Tetesi: Tarehe 21/12/2024 Mbowe atatangaza rasmi kutogombea uenyekiti na atamuunga mkono Tundu Lissu

Mpira uko kwa Mbowe sasa, aondoke kwa heshima au aendelee kung'ang'ania madarakani ili AAPUUZWE kama Lipumba, Cheyo, Dovutwa na wengineo.
 
Atakuwa fala yaani uondokewe kwenye nafasi Kwa shinikizo tena baada ya kudhalilishwa?

Ningekuwa Mimi Bora nishindwe kwenye kura,huo sio ukamanda ni udhaifu 🤣🤣👇👇

View: https://x.com/VisitTanzania1/status/1869806482067468715?t=LlaES2D-6mc03txvubLHQA&s=19
 
Good move, niliwaambia mapema kuwa Mbowe na Lissu hawajakutana barabarani.

 
Unaweza kumtetea tajiri kwa kumtukana mshindani wake, tajiri akakushangaza siku ukiwakuta wako meza moja na uliyemtukana kwa niaba yake wanakula bia na kucheka😄
Duh, kuwa na kiwango Cha maneno muhimu
 
Habari zaidi zinasema mh Mbowe ataelekeza nguvu zake zote kuunganisha wanaCHADEMA wote ili kuing'oa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu wa 2025.
Akifanya hivi, heshima yake iliyo anza kumegeka itasimama.
Lakini ni vigumu sana kwake sasa kujiondoa moja kwa moja kwenye mtego ulio kuwa umemnasa. Kila atakalo fanya watu watatazama vitendo na maneno yake kuhakikisha hakuna ukoko ulio salia unaoweza kuchafua juhudi za CHADEMA chini ya uongozi mpya.
 
Unaleta habari nyeti, unafanya pre empty kutuliza wanaomuunga mkono lissu au unawaanda kisaikolojia wanaotaka mbowe aendelee kuwa mwenyekiti? Au una balansi tension za pande mbili ambazo ndani ya saa 48 zinatimbana? Basi hii tetesi iwe kweli
 
mkuu, hapo ulipo agiza chochote (sio kilevi) Nita-clear bill. wanipe lipa namba.

JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Habari zaidi zinasema mh Mbowe ataelekeza nguvu zake zote kuunganisha wanaCHADEMA wote ili kuing'oa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu wa 2025.
 
chadema imeshaingia kwenye mioyo ya watu wengi kama chama chenye uwezekano wa kuwa mbadala wa CCM bila kujali kuwa chama kiliundiwa kaskazini wala kuongozwa na wa kaskazini.
 
Habari za uhakika kabisa kutoka ndani ya familia ya Freeman Mbowe ni kwamba amekubali ushauri wa wanafamilia na wazee wa CHADEMA kutogombea uenyekiti wa CHADEMA na badala yake atakikabidhi chama kwa Lissu.


Habari zaidi zinasema mh Mbowe ataelekeza nguvu zake zote kuunganisha wanaCHADEMA wote ili kuing'oa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu wa 2025.

Yote sawa, atapitishwa, lakini Lisu aache kabisa KUROPOKA.

MGEMA AKISIFI TEMBO HULITIA MAJI NDICHO ANACHOFANYA LISU.

LAZIMA KUWA NA KABA YA ULIMI

ANAROPOKA SANA. HAFAI KUWA KIONGOZI WA JUU
 
Sasa yale maigizo pale kwake yalitoka wapi?
Pamoja na ule usanii lakini bado nadhani ktk siku 2 hz alizojipa kutafakari bila shaka atakuwa ameona na kujiridhisha wanachadema walio wengi wanataka nn!!.
Ni dhahiri tulio wengi tunataka kijiti apewe Lissu, huyu ndio kiboko cha ccm hii ya kihuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…