Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Huwa najiuliza hizi signal wanazopeana za kuacha kitu sehem then mwengine anachukua na kuacha signal kuwa amepokea mzigo.. Hizo signals wanakuwa wamepewa kwenye training zao huko ujasusini collages au wanajiongeza tu juu kwa juu!?
 
Huwa najiuliza hizi signal wanazopeana za kuacha kitu sehem then mwengine anachukua na kuacha signal kuwa amepokea mzigo.. Hizo signals wanakuwa wamepewa kwenye training zao huko ujasusini collages au wanajiongeza tu juu kwa juu!?
Ni kozi maalum pia signal ambazo hutumika kutokana na kazi hivyo wote wahusika wanakuwa wanafahamu hii ni kuficha kwa wengine wasijue kinachoendelea

Code
 
Huwa najiuliza hizi signal wanazopeana za kuacha kitu sehem then mwengine anachukua na kuacha signal kuwa amepokea mzigo.. Hizo signals wanakuwa wamepewa kwenye training zao huko ujasusini collages au wanajiongeza tu juu kwa juu!?

Nimewakumbuka wale washenzi wa msumbiji waliokuwa wanafanya uharamia Mtwara na kibiti

Mbwa wale walikuwa na code balaa. Ila heshimuni jeshi letu na TISS yetu.

Hizi nyingine shutuma za TISS sijui uvccm ni very minor.
Inatosha [emoji23][emoji23]
 
Aisee tupia cha 30 watu tuendelee na mambo mengine kabla lile lichizi @chizimaarifa halijatoka huko kwenye mibange yake kuja kukutukana
 
Be blessed mdau[emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji108][emoji108]
Samahani, kama ikukupendeza jaribu kuisimulia story ya huyo bwana Ames!!!!!! Ni bonge moja la stori,lakini ni bora zaidi hasa kwa lugha yetu pendwa ya kiswahili!!!

Kutafsiri siyo kazi, kazi ni kuinogesha na kuipa madoido kwa lugha yetu. Naamini hiki kipaji unacho!!!!!!!! Halafu tuache tuamue nani zaidi kati ya :

Oleg Gordievsky vs Aldrich Hazen "Rick" Ames



Aldrich Hazen "Rick" Ames (/eɪmz/; born May 26, 1941) is a former CIA counterintelligence officer who was convicted of espionage on behalf of the Soviet Union and Russia in 1994. He is serving a life sentence, without the possibility of parole, in the Federal Correctional Institution in Terre Haute, Indiana.

Nb: Kwa Majasusi, Ames inasemekana mpaka leo yeye ndiye the greatest spy ever mpaka sasa!!!!!!!!!!

Nb: Vipi Putin????? Dunia ni zaidi ya tunavyoiona mimi na wewe!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nimewakumbuka wale washenzi wa msumbiji waliokuwa wanafanya uharamia Mtwara na kibiti

Mbwa wale walikuwa na code balaa. Ila heshimuni jeshi letu na TISS yetu.

Hizi nyingine shutuma za TISS sijui uvccm ni very minor.
Inatosha [emoji23][emoji23]
Hebu dadavua hizo code za hao wahuni waliokuwa wanasumbua nchi yetu, pongezi Kwa vyombo vyetu vya usalama sio vya mchezo mchezo
 
Code gani mkuu halafu hivi walikuwa wakifadhiliwa na nchi yeyote ya huko majuu au walikuwa wamevimbiwa mibange

Kama hizo tu za jamaa. Ukisoma unaeza dhani ni story tu.

Lakin mzee, code zinaachwa kuwa walipita wapi, exchange zifanyikie wapi.

