Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

mpendwa,

tatizo hapo ni hormonal imbalance! (akina riwa wanelewa vizuri).

lakini kiukweli, katika hali ya kawaida, hiyo mimba inayoshika siku ya sita baada ya "kuona mwezi" haipo!

kilicho "possible" kwa huyo ndugu yako ni kuwa alishika mimba huko nyuma kwa "tendo la nyuma zaidi" hapa namaanisha kuwa, kibaolojia, mbegu ya mwanaume inapomwagwa ukeni, hukaa hadi zaidi kidogo ya saa 24 kabla haijafa na ikitokea yai likapevuka kabla hazijafa, basi mama atapata mimba. nina maana kuwa tendo la ndoa laweza kutokea mfano, jumapili usiku saa 23.00 na mtu akashika mimba jumanne usiku saa 22.59 kutokana na mbegu zilizomwagwa jumapili! watoto wa namna hii wengi wao huwa wa kike!

muhimu kuelewa kuwa, linapoingilia kati tatizo la timing imbalance kati ya oegesterone na progesterone, ndo hutokea ovulation ikatokea wakati ukuta wa mji wa mimba (uterus) unabomoka (menstruation discharge)! kwa hiyo fertilization inaweza kutokea huku kukiwa na kiwingu cha hedhi na siku chache baada ya hedhi, mimba ikatunga!

wapendwa, zingatieni kuwa mwanamke ni kiumbe kitakatifu kilichojaa rutuba, ukijihusisha na mwanamke, mkumbuke muumba wako!

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God!
 
Na darasa hujaaje? Watoro wote wanakuja siku hiyo.
Nakumbuka mwalimu wetu alikuwa mdada akaja amelewa siku hiyo.

ha ha ha.....hii topic inapendwa sana....hata mashuleni ikifikia mada ya reproduction hakuna mwanafunzi atakaesinzia siku hiyo.
 
mh! hapo itakuwa mtu kapigwa changa la macho, ingawa pia inawezekana sana mwanamke akapata ujauzito in previous month then akaendelea kubleed kama Riwa alivyosema, so mwambie kwa sasa asikatae ujauzito as long as haikuwa mara yao ya kwanza kufanyana, kama walishafanyana huko nyuma then inawezekana kitu kimewaka so walee mimba kwa sasa mtoto akishazaliwa kama baba anaona kasingiziwa akapime DNA tu, ila kama hamtaki mtoto kwanini mnatiana kavu kavu?
 
Yan hii topic ina wapenzi wengi mashuleni
 
Kuna uwezekano mkubwa wa hapo kwenye 'red'....kifiziolojia, ni impossible mwanamke kupata ujauzito siku ya 6 tangu AANZE hedhi. Hedhi ni mzunguko wa mwezi mzima (inategemea na urefu wa mzunguko wa mwezi lakini ni kuanzia siku 26 - 32), lakini uwe mzunguko mfupi au mrefu...haiwezekani kupata mimba siku ya 6 kwa hali ya kawaida! Siku za hatari ni kuanzia siku ya 11 tangu AANZE hedhi mpaka siku ya 18.

Kuna baadhi ya wanawake huwa wanapata hedhi wakiwa na mimba changa (mwezi wa kwanza au miwili ya mwanzo), japo huwa si nyingi kama ilivyokuwa kawaida, lakini ni rahisi kwa mwanamke kuiconfuse na hedhi ya kawaida kwani huja kipindi kile kile mwanamke huyo anataraji kupata hedhi.

Inawezekana lakini 'is a rare phenomenon' kama kuta za nyumba ya uzazi 'uterus' zitatunza spermatozoa (mbegu za kiume) na kuzitoa taratibu (extended slow reliese) mpaka siku ya 14 (ovulation day) aprox. 8days!! Hence physiologically possible!
 
Elimu hiyo inakuwa 'reliable' kama unafahamu mzunguko wa mpenzio ni wa siku ngapi...maana mzunguko unatofautiana kutokana na urefu wa mzunguko kati ya wanawake. Wanawake wachache wana mzunguko wa siku 21 (mfupi), na wengi wana mzunguko wa kati ya siku 28 hadi 30, wanawake wachache tena huwa na mzunguko wa zaidi ya siku 30 (mrefu).

Hata hivyo...mizunguko yote (mifupi, kawaida, na mirefu) ina matukio mawili makubwa ambayo yanakuwa controlled na mabadiliko ya hormones kwenye mwili wa mwanamke (sitaingia kwenye details za hormones, huitaji sana kujua)..matukio hayo mawili makubwa ni 'Hedhi' - kutoa damu ya hedhi; na 'ovulation' au kutolewa kwa yai la kike, yai hutolewa kati kati ya mzunguko wa mwezi. Yai likitolewa, lina siku 3 au 4 kurutubishwa. Na pia, mbegu za kiume (manii) ikimwagwa ukeni, ina mpka siku 3 za kuwa hai na kuweza kurutubisha yai.

