myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 166,767
- 705,461
Nimefika jirani...Naona mambo ni moto huku. myoyambendi @ulimkafu @bianca23
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimefika jirani...Naona mambo ni moto huku. myoyambendi @ulimkafu @bianca23
Hatari34
Maafisa wa operesheni hii kwa upande wa uingereza walijipanga vilivyo chini ya mwanamama Oliver price. Na walihitaji usaidizi kutoka kwa wenzao wa PET. Kwa sababu Japo Oleg ikiwa atafikishwa Hadi Finland Salama ,bado kutakuwa na kipengele kwa mamlaka za serikali ya Finland ,maana Japo hii ilikuwa ni nchi huru na haipo kwenye muungano wa Soviet, bado Russia walikuwa na nguvu ya usemi kwa serikali hiyo. Kutokana na hili M16 walipiga mahesabu,endapo Oleg atajulikana alipitia Finland , serikali ya nchi hiyo ingepata shinikizo kubwa kutoka kwa Russia,kwa Nini imeruhusu msaliti kupita au kumficha. Hivyo ikapendekezwa Veronica na afisa mwingine watamsafirisha mtoro wao Hadi kaskazini kabisa mwa Finland huku wakisindikizwa na gari la maafisa wa shirika la kijasusi la pET la Denmark Hadi kwenye mji wa tromsø ulioko Norway . Kisha wakiwa huko waombe ndege ya kijeshi kuja kuwafuata. Lakini ikaonekana Bora utumiwe usafiri wa ndege za kawaida za abiria Ili kupunguza kushtukiwa na mamlaka za Russia au Finland.
Kwa upande wa maafisa walioko Moscow wa M16 ilihitajika itungwe ya sababu inayowafanya kusafiri umbali mrefu Hadi Finland Helsinki ,ambapo hata KGB wakiisikia wataamini.
Stori ilikuwa kama ifuatavyo: Mke wa afisa wa M16 Arthur gee aitwaye Rachel ,ajifanye anaumwa homa Kali ya mgongo hivyo wangepaswa kusafiri Hadi Helsinki Kwa gari na mumewe Arthur. Na afisa mwingine Ascot pamoja na mkewe Carolina wangekuwa sehemu ya safari hii wakiwa na gari Yao kwa ajili ya kuwapa kampani maafisa wenzao wanaoenda kumwona daktari huko Helsinki Finland. Na pia Ascot na mkewe wangepaswa kusafiri na mwanao mchanga wa kama miezi 15 aliyeitwa Florence. Sababu hizi waliona kabisa ingewashawishi KGB na wasingehisiwa kwamba wanampango wa kumtorosha mtu ,Japo walitegemea lazima watakuwa wanafuatiliwa na maafisa KGB hususan kwa gari zinazofanya road patrol......
Tukirudi huko London ni kwamba maafisa wa M16 walitaka kufikisha ujumbe kwa Margaret thatcher kwamba Sasa operation PIMLICO ya kumtorosha mr Collins au Oleg , ipo under way hivyo alipaswa kujulishwa . Lakini muda huu thatcher alikuwa kwenye kasri ya balmoral aliyokuwa anaishi queen Elizabeth . Na huu ulikuwa ni utaratibu uliokuwepo ,kwamba P.M. wa uingereza lazima akakae kwa malkia kwa kipindi Cha siku au wiki kadhaa. Hivyo mshauri wa thatcher alipaswa kuupeleka ujumbe huu Hadi huko alikokuwa . Kipengele kikawa kasri ya malkia haiingiliwi hovyo hovyo na ujumbe huu ulihitaji approval kutoka kwa P.M binafsi Tena kwa maneno sio kwa simu kutokana na unyeti wake .
