35
Haikujulikana ni muda gani , Moscow waligundua kwamba Oleg haonekani Tena na makachero wa KGB,baada ya kufika kwake na kufanya thoroughly search kwenye makazi yake lakini hawakuweza kupata information zozote zile za kuweza kujua amaeenda wapi ,na pia majirani wa eneo Hilo la Leninsky prospekt hawakuweza kutoa maelezo ya kueleweka ila ilikuja semekana alionekana anakimbia jogging karibu na kituo Cha treni ,... Ulikuwa ni uzembe mkubwa kuwahi kufanywa na KGB na mpaka Leo hii wanajutia kuhusiana na hili tukio . Haikujulikana kwanini KGB waliamua kupotezea kumtafuta punde tu walipopata taarifa za kutoonekana kwake. Maafisa kadhaa wa KGB walitengeneza theory na kuamini labda Oleg alijiua....................a fatal mistake.
Baada ya timu ya utoroshaji ya M16 kupaki kila kitu eneo lile ,Oleg alipaswa kuingia kwenye Buti ya gari iliyokuwa inaendeshwa na afisa Arthur gee. Baada ya hapo Buti ya gari ikafungwa kwa ajili ya safari ya kuelekea Finland. Wakatokea main road na Sasa gari hizo zikawa zinaongozona huku Moja ya gari hiyo akiwa amefichwa jasusi ambaye endapo akikamatwa na Russia huenda watamgawanya vipande[emoji28]. Arthur gee na mkewe wakati safari inaendelea walisikia miguno,na sauti za kugonga kutokea kwenye Buti. Ni kwamba muda huo Oleg alikuwa anapambana kuvua nguo Ili azibadilishe na kuvaa alizopewa . Lakini kutokana na ile Hali ya harufu iliyokuwa inatoka ya sigara,jasho na sabuni ingetosha kugundua Kuna binadamu kwenye Buti na wale mbwa wa maafisa wa mpakani wanaonusa mpakani.
Kutokana na joto la kwenye Buti kuzidi kuwa Kali na hewa kuwa nzito, Oleg alikunywa vidonge fulani vya sedative Ili kupata ahueni. Alivuta picha akifika mpakani mwa Finland halafu wamkute akiwa kwenye Buti[emoji1][emoji1]. Hakika haikuwa good imagination
Magari ya maafisa Hawa yalifika kwenye mji wa Vyborg lakini kulikuwa na msongamano kutokana na ukaguzi uliokuwa ukifanyika kituo Cha mbele Cha mpakani . Hivyo gari zikawa zinatembea taratibu. Baada ya Kama maili Kumi kutoka mji wa Vyborg Sasa walifika eneo la mpaka kati ya Finland na Russia lililokuwa na ulinzi mzito wa kijeshi lililokuwa na upana wa kama kilomita 20. Kulikuwa na vizuizi vitano zaidi kutoka hapo walipo Hadi mpaka rasmi wa Finland. Vizuizi vitatu upande wa Russia na viwili upande wa mpaka wa Finland.
Kizuizi au barrier ya kwanza walivuka pasipo kukaguliwa document zozote.lakini maafisa hao walipigwa jicho fulani na huyo mjeda mkaguzi . Lakini halikuwa jicho la kuwapa wasiwasi .
Na kwa upande wa Arthur gee ,akiwa anaendesha baada ya kuvuka barrier hiyo aliwaza endapo kama alibana Buti ya gari alikokuwa Oleg au la . Lakini Buti lilikuwa limebanwa na endapo lingekuwa halikubanwa angesikia linagongagonga.
Maafisa Hawa wakafika checkpoint inayofuata na wakapaki gari pembeni kwa ajili ya kujaza taarifa zao kwenye ofisi za migration hapo . Hapa kutokana na mlolongo kuwa mrefu waliamini itawagharimu muda mrefu kiasi. Arthur na Ascot wakiwa kwenye foleni kujaza taarifa zao kwenye migration desk ,Rachel na Caroline walibaki kwenye magari . Oleg alijua Sasa yupo kwenye eneo la ukaguzi hivyo alitulia tuli. Caroline alimchukua mwanae Florence aliyekuwa analialia kiaina na kumbeba Ili kumbembeleza. Muda huo alisimama kwenye mlango wa gari uliokuwa wazi huku akiongea na Rachel aliyekuwa amekaa kwenye siti ya mbele.. Baada ya muda kidogo afisa mmoja akaanza kupita na mbwa wale wanaonusa Kulia na kushoto kwenye line za magari. Na baada ya muda kidogo yule mjeda na mbwa wake walianza kukaribia gari alilofichwa Oleg.
Mbwa alipokaribia Rachel aliyekuwa amekaa siti ya mbele aliamua kufungua crisp za vitunguu na kuanza kula , nyingine alizimwaga chini kiaina Ili mbwa yule ale. Lakini kutokana na harufu ya kitunguu vilivyopikwa haviendani na mbwa ,mbwa yule baada ya kunusa akiwa na afisa baada ya kuisikia hiyo harufu akapiga chafya kiaina akaondoka na kuzunguka nyuma ambapo muda huo rachel alikuwa amempakata mwanae mdogo akiwa ameegemea Buti. Baada ya kuona mjeda na mbwa wake wanakuja huku upande wa Buti , huyu mwanamama akaanza kumbadilisha mwanae nepi ya mwanaye iliyokuwa imeshaloa[emoji28][emoji28]. Kama bahati tu huyu mama alidondosha chini ikiwa inatoa harufu karibu na Buti ya gari. Huyu mbwa akiwa kwenye cheni iliyokuwa imeshikiliwa na afisa baada ya kunusa , alikutana na harufu ya kuudhi sana kutoka kwenye diaper zilizokuwa zimetupwa chini hivyo akajivuta mbali na hiyo harufu na kuondoka.
