Handeni, Tanga
Tanzania
MGOMBEA UBUNGE CHADEMA AAHIDI BIMA ZA AFYA
Mgombea ubunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA) jimbo la Handeni mjini mkoani Tanga, Andrew Stima,ameahidi endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atawatafutia bima ya afya walemavu na wagonjwa wa akili ili kuweza kupata tiba kwani kundi hilo limesahaurika.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika Viwanja vya Handeni Square,mgombea huyo amesema kuwa,katika makundi ambayo yamesahaurika katika kupata huduma bora za afya,ni kundi la walemavu na wagonjwa wa akili hivyo akipata fursa ya kuwa mbunge atahakikisha analisaidia kundi hilo.
Katibu wa Chadema mkoa wa Tanga Gervas Msigwa amewataka wananchi kupima viongozi kwa sera zao na sio umaarufu wa majina majina yao kwani kwa kufanya hivyo,wanaweza kurudi nyuma kimaendeleo kwa kuanza moja kila mhula wa uchaguzi kuchagua tena kiongozi mwingine
Aidha katibu Chadema jimbo la Handeni Vijijini Ramia Kisalazo amesema wananchi wanatakiwa kujitokeza kupiga kura kwa manufaa yao na familia zao,kwani yeyote ambae hata piga amekubali kuchaguliwa kiongozi,kitu ambacho sio sahihi.