Hivyo Powell akafika Hadi kwenye kasri Hilo la balmoral ambalo lilikuwa ni makazi ya familia ya kifalme kipindi Cha kiangazi tokea 1852. Baada ya kufuata taratibu zote za kiprotokali kuingia jumba Hilo kuonana na thatcher ,alishtuka baada ya kuambiwa ujumbe anaotaka kumpa P.M lazima private secretary wa malkia Sir Philip Moore anapaswa kujua na Haina shida akijua. Lakini huyu powell alikaza Baada ya misuguano kadhaa ya ukiukwaji wa protocol ,sir Philip alimruhusu huyu Powell kuonana na Thatcher. Na hatimaye Thatcher akatoa Go ahead ya operation hii kutokana na Bwana Oleg kuifanyia makubwa uingereza hivyo akatoa blessings zote. Lakini Margaret thatcher asichokuwa anakifahamu muda huo ni kwamba alikuwa anatoa approval kwa operesheni ambayo tayari ishakwisha Anza kitambo[emoji28][emoji28].
Hivyo ujumbe wa hii Approval ukafika Moscow kwa kikosi kazi Cha M16.
Kipengele Cha mwisho kilichobaki walihitaji tu ruhusa rasmi kutoka mamlaka za juu za Russia Ili wapewe special diplomatic number plate za magari Yao na pia leseni za madereva ziwe updated. Kutokana na mlolongo mrefu wa mamlaka za huko hatimaye leseni zao na special diplomatic number plate walipewa Baada ya kufanyiwa ukaguzi karibia wiki na siku kadhaa.Na ni lazima wangepaswa kupewa escort na magari kadhaa ya KGB kutokana na hadhi Yao[emoji848].
Kwa upande wa Oleg nyumbani kwake kwenye kitongoji Cha Leninsky prospekt ,siku hiyo alikuwa anapiga usafi wa kufa mtu ndani kwake. Akafua nguo zake na kuzianika,akasafisha masinki na kuchoma baadhi ya vitu kadhaa na vingine akapanga na nyumba ikawa in shape. Na baada ya hapo aliamua kuacha kama rubble 220 kwa ajili ya kukidhi mahitaji kwa siku kadhaa hapo home kwa mkewe akirudi. Aliwaza sana endapo pesa hizo zitamfikia au zitatiwa mfukoni na maafisa wa KGB endapo wakija kumsaka na kumtafuta baada ya kuja kushtuka haonekani. Haya yote aliyafanya pasipo kuamsha suspicion kwa KGB endapo walikuwa wanamuangalia kupitia kamera za Siri ambazo labda walizipandikiza hapo home. Alitaka kuacha nyumba hiyo ikiwa safi na hakutaka kuacha ujumbe wowote wa maandishi wa Nini sababu zilizompelekea kufanya usaliti huu mkubwa kwa nchi yake ya Russia. Sababu zake alikuwa Nazo moyoni mwake . Baada ya kukamilisha kila kitu akapanga nguo zake kadhaa zilizoenea kwenye mfuko mdogo wa plastiki. Aliweka jaketi jepesi na Kofia ya ngozi ya rangi ya grey pamoja na roadmap ya nchi ya Finland. Sasa ilibidi kutoka majira ya jioni Hadi kituo Cha treni huku akiwakwepa majasusi wa KGB kwa njia ya kijasusi Kali sana aliyofundishwa Miaka takribani 18 nyuma.
Ni kwamba siku hii aliamua kuvalia Sweta ya kijani na siruali ya kijani mpauko pamoja na viatu vya brown vya zamani alivyovichomoa nyuma kabisa ya kabati akiamini havitakuwa na vumbi la radiation kuepusha kufuatiliwa. Hizi nguo alizochagua kuzivaa zilifanana kama rangi ya trakisuti hivyo wanaomfuatilia wangeamini mwamba anaenda mazoezi ya jioni ya jogging.
