Kingine ni kwamba wakuu wa juu kitengoni walitaka kusolve hii ishu kimya kimya kuepusha embarrassment ikija kujulikana na magharibi... Mistake ndio ilipoanzia hapoMuda mwingine mkiwa mnasoma taarifa kama hizi muwe na tafakuri. Mmeambiwa kuanzia cheo Cha Kanali kinahitaji ushahidi ndio atuhumiwe, unadhani ukilichukua swala kama hilo kichwa kichwa utaleta picha gani Kwa Waandamizi wengine kama yeye.
Bado pia na wewe unaendelea kubabwaja tu kama nilivosema hapo juu... Unakataa nini wakati iko wazi na uthibitisho ndio huo kwamba walifeli??? Sijui hata unachobisha ni nn hapaMuda mwingine mkiwa mnasoma taarifa kama hizi muwe na tafakuri. Mmeambiwa kuanzia cheo Cha Kanali kinahitaji ushahidi ndio atuhumiwe, unadhani ukilichukua swala kama hilo kichwa kichwa utaleta picha gani Kwa Waandamizi wengine kama yeye.
Kingine ni kwamba wakuu wa juu kitengoni walitaka kusolve hii ishu kimya kimya kuepusha embarrassment ikija kujulikana na magharibi... Mistake ndio ilipoanzia hapo
Hii ndiyo maana ipo hivi ilivyo kwa sababu imejaa lundo la wajinga. Sasa wewe nini ulichoandika hapa ambacho hakijaandikwa na mwenye thread!? Kwa nn huwa mnapenda kujivua nguo kiasi hiki? Yaani lengo lako kila mtu akujue kama wewe ni mjinga au??Kwa ufaham wangu huyu Oleg, hakuwa agent Mi6 wakt anapelekwa katika ubalozi wa Russia nchini Denmark. Maana Oleg, baba yake naye alikuwa KGB officer. Akiwa Denmark, alichukizwa na matendo ya Russia dhidi ya Czech, ndipo aliamua kubadili nia yake ya kuwa mtiifu kwa Russia. Simu yake moja kwa mkewe kuonyesha kuchukizwa na kitendo hicho cha Russia kwa Czech ndio ilitoa signal kwa shirika la intelligence la Denmark kwamba huenda Oleg anataka kuwa double agent.
Denmark kwakua hawakuwa na skills za kumtongoza high rank official na intel, wakawaomba wabia wao Mi6 wawasaidie. Kwahio hapa, ndipo Mi6 ilimnasa baada ya vikao kama viwili, na cha mwisho alicho insists Oleg kuwa, yupo tayr kwa kuongea nao kuwa double agent kwa sharti moja tu kikao kinacho fuata atakutana na waingereza pekee bila kuwepo raia yyte wa Danish.
Alifanya kazi ba Mi6 nadhani kwa miaka 4 hivi kwa ku leak top Russian secrets na micro films za raia wa Russia walio majajsusi Europe, pia maafisa na raia wa Europe wanaofanya kazi kwa russia. Baada ya miaka minne, alirudishwa russia makao makuu kgb, pale alikuwa ndio ana handle docs zote za siri za Europe nk.
Baada ya miaka minne, alipewa post ingine, safari hii alipelekwa London kwy ubalozi wa russia. Hapa ndio alifanya maangamizi makubwa kwa russia. According to Charles Powell, ambaye alikuwa mshauri wa usalama na katibu wa waziri mkuu Magret, anasema there was nothing more secret in uk than the existence of Oleg and who he was. Mawaziri wala nani, hamna aliemjua than Mi6.
Alipilirudishwa russia, Kwan upande Mi6, wao hawakufanye any attempt ya kuwasiliana naye, ila walimpaga Oleg namb maalum ya simu ya ku initiate mazungumzo wakati wowote wanapo potezana. Pia walipeana signal ya kushika plastic bag, sehm moja maalum nchini russia wakt wowote ikitokea anahisi anafuatiliwa na anahitaji atoroke. Na ili kujibu hii signal, ofisa wa Mi6 atattokea kutoka kwny crowd na kula brand fulani ya chocolate, kama majibu kuwa ameeleweka.
Katika mission zake zote hizo abroad hakuwa na mkewe, na hata siku anatoroka pia alimficha mkewe. Speeches as Reagan kuhusu nuclear, na ile pressure iliokuwa kubwa kuwa mda wowote vita utaanza, ilfanya russia ihisi kuna mtu ndani yao anatoa siri. Kumbuka kuwa CiA walaikuwa wakipewa " drip fed information on need to know basis kutoka kwa Mi6, swala ambalo liliwaudhi.
