Tetesi: Tarehe 21/12/2024 Mbowe atatangaza rasmi kutogombea uenyekiti na atamuunga mkono Tundu Lissu

Tetesi: Tarehe 21/12/2024 Mbowe atatangaza rasmi kutogombea uenyekiti na atamuunga mkono Tundu Lissu

Wasalaam

Habari za uhakika kabisa kutoka ndani ya familia ya Freeman Mbowe ni kwamba amekubali ushauri wa wanafamilia na wazee wa CHADEMA kutogombea uenyekiti wa CHADEMA na badala yake atakikabidhi chama kwa Lissu.

Habari zaidi zinasema mh Mbowe ataelekeza nguvu zake zote kuunganisha wanaCHADEMA wote ili kuing'oa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu wa 2025.

Hivyo wale wote mliokua mnategemea CHADEMA ipasuke na kuvugana imekula kwenu.
Atakuwa fala yaani uondokewe kwenye nafasi Kwa shinikizo tena baada ya kudhalilishwa?

Ningekuwa Mimi Bora nishindwe kwenye kura,huo sio ukamanda ni udhaifu 🤣🤣👇👇

View: https://x.com/VisitTanzania1/status/1869806482067468715?t=LlaES2D-6mc03txvubLHQA&s=19
 
Good move, niliwaambia mapema kuwa Mbowe na Lissu hawajakutana barabarani.

Unaweza kumtetea tajiri kwa kumtukana mshindani wake, tajiri akakushangaza siku ukiwakuta wako meza moja na uliyemtukana kwa niaba yake wanakula bia na kucheka😄
Duh, kuwa na kiwango Cha maneno muhimu
 
Habari zaidi zinasema mh Mbowe ataelekeza nguvu zake zote kuunganisha wanaCHADEMA wote ili kuing'oa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu wa 2025.
Akifanya hivi, heshima yake iliyo anza kumegeka itasimama.
Lakini ni vigumu sana kwake sasa kujiondoa moja kwa moja kwenye mtego ulio kuwa umemnasa. Kila atakalo fanya watu watatazama vitendo na maneno yake kuhakikisha hakuna ukoko ulio salia unaoweza kuchafua juhudi za CHADEMA chini ya uongozi mpya.
 
Unaleta habari nyeti, unafanya pre empty kutuliza wanaomuunga mkono lissu au unawaanda kisaikolojia wanaotaka mbowe aendelee kuwa mwenyekiti? Au una balansi tension za pande mbili ambazo ndani ya saa 48 zinatimbana? Basi hii tetesi iwe kweli
 
Huo ndio uamuzi pekee wa HEKIMA na BUSARA alionao sasa...

Nje ya hapo, anakwenda kudhalilika bila sababu za msingi....

Achilia mbali kushinda uchaguzi iwapo atagombea, lakini hata ikitokea amegombea na akashinda, uongozi wake awamu hii utakuwa mgumu sana....

Na kwa maamuzi yake ya kuendelea, ajue tu kuwa ata - demoralize kundi kubwa la wana CHADEMA, wapenzi (nikiwemo mimi) na mashabiki wa chama hiki...

Kwa kifupi atabaki na watu haohao waliokuja kwake jana kumwaga sumu dhidi ya mpinzani wake Tundu Lissu...

Miaka ya 2009, 2014 na 2019 tulimtetea kweli aendelee kuwa mwenyekiti kwa sababu hakukuwa na mtu sahihi wa kuvaa viatu vyake...

Mwaka huu 2024, mtu sahihi, makini na mwenye misimamo thabiti pengine kuliko yeye amepatikana na karibu dunia nzima inasema HUYU NDIYE MTU SAHIHI KUKALIA KITI HICHO...

Please, ndugu Freeman Mbowe pumzika kwa amani na kwa heshima zote huku ukiwa umekiacha chama kikiwa imara bila lawama tena mikononi mwa mtu sahihi kabisa Mh Tundu Lissu...

