Bloodstone
JF-Expert Member
- Feb 16, 2016
- 920
- 994
Iko deep
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu kipindi cha vita baridi mambo yalikuwa mengi, mengi sanaNimejiuliza sana kuhusu info hizi kubwa hadharani, hivi mahusiano kati urusi na Uingereza yalikuwa katika hali nzuri kweli?
Ni kozi maalum pia signal ambazo hutumika kutokana na kazi hivyo wote wahusika wanakuwa wanafahamu hii ni kuficha kwa wengine wasijue kinachoendeleaHuwa najiuliza hizi signal wanazopeana za kuacha kitu sehem then mwengine anachukua na kuacha signal kuwa amepokea mzigo.. Hizo signals wanakuwa wamepewa kwenye training zao huko ujasusini collages au wanajiongeza tu juu kwa juu!?
somo hiloHuwa najiuliza hizi signal wanazopeana za kuacha kitu sehem then mwengine anachukua na kuacha signal kuwa amepokea mzigo.. Hizo signals wanakuwa wamepewa kwenye training zao huko ujasusini collages au wanajiongeza tu juu kwa juu!?
Huwa najiuliza hizi signal wanazopeana za kuacha kitu sehem then mwengine anachukua na kuacha signal kuwa amepokea mzigo.. Hizo signals wanakuwa wamepewa kwenye training zao huko ujasusini collages au wanajiongeza tu juu kwa juu!?
Aisee tupia cha 30 watu tuendelee na mambo mengine kabla lile lichizi @chizimaarifa halijatoka huko kwenye mibange yake kuja kukutukana29
Kwa kuwa Ames Sasa aliamua kuiuzia KGB information za kijasusi za CIA, alilipwa kiasi alichodai Cha $50000 kama ilivyotarajiwa. Kama ilivyo kwa Oleg , Hivyo hivyo naye aliwamegea Siri za mapandikizi wote wa CIA ndani ya KGB ndani ya ubalozi wa Soviet hapo marekani . Na zaidi Ames aliwaambia Kuna spy wa KGB ndani ya uingereza anayeifanyia kazi M16 .Kumbuka huyu Ames alikuwa kwenye kikosi kazi Cha Gerber Cha CIA kile kilichoundwa kutatua fumbo la SOURCE au TICKLE anayewapa informations za Siri M16. (Lakini kwa mujibu wa wachambuzi wa hii kesi ya Oleg hapo Baadaye , wengine walitoa maoni Yao wakisema huenda Ames hakumjua Oleg personally ,ila alihisi Kuna mole wa KGB anayeifanyia kazi uingereza. Wengine wakadai ni lazima alimfahamu Oleg ndiye source)
Kama kawaida Ames aliendelea kukutana na Chuvakhin . Walikutana kwenye restaurant Moja iliyojulikana kama Joe and mo's restaurant na Chuvakhin akamkabidhi Ames mfuko wa plastiki. Na baada ya kuagana Ames akapanda gari kwa ajili ya kuondoka na alipofika kwenye park way akapaki gari pemben kwa ajili ya kufungua mfuko huo na ndani alikutana na parcel nyingine. Alipoifungua ndani alikutana na vibunda kadhaa vya Dola 100 vyenye thamani ya $50000. na bonus [emoji39][emoji39]. Ames hakuamini ila ndio hivyo alilipwa mkwanja.. Lakini akiwa anaenda home huku Russia walianza msako HEAVY ndani ya KGB ya kumwinda msaliti au wasaliti . Huu ulikuwa ni msako wa kimya kimya.
Siku ambayo Ames anakutana na cherkashin ,kesho yake yaani tarehe 16 siku ya alhamisi , ubalozi wa Soviet hapo London ulipokea ujumbe wa telegram wa ghafla kutoka Moscow. Ujumbe huu Ulifika Hadi kwenye meza ya Oleg mteule mpya wa ubalozi. Alipousoma alihisi kijasho chembamba kikimshuka. Ni kwamba ujumbe ulimtaka arudi Moscow mara Moja kwa ajili ya ku confirm zaidi uteuzi wake wa ubalozi. Na alihitajika awe amefika makao makuu ya KGB hapo Moscow ndani ya siku mbili haraka sana. Na akifika aonane na Victor chebrikov mwenyekiti wa KGB na vilevile Vladimir Kryuchkov mkuu wa idara ya FCD . Alihisi Kuna jambo lilikuwa linaendelea na sio la kawaida.