Kwahiyo CiA wakampa kazi mkuu wao wa CiA counter russia, ya kufuatilia source ya info wanazopata mi6. Ambacho CiA hawakakujua ni kuwa huyo afisa wao, Naye ni agent wa KGB. Huyu afsa ambaye baade CiA walimshtukia, alipopewa kazi hiyo na ili kutoonekana alikuwa compromised, alivujisha document Kibao ikiwepo hisia zake kwa newly appointed boss katika embassy ya Russia jijini London ambaye ni Oleg.
KGB walipoliona Jina lake kutoka kwa source yao, wakamwita arudi nyumbani haraka on pretext ya kulewa promotion. Oleg McHale zilimcheza, ila alijua kukaidi direct order kurudi russia itaonyesha wazi kuwa yupo guilty na angeshughulikiwa. Alirudi russia bila kuwaaga mi6. Alipofika haraka sana walimpeleka kwny jumba lao, wakatilia sumu ya kumlewesha, wakatocha lakn uzuri wa Oleg hakutoa siri ya uhusika wake na Mi6. Wakaamua kuchenj tactics kwa kumpa house arrest, na hapa ndipo baadae aliroroshwa, nadhani kwa operation ilioitwa piplico ..
Nafikiri siyo vema mimi na wewe kuwasemea moja kwa moja waliopo uwanja wa vita.Mkuu hongera kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri! Lkn Point yangu sio kutokuguswa hata kdg bali ni kuguswa wapi kwa silaha gani na kwa kulengwa nani!? Hebu nisaidie kufikiria na hili na unisaidie uwelewa ndugu yako.
Drones zimepiga makazi ya raisi na zimelenga kumpiga na kumuua raisi! Kwa taifa kubwa Kama Russia tunajua linaweza kuguswa Kama unavyosema na nakubaliana na wewe kwenye hilo Lkn kuguswa direct kwenye makazi ya rais huoni Kama kuna udhaifu ama dharau fulani kwa taifa kubwa Kama hilo ambalo tunajua lina ulinzi mkubwa wa anga tena kuguswa/kushambuliwa na taifa dogo ambalo linaomba msaada wa silaha!? Taifa ambalo dogo sana kwa Russia, kiuchumi, kijeshi nk.
Tena linashambuliwa na drones wala sio mijidege mikubwa yakivita yakutisha ambayo hata majina yake kuyataja mtihani. Lkn drones hata Millard Ayo anazo anapigia picha [emoji2]..
Afadhali angeshambuliwa huko kwenye uwanja wa vita Lkn watu wameshambulia kwenye makazi ya rais! Ndugu huoni ni dharau hiyo!?
kutuma junior kumfuatilia senior nalo kosa lingine la kiufundiKumuhufadhi ni ngumu kutokana na cheo alichokuwa nacho.. Kwa cheo hicho lazima wawe na ushahidi wakutosha kumdhibiti Kumbuka hadi muda huo walikuwa wanamhisi tu na yeye anajua wanamhisi tu so anajihami sana.
Na inavyoonekana hao wanaomfuatilia hawana uwezo kamshinda yeye, anajua kuwakataa zaidi wajuavyo [emoji23]
unaelewa Nini ukiambiwa mtu anacheo Cha kanali hata jeshini hili kundi uliogope ,huwezi ukawa unajifanyia TU mambo lazima ujiridhishe ,maafsa Hawa wakikugeuka !KGB wanafanya mistakes sana kwa Oleg,huyu wangemuhifadhi chimbo
Kabisa kabisa....huenda walimuachia uhuru ili waweze kukusanya vizuri ushahidi wa kumtia hatianiKGB wanafanya mistakes sana kwa Oleg,huyu wangemuhifadhi chimbo
Du hujui badoHapa bongo kwa upande wa jeshi la ulinzi vyuo vyao vya mafunzo baadhi vinafahamika mfano chuo cha ulinzi na usalama pale Kunduchi..pia chuo cha maafisa pale Monduli na makambi ya mafunzo ya kijeshi kama pale Bagamoyo na kadhalika.
Jeshi la polisi pia baadhi vinafamika mfano CCP moshi pale..pia nishakutana na chaka la polisi lililojificha kule milimani Kidatu kwenye uzalishaji wa Umeme watu wanakula trainning huko n.k n.k
SWALI:
Vipi kuhusu vyuo vya usala wa taifa yaan tiss hata bongo hawa watu wanakula trainings wapi?? Au wao ni kwenda nje tuu???
