mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 4,072
- 12,119
- Thread starter
- #101
SEHEMU YA 5
Kiukweli mama yake Oleg , hakufurahishwa sana na mwanaye huyu mdogo kujiunga kitengoni. Hii ni kwa sababu ya historia na misukosuko aliyopitia .Alimwona kama mwanaye amejiunga na idara ya mashetani waliohusika kuyaharibu sehemu ya maisha yake,Sasa mwanaye naye anajiunga huko Tena .hakika kulimchanganya sana mwanamama huyu. Lakini mwanaye baada ya kurejea kutoka ujerumani mashariki Alimwona mama yake kama Hana furaha kabisa Japo ilikuwa ni kazi yenye status ya Hali ya juu kwa wakati huo. Oleg alimwambia mama yake kwamba hatakuwa anafanya kazi ndani ya KGB hapo Russia Bali kama afisa mwakilishi (balozi ) nje ya nchi ya urusi. Alijaribu kumshawishi sana mama yake asiichukulie kazi ya kitengo in negative way.ila ndio hivyo mwana mama hakuafiki kabisa moyoni mwake Japo hakuwahi onyesha waziwazi. Kwa kifupi Olga na mmewe mzee Anton hawakuwa pride na mwanao kuifanyia kazi kitengo ,lakini watafanyaje Sasa ,kitengo kishamchagua..
Baada ya kurudi kutoka ujerumani mashariki kwenye field yake ya mwisho ,alikutana na rafiki yake, stanislav kaplan kwenye mapumziko mafupi karibu na fukwe za bahari nyeusi. Waliamua kukutana kwa mara ya mwisho kama raia wa kawaida kabla ya kujiunga rasmi kuwa maafisa wa wa ujasusi kwenye nchi zao . Kwa mfano stanislav baada ya kumaliza mafunzo hapo Moscow alitarajiwa kujiunga na idara ya ujasusi ya Czechoslovakia iliyojulikana kama StB. Walikutana ,wakanywa ,wakijipongeza, vilevile wakipeana michapo ya totozi walizozifukuzia,miziki, na zaidi wakipondea mfumo mzima wa kikomunisti uliokuwa unatawala nchi zao. Vilevile stanislav akampa Oleg kijarida kidogo Cha mashairi ya kumponda Stalin kilichoandikwa na Yevgeny Yevtushenko kilichokuwa banned nchini urusi kabla ya kuachana.
Baada ya kutengana na rafiki yake bwana Oleg alihitajika kufika kwenye academy ya KGB iliyojulikana kama "Red banner".elite training academy. Hii akademi ipo porini maili 50 kaskazini ya Jiji la Moscow. Hii akademi ilipewa codename "school 101".
Hapa bwana Oleg pamoja na Maafisa wenzake wa KGB 120 walipewa mafunzo ya mwisho kabisa .walizamishwa kwenye Siri nzito za mfumo wa kisoviet.walifundishwa namna ya kuwatambuana wao kwa wao ,combat skills, kutumia silaha za aina mbalimbali. Vilevile walifundishwa kutumia lugha za uficho wanapowasiliana wao kwa wao. Na la Zaidi na kubwa zaidi walifundishwa namna ya kukwepa kufuatiliwa endapo wanahisiwa ni ma spy .( " surveillance detection). Mafunzo haya pia yalijukulina kama dry-cleaning au proverka kwa kirusi. Hapa wanafundishwa namna ya kuhisi kama unafuatiliwa ,namna ya kukwepa kama unafuatiliwa kwa njia ya kutotambulika na
kumchanganya anayekufuatilia kwa kumkwepa kwa ustadi wa Hali ya juu.
Walifundishwa pia namna ya kutuma na kupokea infos baina yao wakiwapo kazini ,kuacha signal , kutumia wino wa Siri kuandikia,matumizi ya kamera ,vinasa sauti .n.k. Pia maafisa waliotarajiwa kufanya kazi nchi za magharibi walipewa semina za kutosha kuhusu nchi hizo ikiwemo tamaduni , lugha n.k. Walifanyiwa kama ibada ya kukiri imani na kuutumikia mfumo wa kistalini na ukomunisti kwa ujumla.Na mwisho waliapizwa viapo vizito vizito na manuizo ya kutosha na rasmi kuwa maafisa wa KGB.
Baada ya hayo yote bwana oleg alipewa jina lake rasmi la kijasusi.Na mfumo huu wa kupewa jina lako la kispy lilikuwa linafanyika randomly kwa kuchaguliwa jina kwenye list ndefu ya majina yaliyoandikwa kwenye kitabu maalumu. Jina analopewa afisa wa KGB kikanuni lilipaswa kufanana na jina lako rasmi ulilopewa na baba na mama yako. Kwa mfano bwana Oleg alipewa jina la Guardiyetsev. Kulikuwa Kuna sababu ya kupewa jina la kijasusi linalofanana kidogo na jina lako orijino. Hii ilisemekana kwamba ikatokea mtu anakufahamu kwa jina lako halisi , halafu akakuita kwa jina lako hilo, isije ikamchanganya ambaye anakujua kwa jina lako la kijasusi , kwa maana atahisi amesikia vibaya kutokana pseudonym ya majina hayo na yatakavyotamkwa.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa bwana Oleg , na pia kama sehemu ya kuwa afisa rasmi , ilikuwa ni lazima kwa maafisa hao kujiunga na chama Cha siasa Cha nchi yao .communist party. Kulimfanya ku doubt sana lakini ndivyo utaratibu ulivyotaka. Mpaka kufikia majira ya kiangazi mwaka 1963 ,bwana Oleg alikuwa rasmi Sasa ni afisa wa KGB.