Na mara Moja Oleg akafanya mawasiliano na maafisa kadhaa wa M16 waonane huko Bayswater ilipo safe house. Walijadiliana na hao maafisa kwa kina endapo bwana Oleg aitikie wito wa kwenda Moscow au M16 wachukue maamuzi magumu ya kumficha Oleg na familia yake yote ndani ya safe house. maana ni kama taa nyekundu imeshaanza kuwaka.
Ni kwamba tangu ateuliwe , Moscow walikuwa kimya pasipo kusema kitu chochote. alitegema na kutarajia pongezi kutoka kwa wakubwa wa kitengo lakini haikuwa hivyo na kingine kikichomshtua Oleg ni kwamba tokea ateuliwe Kuna documents muhimu za kiofisi hajakabidhiwa Hadi muda huo. Haya yote yalikuwa yakijadiliwa kwenye safe house .
Oleg aliwaza labda kwakuwa aliteuliwa pasipo mwenyekiti wa KGB hakuwepo Moscow ,hivyo alihitaji Oleg afike Moscow kwa ajili ya mwenyekiti chebrikov kutoa mkono wa heri .
Oleg aliwaza endapo kama Moscow wameshagundua jambo dhidi yake la usaliti , kwanini wampe siku mbili awe amefika badala ya siku Moja? maswali haya yote aliyachanganua Ili kujua wito huu wa ghafla ulihitaji Nini. Maana kama tangazo rasmi la uteuzi wake lilitoka rasmi , imekuwaje aitwe mara ya pili nyumbani? Vilevile aliwaza endapo kama kweli walimhisi ni spy dhidi ya nchi yake ,basi angetumiwa kikosi kazi Cha WASIOJULIKANA Cha thirteenth department ndani ya KGB kije Hadi London kimteke kimya kimya na kumpeleka Hadi Moscow. Na la Zaidi kama kungekuwa na confirmation muhimu kwanini wasingezituma kwa njia ya telegram maana kama tangazo rasmi la uteuzi wake lilishatoka miezi miwili au mitatu nyuma. Nini Cha ziada walikihitaji ? . Na kingine ambacho kilikuwa ni kama wake up call , ni wito huu uliotumwa kwa njia ya telegram ulitoka Moja kwa Moja kwa mwenyekiti wa KGB . kiufupi maswali aliyokuwa anajiuliza na ku discuss yeye na manjagu hao wa M16 yalikuwa ni mengi kuliko majawabu. Swala likabaki Moja tu . alihitajika kurudi Moscow mapema iwezekanavyo na kwa haraka. kikao kilitamatika kati ya Oleg na M16 safe house pasipo kufikia solution ya kueleweka.
Tukirudi kwenye makao makuu ya M16 jengo la century house maafisa wa ngazi za juu ikiwemo Chris curwen mkuu wa kitengo,John deverell na afisa Simon brown (huyu afisa mpya ndio alikabidhiwa jukumu la kukutana na Oleg kwenye safe house) waliamua kulipa hili swala la Oleg uzito wa aina yake maana one mistake ndani ya sekunde walikuwa wanaenda kumpoteza NOCTON mazima . Baada ya kikao kizito Cha Hawa maafisa kudiscuss faida na hasara pamoja na ku predict madhara yatayotokea Ikiwa Oleg aende au asiende walihitimisha kwa kumwachia Oleg mwenyewe kufanya maamuzi yake binafsi ya mwisho.
