mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 4,072
- 12,119
- Thread starter
- #61
SEHEMU YA 4
Baada ya kufika huko alifanyiwa usahili na mwanamke mmoja wa makamu . Usahili huo alifanyiwa kwa lugha ya kijerumani na mwanamama alifurahishwa na bwana mdogo alivyokuwa ana respond . Kwa kifupi bwana Oleg alikuwa tayari kitengo kimemwelewa na akajikuta ndani ya system . Tokea mwanzo ni kwamba Oleg hakuwahi kuomba kujoin kitengoni Bali kitengo kilimchagua ajoin.
Muda wa Oleg kuwepo chuoni ulikaribia kuisha alipopata nafasi ya kazi huko kwenye ubalozi wa urusi huko ujerumani mashariki kama sehemu ya masomo yake . Hii ilikuwa ni kazi ya miezi sita kupata uzoefu tu akiwa kama mtafsiri wa ubalozini . Alifurahishwa kwa kazi hii nje ya urusi na alifika huko tarehe 12 agosti 1961 na kupelekwa kwenye hostel za wanafunzi zilizopo kwenye kitongoji Cha karlshorst.
Kipindi hicho anawasili huko ujerumani mashariki kulikuwa na machafuko na raia wengi walikuwa wanatoroka nchi na kukimbilia ujerumani magharibi. Kutorokea huko west Germany kuliwapa mwanya waweze kwenda nchi za ulaya magharibi na marekani kukimbia utawala wa kikomunisti wa Soviet.
Inakadiriwa raia milioni 3.5 ambao ni kama 20% ya raia wote wa ujerumani mashariki walikuwa wanakimbia nchi Yao kutoka kwenye utawala wa kikomunisti wa kisoviet.
Kesho yake Oleg anaamka baada ya kufika huko na alikuta mitaa ya Jiji la East Berlin Kuna makatapila na matrekta. Ni kwamba serikali ilianzisha kampeni ya kudhibiti Raia kukimbia nchi kwa kuanza kujenga ukuta. UKUTA WA BERLIN. kiuhalisia huu ulikuwa ni kama ukuta wa gereza kudhibiti Raia kutorokea nchi nyingine. Ulikuwa ni ukuta wa zege nzito wenye urefu wa zaidi ya mile 150,wenye senyenge ,mahandaki ,na vizuizi vya magari n.k. Haya yote Oleg alikuwa anajionea mubashara,akiona madhila yaliyokuwa yanaendelea kwa raia waliojaribu kutoroka. Ukuta huu ulikuwa na maafisa wa usalama walioamriwa kumpiga chuma raia yoyote atakaejaribu kupanda ukuta akitaka kutoroka . Haya mambo yalimtisha bwana mdogo huyu akiwa na miaka 22 tu,lakini haikumzuia kutekeleza order za wakubwa wake.
Krismasi ya mwaka huo alifanya mawasiliano ya Siri na ndugu yake, Vasili namna gani wangeonana kwenye mji wa Leipzig. Ingawaje ni ndugu Oleg hakuwahi jua kaka yake anafanya Nini ndani ya ujerumani mashariki naye hakujua bwana mdogo anafanya nini ndani ya ujerumani na hakuna aliyemuuliza mwenzake. Kilichowafanya kukutana ni kuhudhuria tamasha la krismasi mjini hapo lililojulikana kama Christmas oratorio. Hapo wangeshuhudia bendi za live,kucheza kunywa wine n.k. kuwepo kwake huko east Germany na aliyoyashuhudia kwa namna Moja kulimuathiri . Alishuhudia rasmi mgawanyiko wa kiitikadi baina ya nchi za ulaya. Ulaya mashariki na ulaya magharibi na kwa namna nyingine alionja uhuru wa kibepari alioukosa kwenye nchi yake ya nyumbani.
Mwaka 1962 julai 31 aliitwa nyumbani na kuripoti Moscow .