Na kweli alitoka na kubana mlango vizuri ,Kisha akaanza jogging mdogomdogo kuelekea uelekeo wa barabara iliyokuwa inaenda Hadi kituo kikuu Cha treni. Nyuma yake kulikuwa na mtu anafanya jogging bonge hivi ,Oleg akajua tu huyu ni walewale wa timu inayomfuatilia . Baada ya kufika umbali mrefu kiasi ambapo sio rahisi yule bwana kumfikia kutokana na unene wake akaongeza Kasi Kisha alachepukia kwenye miti miti na kuanza kuitafuta njia inayoenda kituo Cha treni. Hapa alitumia njia zote za kijasusi za kukwepa kufuatiliwa na kweli akafika . Alipanda treni inayoenda Leningrad na saa kumi na Moja kamili jioni treni ikaanza safari . Oleg baada ya ku scan watu wote humo ndani kijasusi na akaona hamna anayemhisi ni njagu aliamua kunywa vidonge kadhaa vya usingizi na akalala kwenye siti hiyo Pana ya treni.
.......
Kwa upande wa Finland maafisa wa M16 Oliver na Simon brown walifika kwenye hotel Moja jijini Helsinki na kukutana na afisa mwingine aliyekwisha tangulia kufanya survey ya sehemu ya Kukutana na pia kukodisha magari kwa ajili ya operation hii ya PIMLICO . Magari yaliyokodishwa gari ndogo ambazo ni Brand New Volvo. Pia waliweza kukutana na na maafisa wa PET ambao ni Eriksen na Larsen . Hivyo ilipangwa sehemu ya Kukutana kwa upande wa ndani ya mpaka wa Finland ilipaswa kuwa sehemu ya msituni sehemu ambayo gari za magogo huingia na kuchukua magogo na kugeuza na kuingia main road ila iwe ni karibu na mpaka kati ya nchi hizo mbili....
Huku kwenye makazi ya katuvosky prospekt Moscow wanakoishi maafisa wa M16 nako maandalizi yalikuwa yakiendelea vyema . Rachel gee na Caroline Ascot wake wa maafisa wa M16, Arthur na Ascot walikuwa wanapack vitu kwa ajili ya safari. Buti zilipaswa kuwa wazi kwa ajili ya Oleg kufichwa huko na familia yake (wao walidhani Oleg angeweza kutoroka na familia mzima)
Baada ya taratibu zote kukamilika ya Hadi ubalozini .safari ikaanza rasmi saa Tano usiku . (Oleg yeye alianza safari kwa treni kuanzia saa kumi na Moja jioni ya siku hiyo.)
Arthur gee na mkewe rachel wakiwa kwenye gari Yao ndogo aina ya ford ,huku Ascot na mkewe na mwanao mdogo wakiwa kwenye gari ndogo aina ya Saab Walianza safari ndefu ya kwenda Helsinki Finland. Kutokana na maafisa Hawa kuhisi huenda gari walizokuwa wanaendesha huenda zimepandikizwa vinasa sauti ,hawakuwa wanapiga stori zozote zinazohusiana na operation hii . Zaidi Rachel mke wa Arthur ile ya kuzuga alikuwa ana complain maumivu ya mgongo ili kuzidi kuwachanganya KGB endapo kama walikuwa wanawasikiliza muda huo.........