Wanasema kwamba nanukuu:" The key to successful gambling is intuition ,the sixth sense that enables a player to predict events and read opponent's mind .." Swala likabaki Je ni kitu gani chochote KGB walichokuwa wanakijua kumhusu Oleg ? Ni kwamba Oleg alijaribu kuwaza endapo kama KGB wanajua chochote kumhusu basi alipredict Nini kingefuata baada ya hapo. Kwa kifupi ni kwamba Russia walikuwa wanajua lakini walijua kwa uchache sana kumhusu Oleg.
Ni kwamba Kanali victor budanov mkuu wa kitengo Cha counter-intelligence ndani ya KGB alikuwa ndio mtu hatari na aliyeogopwa sana kitengoni kwa wakati huo. Aliamua kuingia mzigoni wa kumsaka msaliti ndani ya KGB baada ya kuambiwa Kuna pandikizi ndani ya kitengo Chao na maafisa wakubwa wake wa kitengo. Kwa kifupi huyu pandikizi au mole hakuwahi mfahamu ni nani haswa . Kumbuka Ames alikuwa akiwapa informations kwamba Kuna pandikizi kwenye idara ya KGB anayetumika na uingereza. Hapo bwana huyu akaamini ikiwa ni kweli basi Moja kwa Moja atakuwa ndani ya ubalozi wa Soviet hapo London .Kwa kifupi suspect hakuwa Oleg peke yake ,Bali pia Nikitenko ambaye huyu alikuwa anachuana na Oleg kutaka cheo hicho Cha ubalozi . Na watatu alikuwa ni afisa mwingine ambaye ni parshikov Japo huyu alikuwa less suspected. Ni kwamba huyu kanali budanov hakuwa na uhakika sana kama Oleg ndiye msaliti maana aliamini msaliti anaweza kutokea sehemu yoyote ile duniani mbali na uingereza. Lakini akaamini kwamba endapo mtu (Oleg) akirudi Moscow kama ni msaliti au sio msaliti nafsi yake itamjulisha tu.. Alikuwa sahihi. ....
Lakini Oleg akiwa bado London alipokea ujumbe wa pili wa telegram kutoka Moscow tarehe 17 ijumaa. Ujumbe huu ukimtaka akiwa anarudi Moscow aje na maelezo kadhaa na ya KINA kuhusiana na matatizo baina ya Russia na uingereza hivyo aje na facts na awe amejiandaa vya kutosha kwa discussion.[emoji848][emoji848]
Kwa upande wa nje ilionekana ni kama Anaenda ku discuss kikao Cha kawaida kama ilivyo desturi .......[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Jioni yake siku hiyo bwana Oleg alikutana Tena na maafisa wale wa M16 Katika kikao hiki walijadili sana kwa uzito swala hili na wakamwambia endapo akichukua uamuzi wa kuwatoroka KGB ,ni kwamba nchi ya uingereza itamlinda yeye pamoja na familia yake maisha Yao yote ,Na kama akiamua kwenda huko Moscow kuitikia wito na likampata la kumpata huko basi wao kama uingereza watakuwa na deni la kulipa kwa kumpoteza mtu muhimu aliyeisaidia nchi hiyo na dunia kwa ujumla[emoji848].
Lakini mwanamama Veronica price kumbuka tokea mwanzo Oleg akiwa huko Denmark walikuwa wameshachora mpango mzima wa kumtorosha Oleg Moscow endapo mambo yangeenda kombo kwa bwana huyu. Huu mpango ulikuwa tayari muda wowote ,na Sasa M16 wakaona huu mpango utakuwa practically muda wowote ule kuanzia Sasa kutokana na swala Oleg kuitwa huko Moscow lipo njia panda . (Hii operation ya kijasusi ya kumtorosha Oleg nje ya Russia tutaijadili in deep A to z). Baada ya kikao hicho mwanamama alimpa pakiti mbili ndogo zilizokuwa na vidonge Fulani bwana Oleg.
Vilikuwa vya kazi maalumu........
Jioni hiyo Oleg Gordievsky aliporudi kwa mkewe Leila, alimwambia anatakiwa aende Moscow kwa maswala kadhaa ya kiofisi hivyo atasafiri na siku chache tu mbeleni atarudi. Mkewe alihisi Kuna utofauti kidogo kwa mumewe usiku huo akionekana na wasiwasi kwa kiasi fulani. Hilo likapita. Sasa Bwana..
