Uchaguzi 2020 Tarehe 28/10/2020: Siku ya kuweka Historia kuu Tanzania

Na wajinga ni mashabiki wakubwa wa ccm, sijui itakuwaje sasa

Sasa sijui wajinga ni kina nani, Chadema na wanao chagua M'kiti, Katibu Mkuu, Naibu katibu Mkuu na mgombea mwenza vilaza. Wajanja wanaongozwa na wajinga, Washika taa hawaoni. Poleni sana.

Wasomi wote katika uongozi wamewakimbia. Na safari hii huyo mnaemwita mshamba ndio atakae teketeza Chadema na upinzani kwa ujumla.

Na CCM yenye viongozi wajinga ndio itatawala miaka 100 ijayo. Vipanga wa CCM Oyeeeeee.
 
Tuwahamishe watu wakapige kura kwa nguvu hapo October mwaka huu ili Tanzania iweke historia mpya mwaka huu
Nimejifunza mengi sana kwenye mkutano fulani mh.lisu watu wako kimya ila wana mengi moyoni nimewaona hata wana ccm ninawafahamu wamemuelewa lisu.tuombe Mungu maana huyu Mungu ni wa wote
 
Hizo zote propoganda. hakuna kosa kubwa kama kumchaguwa mtu mwenye ghadhabu kama Tundu Lissu. Kwanza si mstaarabu. Domo lake limejaa matusi siku zote. Hata sasa hivu yuko kwenye shida kwa kuzuiliwa kutoa matusi, ndiyo maana anapwaya. Mimi na pamoja wengine tumotoka mbali na kuona mengi. Enzi zetu za sekondari tulikuwa trunadhania kumchaguwa mtu mtukutu na asiyesikia ya waalimu ndiyo kunatupa kiranja wa upande wetu.

Lakini ikitokea kumchaguwa kaka wa namna hiyo anageuka mbogo na kutoa vibano kwa wanafunzi. Huyu Lissu hata kabla hajapewa kura tayari ana dharau na majivuno. Nilisikia siku moja akisema yeye mtoto wake hasomi sekondari za kijinga za TZ. Akiingia madarakani ujuwe ndiyo basi elimu itakufa. Hivi Lissu ana uchungu gani na TZ. Uanaharakati na siasa ni vitu mbalimbali. Wanaharakati siku zote ni kutafuta mabaya ya nchi na kuficha mazuri ili agenda yao itimie.

Hao ni watu ambaohugharimiwa na mabeberu , kwa hiyo wakipata pesa wanaambiwa nini cha kutafuta na nam,na ya kukitafuta. Uana harakati ni ajira, ajira kutoka kwa wenye pesa kwenda kwa wenye njaa kama Lissu. Kwa vile uuanaharakati unalipiwa kwa $$$ ndiyo maana unaona watu wanaspiga kelele karibu mishipa ya shingo kupasuka.Do not and never trust mwanaharakati Tundu Lissu.
 
Watz wameshasema hapana..... Hawataki tena dikteta na mharibifu wa uchumi wa nchi na watu wake... magufuli na ccm yake iliyooza na kunuka mtaani
 
Kule mnakoshinda wanayaharibu matokeo kwa kuvipa vyama vileee number isiyokuwepo.

Utaona DP 5%, ADC 7%, NCCR 6%, CHAUMA 10% , ACT 30% ,CCM 15%, Chadema 27%,

Halafu mnabaki mmeduwaa.
 
Kule mnakoshinda wanayaharibu matokeo kwa kuvipa vyama vileee number isiyokuwepo.
Utaona DP 5%, ADC 7%, NCCR 6%, CHAUMA 10% , ACT 30% ,CCM 15%, Chadema 27%,
Halafu mnabaki mmeduwaa.
Nguvu ya umma itaamua mwaka huu!!
 
Lissu ana ghadhabu gani?? Embu fafanua??? Sie kama watanzania tulimsikia akiwa kanisani singida akitoa shukrani alisema hatolipa kisasi kamwe kwa yeyote aliyemfanyia mabaya.

Ni matusi gani pia aliyotukana Lissu??? Embu fafanua???

Ni lini Lissu alisema mtoto wake hawezi kusoma shule za Africa??? Alafu kwa mfumo wa Elimu wa a Tanzania unafikiri unawapa elimu bora watoto wa masikini wa Tanzania kwenye karne hii ya sayansi na teknolojia???
 
Nimejifunza mengi sana kwenye mkutano fulani mh.lisu watu wako kimya ila wana mengi moyoni nimewaona hata wana ccm ninawafahamu wamemuelewa lisu.tuombe Mungu maana huyu Mungu ni wa wote
Kweli kabisa. Watanzania wana maamuzi magumu ya kufanya mwaka huu. Na wahasishwe zaidi wasiogope wala kusita kufanya maamuzi magumu mwaka huu!!
 
Kwangu mimi tarehe 28/10/2020 itakuwa ni siku ambayo mfanowe ni tarehe 9/12/1961 tulipopata uhuru na hivyo kujinusuru kutoka mikononi mwa wakoloni weupe waliotukalia kwa miaka karibu 40!