Cha ajabu nini hapo mkuu!?Du hujui bado
Oho14
Ni rasmi Sasa Oleg angekuwa mshirika wa karibu wa M16, kwa kuwafanyia kazi kwa kuwavujishia Siri . Lakini alimwambia bwana Hawkins atawafanyia kazi kwa masharti kadhaa.
La kwanza ni kwamba hakutaka majasusi atakaowataja waingie matatizoni, pili hakutaka kupigwa picha au kurekodiwa kwa Siri kwa namna yoyote ile na la mwisho hakuhitaji pesa yoyote au malipo ya namna yoyote ile.hizo ndizo condition zilizowekwa na bwana Oleg. Hizi standards alizoambiwa bwana Hawkins zilimpa wakati mgumu kidogo . Kwa mfano Hawkins alijiuliza kwanini huyu bwana anawalinda wenzake ,pili inakuwaje jasusi kama yeye anakataa malipo ya pesa . Maana pesa kwenye ulimwengu wa ujasusi ni kichocheo kizuri na motisha kwa jasusi na vilevile inampa thamani. Na swala la au kipengele Cha kutokupigwa picha hakikuwa kizito maana wangeweza kumpiga picha pasipo yeye kujua.
Kiuhalisia Oleg Gordievsky kutotaka majasusi wa nchi yake wasiingie matatizoni ni kwamba alikuwa anajilinda yeye mwenyewe , kwa maana kwa mfano ingetokea amewachomesha hao spies wa KGB kwa M16 au PET na kukamatwa au kufukuzwa kutoka Denmark ,ingeleta mtafaruku miongoni mwa KGB wakiamini huenda Kuna msaliti miongoni mwao kwa wao na ni kwamba lazima Oleg angehisiwa maana hao majasusi ikiwa wangekamatwa lazima wangehojiwa na kutaja washirika wenzao. Pili kukataa pesa kwa bwana Oleg , kwamba asilipwe ni kwamba hakutaka kuwa na pesa nyingi halafu aitumie extravagantly kiasi kwamba ikazusha suspicion kwa maboss wake mwisho wa siku ashtukiwe.
Ni kwamba bwana Hawkins haya masharti yote yaliyotolewa na Oleg aliyatuma kwa M16 huko London kupitiwa upya na Sasa rasmi ikawa kwamba bwana Oleg na Hawkins walitakiwa kukutana mara Moja au mbili kwa mwezi kwenye safe house iliyoandaliwa hapo jijini Copenhagen.
Kikao Cha kwanza Cha Hawa majasusi wawili kilianza na Oleg alianza kutema Siri kuhusiana na organizational structure ya KGB. Kila department na kiongozi wake ,namna ya kulipwa , promotion,mafunzo,n.k . Haya yote bwana Hawkins alikuwa Anayaandika kupitia wino maalumu wa Siri pamoja na kurekodi kila alilolizungumza bwana Oleg Kwa Siri pasipo yeye kujua. Ajabu ni kwamba licha ya Siri alizokuwa anatoa bwana Oleg , hakuwahi kumuuliza lolote Hawkins kuhusu M16. Hizi taarifa zilivyofika huko makao makuu uingereza ,ziliwavutia sana wakubwa wa kitengo kutokana na unyeti wa taarifa hizo kuhusu their rival KGB. Kumbuka Bwana Oleg alikuwa ni deputy ambassador,hivyo alikuwa na access ya taarifa nyeti na za Siri za KGB.
Oleg aliweza kutoa details za kutosha kuhusiana na idara aliyowahi kuifanyia kazi miaka kadhaa nyuma ya FCD , namna ya kupandikiza majasusi illegals sehemu mbalimbali duniani, operation za Siri kwenye nchi tofauti na malipo yanavyofanyika na kila methodologies zilizokuwa zinatumika.
Baada ya kukusanya taarifa zote hizi bwana Hawkins alizitafsiri kutoka kijerumani to kingereza Kisha kuzichakata na kuzihifadhi kwenye kaseti na kuzituma uingereza kwa kutumia diplomatic bag.
Diplomatic bag ni begi ambalo hutumika na maafisa wa ubalozini ambalo ukiwa nalo airport haliwezi kukaguliwa kilichopo ndani .
Hivi ndivyo taarifa hizo za Siri zilikuwa zinatumwa uingereza pasipo kugundulika.
Ni kwamba hata mkewe Yelena hakujua bwana ake Nini kinaendelea kwenye maisha yake. Na hili swala Oleg alimficha maana laiti mkewe angejua lazima angemrepoti mumewe na mwisho wa siku yawe mengine .wanasema kwamba " A spy has to deceive even his nearest and dearest" . Ndicho alichokifanya bwana Oleg..