Nae Oleg akiwa kwenye safari ya treni ,usiku majira ya kama saa Tisa na nusu alikurupuka usingizini ni baada ya kushtuliwa na mtu aliyekuwa amekaa nae kumwambia alidondoka kwenye siti wakati ameuchapa usingizi. Alijinyanyua na kujiweka sawa huku watu wengine kwenye siti za mbele wakipiga stori za hapa na pale . Safari iliendelea ikiwa limebaki kama zaidi ya lisaa kufika Leningrad. Na kweli ilipotimia saa kumi na Moja kamili asubuhi treni hiyo ilifika kituo kikuu Cha treni Cha Leningrad. Baada ya hapo bwana Oleg alishuka na akadandia taxi zinazoenda kituo kingine Cha treni zinazoenda Helsinki Finland . Kituo hiki kiliitwa Finland station.Wanahistoria wanasema kituo hiki ndicho alichofikia bwana Lenin akitokea uswisi katika harakati za mapinduzi ya 1917 dhidi ya Bolsheviks. Na Ilipofika saa Moja asubuhi Oleg alipanda Tena treni inayoenda Finland kupitia mji mwingine wa Zelenogorsk. ilipotimia saa mbili asubuhi Oleg alishuka kwenye treni kwenye baada ya kufika Mji huo wa Zelenogorsk ambao zamani ulikuwa ni mji wa Finland ulioitwa Terijoki. Muda huo ndio kwanza mji unaanza kuchangamka .Oleg aliwaza mpaka muda huo kulikuwa hakuna uwezekano wa kuwa anafuatiliwa lakini aliamini mpaka muda huo KGB Moscow watakuwa alerted kwamba haonekani na kapotea kwenye radar zao na kutuma alarm kwenye vituo vyote vya mpakani... Alikuwa sahihi.
Oleg alipanda basi linaloenda hadi mji wa Vyborg lakini baada ya mwendo kiasi kabla ya basi Hilo kufika mjini alishuka njiani akizuga anajisikia kichefuchefu kutaka kutapika . Na kweli dereva alisimamisha na Oleg akashuka akimsihi aendelee tu na safari. Kutokana na eneo Hilo kuwa ni porini kiasi lenye nyasi wa kutosha hapo ndio palipaswa kuwa ndilo eneo la rendezvous point ila kulikuwa na mbu sana . Aliamua kuchukua maamuzi ya kutembea Hadi mji wa Vyborg kwa mguu kupiga gambe. [emoji848].Kumbuka muda huu nao maafisa wa M16 Walikuwa wanakaribia eneo hili wakiwa njiani na gari.
Oleg muda huo akiwa ajiamini na woga alianza safari kwa mguu Hadi mji wa mbele wa Vyborg. Na ikitokea ameona gari ya patrol za polisi aliwaza kujificha. Lakini badala yake alianza jogging Ili hata akionekana wamhisi anafanya mazoezi kutokana na aina ya mavazi aliyokuwa amevaa.
Na baada ya muda likatokea gari aina ya Lada likasimama. Ndani ya gari alikwepo kijana mdogo akiliendesha ,Oleg akaingia akimtathmini huyo dogo kama ni mjeshi au afisa kipenyo lakin akakuta sio .
Alipofika mji wa Vyborg akatoa kama rouble tatu kama nauli akampa dogo huyo ,akasepa. Oleg aliingia kwenye mkahawa mmoja akaagiza beer ya kopo na kuku fried.
Baada ya kupiga bia kadhaa akajihisi mwepesi ,huku mhudumu wa hapo akimkata jicho Oleg kiaina. Oleg akaanza kuhisi harufu ya hatari lakini akaendelea kutulia. Akaendelea kupiga vyombo mpaka ilipofika saa Saba mchana ,na hapo alipata hamaki. Ni baada ya jamaa wawili wakiwa wametinga suti zao kuingia . Oleg alihisi Hali ya hatari ,hapo akazuga Ili amalizie bia na nyingine akaichimbia mfukoni. Alilipa bili na kutoka nje. Alipofika umbali kiasi akageuka nyuma Ili kuona kama wale jamaa wanamuangalia lakini haikuwa hivyo. Sasa Oleg akaanza kukimbia kurudi maeneo ya pale aliposhuka mara ya kwanza na basi.
