Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

Duuhhhhhh, wanaJF kuweni makini na ushauri mnaoupata hapa. In the pool of living organisms, every organism is unique.


Always remember that you are unique, that worked for someone is not necessary that its works for you.
let me be specific - Count from start of the period - twelve days hakuna mimba - siku ya 13 hadi ya 21 hapa unaweza pata mimba - then 22 hadi unacomplete circle hakuna mimba.

Sasa siku ya 13 mpaka 16 uwezekano mkubwa ni mtoto wa kike - siku ya 17 hadi 19 uwezekano ni mtoto wa kiume. - so unapohitaji mtoto wa kiume jitahidi usifanye 13 hadi 16 - jaribu siku ya 17, 18 na 19, then kapime uwezekano ni kidume

Just simple counting.....
 
Me navyojua na nilisha practice hiyo plan kuwa mama akianza period siku ya kwanza na ndio uhesabu moja na kufuatiza zingine hata akimaliza period we endelea kuhesabu ila ifikapo siku ya 13 na 14 na mkifanya ndipo mtoto wa kiume hupatikana . na mkijamiana siku hizo mbili yani siku ya 13 na 14 iwe ndio basi msijamiane tena mpaka baada ya siku kama 3 au nne zipite
 
Naomba kuongeza hapo.mbezu za kiume zinazoweza kutoa mtoto wa kiume huweza kukaa muda wa masaa 48.na zinazoweza kutoa mtoto wa kike hukaa masaa 72.kwa hiyo toka siku ya 11 mpaka siku ya 14 yai linapokuwa released ni masaa 72.KWA HIYO BASI,kama wataka mtoto wa kike wapaswa kufanya tendo la ndoa siku ya 11 au 12 maana mbegu za kutoa mtoto wa kiume zinakuwa zimeishiwa nguvu kabisa ifikapo siku ya 14 na za kike zitakuwa bado zina dunda .ila kwa siku ya 13,14 yenyewe ukifanya tendo la ndoa mara nyingi posibility ya kupata mtoto wa kiume ni kubwa maana speed ya mbegu zitoazo mtoto wa kiume ni kubwa kuliko zitoazo mtoto wa kike.na itakuwa ni ndani ya masaa 48 .
he! kumbe naweza kuchagua hata jinsia ya mtoto ninayetaka? wana JF hii inakaaje?
 
Habari zenu wakuu!

Sasa ni mwaka wa pili toka nimeoa,mpaka sasa mke wangu hajashika mimba, nimeenda nae hospital nyingi,tumeambiwa sote hatuna tatizo, Kuna doctor mmoja aliniambia nikisha kummega wife, awe ananyanyua miguu juu kama 15 minutes, lakini bado hiyo njia haijasaidia, Wana jamvi kuna njia yoyote ya kufanya ili mke wangu apate mimba?

Naombeni mnijuze au kama kuna daktari yeyote atakayeweza kunisaidia, na mimi mwenzenu natamani kuitwa Baba fulani.
 
Kule ulikompeleka kwa daktari akawa anamchezea, majibu yalikuwa ni nini?
 
kule ulikompeleka kwa daktari akawa anamchezea, majibu yalikuwa ni nini?
Yule daktari niliachana nae, kwa sababu alimwambia mke wangu itabidi alazwe, ndio nikashtukia dili.
 
Pole sana muombeni mungu atawasaidia msikate tamaa, mtangulizeni mungu kwa kila jambo hakuna linalo shindikana kwake.
 
Jamani awe bwabwa awe boflo au mkate nadhani majibu ya Geoff si mahala pake!samahani kama nimekosea!
 
Hashiki mimba kwa sababu imesawa affect kisaikologia! mkiwa mnado mnafikiria mimba tuu! hebu mreluxe bwana mimba itashika tuu...mbona mapema sana. Kuweni na imani na Mungu atawasaidia tuu...by the way angalia usikute mambo yako ni mkono wa tembo yawe yamesogeza kizazi...
 
Hashiki mimba kwa sababu imesawa affect kisaikologia! mkiwa mnado mnafikiria mimba tuu! hebu mreluxe bwana mimba itashika tuu...mbona mapema sana. Kuweni na imani na Mungu atawasaidia tuu. by the way, angalia usikute mambo yako ni mkono wa tembo yawe yamesogeza kizazi.

Unahisi labda ana dudu kubwa, na imesukumia kizazi mbali?..sidhani, maana ni wengi tu wenye nazo, lakini wanatengeneza watoto vizuri!

Mtangulizeni Mungu kabla ya tendo, na kuweni na IMANI!
 
