Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

Code:
3. Urusi imekuwa defeated.

AJABU NDIYE ALIYEFANYA UMAFIA WA KUMUWEKA DONALD TRUMP MADARAKANI!.
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Trump hakupandikizwa na Russia. Sema Russia alimuunga mkono akiamini Trump ni dhaifu ukilinganisha na Hilary Clinton. Hivyo Russia alijaribu tu kuingilia mifumo ya uchaguzi ili kumsaidia Trump. Trump hawezi kuwa kibaraka wa Russia hata kutekwa!
 
Trump hakupandikizwa na Russia. Sema Russia alimuunga mkono akiamini Trump ni dhaifu ukilinganisha na Hilary Clinton. Hivyo Russia alijaribu tu kuingilia mifumo ya uchaguzi ili kumsaidia Trump. Trump hawezi kuwa kibaraka wa Russia hata kutekwa!
Lego lilifeli au lilifanikiwa? Kama lilifanikiwa kiintelijensia tunaita pandikizi.
 
Trump hakupandikizwa na Russia. Sema Russia alimuunga mkono akiamini Trump ni dhaifu ukilinganisha na Hilary Clinton. Hivyo Russia alijaribu tu kuingilia mifumo ya uchaguzi ili kumsaidia Trump. Trump hawezi kuwa kibaraka wa Russia hata kutekwa!
Code:
Hivyo Russia alijaribu tu kuingilia mifumo ya uchaguzi ili kumsaidia Trump

Kwanza hapo situkwamba arijaribu kuingilia mifumo,bali ni aliingilia na kufanikisha kumuweka Trump madarakani.
Lakini pia suala la Trump kuwa ni pandikizi au siyo pandikizi wa Urusi,bado ni CODE ambayo haijafunguliwa na haiwezi funguliwa hii leo mapema hivi.Uwenda vizazi vijavyo huko mbele wakafunguliwa CODE hizo na suala likiwa wazi.
Turudi kwenye ishu ya KGB tukilinganisha na mashirika mengine.Baadhi ya wadau wanaona kupitia Oleg kuwa KGB ni wachovu ukilinganisha na CIA na M16 kwa tukio hilo la kisaliti katika miaka hiyo 85 na huku wakiendelea kuamini hivyo mpaka leo.
Sasa swali linakuja kuwa,ni vipi KGB wachovu waweze kuingilia mifumo ya uchaguzi na wafanikiwe dhidi ya CIA wasio wadhaifu ukilinganisha na KGB?.[emoji16][emoji38][emoji28]
 
36

Rumours kuhusiana na kutoweka kwa bwana Jasusi zilianza kusambaa sana ndani ya corridor za makao makuu ya KGB kwenye jengo la lubyanka. Idara ya directorate K ambao walikuwa na jukumu la kumfuatilia Oleg kila mahali waliamini kwamba lazima atakuwa yupo Russia , either amelewa na kufa ,au labda kajiua na kujitupa mtoni. Msako ulianza kwenye maeneo ya mito na maziwa yaliopo jiji la Moscow. Maafisa wengine wakasema labda alitoroka kupitia Iran kwa kutumia passport feki. Nae bwana Budanov akasema atakuwa labda amejichimbia mahali kwenye safe house za uingereza. Mkewe , Leila alifuatwa huko kwa baba yake alikokuwa kwenye mapumziko kwenye fukwe za bahari ya Caspian Hadi kwenye gereza la lefortovo kwa mahojiano zaidi..... Swali alilokuwa akiulizwa mara kwa mara ni MUMEO YUKO WAPI. Lakini huyu mwanamama hakuweza kujibu zaidi aliwaambia kama nyie hamjui afisa wenu Yuko wapi ,basi Mimi sijui alipo huku akilia. Baadaye huyu mama alipokuja kuambiwa na hao wanaomhoji, kwamba mumewe alikuwa anafanya kazi na waingereza hakuamini hizo stori na alikataa katu.
Oleg alishawahi mwambia asiamini lolote atakaloambiwa kuhusiana na yeye [emoji28].
Kiufupi watu wengi waliokuwa na uhusiano wowote wa karibu na Oleg hapo Moscow walihojiwa intensively lakini bado haikujulikana haswa yupo wapi Hadi muda huo...,......