Siku kadha Wa kadha katika harakati zake za kazi alikutana na mwanadada mrembo aliyeitwa Leila aliyeva , mpiga chapa wa shirika la WHO mjini Copenhagen ,mwenye asili ya nusu mrusi ,nusu mu Azerbaijan . walikutana hapo ubalozini kwenye hafla fupi ilifanyika na hapo ndipo walipo fahamiana. Kwa kifupi mwamba alimwelewa mrembo huyu mwenye miaka 28 wakipishana miaka 11 na Oleg. Huyu bibiye hakujua Oleg ni jasusi wa KGB. Kwa kuwa mkewe Yelena muda mwingi alikuwa home ,alijiachia kwa Siri na Leila pasipo kushtukiwa ,kwa maana angejulikana na wenzake anamhusiano na huyu mrembo mpya ingekuwa ni disaster.
Oleg alikuwa na mahusiano ya aina mbili . Yeye na Leila ,na pia yeye na M16. A coincidence.
Kwenye tukio Moja ,ni kwamba kijana mmoja ambaye ni jasusi wa PET katika pitapita zake mitaani kipindi Cha winter akiwa anaenda home mitaa ya ballerup ,aliona gari lenye namba za ubalozini (diplomatic number plates) limepaki pembezoni kidogo mwa mtaa. Akalisogelea kwa Siri na kugundua ni gari la ubalozi wa Soviet embassy. Akashangaa imekuwaje gari la ofisi za ubalozi wa urusi linafanya Nini usiku wa saa Moja Tena weekend. Akasogea Hadi karibu nalo na kuona hatua za viatu fresh vikielekea kwenye apartment Moja jirani na hapo umbali wa yadi 200 hivi. Akafuata nyayo zilizokuwa zinaelekea upper stair ya jengo hilo Hadi second floor. Kwenye Mlango jirani alisikia sauti baina ya watu wawili au zaidi wakiongea asitambue ni lugha gani ,ila ilikuja kujulikana ni kijerumani.alichukua note akaandika address ya hiyo nyumba pamoja na zile plate namba. Na baada ya wiki file likatua mezani kwa mkurugenzi wa PET bwana Jørn bruun. Ikasemekana kwamba Kuna afisa wa kisoviet ambaye ni suspect KGB officer alikutwa anazungumza kwa Siri kwenye apartment Moja hivi kijerumani na wenzake mazungumzo yasiyoeleweka. Report ikahitimisha kwamba Kuna suspicion hivyo ifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo. Lakini bwana jørn bruun D.G. Mwenyewe akaamua kuizima hii report kimya kimya na Tena juu kwa juu. Huyu bwana bruun ,ni kwamba alikuwa anajua kinachoendelea kwa kuwa M16 Walimpa taarifa what's going on. Bwana Oleg alikuja kushtuka baadaye kusikia hizi taarifa baada ya kugundua ilibaki kidogo anaswe.
Siku baada ya siku bwana Oleg alianza kuwa point baadhi ya majasusi walioko hapo Denmark pamoja na viongozi wa serikalini walio na ushirikiano na urusi, ambao wapo kwenye payroll ya KGB .
Kwa mfano alimtaja bwana Gert Petersen askari police na pia ni afisa wa uhamiaji mwenye tamaa na mlafi wa pesa. Huyu alikuwa anawasaidia KGB kupitisha illegal ndani ya Denmark na nchi za Scandinavia ikiwemo Sweden.
Naona mambo ni moto huku. myoyambendi @ulimkafu @bianca2334
Maafisa wa operesheni hii kwa upande wa uingereza walijipanga vilivyo chini ya mwanamama Oliver price. Na walihitaji usaidizi kutoka kwa wenzao wa PET. Kwa sababu Japo Oleg ikiwa atafikishwa Hadi Finland Salama ,bado kutakuwa na kipengele kwa mamlaka za serikali ya Finland ,maana Japo hii ilikuwa ni nchi huru na haipo kwenye muungano wa Soviet, bado Russia walikuwa na nguvu ya usemi kwa serikali hiyo. Kutokana na hili M16 walipiga mahesabu,endapo Oleg atajulikana alipitia Finland , serikali ya nchi hiyo ingepata shinikizo kubwa kutoka kwa Russia,kwa Nini imeruhusu msaliti kupita au kumficha. Hivyo ikapendekezwa Veronica na afisa mwingine watamsafirisha mtoro wao Hadi kaskazini kabisa mwa Finland huku wakisindikizwa na gari la maafisa wa shirika la kijasusi la pET la Denmark Hadi kwenye mji wa tromsø ulioko Norway . Kisha wakiwa huko waombe ndege ya kijeshi kuja kuwafuata. Lakini ikaonekana Bora utumiwe usafiri wa ndege za kawaida za abiria Ili kupunguza kushtukiwa na mamlaka za Russia au Finland.
