Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Hakiki ndugu yangu mfumo ndio unao tugharimu.
Mfumo unamfanya kiongozi hata awe ana vision nzuri ya kulikwamua taifa awe chini yake.
Mfumo unataka kulindana na kurithishana madaraka .
Mfumo unataka ujilinde wenyewe kwa hiyo hauwezi mtu kuuvunja mfumo kabla wenyewe mfumo haujakuvunja.

Kwa bahati nzuri au mbaya mtu kama Magufuli aliweza japo kwa kidogo kuugusa mfumo, na watu wengi waligusika ikiwemo hao catholic mission na baadhi ya watu ambao walishajiwekea uhakika wa kulindwa na mfumo.
Bahati mbaya huyo hakuweza kuendelea ,pengine ni mfumo ulitaka asiweze kuendelea maana huo mfumo ulikua upo hatarini.

Kama angemaliza kipindi chake, na anaemfutia akawa ni wa namna yake, na ambaye angufuata pia huwenda kwa miaka 30 taifa lingeweza kuwa na mfumo mpya ambao ni wa maslahi maslahi kwa taifa moja kwa moja.
 
Kila kitu unachokilalamikia hapo kipo nchini bibie... hujui tu.... mshkuru mungu unalala salama na unaamka salama 😊
 
Kila kitu unachokilalamikia hapo kipo nchini bibie... hujui tu.... mshkuru mungu unalala salama na unaamka salama [emoji4]
Hyo kulala salama ni just lazy excuse na watu ka nyie ni conservative you don't want change, Kuna vitu hata vya utendaji wa kawaida wa huduma kijamii hyo inahusikaje na kulala Kwa amani. To me napendelea mabadiliko chanya Kwa nchi yangu kuendana na nyakati sio kutumia old ways zisizotupa namna ya kwenda mbele Sasa Hadi Leo madawati na vyoo vya shule ni changamoto huoni Kuna mahali tumekwama kufikiri. So amani na kulala isiwe chaka la justification ya kuwa wavivu.
 
Kuna watu wanamfananisha huyu wa kwetu na Magreth thatcher !
Anaweza kushabihiana kweli na thatcher?
Jamani jamani hapo ni sawa na kulinganisha mbingu na ardhi, Magreth Thatcher alikuwa next level and smart mno plus mifumo Yao Iko clean huyu watu anajitahidi kiasi chake ila bado. Thatcher ujue alikuwa waziri mkuu kwenye nyakati ngumu hasa mambo mara kuepeleka nchi yake kwenye mipambano mikali bado issue zake na former USSR huyu wetu bado hajakutana na kashikashi kubwa hata ufisadi na rushwa vimekosa dawa nchini mwetu.
Ngoja tumuone Kwa hili la katiba yaweza kuwa legacy yake
 
Ni hatari sana. Tuna kazi ngumu sana kwakweli
Hizo nchi zote zinazojiita tajiri, ukiacha Russia ambayo ina utajiri asilia, mataifa mengine yote uchumi wao ni wa kwenye makaratasi. Ndiyo maana wameweka nguvu kubwa sana kwenye ujasusi. Budget km CIA siyo mchezo kaka! Uingereza aliyetutawala sisi, pamoja na kuondoka, lakini yeye ndiyo anaamua karibu kila kitu chetu. Uingereza wana Taasisi hapa za kumwaga, kwa ujinga wa watu Taasisi hizo wanaamini zina malengo hayo yanayosemwa hadharani..ulishawahi kujiuliza Taasisi km British council ina kazi ya kukuza lugha ya kiingereza hapa nchini!?? Taasisi hiyo imejaa makachero wa uk na watanzania ambao ni mapandikizi..
 
Amani gani gani anasema huyo ndugu, au usalama gani?
Nchi hii kwa wakati huu tuliopo tunaona ni heri mwanzoni wa miaka ile tunapata uhuru.
Hatukuwepo lakini tunasoma katika historia namna nchi ilivyo jiendesha, maendeleo ya mtu mmoja mmoja, maendeleo ya taifa, huduma za jamii, ubora wa elimu, uwepo wa viwanda vinavyozalisha bidhaa, nk nk.

Sasa hivi kila bidhaa ndogo inaagizwa toka nje, sindano ya kushona nguo itoke china?


Hapana kwa kweli kuna sehemu tumekosea sana ,sana ! Haswa kati ya 2005 kuja huku tulipo leo.
 
