Tarehe kama ya leo Yanga SC iligomea mchezo, kwa madai Simba SC kuvaa viatu vya mpira

Timu iliokua inacheza na yanga ni simba au sunderland???
 
Mkuu ikifika ile Tarehe ambayo Mikia walitia mpira kwapani Timu zilipoenda mapumziko match ya Yanga,nishtue.
 
Naam...Wakati wakisubiri kichapo Septemba 30, tuwarejeshe yaliyofichika.
Usisahau na ile Tarehe mliyotia mpira kwapani mapumziko Shamba la Bibi. Na pia ukumbuke Mikia haijawahi kuifunga wala kutoa draw na Yanga match yoyote iliyochezwa September.
 
Usisahau na ile Tarehe mliyotia mpira kwapani mapumziko Shamba la Bibi. Na pia ukumbuke Mikia haijawahi kuifunga wala kutoa draw na Yanga match yoyote iliyochezwa September.
Ha ha ha. Endelea kucheza kwa ramli mkuu

Kikosi gani safari hii cha kufanya hivyo?

Hata hivyo umeandika hali una wasiwasi kuona kuwa zile 5 zitarejea!
 
Ha ha ha. Endelea kucheza kwa ramli mkuu

Kikosi gani safari hii cha kufanya hivyo?

Hata hivyo umeandika hali una wasiwasi kuona kuwa zile 5 zitarejea!
Mkuu nasikia kambi mmeweka Kinyerezi,Mo amegona kutoa hela amekasirika kawapeleka Turkey lakini hakuna lolote la maana mlilorudi nalo.
 
Mkuu nasikia kambi mmeweka Kinyerezi,Mo amegona kutoa hela amekasirika kawapeleka Turkey lakini hakuna lolote la maana mlilorudi nalo.
Hivi mkuu.. Uliona wapi Real Madrid anakwenda Dubai kuweka kambi kujiandaa na Barcelona?

Tumeacha hayo mambo, tunajiamini kukufunga hata tuweke kambi mtaa wa Twiga Kariakoo.
 
Jibu swali wacha kurukaruka, hiyo ilikuwa Simba au Sunderland?
Nimejibu kuwa Simba. Wakati huo ikiitwa Sunderland..

Au hujui kuwa kabla ya kuitwa Simba ilikuwa ikiitwa Sunderland?
 
Yaani timu ianzishwe mwaka 1935 alafu mwaka 1953 hawana viatu hakika wewe shabiki wa mbumbu FC.
 
Yaani timu ianzishwe mwaka 1935 alafu mwaka 1953 hawana viatu hakika wewe shabiki wa mbumbu FC.
Timu ya Taifa ilicheza vifua wazi bila jezi mbele ya Rais wa Sudan na Mwalimu Nyerere uwanja wa Uhuru Julai 4, 1972.

Inakuwaje unashangaa klabu kukosa viatu kwa wakati huo. Ndo maana niaona nyie Vyura wengine hamjui chochote kwenye soka la Tanzania

Chukua hiyo utoe utandu au tongotongo kutoka bwawani, na kama unajiona Kinda, basi acha kubisha usilolijua

Makwasukwasu FC wewe!
 
Bila picha au ushahidi wa video clip,kakojoe ukalale..
 
Mwaka 72 Shida ilikua jezi zimefanana na mwenyeji ikaonekana busara avue jez, wacheze tumbo wazi alafu ulikua mchezo wa kirafiki. Baada ya mapumziko zikaletwa jezi nyingine waka zivaa. Kwaiyo ndugu usidanganye watu ukifikiri wote ni mbumbu fc.
 
Tunazungumzia uhaba wa vifaa. Kuwa miaka ya nyuma hakuna, sasa kama jezi zilifanana kwa fikra zako, si kuna jezi ya away na nyumbani.

Si angebadili rangi tu. Tatizo lipo pale pale uhaba wa vifaa vya michezo.

Ikiwa hujui hilo, utajua kweli kwanini mnaitwa Gongowazi? Au Ndala?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…