Kwa upande wa maafisa walioko Moscow wa M16 ilihitajika itungwe ya sababu inayowafanya kusafiri umbali mrefu Hadi Finland Helsinki ,ambapo hata KGB wakiisikia wataamini.
Stori ilikuwa kama ifuatavyo: Mke wa afisa wa M16 Arthur gee aitwaye Rachel ,ajifanye anaumwa homa Kali ya mgongo hivyo wangepaswa kusafiri Hadi Helsinki Kwa gari na mumewe Arthur. Na afisa mwingine Ascot pamoja na mkewe Carolina wangekuwa sehemu ya safari hii wakiwa na gari Yao kwa ajili ya kuwapa kampani maafisa wenzao wanaoenda kumwona daktari huko Helsinki Finland. Na pia Ascot na mkewe wangepaswa kusafiri na mwanao mchanga wa kama miezi 15 aliyeitwa Florence. Sababu hizi waliona kabisa ingewashawishi KGB na wasingehisiwa kwamba wanampango wa kumtorosha mtu ,Japo walitegemea lazima watakuwa wanafuatiliwa na maafisa KGB hususan kwa gari zinazofanya road patrol......
Tukirudi huko London ni kwamba maafisa wa M16 walitaka kufikisha ujumbe kwa Margaret thatcher kwamba Sasa operation PIMLICO ya kumtorosha mr Collins au Oleg , ipo under way hivyo alipaswa kujulishwa . Lakini muda huu thatcher alikuwa kwenye kasri ya balmoral aliyokuwa anaishi queen Elizabeth . Na huu ulikuwa ni utaratibu uliokuwepo ,kwamba P.M. wa uingereza lazima akakae kwa malkia kwa kipindi Cha siku au wiki kadhaa. Hivyo mshauri wa thatcher alipaswa kuupeleka ujumbe huu Hadi huko alikokuwa . Kipengele kikawa kasri ya malkia haiingiliwi hovyo hovyo na ujumbe huu ulihitaji approval kutoka kwa P.M binafsi Tena kwa maneno sio kwa simu kutokana na unyeti wake .
Hivyo Powell akafika Hadi kwenye kasri Hilo la balmoral ambalo lilikuwa ni makazi ya familia ya kifalme kipindi Cha kiangazi tokea 1852. Baada ya kufuata taratibu zote za kiprotokali kuingia jumba Hilo kuonana na thatcher ,alishtuka baada ya kuambiwa ujumbe anaotaka kumpa P.M lazima private secretary wa malkia Sir Philip Moore anapaswa kujua na Haina shida akijua. Lakini huyu powell alikaza Baada ya misuguano kadhaa ya ukiukwaji wa protocol ,sir Philip alimruhusu huyu Powell kuonana na Thatcher. Na hatimaye Thatcher akatoa Go ahead ya operation hii kutokana na Bwana Oleg kuifanyia makubwa uingereza hivyo akatoa blessings zote. Lakini Margaret thatcher asichokuwa anakifahamu muda huo ni kwamba alikuwa anatoa approval kwa operesheni ambayo tayari ishakwisha Anza kitambo[emoji28][emoji28].
Hivyo ujumbe wa hii Approval ukafika Moscow kwa kikosi kazi Cha M16.
Kipengele Cha mwisho kilichobaki walihitaji tu ruhusa rasmi kutoka mamlaka za juu za Russia Ili wapewe special diplomatic number plate za magari Yao na pia leseni za madereva ziwe updated. Kutokana na mlolongo mrefu wa mamlaka za huko hatimaye leseni zao na special diplomatic number plate walipewa Baada ya kufanyiwa ukaguzi karibia wiki na siku kadhaa.Na ni lazima wangepaswa kupewa escort na magari kadhaa ya KGB kutokana na hadhi Yao[emoji848].
