Tarime, Mara: Mmiliki wa mabasi ya Zacharia awapiga risasi maafisa wa Usalama wa Taifa, ashikiliwa na Polisi

Tarime, Mara: Mmiliki wa mabasi ya Zacharia awapiga risasi maafisa wa Usalama wa Taifa, ashikiliwa na Polisi

Kwa ninyi wa Dar na miji mingine mikubwa mna bohari za GPSA. Huku wilayani hayo mambo hakuna. Gari za serikali zinajaza mafuta katika vituo binafsi, kwa makubaliano maalu ya kutumia vocha ama vitabu, then malipo baadae!
Meneja wa kituo keshasema wao walikuwa wamefunga kituo saa hizo na hakuna mauzo, una semaje hapo? hao ni maafisa majambazi tuu na wasio julikana hadi wachapwe Shaba ndio wanajulikana. Nadhani hiyo ndio dawa pekee iliyobaki.
 
Siku zote uongo hujitenga na ukwel ndyo maana wameshindwa kutengeneza movie inayoelweka
Kusema uongo, hasa kwa public, ni kazi sana maana hata pale ambapo new facts zinapoibuka wewe unalazimika ku maintain uongo wako.... Angalia RC anavyopata shidaa
 
Hata kama bwana...Yani TISS na Ujanja wao woteee wameshikwa pabaya sana na huyu jamaa. Miaka ya Mwinyi na Nyerere walikuwa wakikufuata mzee hata hatukusikii kabisa, yaani tunakuja kupewa taarifa tu kwamba umepotea tu. Lakini siku hizi, hahahahaha kila mtu anajua kuna mkono wa Serikali kabisa.
Swali muhimu la kujiuliza je sheria yao inawaruhusu kuvamia na arrest ?
 
Kwa ninyi wa Dar na miji mingine mikubwa mna bohari za GPSA. Huku wilayani hayo mambo hakuna. Gari za serikali zinajaza mafuta katika vituo binafsi, kwa makubaliano maalu ya kutumia vocha ama vitabu, then malipo baadae!
Wenye kituo wamesema saa kumi na mbili huwa wanafunga kituo chao sasa saa mbili walikuja kufanya nini?
 
Hawa watu walichokifanya kwa mzee wa watu sio kitu kizuri kabisa najaribu kuimagine mzee kama peter zakaria anakumbana na sekeseke LA vijana watano tena wenye mafunzo ya kijeshi pamoja na silaha kwa na uzee ule kwa kweli sio fair ata kidogo tuweni na huruma na damu za watu tuwe na moyo wa kiubinadamu kama anakosa adhibitiwe kisheria na sio kwa style hii koz kwa utawala huu naamin hakuna alie juu ya sheria na kama basi hajavunja sheria aachwe afanye yake koz linapokuja swala LA chama yule mzee kasaidia mengi sana msipishane kwa jambo dogo akaonekana wa kazi gani koz jamaa ktk awamu hii kasumbuka sana kuna siku amedodosha machozi kanisan kwa jinsi anavyosakamwa na watesi wake hope viongozi wenye mamlaka kimkoa au kiwilaya wanamchonganisha kwa mkuu wa kaya .busara zaidi zitumike kutatua hili swala
alishindwa mini kuhama Hugo mzee nae?,pesa anayo angehamisha investment zakekama aliona wanamsonga songa.
 
Kwanza naomba nishukuru Jf kurudi , nimefurahi Sana Sana hasa Madini ya humu jf.....kwa Leo nawasalimia wadau wote niliwamisi sana
 
Leo ndyo nimejua kuwa JF imerudi hewani rasm,usiku wa leo sitalala!
 
By Waandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Tarime. Tukio la kukamatwa kwa mfanyabiashara wa Kanda ya Ziwa, Peter Zakaria limechukua sura mpya baada ya familia na walioshuhudia tukio hilo kutoa maelezo yanayokinzana na Mkuu wa Mkoa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini Tarime jana, baadhi ya walioshuhudia tukio hilo, akiwemo msemaji wa familia, Samuel Chamete na meneja wa kituo cha mafuta ambako tukio hilo lilitokea, Samuel Athumani walisema taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima inakinzana na ukweli.

“Nilikuwepo na nilishuhudia tukio kuanzia mwanzo hadi mwisho. Wale watu hawakuja kujaza mafuta kwa sababu kituo kilishafungwa tangu saa 12:00 jioni,” alisema Athumani.

Alisema, “Baada ya kuona gari lao limesimama muda mrefu bila wahusika kushuka, nilimtuma mfanyakazi kuwauliza iwapo wana shida tuwasaidie na wakajibu hawana shida.”

