Kwangu mimi tarehe 28/10/2020 itakuwa ni siku ambayo mfanowe ni tarehe 9/12/1961 tulipopata uhuru na hivyo kujinusuru kutoka mikononi mwa wakoloni weupe waliotukalia kwa miaka karibu 40!
Ninayo matumaini makubwa kuwa siku hiyo tutapata uhuru tena na kuweza kujinusuru kutoka mikononi mwa hawa wakoloni wetu weusi, CCM waliotukalia kwa miaka zaidi ya hiyo 40!
Wengine tunajua kwa nini Magufuli, akiwa hana uwezo, alisukumiziwa utawala wa taifa hili kwa sifa kuu tatu...ujeuri wake, uthubutu wake na uzoefu wake ndani ya tawala zilizomtangulia.
Tahadhari.
Kwa kiongozi mwenye huruma, busara na hekima, anayejali, mfadhili, mtulivu na msikivu, sifa hizi ni kichocheo cha utawala imara na wa maono unaozingatia sheria na katiba, utawala usioyumbishwa katika kutoa haki na utawala usiosita kukiri kosa na kujirekebisha.
Kwa kiongozi asiye na huruma, busara wala hekima, asiyejali, mkatili, anayekurupuka na mwenye kiburi, sifa hizi ni kichocheo cha utawala wa kifashisti na mateso, utawala usioheshimu sheria na Katiba, utawala unaobagua katika utoaji wa haki na utawala usiopenda kukosolewa.
Je kwa sasa tuko wapi?
Mengi yamesemwa na hivyo sitakuwa na haja ya kuyarudia isipokuwa kuhusu moja tu, ufisadi. Kwa miaka mingi ufisadi umekuwa ukidaiwa kupigwa vita, je leo tunaweza kujidai tumeutokomeza ufisadi nchini?
Jibu langu ni hapana, ufisadi haukutokomezwa na badala yake, chini ya Magufuli, aina mpya ya ufisadi ambayo ni mbaya kuliko wa awali uliandaliwa, ukalelewa, ukakua na sasa matunda yake yanavunwa
Ni ufisadi gani huo?
Ni ufisadi wa serikali. Ufisadi huu unaolitafuna taifa sasa hivi ni ule unaoendeshwa na vyombo vya dola vya serikali ikisimamiwa na kiongozi wake mkuu. Wafanya kazi, wakulima, wafanya biashara na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) wote ni waathirika wa ufisadi huu.
Serikali ikiwa ndiyo fisadi mkuu imeamua kuvitumia vyombo vya dola na idara za serikali kuyafisadi makundi haya. Wafanya kazi wanayimwa haki zao, wakulima wanadhulumiwa mazao yao, wafanya biashara wananyang'anywa pesa zao na NGOs kuzuiwa pesa zao.
Hebu fikiria, wote waliowahi kutuhumiwa kwa ufisadi huko nyuma wamekaribishwa ndani ya CCM, chama kinachoongoza serikali na wote wamerudi. Wengi wa watuhumiwa hawa wameteuliwa kugombea ubunge na walioachwa wanaahidiwa ajira kwenye hizi kampeni.
CCM imeamua rasmi kwamba UFISADI ndio sera yake. Ufisadi wa sasa ni state sponsored na vyombo kama TRA, TCRA, TAKUKURU na idara za serikali vimegeuka na kuwa vya unyang'anyi katika mpango kabambe wa kuwafilisi raia wa nchi hii wasiokubaliana na uovu huu.
Magufuli ameweza kufanikisha yote haya kwa ujeuri wa kutisha, uthubutu wa kutisha na uzoefu wa miaka zaidi ya ishirini. Kumbukeni kile alichoapa siku chache baada ya kutangazwa mshindi kwamba wastaafu wasiwe na hofu, walale bila wasiwasi kwani atawalinda.
Na sasa anapita akitaka aongezewe awamu ya pili, kweli! Hapana, Mh. Tundu Antiphas Lissu, njoo uliokoe taifa lako linaloangamia!