Kwa upande wa Oleg nyumbani kwake kwenye kitongoji Cha Leninsky prospekt ,siku hiyo alikuwa anapiga usafi wa kufa mtu ndani kwake. Akafua nguo zake na kuzianika,akasafisha masinki na kuchoma baadhi ya vitu kadhaa na vingine akapanga na nyumba ikawa in shape. Na baada ya hapo aliamua kuacha kama rubble 220 kwa ajili ya kukidhi mahitaji kwa siku kadhaa hapo home kwa mkewe akirudi. Aliwaza sana endapo pesa hizo zitamfikia au zitatiwa mfukoni na maafisa wa KGB endapo wakija kumsaka na kumtafuta baada ya kuja kushtuka haonekani. Haya yote aliyafanya pasipo kuamsha suspicion kwa KGB endapo walikuwa wanamuangalia kupitia kamera za Siri ambazo labda walizipandikiza hapo home. Alitaka kuacha nyumba hiyo ikiwa safi na hakutaka kuacha ujumbe wowote wa maandishi wa Nini sababu zilizompelekea kufanya usaliti huu mkubwa kwa nchi yake ya Russia. Sababu zake alikuwa Nazo moyoni mwake . Baada ya kukamilisha kila kitu akapanga nguo zake kadhaa zilizoenea kwenye mfuko mdogo wa plastiki. Aliweka jaketi jepesi na Kofia ya ngozi ya rangi ya grey pamoja na roadmap ya nchi ya Finland. Sasa ilibidi kutoka majira ya jioni Hadi kituo Cha treni huku akiwakwepa majasusi wa KGB kwa njia ya kijasusi Kali sana aliyofundishwa Miaka takribani 18 nyuma.
Ni kwamba siku hii aliamua kuvalia Sweta ya kijani na siruali ya kijani mpauko pamoja na viatu vya brown vya zamani alivyovichomoa nyuma kabisa ya kabati akiamini havitakuwa na vumbi la radiation kuepusha kufuatiliwa. Hizi nguo alizochagua kuzivaa zilifanana kama rangi ya trakisuti hivyo wanaomfuatilia wangeamini mwamba anaenda mazoezi ya jioni ya jogging.
Na kweli alitoka na kubana mlango vizuri ,Kisha akaanza jogging mdogomdogo kuelekea uelekeo wa barabara iliyokuwa inaenda Hadi kituo kikuu Cha treni. Nyuma yake kulikuwa na mtu anafanya jogging bonge hivi ,Oleg akajua tu huyu ni walewale wa timu inayomfuatilia . Baada ya kufika umbali mrefu kiasi ambapo sio rahisi yule bwana kumfikia kutokana na unene wake akaongeza Kasi Kisha alachepukia kwenye miti miti na kuanza kuitafuta njia inayoenda kituo Cha treni. Hapa alitumia njia zote za kijasusi za kukwepa kufuatiliwa na kweli akafika . Alipanda treni inayoenda Leningrad na saa kumi na Moja kamili jioni treni ikaanza safari . Oleg baada ya ku scan watu wote humo ndani kijasusi na akaona hamna anayemhisi ni njagu aliamua kunywa vidonge kadhaa vya usingizi na akalala kwenye siti hiyo Pana ya treni.
.......
Kwa upande wa Finland maafisa wa M16 Oliver na Simon brown walifika kwenye hotel Moja jijini Helsinki na kukutana na afisa mwingine aliyekwisha tangulia kufanya survey ya sehemu ya Kukutana na pia kukodisha magari kwa ajili ya operation hii ya PIMLICO . Magari yaliyokodishwa gari ndogo ambazo ni Brand New Volvo. Pia waliweza kukutana na na maafisa wa PET ambao ni Eriksen na Larsen . Hivyo ilipangwa sehemu ya Kukutana kwa upande wa ndani ya mpaka wa Finland ilipaswa kuwa sehemu ya msituni sehemu ambayo gari za magogo huingia na kuchukua magogo na kugeuza na kuingia main road ila iwe ni karibu na mpaka kati ya nchi hizo mbili....
Huku kwenye makazi ya katuvosky prospekt Moscow wanakoishi maafisa wa M16 nako maandalizi yalikuwa yakiendelea vyema . Rachel gee na Caroline Ascot wake wa maafisa wa M16, Arthur na Ascot walikuwa wanapack vitu kwa ajili ya safari. Buti zilipaswa kuwa wazi kwa ajili ya Oleg kufichwa huko na familia yake (wao walidhani Oleg angeweza kutoroka na familia mzima)
Baada ya taratibu zote kukamilika ya Hadi ubalozini .safari ikaanza rasmi saa Tano usiku . (Oleg yeye alianza safari kwa treni kuanzia saa kumi na Moja jioni ya siku hiyo.)
