bwana Nikitenko afisa mwenzake alianza kupata infos za bwana Oleg tokea mwanzo kutoka kwa maafisa kadhaa wa hapo ubalozini kuhusiana na mwenendo wake. Huyu Nikitenko naye alitamani hii nafasi ya kuwa balozi .

Lakini mwezi January bwana Oleg aliitwa nyumbani Moscow kwa ajili ya kupewa ilichodaiwa ni briefings kuhusiana na uteuzi wake [emoji39][emoji39]........ .........haikutarajiwa
Ndani ya mashirika ya kijasusi ya uingereza M16&M15 kulizuka majadiliano mazito kidogo ,mbona mtu wao a k.a NOCTON ameitwa nyumbani Moscow? Mjadala ulikuwa mpana na mmoja wa afisa akatoa maoni yake kwamba ikitokea tukamruhusu kuondoka bwana Oleg, uwezekano wa kumpoteza ni mkubwa mno.
Kwa upande wa Oleg alijiamini hakukuwa na la kumtisha kwa kuitwa kwake. Na pia huko Moscow kulikuwa hakuna ishara ya Jambo lolote linaloweza kutokea dhidi ya Oleg
Wengine wakatoa maoni labda ni power struggle ya kiti Cha ubalozi baina ya Oleg na Nikitenko .hivyo wakahisi labda kuitwa kwa bwana Oleg ni wivu tu kwa ambao hawakutaka Oleg awe balozi. A sense of guilty .
Bwana Oleg alikutana na maafisa kwenye kikao Chao Cha mwisho kwenye safe house Kabla ya kuondoka uingereza. Pia kwenye kikao hiki mwanamama Veronica price alimkumbusha mpango wa M16 Uliokuwa drafted tayari miaka kadhaa nyuma ulioitwa PIMLICO. Huu ulikuwa ni mpango mahsusi wa kumtorosha Oleg Gordievsky nje ya Urusi endapo mambo yakimwendea kombo akiwa huko Urusi. Kikao kikatamatika.


Baada ya Oleg kuwasili kwenye makao makuu ya idara ya FCD huko Moscow,alipokelewa na mkuu wa idara hii wakati huo akiwa ni Nikolai gribin na akapewa briefings kwamba yeye ndio top candidate anayependekezwa kuchukua viatu vya Arkadi guk kama balozi.lakini ki protokali tangazo rasmi la uteuzi wake ulipaswa kufanyika mwaka unaofuata. Lakini Siku chache baadaye kwenye kikao Cha ndani Cha KGB Oleg alitangazwa kama balozi aliyetarajiwa wa ubalozi wa London. Hili swala lilimkwaza gribin . Hakutaka iwe mapema kiasi hiki. Lakini ndio hivyo kupitia Kikao hiki,tangazo la uteuzi likawa limetoka rasmi. Oleg alifurahia sana

