The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Mwalimu wa dini wa shule za madrassa huko Tarime amekamatwa kwa tuhuma za kunajisi watoto wadogo.
Soma mwenyewe hapa chini.
======
MWALIMU wa madrasa kwenye Msikiti wa Kebeyo, Kijiji cha Getenga, Tarafa ya Inchugu wilayani Tarime mkoani Mara, Shaban Harun (37) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Sirari kwa tuhuma za kuwanajisi wanafunzi wake wawili wenye umri wa miaka minane kila mmoja.
Inadaiwa kuwa mwalimu huyo alifanya ukatili huo dhidi ya watoto hao (majina tunayahifadhi) baada ya kuwapeleka kwenye chumba anachoishi na kuwafanyia vitendo hivyo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Getenga, Julius Makuri alidai: "Wakazi wa Kitongoji cha Kebeyo, Kijiji cha Getenga tumesikitishwa na kitendo cha mwalimu huyo kuwatendea vitendo vya kinyama watoto wadogo ambao ni wanafunzi wake.
"Tunaomba sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia mbaya dhidi ya watoto ambao ni taifa la kesho."
Wazazi wa watoto hao Magreth Sabai na Joyce Gesere, walikutwa na Nipashe wakiwa na watoto wao, nje ya Kituo cha Polisi Sirari.
Nipashe