Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

hivi kwanini watu hawajachangia hadi sahzi et......mi nashangaaaaa!
 
Boy me nafikiri ni ndani ya mwez wa tisa,nimeshawah kusikia mama mjmzto akilalamika kuwa ana mwez wa tisa lakin ngoma bado, so kwa fkra zangu ni katkat ya mwez au wiki ya tatu!!! Ni hayo tu!
 
Guyz.
Mi huwa sielewi miezi halali ambayo mama mjamzito anaishi na mimba.
Hivi huwa anajifungua anapoanza mwezi wa tisa au baada ya kuumaliza mwezi wa tisa?
Please help me.




ni wiki 39 maximum.lakini anaweza kuzaliwa kuanzia wiki ya 36.toka mimba kutungwa
 
Umri halali wa Mimba ni Siku 280.
Yaani Wiki 40 (+ / - 2 weeks)
Kwa hesabu sahihi za hapo juu, ni mwisho wa mwezi wa tisa ndipo unatimiza wiki 40 au siku 280,

Kama mama atajifungua two weeks before basi atakuwa ameiSHI NA miezi nane na wiki 2 (yaani katikati ya mwezi wa tisa wa Mimba)

Kama mama atajifungua two weeks after, basi atakuwa ameishi na mimba Miezi tisa na wiki 2 (hizi wiki mbili ni za mwezi wa kumi)

na Mimba haihesabiwi toka siku uliyojamiiana na kutunga.

Mimba inahesabiwa kuanzia siku ya kwanza uliyoanza ku'bleed, then by 14 days toka siku hiyo ndipo una'consive.

Kwa hiyo ukitoa hizi siku 14 toka umeona siku zako za mwisho, kiuhalisia ujauzito wenyewe toka unaingia hadi unatimiza umri ni wiki 38 kamili, ila ni lazima ujumlishe hizi siku 14 (wiki 2) ili kupata umri kamili wa mima.

Nawasilisha.
 
thanks sasa nimejua maana nilikua nashangaa? sasa nimeelewa vyema
 
2mbo linaanza kuonekana miezi mingapi?
Mimi siyo mtaalamu ila nafikiri pia inachangia na mwili wa mtu wengine matumbo yaanza kuonekana mapema sana hata miezi miwili mitatu utamhisi tayari lakini wengine unapomhisi ndo anakaribia kujifungua.
 
nahitaji kushika mimba nilichoma sindano za uzazi wa mpango mwaka 2010 mbili tu ambazo mwisho wake ulikuwa mwezi wa saba mwaka huohuo lakini sikutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango mpaka leo lakini sijashika mimba hapa inakuwaje madoctorz
 
Je unapata siku zako kama mzunguuko ulivyo? Tangu ulipomaliza yaani mwisho wa sindano,umejaribu vya kutosha kumpata mtoto. Ni vizuri Ma doudou urudi katika thread yako kujibu hoja ili madokta wanapokuja majibu yanakuwa ya uhakika. Mie si dokta lakini toa shaka hilo mbona tatizo lenye ufumbuzi hapa JF.
 

Swali la msingi kuliko yote ni hilo la kupata siku zake, na zipo sawasawa ama hovyohovyo?
 

siku zipo sawa na sijawahi miss hata siku moja
 
Kama umeolewa ningekushauri mshirikiane kwa karibu sana na mume wako. Sio lazima mara zote tatizo liwe kwa mwanamke, kuna nyakati wanaume pia wanaweza kuwa ni/na tatizo katika mchakato mzima wa kurutubisha (fertilize) yai.
 
Ma dou dou unatakiwa kuvuta subra madokta wakija nadhani ufumbuzi utapatikana.
 
siku zipo sawa na sijawahi miss hata siku moja

kama huwezi kujali, hebu weka kalenda yako hapa ya kuanzia January mpaka March,
yaani January ulianza Period lini na kumaliza lini, kwa kwa Feb na March hivyo hivyo, tukusaidie kupata Mimba,

lakini angalizo lazima lizingatiwe kuwa Mwenzio naye yupo sawasawa kwa maana ya mbegu zake zina uwezo wa kutungisha mimba (Japo ni uwanja mpana)
 
Madokta wameshaacha mgomo, nenda tu ukawaone moja kwa moja na mume wako mwende nae!, usitanie tatizo kwa kutaka matibabu ya bure hapa!
 
indano ya aina gani umechoma! zipo za aina nyingi, kama unakumbua weka hapa jibu utapata! pia si kila ufanyapo mapenzi unapata mimba. jaribu kutegeshea mumeo siku ya 12 mapka 16 tangu upate siku zako, utaona majibu haraka. msifanye kila siku kwani mbegu zitakuwa chache na hafifu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…