Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 32,639
- 42,908
Interesting.... msaliti ana maisha mafupi mno.23.
Taarifa za Siri alizokuwa anatoa bwana NOCTON kwa M16 ,na kuwamegea CIA zilianza kuwatamkia lakini kamwe M16 walificha identity ya source hawakutaka CIA wajue. Ingawaje marekani walikuwa na muscles in terms of money na resources lakini hawakuweza kupata information ambazo ziko valuables kama za Oleg .
Lakini humuhumu CIA bwana Ames taratibu alianza kuinuka tena. Baada ya kurudi kutoka mexico kikazi akiambatana na mchepuko wake Rosario dupuy, waliamua kuanzisha makazi mapya huko falls church , Virginia katikati ya vitongoji vya Washington 1983. Kutokana na rekodi ya kazini kuwa mbovu , hususan umalaya na pombe alipandishwa cheo akawa mkuu wa idara ya counter-intelligence ndani ya CIA. Baadaye Rosa alikubali kuolewa naye baada ya kuona mzee baba kapanda cheo. Hatimaye akapata credit card mpya akatumia kununulia fanicha za $5000 .. na kulipa bili ya simu ya mkewe huyo kwa mwezi kama $400. Kwa mshahara wa $45000 kwa mwaka na hayo matumizi ni kwamba usingemtosha hata kidogo. Kwa kifupi huyu Ames alikuwa na uhitaji mkubwa wa fedha za matanuzi na mkewe huyu mpya.
Ni kwamba kipindi hiki boss mpya wa CIA chini ya utawala wa Ronald Reagan alikuwa bill Casey.Huyu Casey alikuwa amepandikiza baadhi ya majasusi ndani ya Russia aliokuwa ana operate nao kupata taarifa za Soviet. Ames alikuwa anajua identity ya baadhi ya hao maagent waliopandikizwa ndani ya Russia. Kwa mfano Ames alikuwa anajua taarifa kwamba Kuna watu walioko huko Russia wanafuatilia treni zilizokuwa zinasafirisha nuclear warheads kupitia reli ya trans-siberia huko mashariki mwa Urusi. Na kubwa zaidi Ames alikuwa na info kwamba shirika la M16 wanajasusi wao ndani ya KGB anayewapa informations za urusi lakini uingereza wanaficha identity yake ................... .......... Zaidi bwana Ames alikuwa broke na alihitaji pesa ..... [emoji848].
Ngoja turudi huku uingereza kidogo
Mwishowe M16 waliona ni busara kumshirikisha Margaret thatcher kwenye case ya file la NOCTON. Ikawa swala la NOCTON linajulikana na wanasiasa watatu pekee uingereza kwa wakati huo yaani P.M . Thatcher, mshauri wake na private secretary wake pekee .
Tarehe 23 December 1982 M16 Walimpa Margaret thatcher file la NOCTON ,hii ni kutokana na thamani ya taarifa nyeti za Siri alizokuwa anatoa bwana Oleg. Hii ni baada ya miezi sita tokea Oleg atue hapo uingereza kikazi kama afisa wa ubalozi wa Soviet hapo London. Ni kwamba Margret thatcher aliambiwa na maafisa wa ngazi za juu wa M16 kuwa Wana agent wao special ndani ya KGB kwenye ubalozi wa Soviet hapo London. Lakini hakuambiwa jina lake ni nani kuepusha leakage . Maana wanasiasa ni ropo ropo muda wowote anaweza ropoka.
Upande wa pili ingawaje Oleg na ushirikiano wake na M16 ulikuwa unanoga ,huku ubalozini kwake kulikuwa kwa moto.. waliosema huwezi kuwatumikia mabwana wawili hawakukosea.
Guk balozi na msaidizi wake walianza kumtilia wasiwasi Oleg na ikaanza vitimbi.
Kwa mfano mara ya kwanza baada ya Oleg kutua hapo ubalozini Hawakumpenda . Hii ni kwa sababu Oleg alikuwa smart muda wote hakuwa mnywa vodka kama wao halafu alikuwa anaonyesha umagharibi umagharibi Fulani hivi ambao wenzake hawakumwelewa . Kwa mfano hafla zilizofanyika hapo ubalozini ,yeye Oleg alikuwa na ule u gentle man wakuwamiminia watu vinywaji ,na hata chakula chake alipendelea kula sandwiches na matunda na kingine vijisikukuu vya mashujaa wa huko Russia hakuvizingatia kivile kama wenzake ,na pombe aliyokuwa anaitumia ni wine tu. Sasa bwana Oleg akawa anasemwa kiaina na wenzake kwamba huyu mwenzetu vipi haeleweki.
Oleg alijua yaliyokuwa yanaendelea nyuma ya mgongo wake. Kwa kifupi Oleg umaarufu wake ulikuwa unaporomoka kwa Kasi sana. Hii ni kutokana na ubize wake kuwa feed M16 taarifa za kiintelijensia . Kumbuka kila mfanyakazi au afisa wa ubalozi lazima kunakuwa na annual report kumhusu yeye ambayo Huwa inatumwa huko Moscow. Swala likawa linamtatanisha Oleg Je what if atarudishwa nyumbani kutokana na poor performance kazini?.
M16 wakaona ni busara kuongeza reputation ya Oleg kazini kwa kucheza mchezo mmoja . Maana ikitokea akarudishwa Moscow haraka au kubadilishwa kituo Cha kazi nje ya. Uingereza itawagharimu wao.
Ni kwamba kutokana na info za kijasusi waliopenyezewa na oleg wakaona kikwazo kikubwa ni Igor titov boss wa Oleg ambaye ndio alikuwa balozi wa Russia . M16 waliamua kumuondoa . Magazeti ya uingereza yakaandika na kumtuhumu titov kwamba anajihusisha na maswala ya ujasusi nchini humo. Mamlaka ya serikali ikachukua hatua na ikamfukuza pamoja na maafisa kadhaa wa Russia walioko nchini humo. Na baadaye maafisa wengi kwenye nchi mbalimbali za magharibi zikatimua baadhi ya maafisa wa Soviet. Hii ikatengeneza njia kwa Oleg kuendelea kupanda rank Kwa maana ilitarajiwa angechukua nafasi ya titov. Ila nafasi ya titov akapewa arkadi guk na yeye akawa deputy. Mpaka katikati ya mwaka 1983 Oleg umaarufu wake uliongezeka maradufu ndani ya ubalozi huo. Na hii haikuzua wasiwasi wowote. Hatimaye akawa na access ya taarifa nyeti za kiintelijensia . Oleg alikuwa na kila sababu ya kuwa na ujasiri . Kwa maana Sasa hata information anazotoa zinatua Moja kwa Moja kwa Margaret thatcher. Lakini biblia ilishasema adhaniaye amesimama na aangalie asianguke[emoji3578][emoji3578][emoji3578]
Mwezi April 1983 ,bwana Arkadi guk balozi wa Soviet wakati anarudi kwenye makazi yake mtaa wa 42 Holland Park, alikuta barua imeachwa kwenye sanduku la posta la nyumba hiyo . Hii barua ilikuwa ni ya top secret mwandishi akitaka kushirikiana na urusi na kuwapa info za sababu za titov kufukuzwa uingereza na pia contact number za yeye kupatikana na mwisho wa barua ilisainiwa Koba.
Nini nani huyu anayejiita Koba?
Shusha madini kamanda....