Pole kwa mkasa wa vyeti Feki! Haya yameefanyika kwa maslahi makubwa ya Taifa. Tunashukuru JPM ametuingiza uchumi wa kati ameusimamia vyema wakati wa korona hata waliokumbele yetu kwa mbali kwa sasa wanatuonea wivu, njia aliyochukua juu ya COVID-19 Dunia yote inafuata. Waliosema tusifanye kazi tujifungie kwa kuwa kuna korona leo wanakusanya watu bila aibu! Sidhani kama kuna haki. Kodi na maduhuli ya Serikali yanalipwa vyema sasa kuliko wakati mwingine, lipa hata elfu tatu tu ya umeme moja kwa moja kwenye akaunti kupitia GePG ya Serikali! Lazima achukiwe na wachumia tumbo wote, na amekubali kujitoa kwa ajili yetu,tano tena aendelee kujenga Nchi!