Utakuwa mjinga wa kupindukia kuamini kuwa unaweza kuibadilisha hali hiyo hiyo kwa kuoiga kura wakati huna chaguo. Wanaoteka na kuua ndiyo wagombea pekee waliosalia, kwa kuwapa kura hao hao wauaji, unabafili nini? Use your brain ili uone ulichopungukiwa.
Fikiria kuwa serikali na chama kinachoteka na kuua watu, kiongozi wake ni Samia, na Samia ndiye mgombea pekee, akisindikizwa na wagombea wa vyama bandia vilivyoanzishwa na CCM, kama una akili timamu, utawezaje kusema uende kupiga kura kama njia ya kuondoa utekaji na mauaji ya watu, kwa kwenda kumpigia mgombea yule yule anayeruhusu huo utekaji na mauaji? Hapo unaenda kupiga kura kuleta mabadiliko au unaenda kubariki utrkaji na mauaji yaendelee?
Mzee Butiku na Warioba ni watu wenye heshima kubwa nchi hii, na uzakendo wao hauna mashaka. Wamekemea utekaji na mauaji, wanajua kuwa haki hiyo ili kuweza kuiondoa kwa njia ya amani ni uchaguzi ulio huru na wa haki, ndiyo maana wakitamko wazi kuwa kufanyike mabadiliko na maekebisho kwenye sheria, Tume ya uchaguzi na mfumo mzima wa uchaguzi. Watekaji na wauaji kwa vile ndio wente mamlaka, wameyagomea hayo mambo yote. Wamekataa na kuzuia wagomvea kutoka chama cha upinzani, kama una akili tumamu, unaenda kwenye huo uchaguzi ili ukafanye nini, wakati mgomvea ni mmoja tu? Hivi una uwezo wa kuchagua kama una kitu kimoja tu?