Kwa mara nyingine bwana Oleg akawa ameokoka kugundulika kutokana na harufu ya diaper au nepi ya mtoto iliyokuwa imetupwa[emoji3578][emoji3578][emoji3578][emoji108].
Baada ya muda waume zao walirudi baada ya kama dakika kumi na Tano za kujaza taarifa zao. Na baada ya muda alikuja afisa wa migration na kuwakabidhi passport zao Kisha wakaagwa na kuondoka.
Kizuizi Cha mwisho kilikuwa ni Cha ukaguzi wa passport hivyo baada ya kufika hapo walitoa passport zao kwa maafisa wa uhamiaji wa Finland kwa ukaguzi wa mwisho. Na kweli baada ya kukaguliwa walirudishiwa passport zao na afisa akanyanyua chuma kuruhusu Sasa kuingia FINLAND.
Baada ya muda Oleg alihisi Sasa wapo kwenye lami kutokana speed ya gari kuongezeka .. alianza kusikia mziki ukitokea kwenye redio hapo oleg alihisi roho yake ikisuuzika Sasa yupo ndani ya Finland.. Baada ya kuendesha kama mwendo wa dakika 20 walikutana na gari ndogo aina ya Volvo ikiwa imepaki pembezoni mwa njia ya vumbi inayoelekea msituni . Ndani ya gari Hio kulikuwa na maafisa wa PET wawili Eriksen na Larsen.wakasimama . Baadaye akajitokeza martin shawford kwenye miti miti akasimamisha na ghalfa naye mwanamama Oliver price aliyesuka hii plan ya PIMLICO alijitokeza. Baada ya kukutana hapo wote it was an emotional moment ever . Baadaye walifikia Buti aliyokuwamo Oleg . Baada ya kutoka kwenye Buti alitaka kudondoka chini kutokana wenge na Hali ya kizungu zungu na pia miguu ikiwa imechoka kutokana na kujikunja muda mrefu. Alisimama na kunyanyua mikono yake miwili na kuibusu huku akitabasamu . Alienda Hadi kwa Rachel na Caroline waliokuwa wamesimama pembeni ya gari.akawabusu mikono Yao kama alama ya shukran kwao.
Baada ya hapo alibadili nguo na zile nguo chafu alizovua zikawekwa kwenye mfuko na kutupwa kwenye buti ya gari . Baadaye Oleg akapanda kwenye gari muda huu anaendesha mwanamama Oliver price,huku yeye akikaa siti ya nyuma na Mr. Brown, wakielekea kaskazini kabisa mwa Finland . Simu zilipigwa kwenye kituo Cha mbele Cha Petrol ,kuwataarifu makao makuu nchini uingereza. Wakuu wa kitengo walipongezana kana kwamba wamefanikiwa kumtuma mtu mwezini na kufika Salama.[emoji108][emoji108][emoji3578].
Walifika kwenye hotel Moja usiku kwenye mji wa Helsinki na kuagizwa msosi heavy kwa timu hii iliyofanikisha hili zoezi. Na kwa mara ya kwanza waliweza kujua jina lake halisi la Oleg Gordievsky. Baada ya mapumziko waliendelea na safari na jumapili walifika kwenye mpaka Finland na Norway kwenye mji wa Karigasniemi baada ya kukaguliwa Wakapita . Safari iliendelea na Na mwisho wakafika hoteli Moja iliyo kwenye mji wa tromsø . Baada ya kupumzika Oleg na timu yake kesho yake waliruka kwa ndege wakiwa na passport feki Hadi Jiji la Oslo na hapo wakapanda ndege nyingine Hadi LONDON..............
Timu iliyomtorosha Oleg( Arthur ,Ascot pamoja na wake zao) nje ya Russia wao walibaki mjini Helsinki. Hapo waliyafanyia usafi magari hayo ili kuondoa ushahidi wowote kumhusu Oleg kabla ya kurudi Moscow. Japo walitambua wakifika Moscow lazima na ikajulikana Oleg alitoroka basi maafisa wote wa ubalozi wa London Moscow lazima wangefukuzwa wote.... Hadi na balozi mwenyewe
Na baada ya siku chache baadaye balozi mteule mpya wa uingereza nchini Russia kukabidhi hati ya utambulisho wake Kremlin sir Bryan cartledge , Walikuwa wamepozi kwa ajili ya picha ya pamoja na staff nzima hapo Moscow akiwemo Arthur gee na Ascot. Wakiamini kwenye vichwa vyao muda sio mrefu watatimuliwa baada ya Oleg kugundulika yupo uingereza.....
Huku makao makuu KGB ndio kwanza wakawa wameshtuka kwamba jasusi Oleg kapotea .. kimbembe kikaanza kumsaka .. Akaitwa rafiki yake Oleg bwana lyubimov kwa ajili ya mahojiano makao makuu........
Moja ya kizuizi Cha kijeshi Cha mpakani kwenye mji wa Vyborg kwenye mpaka kati ya Russia na Finland walipopita Oleg na maafisa wa M16 . Ni Moja kati ya mpaka uliokuwa unalindwa kipindi hicho .