Kazi ipo price must be paid bila hivo ngumu kutoboa
Kwa Tanzania hata wananchi wenyewe hatuko tayari kulipa gharama za mafanikio. Hili nililiona enzi ya JPM nilikua nafanya kazi mahali ktk taasisi fulani sasa wakati jpm anabadilisha mifumo mingi kwenye maeneo mbali mbali ikiwemo mfumo ule wa malipo kwa control number asee watu walikuwa hawamtaki hata kidogo maana aliwapokonya ulaji mwingi na wakawa hadi wakimuombea mabaya.

Siyo hapo tu ata ile system ya kubana fedha toka kwa mafisadi, kufanya review ya wafanyakazi serikalini (na kuwatoa wafanyakazi hewa) na mifumo mingine yenye tija kwa taifa mbeleni kitu ambacho kilifanya maisha yawe magumu kwa muda huo Watu hawakuwa tayari kuvumilia hali hiyo. Wakaanza kusikika "bora kikwete bora kikwete "😂
Kifupi watanzania wanapenda aina ya uongozi ambayo ni nyoro nyoro isiyowabana utasikia tu wakisema "hata kama kuna watu wanapiga si mradi tuko hai na tuna amani Mungu atatusaidia tu huko mbeleni" 😂 😂 😂
 
Kwa kweli nami nilishangaa sana kumlinganisha na thatcher, ishu ndogo kabisa ya ubadhilifu kwa mujibu wa ripoti ya CAG inatosha kabisa kujua hapa ni yale yale tu.


Nadhani hata hili la katiba ni heri lingeachwa maana tunaweza kupata katiba mpya ambao hii ya sasa ingekuwa ya afadhali.
 

Huyu Oleg ni kwamba anasifiwa maana bila yy kuna uwezekano kungekuwa na vita ya nuclear kati ya mataifa. Na taarifa alizozitoa ni kuwataja raia wa wingereza marekani na mataifa mengine ya Europe wanaotoa siri zao kwa Russia, na raia gani wa Russia ni jasusi. Kwahyo sio kweli kuwa russia ilichezewa, ila pia Russia ilichezea wengine vibaya sana.
 
[emoji2][emoji2]jambo la rushwa na CAG limekosa tu kuchukuliwa hatua sembuse maamuzi magumu ya Thatcher Kwa nchi yake.
Hata hyo katiba ingetakiwa kufanyiwa amendment ya baadhi ya mambo pia na hyo katiba bila political ya will aliyeko madarakani hasa Kwa Africa Huwa ni useless tu
 
Aisee kazi kubwa inahitajika nikisoma hii story ina reflect mengi hata vita vya Ukraine si Bure Wala. Ila kuwekeza kwenye intelligence makini ni muhimu Kwa msitakabali wa taifa lolote makini
Hata vita huwezi kupigana kama huna taarifa za kijasusi, lazima ujue nguvu ya unayetaka kupigana nae, technolojia ya silaha na nguvu ya silaha, hali ya askari wake pamoja na raia. Idara ya ujasusi ina impact kubwa sana kwenye maisha yetu
 
Amani na uzalendo imekuwa chaka la kuficha uzembe na ukosefu wa uwajibikaji Kwa nchi yetu.
Imagine kulikuwaga na viwanda kwenye elimu Tanzania ilifuta ujinga Kwa raia wake, education ilikuwa for self reliance mashule ka technical school zilikuwa zinazalisha watu Bora sikuhizi viwanda vyote vimekufa, elimu sikuhizi mtu ana maliza form four hajui hata kusoma tumekuwa taifa la wachuuzi na dampo la bidhaa la wachina. Na hapo tutasingizia wazungu mara hatuna uwezo tunaanuliwa Kila kitu na colonial master [emoji2][emoji2][emoji2] hiii in magufulis voice
 
Hata vita huwezi kupigana kama huna taarifa za kijasusi, lazima ujue nguvu ya unayetaka kupigana nae, technolojia ya silaha na nguvu ya silaha, hali ya askari wake pamoja na raia. Idara ya ujasusi ina impact kubwa sana kwenye maisha yetu
Kwangu Mimi idara ya usalama inabidi kuwezeshwa maana ndio core au engine ya ku drive change. Ila ikiwa blind na mambo yote yanakuwa blind vile vile na huwezi shindana na kitu usichokijua nguvu yake lazima upigwe
 
💯💯👍
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…