Siku ya TAREHE 18 MWEZI MEI 1985 ilikuwa ni siku nzito sana katika ulimwengu wa kijasusi .
Siku hii bwana Aldrich Ames huko Washington alienda benki na mkewe Rosario dupuy kuweka fedha kiasi Cha Dola elfu Tisa hivi ,na kwa kifupi tu alimwambia mkewe fedha hizo ni mkopo alioupata kutoka kwa rafiki yake...............[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] Haukuwa mkopo huu.....zingatia Hilo[emoji3578][emoji3578][emoji3578]
Lakini kwa upande wa Moscow , KGB walikuwa wanamsubiri bwana OLEG GORDIEVSKY awasili akitokea London kwa hamu kubwa sana. Kanali victor budanov ndiye aliyeagiza nyumba ya Oleg iliyopo mitaa ya Leninsky prospekt ipekuliwe vya kutosha ,na kupandikizwa vinasa sauti pamoja na kamera za Siri kabla ya Oleg kuwasili. Kwa kifupi nyumba nzima ilifanyiwa bugging na mafundi au technicians wa kitengo cha K Directorate na baada ya kumaliza kazi wakabana vitasa vyote vya mlango wa mbele wa nyumba hiyo wakatokomea.(WALI LOCK VITASA VYOTE VITATU)........
Katika upekuzi huo , budanov hakukuta la kumtilia mashaka sana bwana Oleg .
Lakini kama tu CIA walivyoanza kutumia njia za triangulation na elimination methods za kuchora pattern na kuunganisha dots mpaka wakajua SOURCE wa M16 ni Oleg ,naye bwana huyu alifanya hivyo .
Alianza kupitia mafaili mbalimbali ya Oleg tokea akiwa anafanya kazi Denmark miaka kadhaa nyuma .Alianza kuunganisha matukio kadhaa kama ifuatavyo: uhusiano wake na stanislav Kaplan wa Czechoslovakia kipindi akiwa chuoni, vilevile Oleg alikuwa yupo interested sana na western culture and literature. Maana kwenye upekuzi wa nyumba ile budanov aliweza kupata kitabu Cha mashairi Cha William Shakespeare. Akazidi kuunganisha matukio jinsi pia visa application ya Oleg ilivyofanyiwa kazi haraka kuwa approved ndani ya siku 22 badala ya siku 30 kama utaratibu ulivyotaka.
Budanov aliendelea kuchora pattern kuunganisha matukio kadhaa dhidi ya OLEG, kwa mfano huyu agent akiwa nchi za Scandinavia ,ndipo majasusi au watu potential waliokuwa wanafanya kazi na KGB waligundulika na kukamatwa .mfano ni Haavik na treholt wa Norway , vilevile afisa berling wa Sweden . Je Oleg alihusika katika kuwachomesha Hawa? aliwaza budanov. Na la Zaidi ni kukamatwa na kushtakiwa kwa bwana bettaney au Koba afisa wa M15 kipindi huyu Oleg akiwa uingereza. Na la zaidi Bwana budanov aliendelea kupata clue ,jinsi balozi wa London wakati huo bwana Arkadi guk na Igor titov walivyofukuzwa na mamlaka ya serikali ya uingereza kwa kufuatana. Na lingine ni kwamba budanov alipata clue nyingine , kipindi Oleg akiwa anafanya kazi huko Denmark 1973 ,aliomba ruhusa kukutana na afisa wa M16 aliyeitwa bromhead na kupewa ruhusa na wakubwa ,lakini baada ya hapo hakuna kilichokuwa kikiendelea na hakuna Repoti yoyote iliyofika mezani kwa wakubwa .(Kama mnakumbuka huyu bromhead baada ya kukutana na Oleg kipindi akiwa Denmark alipotea kwa kipindi fulani kabla ya kuja kukutana Tena na oleg.... haikujulikana nini sababu....)