Nyie mnaona maderu rais wa mawe tu, nyingine huwa ni code za matukio fulani fulani. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
30

Tulipoishia part one ndio tunaanzia hapa..............,,............[emoji3578][emoji3578][emoji3578]





Ndani ya Moscow baada ya Oleg kufika mbele ya mlango wa nyumba yake na kubaini kitasa Cha Tatu kipo locked hakutaka kuamini kabisa labda alisahau kufunga vitasa vyote. Ni dhahiri alikuwa na uhakika hakufunga kitasa hiki Cha Tatu na hakuwahi kuwa na ufunguo wake. Kwa kuwa naye ni jasusi mbobevu anayejua medani za kijasusi rasmi Sasa akajua KGB wanamfuatilia. Kijasho chembamba kilimtoka, aliamini muda wowote atakuwa mfu. Na adhabu ya msaliti aliijua . Ni kwamba atatiwa ndani ,Kisha atahojiwa kwa mbinu zote na ateme data za kila aina alizonazo ,na mwisho ni BULLET IN THE HEAD na mwisho kuzikwa kama mbwa na kaburi lake lisikae lijulikane kamwe. Mawazo haya yote yalimfanya agande kifikra kwa sekunde kadhaa.
Akiwa kwenye Lindi la mawazo akazidi kutafakari endapo KGB walikuwa wanajua mambo yake yote ya Siri ni kwamba wasingemruhusu muda huo aweze kufika Hadi mlango wa nyumba yake. Angekamatwa kulekule airport na Moja kwa Moja angepelekwa kwenye torture chamber zilizoko kwenye basement ya jengo la lubyanka makao makuu ya KGB. Mpaka hapo alijua ashashtukiwa ila walikuwa hawana ushahidi wa kutosha kumtia hatiani. Kwa cheo Cha ukanali alichokuwa nacho Oleg wakati huo , sio rahisi kumtuhumu juu juu tu na tuhuma za usaliti ilihitajika jitihada zaidi za kumtia hatiani na pia hata kama akitiwa hatiani kulikuwa na utaratibu KGB wa kuwapa mateso makali maafisa (torturing) wenye vyeo vya ukanali. Kumnasa msaliti au spy kulikuwa na hatua kadhaa zilipaswa kuzingatiwa. Kumwangalia kwa ukaribu suspect, kumsikiliza kila jambo huyu suspect na mwisho kumsubiri ajae kwenye 18 na afanye mistake Moja tu Ili kumnasa red handed . Hili bwana Budanov aliyekuwa anamtilia mashaka Oleg alilizingatia. Advantage kubwa aliyokuwa nayo Oleg ni kwamba alikuwa anajua anafuatiliwa na majasusi wenzake....
Muda huu wote akiwa anatafakari , alikuwa bado mbele ya mlango na alihitaji kuingia ndani kipengele kikawa kitasa Cha Tatu funguo zake Hana. Hapo hapo akaenda jirani kwenye nyumba ya afisa mwenzake ambaye alikuwa ni mtaalamu wa vyuma vyuma ,na kweli akamsaidia kufungua mlango ule na mwamba akazama ndani. Hii nyumba ya Oleg tayari ilishafanyiwa upekuzi na kupandikizwa vinasa sauti na kamera za Siri kila Kona ya chumba. Baada ya kujua Hilo akawa mpole hakutaka kuonyesha ku panick maana aliona akipaniki na nyumba hiyo alihisi tayari Kuna camera za Siri basi watakuwa wanamwona jinsi anavyofanya hapo ndani muda huo. Kwa haraka haraka nyumba hiyo unaweza sema hakukuwahi kuingia mtu kutokana na vitu kuwa in placed kama vilivyoachwa . Lakini kwa Oleg alijua tu hapa kulikuwa na kikosi Cha majasusi walifika ,wakafanya Yao Kisha wakasepa.
Usiku huo bwana Oleg hakulala sana kutokana na mawazo mengi yakimwandama na swali likiwa NI NANI ALIYENISALITI , na KGB WANAJUA NINI KUMHUSU?.[emoji28][emoji28][emoji28]
Kesho yake aliamka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda makao makuu ya KGB. Na kweli alipofika alikutana na bwana Nikolai Gribin . Na gribin afisa mwenzake akamwambia kuna mahojiano na wakuu wa KGB hivyo ajipange .alimwambia hayo maneno kiutani utani.. lakini katikati ya utani Kuna ukweli mchungu nyuma yake......
Na kweli baada ya kama lisaa hivi bwana Oleg aliitwa kwenye ofisi ya deputy wa idara ya FCD bwana Victor Grushko.....
 
Aiseee....
 
Wazo zuri sana ngoja tumalize hiki kipengele [emoji3578][emoji3578]
 
kitasa hatimaye hiki hapa,kimefunguliwa..tuendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…