Uchaguzi 2020 Tarehe 28/10/2020: Siku ya kuweka Historia kuu Tanzania

Uchaguzi 2020 Tarehe 28/10/2020: Siku ya kuweka Historia kuu Tanzania

Inawezekana ikawa watanzania walishafanya maamuzi tangu 2010 sema maamuzi yao hayakuheshimiwa. Lazima njia za wizi zitambulike na zizuiwe 100%
Mwaka huu watanzania wameshasema wanapiiga kura na kuzilinda kituoni. Matokeo yote kuanzia udiwani, ubunge hadi uraisi wanachukua kituoni. Full stop.
 
Acha tu! Mie Kuna dogo ninamfahamu hadi amerudi kijijini. Hana ajira tangu amalize chuo mwaka 2015. CCM hawastahili hata kupewa tena mwezi mmoja baada ya October 2020!
Shida wajinga ndio uchagua hatma ya wengi
 
Acha tu! Mie Kuna dogo ninamfahamu hadi amerudi kijijini. Hana ajira tangu amalize chuo mwaka 2015. CCM hawastahili hata kupewa tena mwezi mmoja baada ya October 2020!
Shida wajinga ndio uchagua hatma ya wengi
 
Ila Meko hali yake ni mbaya sana. Kwenye mikutano iliyo mingi anaonekana kukosa furaha. Mara nyingi anaonekana mnyonge na mwenye kutumia nguvu kubwa wakati anapozungumza.
 
Ila Meko hali yake ni mbaya sana. Kwenye mikutano iliyo mingi anaonekana kukosa furaha. Mara nyingi anaonekana mnyonge na mwenye kutumia nguvu kubwa wakati anapozungumza.
Matokeo ya udhalimu siku zote sio mazuri. Huwezi kufanya udhalimu kuanzia kwa watu wa Chama chako, wapinzani hadi watanzania wengine alafu ukabaki salama.

Mwaka huu hapo October Meko anaanza kupigwa ana CCM wenyewe alafu watanzania tunaanua matanga!!

Huyu jamaa kawatesa kina Kinana, Makamba, Kikwete na kuwanyanyasa Kama watoto, ons yaliyowatokea kina Lissu na wabunge wa upibzani. Ona yaliyowatokea wafanyabiashara, kwa kifupi tu atapata support ya Nani huyu mtu???
 
ARUSHA, TANZANIA

PART 2 ;MDAHALO WA MGOMBEA WA CHADEMA NA CCM NGAZI YA KATA ;MZOZO MKALI HATUGOMBANI

 
Mpaka wanyama wameshaitambua siku hii muhimu sana
IMG-20200919-WA0086.jpg
 
UKAWA ikiongozwa na Mzee Lowassa 2015 angalau walionyesha nia na uwezo na kukaribia "penalt box" ya CCM. Mwaka huu mpira unachezewa nusu uwanja huku mlinda goli wa CCM akiwa hajagusa hata mpira! Lissu akipata hata 20% ya kula zote nashauri apewe Ubunge wa kuteuliwa!
..jifunze kuandika kwanza ....pia jaribu kutoonesha kila mtu namna ubongo wako umejaa tope , jaribu kuwa mkimya itakusaidia
 
Sio mara zote
Sasa Kama unakuta mtu hata uwezo wa kununua ndala Hana lkn anachagua ccm anashangilia kununuliwaa kwa ndege Hali yeye na ukoo wake wote hata ukiwauza hawana hata nauli ya kufika airport,Sasa Hawa wapo wangapi.Ccm inategemea kura za vijijini kwenye Giza.
 
19 September 2020
Arusha , Tanzania

MDAHALO WA LEO : LIVE / MUBASHARA
Makada wa CHADEMA na CCM wanashindanisha hoja za vyama vyao ili kuwezesha wagombea wao wa Urais, ubunge na udiwani 2020 kupata kura

LISU NI NABII AMELETWA / HAKUNA WA KUMFANANISHA MAGUFULI

 
Kwangu mimi tarehe 28/10/2020 itakuwa ni siku ambayo mfanowe ni tarehe 9/12/1961 tulipopata uhuru na hivyo kujinusuru kutoka mikononi mwa wakoloni weupe waliotukalia kwa miaka karibu 40!