Ninayo matumaini makubwa kuwa siku hiyo tutapata uhuru tena na kuweza kujinusuru kutoka mikononi mwa hawa wakoloni wetu weusi, CCM waliotukalia kwa miaka zaidi ya hiyo 40!

Wengine tunajua kwa nini Magufuli, akiwa hana uwezo, alisukumiziwa utawala wa taifa hili kwa sifa kuu tatu...ujeuri wake, uthubutu wake na uzoefu wake ndani ya tawala zilizomtangulia.

Tahadhari.

Kwa kiongozi mwenye huruma, busara na hekima, anayejali, mfadhili, mtulivu na msikivu, sifa hizi ni kichocheo cha utawala imara na wa maono unaozingatia sheria na katiba, utawala usioyumbishwa katika kutoa haki na utawala usiosita kukiri kosa na kujirekebisha.

Kwa kiongozi asiye na huruma, busara wala hekima, asiyejali, mkatili, anayekurupuka na mwenye kiburi, sifa hizi ni kichocheo cha utawala wa kifashisti na mateso, utawala usioheshimu sheria na Katiba, utawala unaobagua katika utoaji wa haki na utawala usiopenda kukosolewa.

Je kwa sasa tuko wapi?

Mengi yamesemwa na hivyo sitakuwa na haja ya kuyarudia isipokuwa kuhusu moja tu, ufisadi. Kwa miaka mingi ufisadi umekuwa ukidaiwa kupigwa vita, je leo tunaweza kujidai tumeutokomeza ufisadi nchini?

Jibu langu ni hapana, ufisadi haukutokomezwa na badala yake, chini ya Magufuli, aina mpya ya ufisadi ambayo ni mbaya kuliko wa awali uliandaliwa, ukalelewa, ukakua na sasa matunda yake yanavunwa

Ni ufisadi gani huo?

Ni ufisadi wa serikali. Ufisadi huu unaolitafuna taifa sasa hivi ni ule unaoendeshwa na vyombo vya dola vya serikali ikisimamiwa na kiongozi wake mkuu. Wafanya kazi, wakulima, wafanya biashara na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) wote ni waathirika wa ufisadi huu.

Serikali ikiwa ndiyo fisadi mkuu imeamua kuvitumia vyombo vya dola na idara za serikali kuyafisadi makundi haya. Wafanya kazi wanayimwa haki zao, wakulima wanadhulumiwa mazao yao, wafanya biashara wananyang'anywa pesa zao na NGOs kuzuiwa pesa zao.

Hebu fikiria, wote waliowahi kutuhumiwa kwa ufisadi huko nyuma wamekaribishwa ndani ya CCM, chama kinachoongoza serikali na wote wamerudi. Wengi wa watuhumiwa hawa wameteuliwa kugombea ubunge na walioachwa wanaahidiwa ajira kwenye hizi kampeni.

CCM imeamua rasmi kwamba UFISADI ndio sera yake. Ufisadi wa sasa ni state sponsored na vyombo kama TRA, TCRA, TAKUKURU na idara za serikali vimegeuka na kuwa vya unyang'anyi katika mpango kabambe wa kuwafilisi raia wa nchi hii wasiokubaliana na uovu huu.

Magufuli ameweza kufanikisha yote haya kwa ujeuri wa kutisha, uthubutu wa kutisha na uzoefu wa miaka zaidi ya ishirini. Kumbukeni kile alichoapa siku chache baada ya kutangazwa mshindi kwamba wastaafu wasiwe na hofu, walale bila wasiwasi kwani atawalinda.

Na sasa anapita akitaka aongezewe awamu ya pili, kweli! Hapana, Mh. Tundu Antiphas Lissu, njoo uliokoe taifa lako linaloangamia!
 
Nipo kahama hapa submarine panatoka macontainer ya kupogia kura kila siku chadema fuatilieni na kuna watu waccm wanakaa hapa akiwemo kishimba aliyekuwa mbunge wa sasa wa ccm embu fuatilieni mujihakikishie
 
Hilo halina mjadala
 
Mkuu andiko limeenda shule. Asante sana na Mungu akubariki
 
Nipo kahama hapa submarine panatoka macontainer ya kupogia kura kila siku chadema fuatilieni na kuna watu waccm wanakaa hapa akiwemo kishimba aliyekuwa mbunge wa sasa wa ccm embu fuatilieni mujihakikishie
Jiitahidi utuletre na kaphoto tuwanyoshe hawa. Dawa yao ni timing
 
Ni kweli kabisa ndugu! Kuna unyang’anyi mkubwa sana unaendelea sasaivi Tanzania dhidi ya watanzania unaofanywa na TAKUKURU, TRA,TCRA na DPP
 
Umma huu usiutegemee kabisa, Mnakubaliana wanakukimbia.
Kwa mfano niliouona kwenye kura za maoni za wajumbe wa Ccm mwaka huu, Nina imani kwa asilimia 100 kuna historia kuu lazima iandikwe mwaka huu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…