Meneja huyo alisema baada ya kumaliza kuangalia taarifa ya habari ya saa mbili usiku, bosi wake (Zakaria) aliaga ndipo ghafla watu wawili walitoka ndani ya gari na kumkamata ili kumuingiza kwa nguvu ndani ya gari lao.

Alisema Zakaria alipiga kelele akimwita kwa jina lake ili akamsaidie.

“Nilikimbilia eneo la tukio nikasikia sauti ya mpige risasi huyo. Hapo ndipo nikasikia milio ya risasi na ghafla nikawa nimeshakamatwa na kulazwa chini na watu hao,” alisema Athumani.

Alisema kuwasili kwa basi la kampuni ya Zakaria kutoka Mwanza kuliwaokoa kwa kuwa abiria, wafanyakazi na wananchi wengine wakiwamo waendesha pikipiki walikwenda kutoa msaada.

Samuel Chomete (65), msemaji wa familia alisema tukio hilo limeibua hofu kuhusu usalama na uhai wa Zakaria kutokana na jinsi lilivyotokea na taarifa zilizotolewa na viongozi na mamlaka za Serikali.

“Hatujui lengo la waliojaribu kumteka mdogo wangu Zakaria, lakini tunaamini hawakuwa na nia njema ndiyo maana walifika usiku bila taarifa kama wanaokwenda kukamata jambazi,” alisema Chomete.

Alisema licha ya kuwa mfanyabiashara maarufu na kada wa CCM, Zakaria pia ni mfadhili wa masuala mbalimbali ya chama na kijamii ambaye angeweza kuitwa na kwenda mwenyewe Polisi iwapo alihitajika kwa jambo lolote.

“Tunamshukuru Mungu aliweza kupambana na watu kujitokeza kumsaidia. Pengine naye angepotea kama wengine wanaoripotiwa kupotea katika siku za hivi karibuni,” alisema.

Alisema, “Tumeiachia Serikali usalama na maisha ya Zakaria, akidhurika hata kidole familia tutaelekeza lawama zote dhidi ya Serikali kwa sababu imethibitika wahusika ni watumishi wa Serikali.”

Akizungumza na Mwananchi jana, mkuu wa mkoa wa Mara, Malima alisisitiza usahihi wa taarifa yake kwa vyombo vya habari juzi akisema iwapo walioshuhudia wana kauli na maelezo kinzani, ukweli utajulikana suala hilo likifikishwa mahakamani.

“Nisikilize kwa makini, mimi ndiye mkuu wa mkoa, nimetoa taarifa juzi kwa waandishi wa habari na mwakilishi wa Mwananchi alikuwapo. Kama familia na mashuhuda wanasema tofauti mimi siwezi kusema lolote. Tusubiri suala hilo lifike mahakamani na yote yatajulikana huko,” alisema.

Malima alisema, “Siwezi kusema hivi jana halafu kesho niseme vingine na keshokutwa niseme tofauti. Mwananchi ni chombo makini mtaamua namna ya kushughulika na kauli kinzani mnayopata kutoka kwa mashuhuda na familia.”

Juzi akizungumzia tukio hilo mjini Musoma, Malima alikanusha taarifa zilizodai Zakaria alikuwa ametekwa akisema alikamatwa na maofisa usalama waliomdhibiti baada ya yeye kuwajeruhi kwa risasi wenzao wawili walioshuka kwenye gari walipofika kujaza mafuta kwenye kituo chake mjini Tarime.

Fedha zatoweka

Chomete aliyesema alionana na Zakaria muda mfupi kabla ya kuzungumza na Mwananchi, alisema familia haijui ziliko Sh16.3 milioni alizokuwa nazo Zakaria kwenye mkoba muda mfupi kabla ya kukamatwa.

Mwenyekiti wa mtaa wa Starehe mjini Tarime kilipo kituo cha mafuta tukio lilikotokea, Bashiri Selemani alisema,

“Kwa siku tatu mfululizo nililishuhudia gari lililohusika katika tukio likiwa limeegeshwa nyuma ya kituo cha mafuta cha Zakaria wakijifanya kulifanyia matengenezo, hii inaonyesha walikuwa kwenye mtego kufuatilia nyendo za Zakaria.”

Selemani pia ni diwani wa Nyamisangura na makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Tarime
 
adam Malima akiingia kichwa kichwa kwenye hili atadhalilika vibaya mno !
“Kwa siku tatu mfululizo nililishuhudia gari lililohusika katika tukio likiwa limeegeshwa nyuma ya kituo cha mafuta cha Zakaria wakijifanya kulifanyia matengenezo, hii inaonyesha walikuwa kwenye mtego kufuatilia nyendo za Zakaria.” - Bashiri Selemani, M/Kiti wa Mtaa
 
Back
Top Bottom