Mfano: Tuchukulie mwanamke mwenye mzunguko wa kawaida (yaani siku 28 hadi 30 tangu kuanza hedhi mpaka hedhi itakayofuatia)...kwa kawaida wanawake wanapata hedhi kwa siku 4 - 7, ukihesabu tangu mwanamke anapoanza kutoa damu ya hedhi, yai litatolewa siku ya 14 au 15. ukijumlisha siku 4 za uwezekano wa kurutubisha yai (inakuwa 18 au 19), na ukitoa siku 3 ambazo mbegu zinakuwa hai ukeni (inakuwa 11 au 12)...Kwa hiyo basi, kwa mwanamke mwenye mzunguko wa kawaida wa siku 28 hadi 30, siku zake za hatari za kushika mimba ni kuwanzia siku 11 tangu aanze hedhi hadi siku ya 19 tangu aanze hedhi!

kwenye red, Yai la mwanamke (binadamu) halikai zaidi ya 24 hrs (siku moja), lisubiri nini?! Only 12-24hrs! Hivyo rekebisha hapo penye red! Baada ya siku ya 15, 48hr after ovulation, sitarajii mtu awe mimbadi! Huwezi kum-mimba baada ya siku ya 15 kwani yai litakuwa limekufa! Hii ni kwa wale wasiotumia majira! Wanaotumia majira wao hawatabiriki!
Inawezekana lakini 'is a rare phenomenon' kama kuta za nyumba ya uzazi 'uterus' zitatunza spermatozoa (mbegu za kiume) na kuzitoa taratibu (extended slow reliese) mpaka siku ya 14 (ovulation day) aprox. 8days!! Hence physiologically possible!
 
mh! hapo itakuwa mtu kapigwa changa la macho, ingawa pia inawezekana sana mwanamke akapata ujauzito in previous month then akaendelea kubleed kama Riwa alivyosema, so mwambie kwa sasa asikatae ujauzito as long as haikuwa mara yao ya kwanza kufanyana, kama walishafanyana huko nyuma then inawezekana kitu kimewaka so walee mimba kwa sasa mtoto akishazaliwa kama baba anaona kasingiziwa akapime DNA tu, ila kama hamtaki mtoto kwanini mnatiana kavu kavu?

Ukiingia kwenye uwanja wa mapenzi we amini yote! Vinginevyo utapata shambulizi la moyo (heart attack) teh teh teh x 3!
 
Kwa experience yangu kwenye clinical medicine na pia public health (jumla ya miaka 13 now) sijapata kusikia mwanamke mwenye circle ya siku 14, hapa Tanzania! Wapo wachache sana wenye circle ya siku 21, wengi ni wa siku 27/28 hadi 30, na mara nyingi ushauri wangu huwa naugeneralize hapo..unless mhusika awe certain kuwa ana circle fupi zaidi ya hapo..then atapata ushauri specific kwa urefu wa cirlce yake!

Nilipokuwa 15 yrs kwa miezi 6 mfululizo niliingia hedhi kila baada ya siku 14. Kwa kuwa nilikuwa mtoto ktk shule ya bweni headmistress alinipeleka hospital ya rufaa. Dokta alinifundisha kuwa ovaries ziikomaa kwa kupishana. Yaani kila upande ulijitegemea ktk tofauti ya siku 14. Alinionya kuwa sina safe days siku yoyote nitajamiiana nitapata mimba. Hali hiyo iliendelea kwa miezi 6. Baadaye nilianza mzuguko wa siku 25 kamili bila mabadiliko koala sasa umri 46 yrs(isipokuwa ktk stress &critical weather change e.g. nikienda eneo lenye winter temperatures).

Pia ikumbukwe kuwa sperms huishi kwa 72 hrs ndani ya mwanamke after being ejaculated. Huyu mama alikutana na mumewe siku ya sita baada ya damu iliyodumu siku tatu. Kuna siku 4 kavu (safe) baada ya damu baada ya hapo uwezekano wa fertilisation upo. Kama walikutana siku ya tatu ya dry days na sperm kuwa hai 72 hrs, sio ajabu kupata mimba.
 
Naomba msaada tafadhal,kama nliona tar 8 mwez ule, then tar 10,mwez huu,ni mzunguko wa siku ngapi na danger days ni zipi
 
Naomba msaada tafadhal,kama nliona tar 8 mwez ule, then tar 10,mwez huu,ni mzunguko wa siku ngapi na danger days ni zipi
mwezi ule ndio nini! Unamaana mwezi uliopita au? Unachowezafanya, record tarehe unapoanza siku zako kwa miezi mitatu mfurulizo, ili upate rough estmate ya MC yako na kama regular au irregular! 8-10 ni kama 32days, lakini hii haitoi picha halisi, inabidi iwe hivyo kwa miezi mingi mfululizo ndipo unaweza kusema kama ni ya uhakika au la( regular 32 days cycle or irregular ie, 32 this month, next month 26!)
 