Siku ya jumatatu ,Oleg(Mr. Hanssen muda huo akiwa London) alijikuta yupo kwenye ukumbi wa south ormsby hall kwenye mji mdogo wa Lincolnshire akiwa ameandaliwa hafla fupi ya kumpongeza kama mgeni wa heshima. Hakutegemea kutokana na uchovu aliokuwa nao . Aliwauliza maafisa wa M16 kama anaweza kupiga simu kwa mkewe lakini hawakukubali kutokana na kwamba ingewapa alert KGB.ilikuwa ni mapema sana
Oleg alipelekwa kuhifadhiwa kwenye ngome Moja iliyoitwa fort Monckton kama safe house iliyopo kitongoji Cha Gosport . Na safehouse hii iliitwa Military Training Establishment. .iMTE. Pia ilitumika kama kambi ya mafunzo kwa majasusi wa M16. Hapo alipewa debriefings za hapa na pale na kupewa treatment za hadhi ya juu. Lakini hakusita kuuliza kuhusiana na familia yake . Eneo Hilo la fort Monckton lilikuwa linalindwa maradufu na mara ya kwanza haikuwa rahisi kumtambua huyu mgeni ni nani haswa kwa baadhi ya maafisa wengine wa M16. Lakini baadaye walikuja kumtambua ni nani huyu mgeni mpya waliyenaye.na alipewa jina la uficho la OVATION.
Kutoka SUNBEAM, NOCTON , PIMLICO Sasa ni OVATION. Kwa upande wa CIA wao walimtambua kama TICKLE [emoji28][emoji28].
Case ya Oleg ikawa imeingia rasmi kwenye phase nyingine. Kutokana na information alizowapa mashirika ya kijasusi ya nchi za west, zilisaidia sana kuepusha vita vya nuclear baina ya Soviet na west. Pia info hizi za Oleg zilisaidia kuwafichua Maafisa wa ngazi za juu wa kisiasa waliokuwa serikalini ambao walikuwa kwenye payroll za KGB wakiuza Siri.
M16 wakaanza kujiuliza maswali, Je wawaambie CIA na washirika wengine kuhusiana na hii operation ilivyofanyika na kufanikiwa? Au waitishe vyombo vya habari kwa ajili ya hii taarifa? Na Je baada ya mambo kutokea juu uhusiano wa uingereza na Russia utakuwaje? Uhusiano wa Thatcher na Mikhail Gorbachev utakuwaje? Na kingine M16 Walilopaswa kulifanyia kazi ni familia ya Oleg . Mkewe Leila na watoto wake . Haya maswali M16 Walikuwa wanajiuliza
Baadaye kupitia afisa mmoja wa KGB aliyeitwa vitaly virchenko aliyekuwa anatoa info kwa CIA ,aliwatonya kwamba Kuna jasusi wa KGB anayehusishwa kuifanyia kazi M16 yupo under house arrest akisubiri kesi yake itafikia wapi aliyeitwa Oleg . CIA kwakuwa walimjua kama tickle ,wakawapa info M16. Kupitia hii info M16 walituma maafisa wawili Hadi kwa bill Casey marekani kwenda kumpa A to Z ya Oleg Hadi kutoroshwa kwake. CIA walishangazwa na hizi taarifa zilipotuwa mezani kwao.
Bwana Casey aliamua kufunga safari Hadi fort Monckton kuonana na hii ASSET mpya ya M16 waliyokuwa nayo Ili kupata new infos za Russia kuhusiana na vita baridi na pia kutoa shukran zake binafsi kwa Oleg Kutokana na nondo zake alizokuwa anatoa kwa nchi za west na kuepusha uwezekano wa kutokea vita.... likapita
Miezi kadhaa baadaye Oleg alisafiri Hadi marekani chini ya ulinzi mkali ,Ili kufanya mkutano wa Siri na maafisa wa ngazi za juu wa Baraza kuu la usalama wa taifa la marekani . Maswali yote aliyoulizwa alijibu kwa ufasaha kuhusiana na Russia. Na pia alienda Hadi Langley makao makuu ya CIA kukutana na maafisa wa ngazi za juu wa kitengo kwa ajili ya kikao nao. Alipewa heshima zote alizopaswa kupewa na mambo mengine yakaendelea.....
Kipengele kikawa ni familia yake.
Kwakuwa M16 wanajua baadhi ya maafisa wote wa KGB wanofanya kazi under official diplomatic cover , waliamua kumtokea afisa mmoja wa KGB ambaye alikuwa ni mshauri kwenye maswala ya kisayansi kwenye ubalozi wa Soviet kwenye Jiji la Paris ufaransa. M16 Walimpa ujumbe wa Siri utumwe Hadi Moscow kuhusiana na kuiachilia familia ya Oleg. Mke na watoto wake. Ujumbe ulikuwa unawataka Soviet waiachilie familia la sivyo maafisa wote wa KGB London watimuliwe . Ilikuwa ni ultimatum kwa Russia na walikuwa na wiki mbili za kujibu. Huu ujumbe haukusema kama Oleg yupo uingereza au la .
Huku mkewe Oleg aliendelea kubananishwa kwenye geraza la lefortovo na maswali kuhusiana na alipo mumewe . Wanawe wakiwa shuleni walikuwa chini ya uangalizi wa KGB.Pia rafiki yake Oleg bwana lyubimov naye alitiwa ndani kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na alipo mwamba . Majibu ni Yale Yale . Hakuna aliyejua alipo. Kwa kifupi hili sakata liliwatia watu wengi lockup. Je wapi alipo Oleg?
Mke wa Oleg alipoona maswali yanazidi aliwatolea uvivu waliokuwa wanamhoji na kuwaambia . Nanukuu " Look. Let's be clear. I was a wife. My job was to clean,cook ,shop ,sleep with him, have children ,share the bed and be his friend. I was good at it. I'm grateful he didn't tell me anything. For six years ....I was a perfect wife. I did everything for him . You , the KGB, you have thousands of people with salaries whose job was to check up on people . They checked him and cleared him .. And you come to me and blame me ?. Don't you think that sounds stupid? You didn't do your job. It wasn't my job,it yours. You ruined My life".. Huyu mama alikuwa sahihi.

