Tarime, Mara: Mmiliki wa mabasi ya Zacharia awapiga risasi maafisa wa Usalama wa Taifa, ashikiliwa na Polisi

aibu sana !
 
Wenye kituo wamesema saa kumi na mbili huwa wanafunga kituo chao sasa saa mbili walikuja kufanya nini?
Hilo swali muhimu. Lakini mie nilikua namjibu anaesema kwamba serikali huwa haijazi mafuta kwenye vituo binafsi!
 
Kufikia 2020 tutaona mengi - hapa ni mwanzo wa mkanda. Madai ya katiba mpya kama mwongozo na dira kwa taifa letu yataonekana ya maana katika kipindi hiki.
 
Wakuu hii ishu inaendeleaje au ndo washafunika kombe??
 
Kwa hiyo mkapa alisaini kitu asichokijua? Sheria hiyo imetakataza usalama wa Taifa wasikamate sasa basi kumbe mkapa nae alikuwa mbumbumbu?
Mkuu niuelewa tu wa sheria ndiyo unagomba! Anakatazwa kukamata kwa mgongo wa kazi yake ya Usalama wa Taifa! Lakini kumbuka pia ni raia wa TZ kwa hiyo sheria ya CPA inamruhusu kumkamata mtu ambaye anatenda kosa la jinai mbele yake kama ambavyo raia mwingine yoyote anavyoweza kamata mhalifu yoyote anayetenda kosa la jinai mbele yake!!
 
Nimekuelewa mkuu.
 
Mkuu sheria ya CPA hajabagua kuwa Afisa wa Usalama wa Taifa au raia mwingine yeyote asikamate ila sheria ya usalama wa taifa hairuhusu kama taasisi kukamata ila CPA inaruhusu raia yeyote kukamata mhalifu wa jinai ndio maana raia wanakamata waharifu kila siku na kuwafikisha polisi au ofisi za serikali. Haiwezekani na wala haiingii akilini Afisa Usalama wa Taifa aone mhalifu anatenda kosa mbele yake asimkamate eti kwa kuwa sheria ya Usalama wa Taifa inamkataza kukamata. Just interpretantion of laws ndiyo inakusumbua mkuu.
 
usalama sio law enforcement agency
Kwani wewe kama raia wa kawaida huruhusiwi kukamata mhalifu akiwa anatenda kosa mbele yako?? Kwa taarifa yako CPA yaani Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai inamruhusu raia yoyote kumkamata mhalifu wa makosa ya Jinai na kumfikisha kwa Askari Polisi ambaye atamkamata na kumfikisha Mahakamani. Mkuu kasome sheria ya CPA utajua!!
 
Kwel naamini taratibu juu ya karma juzi tu kuna uzi ulikua unazengea mmiliki wa mabasi ya zakaria kanizurum maliyangu Leo tenaa asee"
 
Sio kila MTU ni mzembe mzembe,hata muwe kikosi usiombe kuwekwa kati na RAIA,
 
Ilikuwaje akawaacha hao wengine waliobaki? Angetandika na hao tu waliobakia.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Ukiwawahi wanaji introduce Nina wasi wasi na mafunzo yao mbona wepesi sana au ndo vijana wale waHuni wahuni wa uvccm

Sure!! huwezi kuji introduce kirahisi hvyo halafu ukajiita Secret service.
Hawa watakuwa wahuni tu walitumwa wakaona wasingizie hvyo ili wasife manake wakurya ni Balaaaa.. VITA ni VITA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…