Tarehe 29 Oktoba, piga kura yako mapema na nenda nyumbani

Kuna msemo unasema za mwizi ni 40
 
Mtu mzima hovyo!!!
 
Umeiweka vizuri sana. Ni bora kukaa nyumbani kuliko kwenda kubariki ufisadi, ujambazi, utekaji, ma mauaji na uuzaji hovyo na kuhamisha wa mali na rasilimali za Tanganyika kwa miaka mitano ijayo kwenda kwa Samia, Abdul, JK na Rostam na genge la wahuni.
 
Mkuu kupiga kura ni pamoja na kurekebisha makosa yaliyptokea kwa kuonyesha kikatiba unayemchagua.
Watanzania lazima tuwe na civics literacy!
 
Haya mambo ya busara kwa sasa hayatakiwi ni kweli uchaguzi ni mara 1 kwa miaka mitano swali ni kwamba?

Kwa nn? Maamuzi ya wananchi hayapewe heshima yake . Watu wanachagua kiongozi A tunapewa kiongozi B
 
Samia na wahuni wenzie kina Rostam Aziz hawatoboi ...mwisho wa samia na wenzie umesha halibika ....hao wahuni awatakuwa na pakukimbilia duniani .... wamesha bugi step
 
Mkuu kupiga kura ni pamoja na kurekebisha makosa yaliyptokea kwa kuonyesha kikatiba unayemchagua.
Watanzania lazima tuwe na civics literacy!
Mfumo mzima wa uchaguzi ni mbovu, washindani halisi ndani ya chama na nje ya chama wamefungiwa. Hii ni coronation, sherere za kumsimika Malkia wa za Tanganyika akisaidiwa na jeshi. Polisi, usalama, na Tume.

Ukiwa mkweli wa moyo wako. Hakuna matakwa ya Wananchi yaliyozingatiwa kuchagua watu wanaowataka. Wanalazimishwa ma Samia ili aseme ana uhalali, nchi imemchagua. Kumbe hata CCM haijamchagua.
 
Utakuwa mjinga wa kupindukia kuamini kuwa unaweza kuibadilisha hali hiyo kwa kupiga kura wakati huna chaguo. Wanaoteka na kuua ndiyo wagombea pekee waliosalia, kwa kuwapa kura hao hao wauaji, unabadili nini? Use your brain ili uone ulichopungukiwa.

Fikiria kuwa serikali na chama kinachoteka na kuua watu, kiongozi wake ni Samia, na Samia ndiye mgombea pekee, akisindikizwa na wagombea wa vyama bandia vilivyoanzishwa na CCM, kama una akili timamu, utawezaje kusema uende kupiga kura kama njia ya kuondoa utekaji na mauaji ya watu, kwa kwenda kumpigia mgombea yule yule anayeruhusu huo utekaji na mauaji? Hapo unaenda kupiga kura kuleta mabadiliko au unaenda kubariki utekaji na mauaji viendelee?

Mzee Butiku na Warioba ni watu wenye heshima kubwa nchi hii, na uzalendo wao hauna mashaka. Wamekemea utekaji na mauaji, wanajua kuwa hali hiyo ili kuweza kuiondoa kwa njia ya amani na kikatiba, ni uchaguzi ulio huru na wa haki, ndiyo maana wakatoa tamko la wazi kuwa kufanyike mabadiliko na marekebisho kwenye sheria za uchaguzi, Tume ya uchaguzi na mfumo mzima wa uchaguzi. Watekaji na wauaji kwa vile ndio wenye mamlaka, na hawataki kuacha ushetani wanaoufanya, wameyagomea hayo mambo yote. Wamekataa na kuzuia wagombea kutoka chama cha upinzani. Kama una akili timamu, unaenda kwenye huo uchaguzi ili ukafanye nini, wakati mgombea ni mmoja tu? Hivi una uwezo wa kuchagua kama una kitu kimoja tu?
 
Hujasema mbadala wako ni upi, kama ni kuandamana, halafu baada ya kuandamana itakuwa ndo unapata kiongozi mpya?
Unampataje katika maandamano?
Tujifunze civics na kuelewa kuwa mtu hudai haki tu lakini una wajibu wa kikatiba vile vile.
 
Nitakachofanya mimi ni juu yangu cha msingi ni kwamba usinishauri cha kufanya tarehe 29 kiwe cha tofauti au sio.
Fanya haki yako ya kikatiba nenda katulie kwako.
Mtavunjwa miguu ,vibaya sana , ila hakuna shida mwamposa anaombea miguu itarudi🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…