Pole sana dada, kuna watu wametoa ushauri mbaya hapa... Wasikukatishe tamaa! Tatizo kama hili lipo sana, kuna ndugu yangu mkewe alikuwa anapata mimba kwashida na baada ya miezi michache inatoka....zilitoka mimba 7 ndani ya miaka 8, uwezi amini mungu alivyo mkubwa mwaka juz alipata mimba baada ya miezi mitatu alikuwa chini ya uangalizi wa daktar, baada ya miez 8 alijifungua vizuri! Ushauri wangu, kwanza undoa hofu kabisa, kama ulibeba mimba ikatoka basi wote mpo fiti, miez saba kitu gani, watu wanakaa miaka kumi bila mtoto, cha muhimu zidisha maombi ww na mumeo labda kuna pepo mchafu! Pili mkamwone daktari wewe na mumeo! Heshimu ndoa yako dada!!!