Ujumbe wa siri wa Ultimatum ulipowafikia KGB kuhusu kuiachilia hii familia Lakini wakatia ngumu wakisema huyo ni msaliti na familia yake lazima ibaki Russia.
Ujumbe huu uliporudi uingereza kwa M16 ,wakaamua kuujibu kibabe zaidi.
Ofisi ya wizara ya mambo ya nje wakaamua kutoa info kwa media kuhusiana na Oleg kutoroka Russia,ila info haikuwa na maelezo ya Zaidi kuhusiana na kutoroka huko. Magazeti ya uingereza kama kawaida Yao vichwa vya habari vikawa kama ifuatavyo.. " The biggest fish ever Netted",[emoji28][emoji28][emoji28] lingine likaandika " Friend Oleg, Master Spy" , lingine likasema " Russia's Ace of spy ;the Super-spy who went West". Lingine likaandika kwa mbwembwe "Our Man in KGB"[emoji38]. Na haikupita muda tokea taarifa kwa umma itoke , serikali ya uingereza ikatimua maafisa Zaidi ya ishirini wa Russia Waondoke ndani ya masaa 48.
Nao Russia wakaamua kufukuza maafisa wote wa uingereza waliokuwa wakifanya kazi Soviet ikiwemo akina Arthur gee na mwezake Ascot ambao walimtorosha Oleg.
Ndani ya KGB wakubwa walianza kutupiana Mpira wa lawama . Kila kitengo ndani ya KGB kilitupa lawama kwa mwenzake kutokana na aibu hii ya mwaka kuhusu Oleg aliyewatoroka . Maafisa wote wa KGB kwenye Jiji la Leningrad walilaumiwa pia kutokana na uzembe walioonyesha mpaka jamaa akawatoroka kizembe. Wengi wa maafisa walifukuzwa kazi au kusimamishwa . Na hili varangati lilimkuta Hadi Vladimir Putin akiwa afisa wa KGB kwenye mji wa Leningrad . Wengi wa maafisa wenzake walitimuliwa .
Kutokana na aibu hii KGB wakaamua kutunga uongo kwa ajili ya kuihabarisha umma wa raia kwamba Oleg alitekwa na kutoroshwa na sio kwamba alitoroka mwenyewe kama inavyodaiwa[emoji28][emoji28][emoji28].
Siku mbili baadaye rasmi sasa maafisa wa uingereza kwenye msafara wa magari nane waliondoka Russia chini ya conyoy ya KGB kwenye ulinzi mkali kupitia mpaka wa Vyborg Hadi nchini finland.

