Tarime, Mara: Mmiliki wa mabasi ya Zacharia awapiga risasi maafisa wa Usalama wa Taifa, ashikiliwa na Polisi

Tarime, Mara: Mmiliki wa mabasi ya Zacharia awapiga risasi maafisa wa Usalama wa Taifa, ashikiliwa na Polisi

Tanzania pia inahitajika elimu kwa umma kuhusu usalama wa taifa, duties, responsibilities na modus operandi zao. Ofisa usalama wa taifa hawana mamlaka ya kuvamia popote na kumkamata mtu yoyote kwa nia ya kumhoji. Wanachotakiwa kufanya kama ni kufanya uchunguzi inapofikia stage ya kufanya arrest, then lazima washirikiane na jeshi la polisi.

Kwa wale wazee wenzangu ambao tulifuatilia ile kesi ya uhaini ya mwaka 1984, tulijifunza mengi kuhusu utendaji wa idara yetu ya usalama wa taifa na na maofisa wake haswa wale mashahidi W, X, Y na Z.

Enzi za Mwalimu Nyerere, hawa jamaa walikuwa siri, hata kuwajua ilikuwa issue, mimi mwenyewe wazazi wangu wote wawili walikuwa watu wa idara hii, nimekuja kujua niko Primary enzi za ile Kesi ya Mauaji Mwanza ya mwaka 1980!. Siku hizi kujulikana imekuwa sifa!, kitu kimoja muhimu sana kuhusu watu hawa, ni watu muhimu sana, na wanahitaji sio tuu kuheshimiwa, bali pia kujiheshimu na kuepuka exposee!, enzi za Mwalimu kulikuwa hakuna modern communications equipment's, sasa hivi zipo, kuna simu, mobile tracking devices, gprs, gps, etc, kwa nini wavamie rais bila usalama wa raia?!, japo taarifa za hili tukio bado hazijatulia, ila pia hawa jamaa zetu, nao pia sometimes ni binadamu, sio malaika, ndio maana hili tukio liliwahi kutokea kule nyuma
TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali Wachunguzwe, Wafumuliwe!
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!.

P.
 
Ila watoa taarifa wa serikali.... duh aisee rationality yao na jinsi wanavyo establish cause-effect relation utadhani wengine hatujaenda shule![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
kiukweli kabisa kwa sisi tunaishi Tarime tunaamini kila mtu ana mapungufu yake ila pia ana mazuri yake
Zakaria ni nguzo ya wilaya ya Tarime
ni msaada mkubwa mno kwa wilaya nzima
kuanzia huduma anazozitoa pia na namna mzunguko ulivyo wa biashara
japo ana kasoro moja tu ya kutokuendana na mabadiliko ama maboresho

katika hili la Zakaria kuna maswali mengi sana
ila majibu pia huenda ni machache au HAYAPO kabisa

ktk biashara siku zote kuna mahasimu ila Hata siku 1 Zakaria tukio kama hilo halijawahi kutokea ktk ofisi yake huenda anajua namna nzuri ya kumalizana nao ila SIO ktk ofisi zake

Zakaria sio kichaa tu kwamba wateja waje kuongeza mafuta alafu ghafla atoe bastola aanze kuwashambulia
je mbona hadi sasa angekuwa ameua watu zaidi ya ile namba ya Waasi wa HAMAS?

Hivi zakaria iwapo angeuwawa ktk hilo shambulio japo hatui huenda hata kama yupo Hai
nani angejitokeza kuwa wale walikuwa wanausalama?

Tanzania yetu huenda ni mimi sijui ni kweli kuwa kazi ya usalama wa Taifa ndilo jukumu lao kama la kipolisi japo sijawahi kuona wakiwa na.sare kama za kipolisi

Zakaria mke wake yupo sero Dodoma hadi sasa kuhusu nyumba walizonunua Mwnza

kiukweli tuweke vyama vyetu vya siasa pembeni tofauti zetu za kisiasa leo tuungane kuhoji hili
coz leo kwake na kesho kwa mwingine

Hapa viongozi wote wa kipolisi na wengine ktk ngazi ya wilaya na mkoa inabidi waje na majibu
vinginevyo wananchi wanaweza kuwa na chuki juu ya vyombo hivi muhimu vya ulinzi

AU NDIYO MAANA WAZIRI AMEPIGWA CHINI?
Ni muombe Rais alifuatilie hili coz kuna mengine yanafanyika ili tu kumharibia jina na kumchonganisha na wananchi ilihali masikini huenda hata hana idea yoyote ile

HAKI KWA ZAKARIA
AWE HAI
AWE MFU
 
Itakuwa walitaka kumfanya kama waalivomfanya mmiliki wa Super Sammy ila akawawahi sasa wana haha.Ina maana jamaa ni kichaa tu afyatue risasi hovyo.Unaenda kutia mafuta halafu unashuka kisha unafyatuliwa risasi
 
Back
Top Bottom