mapema
JF-Expert Member
- Jul 21, 2014
- 640
- 1,881
Hakiki ndugu yangu mfumo ndio unao tugharimu.Siyo tatizo letu, tatizo lipo kwenye mifumo ya Dunia. Somo kubwa unapaswa kujifunza kwenye maandiko km haya..hivi Kama Soviet ilikuwa inachezewa hivi, Tanzania kuna nguvu gani ya kupambana na hawa majasusi kwenye nyanja zote!? Kwenye nchi Kama zetu hayo mataifa makubwa ndiyo yanaamua namna yetu yote ya kujiongoza.
Kuanzia kwenye mifumo yetu ya elimu, siasa, dini nk. Kote huko wamejaza watu wao..! Wao ndiyo wanakuamulia ktk kila kitu. Kwa mfano kanisa katoliki limejaa maafisa vipenyo wa nchi za magharibi..Bakwata nayo imejaa mapandikizi lukuki. Na kwa karibu 80% watu wetu wa usalama wanazalishwa zaidi kwenye shule za kanisa katoliki. Yaani hata ukiingia wewe leo ikulu, mfumo utakufanya uongoze kwa aina ileile ya viongozi uliokuwa unawashangaa!
Mfumo unamfanya kiongozi hata awe ana vision nzuri ya kulikwamua taifa awe chini yake.
Mfumo unataka kulindana na kurithishana madaraka .
Mfumo unataka ujilinde wenyewe kwa hiyo hauwezi mtu kuuvunja mfumo kabla wenyewe mfumo haujakuvunja.
Kwa bahati nzuri au mbaya mtu kama Magufuli aliweza japo kwa kidogo kuugusa mfumo, na watu wengi waligusika ikiwemo hao catholic mission na baadhi ya watu ambao walishajiwekea uhakika wa kulindwa na mfumo.
Bahati mbaya huyo hakuweza kuendelea ,pengine ni mfumo ulitaka asiweze kuendelea maana huo mfumo ulikua upo hatarini.
Kama angemaliza kipindi chake, na anaemfutia akawa ni wa namna yake, na ambaye angufuata pia huwenda kwa miaka 30 taifa lingeweza kuwa na mfumo mpya ambao ni wa maslahi maslahi kwa taifa moja kwa moja.