Hatimaye tarehe 14 November 1985 kwenye mahakama ya kijeshi ilimkuta Oleg na hatia alisomewa mashtaka ya uhaini na kuhukumiwa KIFO in absentia.
Mwaka 1986 Oleg alialikwa na Margaret thatcher kwenye makazi yake kwa ajili ya pongezi[emoji3578][emoji3578][emoji108]. Na mwaka huo huo Oleg alikutana na Ronald Reagan kwenye oval office marekani..
Huko Russia mke wa Oleg aliendelea kushikiliwa under house arrest kwa kisasi na KGB asije kutoroka kama mumewe.[emoji28][emoji3578]. Pia KGB walimwambia Leila endapo akitoa tamko la kuachana na Oleg au talaka Mali zake atarudishiwa zilizokuwa zimeshikiliwa .
Miaka sita ya mivutano kati ya Russia na uingereza kuhusiana na hii familia ya Oleg iliendelea. Uingereza ilitumia nchi washirika kuishinikiza Russia iachilie hiyo familia. Hata thatcher alipokutana na Gorbachev mwaka 1987 ,bado waliendelea kukaza.
Hatimaye ilipotimia 6 September 1991 Russia waliamua kuiachilia familia hii ya Oleg na kusafirishwa Hadi Heathrow London Kisha wakapelekwa na helcopter Hadi fort Monckton Oleg akiwa anawasubiri kwa hamu. Walifanyiwa homecoming ya kutosha . It was an emotional moment.
Miezi mitatu baadaye muungano wa umoja wa nchi za kisoviet ukavunjika RASMI.
Watoto wa Oleg waliendelea masomo shuleni na hawakutumia jina la Gordievsky kamwe .
Na mwaka 1993 Oleg na mkewe walivunja uhusiano wao wa ndoa RASMI. .......
Dah vipi Aldrich yeye ilikuwaje?
 
Inawezekana huu uzi ndio umekwisha, shukrani kubwa kwa mleta mada kwa jinsi alivyojitahidi kuleta episodes mfululizo hadi kuleta raha kufatilia.

My take kuhusu huu uzi, kwa njia moja ama nyingine mimi au wewe msomaji unaweza kuingia mazingira ya watu fulani, kampuni ficho za kijasusi kukutumia kwa fedha kuuza taarifa nyeti za nchi kutoka na wadhifa wako. Usidhubutu kutoa ushirikiano hata chembe, usaliti kwa ardhi uliyotwaliwa ni laana kwako na kizazi chako lakini ikitokea idara za usalama zikaja kushtuka utalipia gharama kubwa wewe na familia yako yote.

Ni vizuri kubakia na somo hili maana hii habari ya Oleg imempa ushujaa na pengine kuishi kama executive citizen wa UK na kuleta ushawishi wa kuwa double agent [emoji23] lakini pengine hatujafikiria kiwango cha damage aliyofanya kwa Taifa lake hadi leo. Oleg kusaidia kuepusha vita ya nyuklia inawezekana ni kachumbari tu ila hiyo vita iliepukwa na mambo mengi wakati ule.

Nimeona niangalie kwa jicho tofauti hasa somo nyuma hii stori.
 
Inawezekana huu uzi ndio umekwisha, shukrani kubwa kwa mleta mada kwa jinsi alivyojitahidi kuleta episodes mfululizo hadi kuleta raha kufatilia.

My take kuhusu huu uzi, kwa njia moja ama nyingine mimi au wewe msomaji unaweza kuingia mazingira ya watu fulani, kampuni ficho za kijasusi kukutumia kwa fedha kuuza taarifa nyeti za nchi kutoka na wadhifa wako. Usidhubutu kutoa ushirikiano hata chembe, usaliti kwa ardhi uliyotwaliwa ni laana kwako na kizazi chako lakini ikitokea idara za usalama zikaja kushtuka utalipia gharama kubwa wewe na familia yako yote.

Ni vizuri kubakia na somo hili maana hii habari ya Oleg imempa ushujaa na pengine kuishi kama executive citizen wa UK na kuleta ushawishi wa kuwa double agent [emoji23] lakini pengine hatujafikiria kiwango cha damage aliyofanya kwa Taifa lake hadi leo. Oleg kusaidia kuepusha vita ya nyuklia inawezekana ni kachumbari tu ila hiyo vita iliepukwa na mambo mengi wakati ule.

Nimeona niangalie kwa jicho tofauti hasa somo nyuma hii stori.
Kitasa ndo basi tena?
 
Back
Top Bottom