Lakini wanasema sisi binadamu Kuna muda inabidi tujifunze kutokana na makosa ya wengine hususan kwa kila unalofanya..... Hili Oleg aliliwaza kutokana kilichomkuta Comrade mwenzake miaka michache nyuma aliyeitwa bwana Vladimir Vetrov.
Huyu bwana Vetrov alikuwa ni jasusi wa Russia aliyekuwa anafanya kazi ndani ya idara ya Line X. Hii department ilikuwa inahusika na ujasusi wa teknolojia na maswala mazima ya technical issues. Huyu bwana kipindi anafanya kazi huko Paris ufaransa kwa miaka kadhaa baadaye akaanza kuifanyia kazi shirika la kijasusi la ufaransa kwa kuwauzia taarifa za Siri za nchi yake . Inasadikiwa alivujisha taarifa Zaidi ya 4000 kwa ufaransa. Na alipewa jina la uficho codename FAREWELL. Matokeo Yake ilipelekea kufukuzwa kwa maafisa 47 waliosadikiwa kuwa ni agents wa KGB na mamlaka za ufaransa waliokuwa nchini humo. Aliporudi Moscow mwaka 1982, huyu bwana Vetrov alikuwa na mgogoro na mpenzi wake Mara kwa mara .Siku Moja akiwa na mpenzi wake ndani ya gari walikuwa wanagombana sana kiasi kwamba askari aliyekuwa on duty akagonga kumtaka huyu bwana kushusha kioo kutaka kujua shida Nini mbona wanagombana. Huyu Vetrov kuona ni askari akadhani ameshashtukiwa na mamlaka kuhusiana na ishu yake aliyokuwa akifanya huko Paris. Hivyo akahisi amekuja kukamatwa. Alimpiga visu kadhaa huyu askari akamuua. Kiuhalisia alikuwa hajajulikana ila ni Hali ya kujishtukia.
Hivyo akakamatwa na kutiwa ndani . Wakati upelelezi ukiendelea alikuja kugundulika ni haini kwa nchi yake akiuza taarifa za kijasusi kwa ufaransa.alitiwa hatiani na Huyu bwana alikuja kuuliwa January 23 siku chache kabla Oleg hajarudi London. Hii Ikamkumbusha bwana Oleg Nini kinawapata wanaosaliti nchi zao.[emoji28]
Baada ya Oleg kurudi London kwa taarifa njema za uteuzi kama balozi , ilikuwa ni jambo la furaha sana kwa makachero wa M16.
M16 waliamini Sasa SOURCE wao atakuwa na access ya taarifa za Hali ya juu akiwa balozi wa Russia nchini uingereza. Na vilevile waliamini Bwana Oleg baadaye anaweza kupewa cheo kikubwa zaidi kama general wa KGB.
Gordievsky aliendelea kusubiria tangazo rasmi kutoka kwa wakubwa la uteuzi huu mpya kwa hamu sana. Hapo London bwana Nikitenko alikuwa akijiandaa kurudi nyumbani Moscow lakini akiwa amekasirika na chuki dhidi ya uteuzi wa bwana Oleg.
Bwana Nikitenko alianza vituko Fulani ikiwemo kumbania bwana Oleg baadhi ya acces ya telegrams ambazo kiutaratibu balozi huyo mtarajiwa alipaswa kuwa na access Nazo. Oleg hakuwaza labda alijua ni kisasi tu kutokana na uteuzi wake.
Baada ya bwana Nikitenko kuondoka rasmi na kwenda kufanya kazi makao makuu huko Moscow ,Oleg aliamini Sasa rasmi taarifa zote nyeti atakuwa na uwezo wa kuzipata kiulaini na M16 Wangefaidi.

Wiki mbili baadaye yaani tarehe 28 April 1985 rasmi Oleg Gordievsky alikuwa balozi wa Russia nchini uingereza. Cheo kikubwa zaidi kama afisa wa KGB. Taarifa zote za kiofisi na makabidhiano ya ofisi yalifanyika. Kiutaratibu afisa anayeachia ofisi lazima aache briefcase iliyo na documents muhimu za Siri ikiwa imefungwa. Baada ya Nikitenko kuondoka ,Oleg akafungua briefcase lakini alichokutana nacho hakikutarajiwa. Ni kwamba alikutana na bahasha iliyokuwa imebeba barua mbili ambazo ndizo zile bettaney aliziacha kwenye makazi guk siku za nyuma. Oleg hakujua ujumbe huu unamaanisha Nini . Na hata alipofikish a hizi taarifa kwa M16 ziliwashangaza ......a red flag .