Baada ya Budanov kupata info zote kumhusu Oleg na kuyaunganisha kwa pamoja hakuitimisha Moja kwa Moja kwamba Oleg ndiye SNITCH ,Bali alimsubiri afike kwanza Moscow Alitaka ushahidi wa Red handed...
turudi kwa Oleg................................
Kabla ya kuondoka London ,Oleg alikuwa na kazi ya kuikamilisha ya mwisho ya KGB.
Ni kwamba mwezi machi nyuma Moscow walituma kiasi Cha euro 8000 ambazo zilikuwa ni noti 20 hivi pasipo mamlaka za uingereza kufahamu. Hizi pesa bwana Oleg alipaswa kuziacha sehemu Fulani maalumu na zije kuchukuliwa na mtu .Huyu aliyepaswa kuchukua alikuwa ni recruit mpya au illegal aliyepandikzwa ndani ya uingereza . ilikuwa sio lazima Oleg ajue ni nani huyu illegal. Huyu illegal alipewa jina la DARIO. kwa hiyo kiasi hicho Cha fedha kilipaswa kwenda kwa huyu DARIO. ilikuwa hivi. technical department ya hapo ubalozini ikatengeneza tofali artificial kama la kuchoma na katikati ya tofali Hilo kulikuwa na uwazi kwa ajili ya kuweka noti hizo za € 8000. Baada ya hapo huyu illegal angepaswa kutoa signal kwa Oleg kwamba Yuko tayari kuzipokea fedha hizo kwa kuacha alama ya chaki ya Blu kwenye nguzo ya taa iliyopo makutano ya audley square ,karibu na ubalozi wa marekani. Na bwana Oleg fedha hizo baada ya kuziweka ndani ya tofali alitumbukiza kwenye mfuko wa plastiki na angepaswa naye kuacha mfuko huo kwenye kichochoro kimoja kilichopakana na fence ya viwanja vya michezo vya Coram kwenye mji wa Bloomsbury. Na huyu DARIO baada ya kupokea hicho kibunda alipaswa kuacha Tena signal kwa ajili ya Oleg ku confirm kibunda kimepokelewa . Hivyo huyu mtu angeacha bablishi au chewing gum iliyotafunwa kwenye nguzo ya zege iliyo karibu na pub Moja iliyopo mitaa ya Sudbury Hill... mpango huu ukaenda vizuri kama ilivyopangwa.. Huu mpango bwana Oleg akawatonya M16.
Na kweli siku hiyo Mida ya jioni tarehe 18 may aliwachukua mabinti zake kwenda kucheza kwenye viwanja vya Coram na ilipofika jioni alidondosha tofali na begi la plastiki. Akiwa anafanya hivyo watu waliokuwa karibu ni mama mmoja ambaye anaonekana anamwendesha mwanae kwenye vile vigari vya kubebea watoto Vya matairi au pram. mtu mwingine aliyekuwa karibu ni mwendesha baiskeli akiwa anaingiza cheni kwenye meno ya pedal ya baiskeli iliyokuwa imechomoka. Huyu mwanamke aliyekuwa na kigari Cha kuendesha mtoto alikuwa ni surveillance expert wa M15 na hicho kijigari kilikuwa na kamera ya Siri imefichwa hapo. Na huyu jamaa mwenye baiskeli alikuwa ni John deverell mkuu wa kitengo Cha surveillance ndani ya M15. dakika kadhaa baadaye akajitokeza jamaa mmoja akiwa anatembea Kwa Kasi ,halafu akasimama akaokota mfuko ule wa plastiki na kusepa . Huyu deverell akawa ameanza kuendesha baiskeli kwa Kasi Ili wamjue huyu bwana ni nani aliyechukua mfuko ule , lakini akawa amechelewa ,baada ya mtu yule kujichanganya katikati ya watu na kutokomea ikawa imeisha hivyo . hawakumjua huyu so called DARIO ni nani.....
Ilipofika siku ya jumapili mchana Oleg aliwabusu mkewe na wanawe kwa mara ya mwisho akiamini huenda hatawaona tena .