Na afahamu tu, Tundu Lissu hawezi ku back down hii vita kirahisi. Watapambana hadi dakika ya mwisho na wasipokuwa makini watararuana na kuacha makovu makubwa chamani na kutibika kwake itachukua miaka kadhaa...

Freeman Mbowe aache kujisifu kupita kiasi hata kujiona yeye ni CHADEMA na CHADEMA ni yeye. Dhana hii ni hatari sana...
mkuu, hapo ulipo agiza chochote (sio kilevi) Nita-clear bill. wanipe lipa namba.

JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Yatakuwa maamuzi Bora kuwai kufanya toka nimeanza kufatilia siasa

Hawa?

GfKa9V3W0AAG_j9.jpeg

Too good to be true!
 
Wasalaam

Habari za uhakika kabisa kutoka ndani ya familia ya Freeman Mbowe ni kwamba amekubali ushauri wa wanafamilia na wazee wa CHADEMA kutogombea uenyekiti wa CHADEMA na badala yake atakikabidhi chama kwa Lissu.

Habari zaidi zinasema mh Mbowe ataelekeza nguvu zake zote kuunganisha wanaCHADEMA wote ili kuing'oa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu wa 2025.

Hivyo wale wote mliokua mnategemea CHADEMA ipasuke na kuvugana imekula kwenu.
Habari zaidi zinasema mh Mbowe ataelekeza nguvu zake zote kuunganisha wanaCHADEMA wote ili kuing'oa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu wa 2025.
 
Akifanya uamuzi huo tutamuheshimu sana, kwani hadi sasa tunaukubali uwezo wake uliokifikisha chama hapo kilipo, lakini tusingependa yeye atuhakikishie kuwa tulichokiamini siku zote kupitia siasa za chadema na taifa kwa ujumla, sicho alichokiamini...

chadema imeshaingia kwenye mioyo ya watu wengi kama chama chenye uwezekano wa kuwa mbadala wa CCM bila kujali kuwa chama kiliundiwa kaskazini wala kuongozwa na wa kaskazini.

Mbowe amwachie TAL hatamwangusha maana wengi tunaikubali misimamo yake na hatuna shaka atatupeleka mbele katika mustakabali wa siasa za nchi hii. People's power ifufuke upya kwa damu mpya katika uongozi wa juu wa chama.

Tunakuomba Mh. Freeman A. Mbowe mwachie Lissu hata kama itakuumiza nafsi ila tutakuheshimu daima.
chadema imeshaingia kwenye mioyo ya watu wengi kama chama chenye uwezekano wa kuwa mbadala wa CCM bila kujali kuwa chama kiliundiwa kaskazini wala kuongozwa na wa kaskazini.
 
Habari za uhakika kabisa kutoka ndani ya familia ya Freeman Mbowe ni kwamba amekubali ushauri wa wanafamilia na wazee wa CHADEMA kutogombea uenyekiti wa CHADEMA na badala yake atakikabidhi chama kwa Lissu.

Habari zaidi zinasema mh Mbowe ataelekeza nguvu zake zote kuunganisha wanaCHADEMA wote ili kuing'oa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu wa 2025.

Yote sawa, atapitishwa, lakini Lisu aache kabisa KUROPOKA.

MGEMA AKISIFI TEMBO HULITIA MAJI NDICHO ANACHOFANYA LISU.

LAZIMA KUWA NA KABA YA ULIMI

ANAROPOKA SANA. HAFAI KUWA KIONGOZI WA JUU
 
Sasa yale maigizo pale kwake yalitoka wapi?
Pamoja na ule usanii lakini bado nadhani ktk siku 2 hz alizojipa kutafakari bila shaka atakuwa ameona na kujiridhisha wanachadema walio wengi wanataka nn!!.
Ni dhahiri tulio wengi tunataka kijiti apewe Lissu, huyu ndio kiboko cha ccm hii ya kihuni.
 
Back
Top Bottom