Ninayo matumaini makubwa kuwa siku hiyo tutapata uhuru tena na kuweza kujinusuru kutoka mikononi mwa hawa wakoloni wetu weusi, CCM waliotukalia kwa miaka zaidi ya hiyo 40!

Wengine tunajua kwa nini Magufuli, akiwa hana uwezo, alisukumiziwa utawala wa taifa hili kwa sifa kuu tatu...ujeuri wake, uthubutu wake na uzoefu wake ndani ya tawala zilizomtangulia.

Tahadhari.

Kwa kiongozi mwenye huruma, busara na hekima, anayejali, mfadhili, mtulivu na msikivu, sifa hizi ni kichocheo cha utawala imara na wa maono unaozingatia sheria na katiba, utawala usioyumbishwa katika kutoa haki na utawala usiosita kukiri kosa na kujirekebisha.

Kwa kiongozi asiye na huruma, busara wala hekima, asiyejali, mkatili, anayekurupuka na mwenye kiburi, sifa hizi ni kichocheo cha utawala wa kifashisti na mateso, utawala usioheshimu sheria na Katiba, utawala unaobagua katika utoaji wa haki na utawala usiopenda kukosolewa.

Je kwa sasa tuko wapi?

Mengi yamesemwa na hivyo sitakuwa na haja ya kuyarudia isipokuwa kuhusu moja tu, ufisadi. Kwa miaka mingi ufisadi umekuwa ukidaiwa kupigwa vita, je leo tunaweza kujidai tumeutokomeza ufisadi nchini?

Jibu langu ni hapana, ufisadi haukutokomezwa na badala yake, chini ya Magufuli, aina mpya ya ufisadi ambayo ni mbaya kuliko wa awali uliandaliwa, ukalelewa, ukakua na sasa matunda yake yanavunwa

Ni ufisadi gani huo?

Ni ufisadi wa serikali. Ufisadi huu unaolitafuna taifa sasa hivi ni ule unaoendeshwa na vyombo vya dola vya serikali ikisimamiwa na kiongozi wake mkuu. Wafanya kazi, wakulima, wafanya biashara na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) wote ni waathirika wa ufisadi huu.

Serikali ikiwa ndiyo fisadi mkuu imeamua kuvitumia vyombo vya dola na idara za serikali kuyafisadi makundi haya. Wafanya kazi wanayimwa haki zao, wakulima wanadhulumiwa mazao yao, wafanya biashara wananyang'anywa pesa zao na NGOs kuzuiwa pesa zao.

Hebu fikiria, wote waliowahi kutuhumiwa kwa ufisadi huko nyuma wamekaribishwa ndani ya CCM, chama kinachoongoza serikali na wote wamerudi. Wengi wa watuhumiwa hawa wameteuliwa kugombea ubunge na walioachwa wanaahidiwa ajira kwenye hizi kampeni.

CCM imeamua rasmi kwamba UFISADI ndio sera yake. Ufisadi wa sasa ni state sponsored na vyombo kama TRA, TCRA, TAKUKURU na idara za serikali vimegeuka na kuwa vya unyang'anyi katika mpango kabambe wa kuwafilisi raia wa nchi hii wasiokubaliana na uovu huu.

Magufuli ameweza kufanikisha yote haya kwa ujeuri wa kutisha, uthubutu wa kutisha na uzoefu wa miaka zaidi ya ishirini. Kumbukeni kile alichoapa siku chache baada ya kutangazwa mshindi kwamba wastaafu wasiwe na hofu, walale bila wasiwasi kwani atawalinda.

Na sasa anapita akitaka aongezewe awamu ya pili, kweli! Hapana, Mh. Tundu Antiphas Lissu, njoo uliokoe taifa lako linaloangamia!
Mwaka huu kitaeleweka
 
Mkuu
Uzuri Magu hadi CCM wenyewe hawamtaki. Naskia kuna operesheni kabambe kushikana uchawi huko CCM sasaivi😂😂😂😂😂

Mkuu mbona sioni sababu ya Trump kuipiga marufuku ,App ya Tilk talk
Eti anadai inachukua taarifa za watumiaji, huku watumiaji wanadai hawana taarifa
 
Back
Top Bottom