Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

naona mkuu kama umeeleza kinyume vile maana siku ya 13, 14, 15, ni mtoto wa kike na a 16,17, 18 ni mtoto wa kiume. siju sana lakini kwa uelewa wangu ni huo kwa mwanamke mwenye menstraion cycle 28days
 
Habari za Weekend Wakuu.

Nikiri kwanza kwamba pamoja na kwamba mimi ni mwana ndoa Mzeefu sasa (miaka Minne sio haba) kuna mambo mengi sana naendela kujifunza. Mojawapo ni hili linalohusu namna ya kupata aidh mtoto wa kike au wa kiume. Kama mada hii ilishawahi jadiliwa hapa nitaomba MNIWIE RADHI.

Nimekutana na watu wengi sana wanahangaika sana namna ya kupata watoto kike au wa kiume (yaani hawana tatizo la uzazi bali wana tatizo la kuzaa watoto wa jinsi moja). Inafikia hatua mpaka wengine wanatoka hadi nje ya ndoa kutafuta watoto wa Kiume ambapo baadhi hufanikiwa na pengine kwa bahaiti nzuri tu na wengine hupata watoto wa aina ile ile waliyokimbia kwa wake zao.
Ni hivi karibuni pia Mwanasoka nyota David Beckham kwa mfano ndio amepata mtoto wa Kike baada ya kuwa nao wa kiume watupu watatu.

Swali kwenu ni hili, je ni kweli kuna fomula ya kuamua whether mtoto awe wa kiume au kike? Kama ipo ni ipi hiyo?

Angalizo naomba tujadili katika namna ambayo haitalazimisha mada hii ipelekwe kule chumbani ambako watoto hawaruhusiwi kuingia.

Naomba maoni yenu wadau
 
Ngoja tusubiri madactari wa jf,mseseve uko wapi, mada hiyo tudadafulie
 
Reactions: SG8
haaaaa! Kumbe hii ipo kitabibu zaidi?
ya nasikia ipio kitabibu zaidi, ila wanadai sina uhakika ukivizia ile siku ya 13 ya danger period unatoa kitu cha kiume, ya 14 unatoa cha kike, 15 ni probability
 
ya nasikia ipio kitabibu zaidi, ila wanadai sina uhakika ukivizia ile siku ya 13 ya danger period unatoa kitu cha kiume, ya 14 unatoa cha kike, 15 ni probability

katika Quran tukufu 'Allah' ametoa hukumu juu ya hilo !
 
Kupata mtoto wa kike au wakiume ni probabity na timing. Mkeo siku anayoanza kupata hedhi anza kuhesabu ile kwenu ni siku ya kwanza. Tendo la ndoa kuanzia siku ya 11, 12, na 13 kuna uwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa kike na tarehe 14, 15, 16 na 17 kuna uwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa kiume. Siku ya 14 ndiyo siku ambayo yai lililokomaa hutolewa toka kt kifuko cha mayai (ovulation). Mbegu ya kiume ina XY chromosomes na yai lina XX. Wakati wa kutengeneza mtoto X moja toka kt yai huungana na X au y ya mbegu. Kama x ya mbegu ikiungana na x ya yai ikatoa xx wakike na kama y ikiungana na x ikatoa xy wakiume. Mbegu ya kiume ambayo y ina nguvu zaidi inaogelea haraka na inaishi muda mfupi (siku 2) na ile ambayo x ina uwezo mkubwa wa kuleta mtoto inaogelea taratibu inaishi muda mrefu(siku 3). Yai likitolewa siku ya 14 husafiri na siku 3-4 hufika kt mfuko wa uzazi. Hivyo kama mmedu siku ya 11,12 na13 hukuta mbegu zile zenye uwezo wa kutoa wakike zipo hai na zile za kutoa wakiume zimekufa hivyo mnafyatua wa kike. Na mkifanya kuanzia 14,15, 16, na 17 mbegu zenye uwezo wa kutotoa wa kiume zinaogelea haraka huku zikiacha zile zenye uwezo wa kutotoa wakike(ujanja kuwahi),hivyo mnafyatua wa kiume. Hands off!
 
Reactions: SG8
Hili somo lilikuwa linanisumbua siku zote lakini leo hatimaye nimelielwa sana. Sasa naelewa ni kwanini we have a baby boy as ilikuwa siku ya 16 (naikumbuka vizuri). Asante sana Mkuu kwa ufafanuzi wako
 


ngoja niongezee....

ni kweli mbegu za xx huweza kudumu kwa mda mrefu sana kuliko zile za xy na sababu kubwa n kwamba mbegu za xx huwa ni nzito maana huwa zimebeba sex linked charachers kama vile circle cell, anaemia, baldnes, diabetis nk....so uwezo wa kuogela huwa ni mdogo ila zikifika ndani basi huweza kudumu kwa masaa 72 kuliko zile za xy amabazo zenyewe zina kasi ya ajabu kuogela lakini wezo wa kudumu ni mdogo amabapo zenyewe hudumu kwa masaa 36 tu na baada ya hapo huwa converted kwenda kwenye proetin na hutumika kama chakula.....

maelezo ya mdau hapo juu ni sahihi kabisa juu ya timing juu ya namna ya kupata mtoto wa kiume au wa kike....fatiia hayo maelezo ..kuna mwana jf aliwahi kuelt mada hii hapa nikamweleza na kumfafanunualia na baada ya kufata ushauri sasa ana mtoto wa kike wa miezi 3.....

ikumbukwe kuwa kupata mtoto wa kike/kiume baba ndiye ana uwezo huo maana yeye ana mbegu za aina zote (xx, na xy) so ni muhimi kujua wakati gani unafaa katika kufanika kupata mtoto wa jinsia unayotaka kama maelezo hapo juu yanavysema.....
 