Akiwa anakimbia pembezoni mwa barabara likatokea Lori la kijeshi akalipiga mkono na kupanda ,akimwomba dereva amsogeze Hadi kibao kilichopo kwa mbele kilichoandikwa post 836 . Dereva ambaye huenda pengine mbali na kuwa mjeda angekuwa pia ni afisa wa KGB . Alimuuliza Oleg Kuna nini huko ukilinganisha ni eneo la pori, Oleg akamjibu Kuna mrembo anamsubiria kwenye dacha Moja ipo ndanindani msituni .(dacha ni nyumba Fulani Huwa zinajengwa msituni za mbao huko Russia kwa ajili ya mapumziko katika majira Fulani ya mwaka). Derevt akatoa tabasamu hivi akiamini jamaa labda anaenda kufanya mambo yake
Na kweli baada ya mwendo kiasi Oleg alimkabidhi dereva huyo rouble tatu akashuka . Baada ya gari Hilo kusepa Oleg aliingia kwenye msitu ulio pembezoni mwa barabara ambapo alidhanj kutokana na plan ya operation hii angetarajia kuona magari ya M16 Kumchukua... Alilala flat chini kwenye majani Ili asionekane na gari zilizokuwa zinapita eneo Hilo . Ni eneo lenye vumbi na mbu wengi sana . Alialala chini akisubir kusikia Gari likisimama maeneo hayo ambayo aliamini huenda litakuwa na maafisa wa M16................&&&&&&&&&&.........&&&&&&&&&&&........................…..........
Nao huku road maafisa wa M16 wakiwa kwenye highway inayotoka Leningrad kuelekea Vyborg bado walikuwa under surveillance ya magari ya KGB. Maafisa Hawa walikuwa na wasiwasi endapo bado watakuwa wanafuatiliwa Hadi eneo ambalo walitegemea kumkuta Oleg amejificha kabla ya kufika mji wa Vyborg.kipengele kikawa ni namna gani watazuga Ili hizo gari za patrol ziwapite. Lakini walikuwa wapo kwenye bracket . Convoy ya gari hizi zilikuwa zinafuatiliwa kwa nyuma na gari mbili za police wa doria ,huku mbele kukiwa na Lori kubwa wao wakiwa wamewekwa kati. Sasa wakaona Hali ikiwa hivi operation itakuwa terminated rasmi na Oleg ataachwa hapo walipokubaliana kumkuta. Kutokana na kufuatiliwa muda mrefu Sasa wakaona wafanye ku overtake gari la mbele Kisha walipolipita wakaongeza speed kiasi .Kwa mbali Sasa wakawa wanayaacha hivyo maafisa Hawa wakachepuka kwenye barabara ya vumbi na kuingia msituni sehemu ambapo barabara hiyo ya vumbi ilitengeneza u -shape . Na walipofika hapo vumbi likiwa limetulia wakashuka . Maafisa Hawa walishuka baada ya kuona kila sehemu kupo clear na hakuna mgurumo wa gari linalokuja eneo Hilo. wakashusha mikeka Ili kutandika kwa ajili ya picnic eneo Hilo. Lakini kama mzimu Oleg alijitokeza kwenye kichaka akiwa amechafuka vumbi ,nywele zimetimka ,huku nguo Zina matope na majani majani. Maafisa Hawa hawakuamini kumuona Oleg amesimama mbele Yao walihisi kama ni wale watu wa kwenye hadithi za fairy tales. Walitegemea kumkuta yeye na familia yake hapo lakini alisimama peke yake kama mshumaa wa pasaka mbele Yao. Naye Oleg alitarajia atakutana na maafisa wawili wa M16 kwa mujibu wa plan ya PIMLICO lakini walikuwa wanne.[emoji28][emoji28].
Oleg baada ya kuwacheki wote wanne aliuliza kwa kingereza apande gari ipi kati ya hizo mbili?
Ni rasmi Sasa Oleg alikuwa amekwepa surveillance ya KGB mpaka hapo .Sasa walitarajia kuanza safari ya kwenda Finland kupitia mpakani ...............
Kisen*geCha ajabu nini hapo mkuu!?
Ndio tatizo la watu weusi.Yan kujua kitu ambacho hata hakikusaidii unaona a big deal kias kwamba mwingine akiuliza unajiona like maisha umeyapatiiiiiiiiaa.
