Tarehe 9-12-1961 ilikukuta wapi?

Tarehe 9-12-1961 ilikukuta wapi?

Ni kweli kabisa mkuu, Enzi hizo kulikuwa na nidhamu na watu wanafuata sheria kweli kweli
Ila leo unajenga unavyotaka
Unaweza kukuta mtu anajenga kukwepa jua lisimchome asubuhi, na mwingine anaamua kuweka ukuta kwenye dirisha la jirani na bwana ardhi hana ubavu maana kapewa hela

Sasa hali inazidi kuwa mbaya siku hadi siku na kuna watu wengi wanaona sawa tu
Sheria hazifuatwi ni virugu tu sio nchi tena limekuwa soko
Nidhamu haiachi njia yake,sema walikuwa waoga. Ingekua nidhamu halisi tusingefika huku.
 
Heri ya siku ya uhuru wadau.

Nikikumbuka siku ya tarehe 09/12/1961 naona ni kama juzi tu kumbe ni miaka kibao imepita.

Nakumbuka siku hiyo tulivyochinja mbuzi nyumbani kusherekea uhuru, nakumbuka mvua kubwa ilivyonyesha mpaka kusababisha maji kujaa ziwa Victoria kupita kingo zake.

Kweli wakati ni ukuta.

Mkuu unakumbuka nini siku hii?
itakua mmebaki wachache tu nchini right?
 
Nje ya mada kidg
Kizazi hiki kimeshindwa kabisa kujenga nyumba kwa mpangilio ukicheki hapo juu nyumba za matope zimekaa kwa mstari
Kizazi kilichopita ama vilivyopita kukilaumu kizazi cha leo si sahihi,ni sawa na kumnyooshea mtu kidole kimoja ili hali vidole vinne vinakusonta wewe. kizazi ch leo kimetokana na kizazi kilichopita. Kama kilichopita ni kizazi kibovu automatically kinachofata nacho ni kibovu, hizo lawama hazina mantiki ila chain yake ni ndefu.
 
Nilikuwa na miaka mitatu tayari.
Kuna mdau kule juu alisema kama kuna uzi utajaa uongo basi ni huu, mie nakumbuka tulifanya sherehe kubwa sana kule kijijini kwetu, ni kumbukumbu isiyofutika miongoni mwa watanzania wengi tuliopo leo na tuliokuwepo ile siku
 
Back
Top Bottom