Reactions: SG8
samahani may be i'm out of da topic bt i think u can help me in this....hivi siku unaanza kuhesabu baada ya kumalizza mzunguko au wakati anaanza mzunguko...mfano siku akianza ndo day 1 au siku akimaliza the next 1 ndo day 1....me navyojua akimaliza ndo naanza kuhesabu mzunguko upya bt kuna dada akautingisha kidogo uelewa wangu kwa kuniambia siku wanayoanza hedhi ndo u start to count the day...pliz msaada wakuu
 
Thanx Dr Kingu hata mimi nimejifunza
 
Thanx Dr Kingu hata mimi nimejifunza
Unaona, kumbe tupo wengi eeeh? Nashukuru sana Dr Kingu na Mkuu Edson kwa ufafanuzi. Nilishaanza kukosa mani maana naona hapa nyumbani tunaanza kuulizana eti mbona kijana ana miaka Minne na kwamba sasa hivi tutafute ka mwanamke, nikabaki najiumauma!!!! Nitaleta feedback hapa panapo majaliwa miezi kadhaa ijayo
 
yap yap,mko sahihi kabisaaaaa!!!ila naomba nyongeza kwa faida ya wengine na mimi pia,hayo yote yanawezafanyika kwa ufasaha sana lakini bado mambo yakawa yaleyale,eitha wakike ama wa kiume mwanzo mwisho,huwa inakuwaje hii?
 

Nilikuwa napita tu ila maada imenivutia so naomba niongezee hapa...
Ni kuwa Dr Kingu kaelezea vizuri ila naona kuna sehem kasahau kidogo kuwa hii kwanza ni ngumu kutokea na ndio maana hata yy kaanza na kusema ni probability na huo u probability unasababishwa na vitu kadhaa kwanza wanawake wanatofautiana mizunguko yao ya hedhi wapo wenye mzunguko wa cku 26, 28, 30, 32 n.k hawa si wote wataendana na alivyoelezea dr kingu itategemea na mzunguko wa wanamke. Dr Kingu kaelezea mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28 wnegine akawaacha, kitu kingine ni kuwa ili ufuate hii calculation unahitaji miezi kadhaa kuusoma mzunguko wako we mwanamke kama mzunguko una badilika badilika mwez huu cku 28 mwez mwingine cku 30 hii njia haikufai muombe Mungu akujalie aina ya mtoto unaemtaka lakin kama mzunguko haubadilik unaweza kubahatisha matamanio yako.
Nimalizie, kwanini wanawake ni wengi duniani kuliko wanaume? Dr Kingu kaeleza jinsi mbegu x zilivyo na uwezo wa kuishi siku 3 huku mbegu Y ziiwa na uwezo wa kuishi siku moja tu so ndo maana wanawake ni wengi kuliko wanaume.
Nawakilisha kwa ufupi maana najua yapo mengi ya kuelezea hapa...
 
Jaman habari za saa hizi?mimi nimeolewa nina mwezi wa 7 sasa sijapata mimba na hospitali nimepima sina shida yoyote na mpangilio wa siku naufatilia.naomba wenye ujuzi mnielekeze.asante
 
Pole sana... Japo ni mapema kuwa na wasiwasi, lakini kuwa makini maana wnaweza kutokea madaktari bandia, ukapewa mitishamba hadi ukakoma. Kwa sasa tulia tu, taratibu anza kuulizia taarifa za hospitali za maana, maana matatizo ya uzazi ni complicated mara nyingine.

Lakini mi nawafahamu zaidi ya watu 10 waliokuja kutapa mtoto zaidi ya miaka 5 baada ya kuoana, tena bila msaada wa nadaktari...
 
Mwenzangu yupo vizuri kwa sababu nilishabeba mimba ikatoka tokea hapo ni matatizo.
 
Jaman habari za saa hizi?mimi nimeolewa nina mwezi wa 7 sasa sijapata mimba na hospitali nimepima sina shida yoyote na mpangilio wa siku naufatilia.naomba wenye ujuzi mnielekeze.asante

Mkamia maji hayanywi.
Hebu relax, fanya tendo with confidence, jibinuebinue uwapo kwenye majamboz, kuwa mbunifu, mkalie mzee mikao ya kata funua, jipagawaishe hadi mwenzako apagawe na kupagawa kwako. Mbona mwezi ujao tu mwenyewe unaanza visirani na kutaka udongo, mara chaki mara kichefuchefu na mara nyingine mimba zisivyo na adabu zinaweza kukufanya uzichukie kabisa nguo za ndani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…