Unalo jibu..wape watu...huna kaa kimya ..sio kuleta habar za kiseng*e kama hiz
SawasawaKutokana na watu kupenda heavy duty topics kama hizi za kiintelijensia,nadhani hii ikikamilika tutashusha nyingine HEAVY [emoji3578][emoji3578][emoji3578][emoji108]. Matumaini yangu tutafurahia na kujifunza
uwe una ni tagKutokana na watu kupenda heavy duty topics kama hizi za kiintelijensia,nadhani hii ikikamilika tutashusha nyingine HEAVY [emoji3578][emoji3578][emoji3578][emoji108]. Matumaini yangu tutafurahia na kujifunza
Heavy duty zinaimarisha ubongo mada ka hizi tulizi miss sana JF. Naomba iendelee kutuletea hizi topic kama namuona buyobe akichabo Kwa mbali [emoji2][emoji2]Kutokana na watu kupenda heavy duty topics kama hizi za kiintelijensia,nadhani hii ikikamilika tutashusha nyingine HEAVY [emoji3578][emoji3578][emoji3578][emoji108]. Matumaini yangu tutafurahia na kujifunza
Kwenda zako huko bwege wewee
Kumbe tokamdaMC Tobby kuna mwamba anaitwa @fbuyobe wa twitter kaikopi na kuipaste uko twitani anachukua maujiko uko
Ndo tumchane huyo boya buyobe ajifanye yake na hiyoKutokana na watu kupenda heavy duty topics kama hizi za kiintelijensia,nadhani hii ikikamilika tutashusha nyingine HEAVY [emoji3578][emoji3578][emoji3578][emoji108]. Matumaini yangu tutafurahia na kujifunza
Itakua poaKutokana na watu kupenda heavy duty topics kama hizi za kiintelijensia,nadhani hii ikikamilika tutashusha nyingine HEAVY [emoji3578][emoji3578][emoji3578][emoji108]. Matumaini yangu tutafurahia na kujifunza
Nakumbuka huyu buyobe Kuna mtu alipostig story yake humu JF alilalamika Kila corner na ku report Uzi ufungwe JF na kweli ukafutwa Sasa nashangaa yeye ku paste za watu wengine na kujichukulia ujiko, ila hata huko Twitter sikuhizi kumevamiwa na vilaza ka wa FB wanachotwa tu akiliNdo tumchane huyo boya buyobe ajifanye yake na hiyo
Alichoandika mwenye thread na mm, kuna mambo mengi ni tofauti sana.Hii ndiyo maana ipo hivi ilivyo kwa sababu imejaa lundo la wajinga. Sasa wewe nini ulichoandika hapa ambacho hakijaandikwa na mwenye thread!? Kwa nn huwa mnapenda kujivua nguo kiasi hiki? Yaani lengo lako kila mtu akujue kama wewe ni mjinga au??
Naona mambo ni moto huku. myoyambendi @ulimkafu @bianca23
Heavy duty zinaimarisha ubongo mada ka hizi tulizi miss sana JF. Naomba iendelee kutuletea hizi topic kama namuona buyobe akichabo Kwa mbali [emoji2][emoji2]
Alichoandika mwenye thread na mm, Luna mambo mengi ni tofauti sana.
Tulia kwanza unywe maji basi
Nakuandalia 25000 kama tuzo ,tumechoka stori za mapenzi , kuachwa ,kufumaniwa ,nk mkuu fanya hiyohiyo KAZI ,tutakuandalia utaratibuKutokana na watu kupenda heavy duty topics kama hizi za kiintelijensia,nadhani hii ikikamilika tutashusha nyingine HEAVY [emoji3578][emoji3578][emoji3578][emoji108]. Matumaini yangu tutafurahia na kujifunza
Ukituma nijulishe niongeze afu 5Nakuandalia 25000 kama tuzo ,tumechoka stori za mapenzi , kuachwa ,kufumaniwa ,nk mkuu fanya hiyohiyo KAZI ,tutakuandalia utaratibu
PamojaUkituma nijulishe niongeze afu 5