Aliwakumbatia kwa nguvu wanawe wawili maria na Ana baada ya hapo akawachia na Moja kwa Moja akapanda taxi na kuelekea uwanja wa ndege wa Heathrow hapo London.
Hivyo rasmi tarehe 19 mei muda wa saa kumi kamili jioni akawa amepanda ndege ya shirika la ndege la Aeroflot akielekea Moscow .
Code gani mkuu halafu hivi walikuwa wakifadhiliwa na nchi yeyote ya huko majuu au walikuwa wamevimbiwa mibangeMbwa wale walikuwa na code balaa. Ila heshimuni jeshi letu na TISS yetu.
Samahani, kama ikukupendeza jaribu kuisimulia story ya huyo bwana Ames!!!!!! Ni bonge moja la stori,lakini ni bora zaidi hasa kwa lugha yetu pendwa ya kiswahili!!!Be blessed mdau[emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji108][emoji108]
Hebu dadavua hizo code za hao wahuni waliokuwa wanasumbua nchi yetu, pongezi Kwa vyombo vyetu vya usalama sio vya mchezo mchezoNimewakumbuka wale washenzi wa msumbiji waliokuwa wanafanya uharamia Mtwara na kibiti
Mbwa wale walikuwa na code balaa. Ila heshimuni jeshi letu na TISS yetu.
Hizi nyingine shutuma za TISS sijui uvccm ni very minor.
Inatosha [emoji23][emoji23]
Code gani mkuu halafu hivi walikuwa wakifadhiliwa na nchi yeyote ya huko majuu au walikuwa wamevimbiwa mibange
Aiseee....30
Tulipoishia part one ndio tunaanzia hapa..............,,............[emoji3578][emoji3578][emoji3578]
Ndani ya Moscow baada ya Oleg kufika mbele ya mlango wa nyumba yake na kubaini kitasa Cha Tatu kipo locked hakutaka kuamini kabisa labda alisahau kufunga vitasa vyote. Ni dhahiri alikuwa na uhakika hakufunga kitasa hiki Cha Tatu na hakuwahi kuwa na ufunguo wake. Kwa kuwa naye ni jasusi mbobevu anayejua medani za kijasusi rasmi Sasa akajua KGB wanamfuatilia. Kijasho chembamba kilimtoka, aliamini muda wowote atakuwa mfu. Na adhabu ya msaliti aliijua . Ni kwamba atatiwa ndani ,Kisha atahojiwa kwa mbinu zote na ateme data za kila aina alizonazo ,na mwisho ni BULLET IN THE HEAD na mwisho kuzikwa kama mbwa na kaburi lake lisikae lijulikane kamwe. Mawazo haya yote yalimfanya agande kifikra kwa sekunde kadhaa.
Akiwa kwenye Lindi la mawazo akazidi kutafakari endapo KGB walikuwa wanajua mambo yake yote ya Siri ni kwamba wasingemruhusu muda huo aweze kufika Hadi mlango wa nyumba yake. Angekamatwa kulekule airport na Moja kwa Moja angepelekwa kwenye torture chamber zilizoko kwenye basement ya jengo la lubyanka makao makuu ya KGB. Mpaka hapo alijua ashashtukiwa ila walikuwa hawana ushahidi wa kutosha kumtia hatiani. Kwa cheo Cha ukanali alichokuwa nacho Oleg wakati huo , sio rahisi kumtuhumu juu juu tu na tuhuma za usaliti ilihitajika jitihada zaidi za kumtia hatiani na pia hata kama akitiwa hatiani kulikuwa na utaratibu KGB wa kuwapa mateso makali maafisa (torturing) wenye vyeo vya ukanali. Kumnasa msaliti au spy kulikuwa na hatua kadhaa zilipaswa kuzingatiwa. Kumwangalia kwa ukaribu suspect, kumsikiliza kila jambo huyu suspect na mwisho kumsubiri ajae kwenye 18 na afanye mistake Moja tu Ili kumnasa red handed . Hili bwana Budanov aliyekuwa anamtilia mashaka Oleg alilizingatia. Advantage kubwa aliyokuwa nayo Oleg ni kwamba alikuwa anajua anafuatiliwa na majasusi wenzake....