Arthur gee na mkewe rachel wakiwa kwenye gari Yao ndogo aina ya ford ,huku Ascot na mkewe na mwanao mdogo wakiwa kwenye gari ndogo aina ya Saab Walianza safari ndefu ya kwenda Helsinki Finland. Kutokana na maafisa Hawa kuhisi huenda gari walizokuwa wanaendesha huenda zimepandikizwa vinasa sauti ,hawakuwa wanapiga stori zozote zinazohusiana na operation hii . Zaidi Rachel mke wa Arthur ile ya kuzuga alikuwa ana complain maumivu ya mgongo ili kuzidi kuwachanganya KGB endapo kama walikuwa wanawasikiliza muda huo.........
Nae Oleg akiwa kwenye safari ya treni ,usiku majira ya kama saa Tisa na nusu alikurupuka usingizini ni baada ya kushtuliwa na mtu aliyekuwa amekaa nae kumwambia alidondoka kwenye siti wakati ameuchapa usingizi. Alijinyanyua na kujiweka sawa huku watu wengine kwenye siti za mbele wakipiga stori za hapa na pale . Safari iliendelea ikiwa limebaki kama zaidi ya lisaa kufika Leningrad. Na kweli ilipotimia saa kumi na Moja kamili asubuhi treni hiyo ilifika kituo kikuu Cha treni Cha Leningrad. Baada ya hapo bwana Oleg alishuka na akadandia taxi zinazoenda kituo kingine Cha treni zinazoenda Helsinki Finland . Kituo hiki kiliitwa Finland station.Wanahistoria wanasema kituo hiki ndicho alichofikia bwana Lenin akitokea uswisi katika harakati za mapinduzi ya 1917 dhidi ya Bolsheviks. Na Ilipofika saa Moja asubuhi Oleg alipanda Tena treni inayoenda Finland kupitia mji mwingine wa Zelenogorsk. ilipotimia saa mbili asubuhi Oleg alishuka kwenye treni kwenye baada ya kufika Mji huo wa Zelenogorsk ambao zamani ulikuwa ni mji wa Finland ulioitwa Terijoki. Muda huo ndio kwanza mji unaanza kuchangamka .Oleg aliwaza mpaka muda huo kulikuwa hakuna uwezekano wa kuwa anafuatiliwa lakini aliamini mpaka muda huo KGB Moscow watakuwa alerted kwamba haonekani na kapotea kwenye radar zao na kutuma alarm kwenye vituo vyote vya mpakani... Alikuwa sahihi.
Oleg alipanda basi linaloenda hadi mji wa Vyborg lakini baada ya mwendo kiasi kabla ya basi Hilo kufika mjini alishuka njiani akizuga anajisikia kichefuchefu kutaka kutapika . Na kweli dereva alisimamisha na Oleg akashuka akimsihi aendelee tu na safari. Kutokana na eneo Hilo kuwa ni porini kiasi lenye nyasi wa kutosha hapo ndio palipaswa kuwa ndilo eneo la rendezvous point ila kulikuwa na mbu sana . Aliamua kuchukua maamuzi ya kutembea Hadi mji wa Vyborg kwa mguu kupiga gambe. [emoji848].Kumbuka muda huu nao maafisa wa M16 Walikuwa wanakaribia eneo hili wakiwa njiani na gari.
Oleg muda huo akiwa ajiamini na woga alianza safari kwa mguu Hadi mji wa mbele wa Vyborg. Na ikitokea ameona gari ya patrol za polisi aliwaza kujificha. Lakini badala yake alianza jogging Ili hata akionekana wamhisi anafanya mazoezi kutokana na aina ya mavazi aliyokuwa amevaa.
Na baada ya muda likatokea gari aina ya Lada likasimama. Ndani ya gari alikwepo kijana mdogo akiliendesha ,Oleg akaingia akimtathmini huyo dogo kama ni mjeshi au afisa kipenyo lakin akakuta sio .
Alipofika mji wa Vyborg akatoa kama rouble tatu kama nauli akampa dogo huyo ,akasepa. Oleg aliingia kwenye mkahawa mmoja akaagiza beer ya kopo na kuku fried.
Baada ya kupiga bia kadhaa akajihisi mwepesi ,huku mhudumu wa hapo akimkata jicho Oleg kiaina. Oleg akaanza kuhisi harufu ya hatari lakini akaendelea kutulia. Akaendelea kupiga vyombo mpaka ilipofika saa Saba mchana ,na hapo alipata hamaki. Ni baada ya jamaa wawili wakiwa wametinga suti zao kuingia . Oleg alihisi Hali ya hatari ,hapo akazuga Ili amalizie bia na nyingine akaichimbia mfukoni. Alilipa bili na kutoka nje. Alipofika umbali kiasi akageuka nyuma Ili kuona kama wale jamaa wanamuangalia lakini haikuwa hivyo. Sasa Oleg akaanza kukimbia kurudi maeneo ya pale aliposhuka mara ya kwanza na basi.
