Huo ndio uamuzi pekee wa HEKIMA na BUSARA alionao sasa...
Nje ya hapo, anakwenda kudhalilika bila sababu za msingi....
Achilia mbali kushinda uchaguzi iwapo atagombea, lakini hata ikitokea amegombea na akashinda, uongozi wake awamu hii utakuwa mgumu sana....
Na kwa maamuzi yake ya kuendelea, ajue tu kuwa ata - demoralize kundi kubwa la wana CHADEMA, wapenzi (nikiwemo mimi) na mashabiki wa chama hiki...
Kwa kifupi atabaki na watu haohao waliokuja kwake jana kumwaga sumu dhidi ya mpinzani wake Tundu Lissu...
Miaka ya 2009, 2014 na 2019 tulimtetea kweli aendelee kuwa mwenyekiti kwa sababu hakukuwa na mtu sahihi wa kuvaa viatu vyake...
Mwaka huu 2024, mtu sahihi, makini na mwenye misimamo thabiti pengine kuliko yeye amepatikana na karibu dunia nzima inasema HUYU NDIYE MTU SAHIHI KUKALIA KITI HICHO...
Please, ndugu Freeman Mbowe pumzika kwa amani na kwa heshima zote huku ukiwa umekiacha chama kikiwa imara bila lawama tena mikononi mwa mtu sahihi kabisa Mh Tundu Lissu...
Na afahamu tu, Tundu Lissu hawezi ku back down hii vita kirahisi. Watapambana hadi dakika ya mwisho na wasipokuwa makini watararuana na kuacha makovu makubwa chamani na kutibika kwake itachukua miaka kadhaa...
Freeman Mbowe aache kujisifu kupita kiasi hata kujiona yeye ni CHADEMA na CHADEMA ni yeye. Dhana hii ni hatari sana...