Muda huu wote akiwa anatafakari , alikuwa bado mbele ya mlango na alihitaji kuingia ndani kipengele kikawa kitasa Cha Tatu funguo zake Hana. Hapo hapo akaenda jirani kwenye nyumba ya afisa mwenzake ambaye alikuwa ni mtaalamu wa vyuma vyuma ,na kweli akamsaidia kufungua mlango ule na mwamba akazama ndani. Hii nyumba ya Oleg tayari ilishafanyiwa upekuzi na kupandikizwa vinasa sauti na kamera za Siri kila Kona ya chumba. Baada ya kujua Hilo akawa mpole hakutaka kuonyesha ku panick maana aliona akipaniki na nyumba hiyo alihisi tayari Kuna camera za Siri basi watakuwa wanamwona jinsi anavyofanya hapo ndani muda huo. Kwa haraka haraka nyumba hiyo unaweza sema hakukuwahi kuingia mtu kutokana na vitu kuwa in placed kama vilivyoachwa . Lakini kwa Oleg alijua tu hapa kulikuwa na kikosi Cha majasusi walifika ,wakafanya Yao Kisha wakasepa.
Usiku huo bwana Oleg hakulala sana kutokana na mawazo mengi yakimwandama na swali likiwa NI NANI ALIYENISALITI , na KGB WANAJUA NINI KUMHUSU?.[emoji28][emoji28][emoji28]
Kesho yake aliamka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda makao makuu ya KGB. Na kweli alipofika alikutana na bwana Nikolai Gribin . Na gribin afisa mwenzake akamwambia kuna mahojiano na wakuu wa KGB hivyo ajipange .alimwambia hayo maneno kiutani utani.. lakini katikati ya utani Kuna ukweli mchungu nyuma yake......
Na kweli baada ya kama lisaa hivi bwana Oleg aliitwa kwenye ofisi ya deputy wa idara ya FCD bwana Victor Grushko.....
Mambo tayari huku..Ujamaa ilikuwa kero sana heri ujamaa wa Sasa hivi ka wa china, na huo ujamaa ndio ulileta hyo chuki
Wazo zuri sana ngoja tumalize hiki kipengele [emoji3578][emoji3578]Samahani, kama ikukupendeza jaribu kuisimulia story ya huyo bwana Ames!!!!!! Ni bonge moja la stori,lakini ni bora zaidi hasa kwa lugha yetu pendwa ya kiswahili!!!
Kutafsiri siyo kazi, kazi ni kuinogesha na kuipa madoido kwa lugha yetu. Naamini hiki kipaji unacho!!!!!!!! Halafu tuache tuamue nani zaidi kati ya :
Oleg Gordievsky vs Aldrich Hazen "Rick" Ames
Aldrich Hazen "Rick" Ames (/eɪmz/; born May 26, 1941) is a former CIA counterintelligence officer who was convicted of espionage on behalf of the Soviet Union and Russia in 1994. He is serving a life sentence, without the possibility of parole, in the Federal Correctional Institution in Terre Haute, Indiana.
Nb: Kwa Majasusi, Ames inasemekana mpaka leo yeye ndiye the greatest spy ever mpaka sasa!!!!!!!!!!
Nb: Vipi Putin????? Dunia ni zaidi ya tunavyoiona mimi na wewe!!!!!!!!!!!!!!!!!!