Boflo,

Mkuu mda wa Miaka 2, kwa maoni yangu ni muda mdogo sana ndani ya ndoa, mimi nilioa na nikakaa kwa muda wa takriban miaka 3, hali ilikuwa kama ya kwako, kwa upande wangu tulipokwenda kwenye vipimo mimi na mama yenu, tatizo lilikutwa kwangu, nikapewa rufaa kwenda jijini Dar es Salaam, na baada ya matibabu mambo yalienda sawa tatizo liliondoka , Daktari aliyenipa tiba anapatikana pale Tumaini Hospitl Upanga anaitwa Dr. Kapona nakushauri uende kumuona Mwenyezi Mungu atajaalia afungue na aondoe matatizo uliyonayo Mkuu Pole sana.
 
Unahisi labda ana dudu kubwa, na imesukumia kizazi mbali?..sidhani, maana ni wengi tu wenye nazo, lakini wanatengeneza watoto vizuri!
Mtangulizeni Mungu kabla ya tendo, na kuweni na IMANI!...

Mpwa ukisogezwa kikazi inasumbua sana kushika mimba....labda jamaa anacheza rafu...kikubwa wamtangulize mungu mbele...
 
Mkuu mda wa Miaka 2, kwa maoni yangu ni muda mdogo sana ndani ya ndoa, mimi nilioa na nikakaa kwa muda wa takriban miaka 3, hali ilikuwa kama ya kwako, kwa upande wangu tulipokwenda kwenye vipimo mimi na mama yenu, tatizo lilikutwa kwangu, nikapewa rufaa kwenda jijini Dar es Salaam, na baada ya matibabu mambo yalienda sawa tatizo liliondoka , Daktari aliyenipa tiba anapatikana pale Tumaini Hospitl Upanga anaitwa Dr. Kapona nakushauri uende kumuona Mwenyezi Mungu atajaalia afungue na aondoe matatizo uliyonayo Mkuu Pole sana.
Asante sana mkuu, kwa ushauri
 
Asante sana kwa aliyetoa hii thread maaa ametusaidia na wengine, naomba muendelee kuchangia kwa hekima wengi tuna hilo tatizo jamani.
 
Maadamu mumeambiwa na doctor kwamba hamuna matatizo ya uzazi muwe na subira na mzidi kumwomba mungu. Mimi nina mfano hai ya watu waliokuwa na tatizo kama lako kwa mujibu wa maelezo yako.

Mdogo wa mke wangu alikaa miaka mitatu bila kupata mimba. Tuka arrange waje DSM toka mikoani wanapoishi kwa ajili ya kwenda kumwona doctor hapo Muhimbili tuliyemwelezea tatizo lao. Walipofika hapa DSM wakiwa wamechelewa kidogo doctor akawa amepata safari ya kikazi ya muda wa mwezi moja huko Norway hivyo akatushauri tumsubiri mpaka arudi.

Huwezi kuamini, ule muda wa mwezi moja waliokaa DSM wakimsubiri doctor, huyo mama akapata mimba. Mpaka sasa wana watoto watano. Ilionekana waliadhirika kisaikolojia na mazingira tu. JARIBUNI KUPUNGUZA WASIWASI NA MBADILISHE HALI YA HEWA MAMBO YATAJIPA TU. POLE SANA
 
Pole sana jamaa yangu. Mi sio Doctor ila nina kaushauri tu. Kuna mazingira amabayo huwa yanaruhusu mama kupata mimba. Mimba ni kupanga na zaidi mimba hupatika kwa furaha na sio kwenye maudhi. Jiandaeni kutengeneza mimba. Inawezekana kuna mazingira ambayo hayamfurahishi mmoja wenu. Inawezekana kuna hisia kati yenu kuwa huyo atakeyezaliwa atakuwaje, atalelewaje nk.

Pia hata ulevi, uvutaji uliokithiri unaweza sababisha upatikanaji wa mimba kuwa mashakani. Msukumo wa familia moja nao ni factor nyingine. Kama mnakiri kuwa nyote mko sawa na kweli mko sawa, basi chunguzeni kasoro zenu, kukosekana kwa upendo wa dhati, ulevi, uvutaji,majivuno ya mmoja wenu na hata kutokuwa na imani na mwenzako na mambo kama hayo. Ukigundua kasoro yoyote ama bibi ama wewe basi ifanyie kazi.

Tulizeni mawazo jadilianeni kwa pamoja kuhusu hilo then mtaamua sasa mnataka nini. Mimi naamini ninyi ndo wa kuamua kupata hiyo mimba ama la. Kusiwepo wa kumlaumu mwenzake hapo mtaanzisha malumbanao ambayao hamtamaliza mpaka mnazeeka.

Angalieni msije mkadanganyika na kalumanzira eti wana dawa! Mtapotea bureee. Mwisho mtangulizeni Mungu zaidi kwa kila jambo.

Kila la kheri Boflo
 
Back
Top Bottom