Tukirudi kwa upande wa bwana Aldrich Ames, afisa wa CIA . Maisha yake yalikuwa hayaeleweki na hata maboss wake huko walikuwa hawampi appreciation ya aina yoyote kutokana na kuwa broke huku madeni yakimwandama plus ulevi wa kupindukia.
Sasa alikata shauri la kutengeneza pesa.
Alitaka kuuza taarifa za kijasusi kwa Russia.
Na kweli mwezi April alipiga simu kwenye ubalozi wa Soviet hapo Washington . Huyu bwana ambaye Ames aliamua kumvutia waya aliitwa Sergey Dmitriyevich Chuvakhin. Akitaka akutane naye kwa kadiri ilivyowezekana
Na kweli wakapanga kukutana muda wa Jioni kama saa kumi siku ya tarehe 16 April. Huyu bwana alikuwa ni specialist kwenye maswala ya kijeshi na alikuwa yupo kwenye list ya CIA kama person of interest ,ikimaanisha alikuwa anafaa kutumiwa na CIA hapo baadaye kama pandikizi lao . Ames aliwaambia baadhi ya maafisa wake kwamba amepata mtu kwa ajili ya kumtumia kupata infos za kijasusi. CIA na FBI wakaweka ngumu kumruhusu Ames. Lakini Ames akiwa na wasiwasi akafosi kukutana na huyu bwana kwenye bar Moja iliyoitwa mayflower ambayo pia ni hotel na haikuwa mbali sana na ubalozi wa Soviet hapo Washington. Baada ya Ames kusubiri muda mrefu huyu bwana pasipo kutokea akaamua kuchukua hatua nyingine . Akaamua kwenda kwenye ubalozi huo wa Soviet Hadi mapokezi akaacha parcel iliyokuwa na address ya balozi wa Russia nchini marekani general stanislav Androsov.

Ndani kulikuwa na note iliyosema nanukuu :" I am H. Aldrich Ames and my job is branch chief of Soviet counter-intelligence at the CIA. I served in new York where I used the alias Andy Robinson. I need $50000 and in exchange for the money, here is information about three agents we're developing in the Soviet union right now..."
Ni kwamba Ames alianza kuuza informations kwa Urusi Ili apate Hela na barua hiyo iliambatana na majina ya agents waliokuwa wanafanya kazi kama KGB lakini ni mapandikizi wa CIA. Aliamua kuchomesha wenzake.......
Pia Ames akawaahidi kwamba atashirikiana nao katika kuwapa info zote kuhusiana na operation za CIA dhidi ya Russia na taarifa nyeti za kitengo...
Sasa Ames akawa anasubiri majibu yake . Barua hii kutokana na unyeti wake ilifika kwa kanali victor cherkashin mkuu wa kitengo Cha kijasusi Cha counter-intelligence hapo ubalozini naye akaamua kuipasisha kwa mkuu wake wa idara ya FCD bwana Kryuchkov na aka approve bwana Ames apewe hela .
Na kweli bwana Ames alikuja kupigiwa simu na bwana Chuvakhin akimtaka wakutane kwenye ubalozi wa Soviet tarehe 15 may. Na kweli Ames akafika na Chuvakhin akamtambulisha kwa mkuu wake Bwana cherkashin. Wakapeana Convo za hapa na pale na mwisho akaambiwa ombi lako limekubaliwa[emoji39][emoji39].
 

Aldrich Ames akiwa kijana kipindi alipojiunga na CIA enzi hizo .



Aldrich Ames akiwa na mpenzi wake Rosario dupuy . Mwanadada huyu kutokana na kupenda matanuzi ilimgharimu Ames pesa nyingi na hatimaye kuanza kuuza informations za CIA kwa KGB Ili apate pesa .



Huyu ni Sergey Chuvakhin ,huyu ndiye aliyekutana na Aldrich Ames kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kutaka kuuza informations za kijasusi kwa KGB




Kanali victor cherkashin mkuu wa kitengo Cha kijasusi Cha counter-intelligence kwenye ubalozi wa Soviet hapo Washington. Huyu bwana ndiye aliye approve bwana Ames apewe hela alizoomba $ 50000 kutokana na Nia yake ya kuwauzia infos.
 
Naona tarehe 18 may haipo mbali.

Ila inashangaza balozi wa nchi kiwa traitor
 
@bianca2023 Ulimakafu @myayobend
 
Wahenga walinena hamna mkate mgumu mbele ya chai ndio hii sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…