kitasa hatimaye hiki hapa,kimefunguliwa..tuendelee30
Tulipoishia part one ndio tunaanzia hapa..............,,............[emoji3578][emoji3578][emoji3578]
Ndani ya Moscow baada ya Oleg kufika mbele ya mlango wa nyumba yake na kubaini kitasa Cha Tatu kipo locked hakutaka kuamini kabisa labda alisahau kufunga vitasa vyote. Ni dhahiri alikuwa na uhakika hakufunga kitasa hiki Cha Tatu na hakuwahi kuwa na ufunguo wake. Kwa kuwa naye ni jasusi mbobevu anayejua medani za kijasusi rasmi Sasa akajua KGB wanamfuatilia. Kijasho chembamba kilimtoka, aliamini muda wowote atakuwa mfu. Na adhabu ya msaliti aliijua . Ni kwamba atatiwa ndani ,Kisha atahojiwa kwa mbinu zote na ateme data za kila aina alizonazo ,na mwisho ni BULLET IN THE HEAD na mwisho kuzikwa kama mbwa na kaburi lake lisikae lijulikane kamwe. Mawazo haya yote yalimfanya agande kifikra kwa sekunde kadhaa.
Akiwa kwenye Lindi la mawazo akazidi kutafakari endapo KGB walikuwa wanajua mambo yake yote ya Siri ni kwamba wasingemruhusu muda huo aweze kufika Hadi mlango wa nyumba yake. Angekamatwa kulekule airport na Moja kwa Moja angepelekwa kwenye torture chamber zilizoko kwenye basement ya jengo la lubyanka makao makuu ya KGB. Mpaka hapo alijua ashashtukiwa ila walikuwa hawana ushahidi wa kutosha kumtia hatiani. Kwa cheo Cha ukanali alichokuwa nacho Oleg wakati huo , sio rahisi kumtuhumu juu juu tu na tuhuma za usaliti ilihitajika jitihada zaidi za kumtia hatiani na pia hata kama akitiwa hatiani kulikuwa na utaratibu KGB wa kuwapa mateso makali maafisa (torturing) wenye vyeo vya ukanali. Kumnasa msaliti au spy kulikuwa na hatua kadhaa zilipaswa kuzingatiwa. Kumwangalia kwa ukaribu suspect, kumsikiliza kila jambo huyu suspect na mwisho kumsubiri ajae kwenye 18 na afanye mistake Moja tu Ili kumnasa red handed . Hili bwana Budanov aliyekuwa anamtilia mashaka Oleg alilizingatia. Advantage kubwa aliyokuwa nayo Oleg ni kwamba alikuwa anajua anafuatiliwa na majasusi wenzake....
Muda huu wote akiwa anatafakari , alikuwa bado mbele ya mlango na alihitaji kuingia ndani kipengele kikawa kitasa Cha Tatu funguo zake Hana. Hapo hapo akaenda jirani kwenye nyumba ya afisa mwenzake ambaye alikuwa ni mtaalamu wa vyuma vyuma ,na kweli akamsaidia kufungua mlango ule na mwamba akazama ndani. Hii nyumba ya Oleg tayari ilishafanyiwa upekuzi na kupandikizwa vinasa sauti na kamera za Siri kila Kona ya chumba. Baada ya kujua Hilo akawa mpole hakutaka kuonyesha ku panick maana aliona akipaniki na nyumba hiyo alihisi tayari Kuna camera za Siri basi watakuwa wanamwona jinsi anavyofanya hapo ndani muda huo. Kwa haraka haraka nyumba hiyo unaweza sema hakukuwahi kuingia mtu kutokana na vitu kuwa in placed kama vilivyoachwa . Lakini kwa Oleg alijua tu hapa kulikuwa na kikosi Cha majasusi walifika ,wakafanya Yao Kisha wakasepa.
Usiku huo bwana Oleg hakulala sana kutokana na mawazo mengi yakimwandama na swali likiwa NI NANI ALIYENISALITI , na KGB WANAJUA NINI KUMHUSU?.[emoji28][emoji28][emoji28]
Kesho yake aliamka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda makao makuu ya KGB. Na kweli alipofika alikutana na bwana Nikolai Gribin . Na gribin afisa mwenzake akamwambia kuna mahojiano na wakuu wa KGB hivyo ajipange .alimwambia hayo maneno kiutani utani.. lakini katikati ya utani Kuna ukweli mchungu nyuma yake......
Na kweli baada ya kama lisaa hivi bwana Oleg aliitwa kwenye ofisi ya deputy wa idara ya FCD bwana Victor Grushko.....