Kwa experience yangu kwenye clinical medicine na pia public health (jumla ya miaka 13 now) sijapata kusikia mwanamke mwenye circle ya siku 14, hapa Tanzania! Wapo wachache sana wenye circle ya siku 21, wengi ni wa siku 27/28 hadi 30, na mara nyingi ushauri wangu huwa naugeneralize hapo..unless mhusika awe certain kuwa ana circle fupi zaidi ya hapo..then atapata ushauri specific kwa urefu wa cirlce yake!
Kutosikia hakumaanishi hawapo!! Too short 14 day-MC inaweza tokea hasa kwa wale wanaoingia kwa mara ya kwanza, au mara chache kutakana na kubadili life style au baada ya kuacha majira na hii inaweza kudumu kwa miezi michache! Shida inakuja kama inapodumu kwa muda mrefu, hapo lazima uchunguzi wa kina ufanyike ili kuhakikisha hakuna tatizo jingine la kiafya k.m. PCOS, TD, nk!
Pia kuna baadhi ya wanawake wanatoa damu kiduchu katikati ya mzunguko,kipindi cha ovulation ( takribani 14 day) kwa wale wa 28 MC!

Kwa kawaida haipasyi kuzidi 2 days! Hii pia inaweza changanywa na hedhi ya kawaida na hivyo kufikili MC imeishia hapo! Wanawake hawa wanatoa yai mara moja kwa mwezi ila tu wakati wa utoaji yai inaambatana na damu! Hata hivyo inaweza kuwa ni dalili mbaya ya ugonjwa kama (endometriosis)!

Wakati wote kama kuna dalili ambayo siyo ya kawaida ni salama zaidi kuchanganya vikongoro vyako kwenda kumuona daktari wa magonjwa ya kina mama!
 
Nilipokuwa 15 yrs kwa miezi 6 mfululizo niliingia hedhi kila baada ya siku 14. Kwa kuwa nilikuwa mtoto ktk shule ya bweni headmistress alinipeleka hospital ya rufaa. Dokta alinifundisha kuwa ovaries ziikomaa kwa kupishana. Yaani kila upande ulijitegemea ktk tofauti ya siku 14. Alinionya kuwa sina safe days siku yoyote nitajamiiana nitapata mimba. Hali hiyo iliendelea kwa miezi 6. Baadaye nilianza mzuguko wa siku 25 kamili bila mabadiliko koala sasa umri 46 yrs(isipokuwa ktk stress &critical weather change e.g. nikienda eneo lenye winter temperatures).

Pia ikumbukwe kuwa sperms huishi kwa 72 hrs ndani ya mwanamke after being ejaculated. Huyu mama alikutana na mumewe siku ya sita baada ya damu iliyodumu siku tatu. Kuna siku 4 kavu (safe) baada ya damu baada ya hapo uwezekano wa fertilisation upo. Kama walikutana siku ya tatu ya dry days na sperm kuwa hai 72 hrs, sio ajabu kupata mimba.

Hapo kwenye red: correction!
Sperms zinaweza kulisuburi yai hata kwa zaidi ya juma moja zima (8 days) kwenye kuta za uterus zikilisubiri kwa usongo yai likatize! Hivi siyo salama kihivyo kutumia siku 3!
 
Nimepata elimu safi sana ya maswala ya uzazi.... Hakuna sababu ya kusingizia tena hapa eti ooh unajua H ndio tulipanga awemtoto wetu wa mwisho ila K ilikuwa bahati mbaya tu, sasa ni mwendo wa science tu!
 
wanaJF nataka kujua cku za mwanamke kushika mimba je¿ Nisiku 2 kabla ya hedhi au ni baada ya hedhi! Msaada kwa wanaofahamu!
 
siku 3 hadi 5 kabla ya hedhi ndio yai linakuwa limeiva likisafiri taratibu kutoka kwenye ovary kuja kwenye uterus kupitia falopian tubes hapo ukipiga bao la uhakika mbegu linaogelekea kwenye uke hadi kwenye falopian tube na hapo fertilization inatokea mimba inatungwa na hilo fertilized yai (mimba changa ) linasafiri kuja kujishika kwenye uterus (mji wa mimba) na hapo mtoto hukua hadi kuzaliwa!!
 
kuanzia cku ya 11 baada ya kupata hedhi hadi cku ya 14 au 15 inategemea na mzunguko wako.hesabu first day the day utakayoona hedhi.NB:uko kwenye ndoa au unataka kuzaa na mume mtu.?
 
Jamani habari zenu wanajamvini, hivi inawezekana mtu akafanya mapenzi kila siku na hasipate mimba, kama ndio ni sababu zipi zinafanya iwe hivyo,
 
Back
Top Bottom