Akiwa anakimbia pembezoni mwa barabara likatokea Lori la kijeshi akalipiga mkono na kupanda ,akimwomba dereva amsogeze Hadi kibao kilichopo kwa mbele kilichoandikwa post 836 . Dereva ambaye huenda pengine mbali na kuwa mjeda angekuwa pia ni afisa wa KGB . Alimuuliza Oleg Kuna nini huko ukilinganisha ni eneo la pori, Oleg akamjibu Kuna mrembo anamsubiria kwenye dacha Moja ipo ndanindani msituni .(dacha ni nyumba Fulani Huwa zinajengwa msituni za mbao huko Russia kwa ajili ya mapumziko katika majira Fulani ya mwaka). Derevt akatoa tabasamu hivi akiamini jamaa labda anaenda kufanya mambo yake
Na kweli baada ya mwendo kiasi Oleg alimkabidhi dereva huyo rouble tatu akashuka . Baada ya gari Hilo kusepa Oleg aliingia kwenye msitu ulio pembezoni mwa barabara ambapo alidhanj kutokana na plan ya operation hii angetarajia kuona magari ya M16 Kumchukua... Alilala flat chini kwenye majani Ili asionekane na gari zilizokuwa zinapita eneo Hilo . Ni eneo lenye vumbi na mbu wengi sana . Alialala chini akisubir kusikia Gari likisimama maeneo hayo ambayo aliamini huenda litakuwa na maafisa wa M16................&&&&&&&&&&.........&&&&&&&&&&&........................…..........
Nao huku road maafisa wa M16 wakiwa kwenye highway inayotoka Leningrad kuelekea Vyborg bado walikuwa under surveillance ya magari ya KGB. Maafisa Hawa walikuwa na wasiwasi endapo bado watakuwa wanafuatiliwa Hadi eneo ambalo walitegemea kumkuta Oleg amejificha kabla ya kufika mji wa Vyborg.kipengele kikawa ni namna gani watazuga Ili hizo gari za patrol ziwapite. Lakini walikuwa wapo kwenye bracket . Convoy ya gari hizi zilikuwa zinafuatiliwa kwa nyuma na gari mbili za police wa doria ,huku mbele kukiwa na Lori kubwa wao wakiwa wamewekwa kati. Sasa wakaona Hali ikiwa hivi operation itakuwa terminated rasmi na Oleg ataachwa hapo walipokubaliana kumkuta. Kutokana na kufuatiliwa muda mrefu Sasa wakaona wafanye ku overtake gari la mbele Kisha walipolipita wakaongeza speed kiasi .Kwa mbali Sasa wakawa wanayaacha hivyo maafisa Hawa wakachepuka kwenye barabara ya vumbi na kuingia msituni sehemu ambapo barabara hiyo ya vumbi ilitengeneza u -shape . Na walipofika hapo vumbi likiwa limetulia wakashuka . Maafisa Hawa walishuka baada ya kuona kila sehemu kupo clear na hakuna mgurumo wa gari linalokuja eneo Hilo. wakashusha mikeka Ili kutandika kwa ajili ya picnic eneo Hilo. Lakini kama mzimu Oleg alijitokeza kwenye kichaka akiwa amechafuka vumbi ,nywele zimetimka ,huku nguo Zina matope na majani majani. Maafisa Hawa hawakuamini kumuona Oleg amesimama mbele Yao walihisi kama ni wale watu wa kwenye hadithi za fairy tales. Walitegemea kumkuta yeye na familia yake hapo lakini alisimama peke yake kama mshumaa wa pasaka mbele Yao. Naye Oleg alitarajia atakutana na maafisa wawili wa M16 kwa mujibu wa plan ya PIMLICO lakini walikuwa wanne.[emoji28][emoji28].
Oleg baada ya kuwacheki wote wanne aliuliza kwa kingereza apande gari ipi kati ya hizo mbili?
Ni rasmi Sasa Oleg alikuwa amekwepa surveillance ya KGB mpaka hapo .Sasa walitarajia kuanza safari ya kwenda Finland kupitia mpakani ...............
Huyu buyobe Kila nyuzi NZuri humu JF Huwa zake mkuu.BUYOBE WA TWITTER KASHAIBA UZI.
AMEKUOMBA?
Wangemumaliza tu kuchelewesha chelewesha akawaachia manyoya sasaKabisa kabisa....huenda walimuachia uhuru ili waweze kukusanya vizuri ushahidi wa kumtia hatiani