Hivyo mwaka huo tarehe 20 august alihitajika kufika makao makuu ya KGB kwenye idara ya FCD. Jengo Hilo la makao makuu lilikuwa na karibu na Kremlin. jengo Hilo lililotumiwa na KGB wakati huo lilikuwa kama hekalu ambalo ni jengo la idara ya bima la urusi. Sehemu ya jengo hili ilikuwa na ofisi za wakubwa wa kitengo,sehemu nyingine ya jengo ilikuwa stoo ya kuhifadhia archives na documents mbalimbali na sehemu nyingine ilikuwa na torture cells.
Baada ya kufika idarani na kuanza rasmi, majukumu yake yalikuwa ni kupitia document na nyaraka za maafisa wa ujasusi waliotumwa nje ya nchi,kupokea taarifa zao za kijasusi na kuzihifadhi. Pia alikuwa na kazi ya kufoji baadhi ya nyaraka kama pasi za kusafiria ,kutengeneza utambulisho bandia kwa majasusi na vilevile kuwapokea waliokuwa wanarudi kutoka kwenye majukumu ya kijasusi.
Mtu aanzapo majukumu ya kazi ya kuajiriwa lazima tapewa orientation za hapa na pale na pia kufahamu wafanyakazi wenzako wa hapo kazini na ma legend wa idarani. Ndivyo ilivyokuwa kwa bwana Oleg. Hapo kwenye idara ya FCD au Derectorates S, Oleg alitambulishwa kwa so called mashujaa wa kijasusi hapo ofisni. Kwa mfano Alitambulishwa kwa bwana mmoja aliyeitwa konon trofimovich au jina rasmi la kijasusi kama Gordon Arnold Lonsdale, aliyekuwa anafanya kazi ya ujasusi kama illegal kwenye nchi nyingine. Jina hili la Gordon Arnold lilitokana na jina la mtoto mdogo wa kanada aliyefariki dunia miaka kadhaa nyuma ,hivyo mwaka 1943 KGB wakaamua kumpa jina hili bwana konon kwa kuwa alikulia marekani tokea akiwa mdogo na kuongea fluent English. Inasemekana huyu alikuwa akiishi London akiwa kama muuza boligamu au bablishi.kazi yake hapo London ilikuwa kukusanya taarifa za kijasusi za jeshi la majini la uingereza na pia kupandikiza majasusi wengine sehemu mbalimbali ndani ya uingereza (Portland spy-ring). Huyu bwana alikuja kukamatwa baada ya uingereza kutonywa na CIA, hivyo akafunguliwa mashtaka ya uhaini .Lakini kesi yake ilisitishwa kusikilizwa na mahakama za uingereza kutokana na mahakama kutokuwa na uhakika na jina lake. Alirudishwa Moscow kutokana na kubadilishana wafungwa (swapping). baina ya uingereza na urusi. Hii ni baada ya kukamatwa kwa mfanyabiashara wa uingereza nchini urusi kwa tuhuma za ujasusi.
Pia Oleg Alitambulishwa kwa bwana mmoja aliyeitwa Vilyam Genrikhovich fisher au jina lingine Rudolf Abel. Huyu alikuwa anafanya ujasusi ndani ya marekani kama illegal na alikamatwa baadaye na kuhukumiwa miaka 20 jela. Lakini marekani walibadilishana na urusi pamoja na mfungwa wa kimarekani aliyeitwa Gary powers aliyekuwa rubani wa ndege iliyotunguliwa ndani ya anga la Soviet aina ya U-2 spy plane mwaka 1962.
Na pia mwisho bwana Oleg Alitambulishwa illegal mwingine aliyekuwa raia wa uingereza aliyejulikana kama Kim Philby. Huyu bwana aliajiriwa na NkVD kabla ya kuwa KGB mwaka 1934 .huyu alikuwa anafanya kazi idara ya ujasusi ya M16 uingereza lakini anatoa Siri za idara yake na kuzituma huko Russia na baada ya kuona mchezo wake ni hatari endapo akikamatwa na uingereza akaamua kutokomea Moja kwa Moja urusi 1963.hili lilifedhehesha sana uingereza wakati huo. Ndivyo ilivyokuwa utambulisho
Bwana Oleg miaka miwili baada ya kujiunga na idara hii ya directorate S alitambua rasmi Sasa ameingia kwenye dunia nyingine kabisa tofauti na binadamu wa kawaida . Hii ni kwa sababu ya kujua mambo mazito katika ulimwengu wa kijasusi ndani ya muungano wa kisoviet.
Mbali na kuwa JASUSI bobevu ,aliamini hataweza kutumwa kama illegal kukusanya taarifa za Siri kwenye nchi nyingine .