Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Aaa Mkuu hivi wewe tukio la Oleg utafananisha na kuingilia huo uchaguzi wa US? Urusi pigo walilopata kwa Oleg ni kubwa sana mkuu yaani waliumizwa sana. Kwao ilikua ni pigo sana kwa taasisi yao hiyo maana miaka michache badae Soviet ilibomoka vipande vipande na rasmi vita baridi ikawa imeisha. Sasa ukisema kwamba nae Russia ameonesha umwamba kwa kuingilia uchaguzi eti kuwa ndio ametoa pigo kwa Us ahaaa no sidhani kama zinalingana kwa uzito mkuu
Yaani mkuu mimi nadhani udhaifu ama uhodari wa hizo agency ni kutokana na faida na hasara wanazosababisha kwa nchi zao kwa ujumla.... kwamba Mi6 hasara waliopatia Kgb ni kubwa mno lknFSB hasara walioipatia CIA/US ni ndogo na pengine hata hatujui wao walipata faida yoyote hapo.
 
Usaliti ni kitu kibaya sana hasa tukiaminiwa na Ina damage mbaya usaliti ndio uliofanya USSR kuvunjika loh.
Changamoto watu Huwa ni wabishi sana
 
Na kwa nini West wafurahie sana kuepushwa kwa vita wakati USSR aliitaka kwa hamu sana hiyo vita?.

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu!Ishu ya 85s huko,imekuwa wazi leo 2020.Ishu ya 2015s hivi,haiwezi kuwekwa wazi leo kwa kina.
SMO inaendelea huko Ukraine na ndani yake kunatuhuma juu ya U.S.A kuweka lebo za kikemikari huko.
Kupitia suala la Oleg,west ndiyo waliofurahia sana na kuepushwa na vita.Kwa nini furaha iwe kubwa kiasi hicho kama kweli hawakumuogopa USSR?.
 
Hv unafikiri jamii itakuchukuliaje ukiwa unagombana na kichaa, kichaa ni kumuepuka tu au ukiamua kukabiliana nae basi uchukue tahadhali.
 
AFTERMATH.

Baada ya haya yote, kesi ya Oleg imebaki kuwa Case study kwa vyombo vya usalama vya nchi za magharibi Hadi Sasa. Kutokana na hadhi aliyopewa ,ameshasafiri nchi mbalimbali za dunia , ikiwemo New Zealand, South Africa, Australia, Canada, ufaransa, ujerumani, Israel, Saudi Arabia na nchi za Scandinavia Katika kutoa Somo kwa Mashirika ya kijasusi ya nchi hizo. Nchi nyingi duniani zililazimika kubadili muundo wa kiutendaji kwa taasisi za kijasusi za nchi hizo kutokana na hili swala la Oleg.
Maafisa mbalimbali wa M15 na M16 waliohusika na kesi hii ya Oleg wengine ni wastaafu ,na baadhi wametangulia mbele za haki na wengine bado kazini mpaka stori hii ilipowekwa kitabuni. Na wengi wa maafisa walibadilishwa vitengo waliohusika na Hili swala la Bwana Oleg Ili kuficha identity zao .
Na kwa upande wa bwana Aldrich Ames , madhara aliyoisababishia CIA ni kwamba ilipoteza majasusi wake wengi kwa Siri alizokuwa anatoa kwa nchi ya Russia. Na inakadiriwa Bwana Ames alipata kiasi Cha Dola milioni 4.6 kutokana na information alizokuwa anatoa kwa Urusi na wengi wa majasusi wa CIA waliokuwa Soviet walipotezwa mazima.
Yote kwa yote bwana Ames alikamatwa na maafisa wa FBI tarehe 21 Feb 1994 ,akiwa na mpenzi wake Rosario dupuy na kutiwa ndani.
Miezi miwili baadaye alikutwa na kesi ya kujibu kuhusiana na ujasusi na akafungwa kifungo Cha maisha jela . Mkewe Rosario dupuy alikutwa na hatia na kosa la ukwepaji Kodi na kosa la kutaka kufanya uhaini , na alipewa kifungo Cha miaka mitano baada ya plea bargaining. Kwa Sasa Ames ni mfungwa namba 40087-083 na anaitumikia adhabu yake kwenye geraza la federal correctional institution Terra Haute huko Indiana marekani.
Baadaye Ames alipohojiwa akiwa gerezani 1997 Alikiri na kusema aliwasaliti wengi kwa ajili ya pesa na akasema hakuwahi mjua Oleg na hakumsaliti.
Swala la nani aliyemchomesha Oleg mpaka Sasa limebakia kuwa kitendawili au fumbo la imani.




Aldrich Ames akitiwa pingu na makachero wa FBI muda mfupi baada ya kukamatwa 1994. Hii ni baada ya kuvujisha Siri za CIA kwa KGB kwa zaidi ya miaka 10.





Aldrich Ames na mkewe Rosario dupuy wakiwa kwenye arrest photography.muda mchache baada ya kukamatwa . Rosario aliachiliwa baada ya kukamilisha kifungo chake ,ila mumewe Aldrich still yupo jela.




Credit: ziende kwa
1.Ben MacIntyre@The spy and the Traitor.2018
2. Duka la vitabu la Elite Bookstore pale Shoppers Plaza Dodoma
3.wana jf wote na wale wote walionipa maua yangu[emoji39][emoji39][emoji39] Appreciation kwao for their encouragement.
 
Nikichojifunza ni kwamba ukiisaliti nchi yako kwa namna yoyote ,lazima utalipa high price even the blood price of your loved ones.
Oleg naweza kusema ni bahati ilikuwa upande wake ,kama ilivyo tu kwa ilivyokuwa kwa Kim Philby ambaye naye yupo huko Russia kwa Siri .
Yote Tisa KGb itabaki kuwa Moja ya taasisi nyeti ya kuigwa kama mfano kwa nchi nyingi duniani mpka sasa japokuwa Ili collapse mwaka 1991.




 

Asante nadhani kuna nyingine inafata
Tutaomba utuwekee link hapa tuanze nayo pia
Nashukuru usimuliaji wako haukuwa wa kujivuta vuta kama wasimuliaji wengine wanaishia katikati
 
Hii stori ya Oleg Gordievsk niliwahi kuiona kwenye Tv documentary.
Kipindi kilikua kinaitwa Double Agent.
Oleg Gordievsk "The spy who saved the World."
Ukiona kwenye documentary utaifurahia zaidi hasa pale kwenye check point walipokua wanamtorosha Oleg kwenye buti la gari, kulikua na tension kubwa sana ila mchezo waliofanya maafisa wa MI6 kuwazidi akili KGB na mbwa wao akili kubwa sana ilitumika. KGB hawatokuja kusahau kamwe.
 
Asante mkuu [emoji122] [emoji122]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…