TARURA: Ni kweli Daraja la Mto Mngeta lilitumia Tsh. milion 31

Mbao ya mkarati ya 2x6 uku kwetu inauzwa elf40,, na nguzo moja ya futi 20 inauzwa elf15 adi elf 20.. ilo daraja zima ni around million 5 adi 8,,
Mlimba kwenyewe ukienda mlimba mjini KWENYE yard za mbao,
[emoji117]2× 6 Bei ya rejareja Ni elfu 8 (8,000)
[emoji117]Nguzo ya futi 20 Bei ya rejareja Ni elfu 20 (20,000)

Hizo Bei labda uko dar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkarati ndio mti gani wadau?
Maana nime Google imekuja mkaratusi
 
Huyu Meneja wa TARURA nae hajielewi kbs. Kwanini asije na ufafanuzi ni gharama kiasi gani zilihitajika kutengeneza daraja la zege. Maana unaweza kukuta hilo daraja ni gharama ndogo endapo lingetumia sementi. Kwa hiyo baada ya miaka 10 mambo yanarudi kulekule.

Approximation inasema 15 years!

Pambana Chief! Nchi huru hii!
 
[emoji16][emoji3][emoji23][emoji2][emoji2][emoji1][emoji1][emoji28][emoji38][emoji38][emoji2][emoji23][emoji16][emoji16]
Wakafanya Watakavyo Sasa Hivi

Ukipata mtu Anakuzidi kwa unafiki “term” hii......
Nishtue.....!!
 
SIKU Moja baada ya Mbunge wa Jimbo la Mlimba Mkoani Morogoro, Godwin Kunambi kutembelea Daraja la Mto Mngeta lililogharimu Sh Milioni 30 hatimaye Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Wilaya ya Kilombero ametolea ufafanuzi gharama za ujenzi huo.

Mhandisi Robert Magogo ambaye ni Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilombero ametolea ufafanuzi wa Ujenzi wa mradi huo akisema gharama zilizotajwa ni sahihi huku akieleza kuwa lina uwezo wa kudumu kwa miaka 10 hadi 15.

Akifafanua ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi Magogo amesema Daraja hilo lina urefu wa Mita 40, kina cha Mto kikiwa ni Mita 4, upana wake Mita 5 na hivyo kufanya gharama za Daraja kuwa Milioni 27.

Mhandisi Magogo ameeleza kuwa gharama ya barabara kuingia na kutoka darajani ni Sh Milioni 4 na kufanya jumla yake iwe Sh Milioni 31.

" Urefu wa wa nguzo zilizotumika ni Mita 7 na unene wake ni Mita 0.5, Mbao ni Inchi 3 kwa 8 na Inchi 3 kwa 10 na aina ya Mti ambao Mbao zake zimetumika ni za Mti aina ya Mkarati, niwahakikishie kuwa daraja hili ni imara na litakua na uwezo wa kupitisha Tani 10 na litadumu kwa miaka 10 hadi 15," Amesema Magogo.

Kwa upande wake Mbunge Kunambi amesema Daraja hilo litaokoa uhai wa wananchi ambao kwa muda mrefu wamekua wakipata changamoto ya kivuko kwani Mto huu una mamba ambao wamekua wakisababisha Vifo vya wananchi wetu," Amesema Kunambi.

WhatsApp%2BImage%2B2021-07-29%2Bat%2B9.44.28%2BPM.jpeg
Mbunge wa Jimbo la Mlimba Morogoro, Godwin Kunambi (wa pili kutoka kushoto) akiwa kwenye Mtumbwi akivuka Mto Mngeta Februari mwaka huu ambapo aliitembelea Mto huo ukiwa hauna kivuko

WhatsApp%2BImage%2B2021-07-29%2Bat%2B9.46.38%2BPM.jpeg
Picha zikimuonesha Mbunge Jimbo la Mlimba Morogoro, Godwin Kunambi akipita juu ya daraja la muda ambalo amefanikisha ujenzi wake. Daraja hili litakua na uwezo wa kupitisha Tani 10 na litadumu kwa muda wa miaka 10 hadi 15.

WhatsApp%2BImage%2B2021-07-29%2Bat%2B9.46.40%2BPM.jpeg
Milioni 31?
 
Unajisifu kabisa umetoa comment ya msingi!?

You are a disease like any other!

You deserve to be contained !
Kuwa kwako Verified member sio kigezo cha kuhoji comments za msingi na zisizo za msingi, unaweza ukanipa kesi ya ugaidi ukiona comment yangu sio ya msingi.
Mama alisema wasomi walio nje ya nchi hawajaisaidia chochote nchi hii, na wewe huenda ni msomi wa ndani na hauna msaada humu JF.
 
SIKU Moja baada ya Mbunge wa Jimbo la Mlimba Mkoani Morogoro, Godwin Kunambi kutembelea Daraja la Mto Mngeta lililogharimu Sh Milioni 30 hatimaye Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), Wilaya ya Kilombero ametolea ufafanuzi gharama za ujenzi huo.

Mhandisi Robert Magogo ambaye ni Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilombero ametolea ufafanuzi wa Ujenzi wa mradi huo akisema gharama zilizotajwa ni sahihi huku akieleza kuwa lina uwezo wa kudumu kwa miaka 10 hadi 15.

Akifafanua ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi Magogo amesema Daraja hilo lina urefu wa Mita 40, kina cha Mto kikiwa ni Mita 4, upana wake Mita 5 na hivyo kufanya gharama za Daraja kuwa Milioni 27.

Mhandisi Magogo ameeleza kuwa gharama ya barabara kuingia na kutoka darajani ni Sh Milioni 4 na kufanya jumla yake iwe Sh Milioni 31.

" Urefu wa wa nguzo zilizotumika ni Mita 7 na unene wake ni Mita 0.5, Mbao ni Inchi 3 kwa 8 na Inchi 3 kwa 10 na aina ya Mti ambao Mbao zake zimetumika ni za Mti aina ya Mkarati, niwahakikishie kuwa daraja hili ni imara na litakua na uwezo wa kupitisha Tani 10 na litadumu kwa miaka 10 hadi 15," Amesema Magogo.

Kwa upande wake Mbunge Kunambi amesema Daraja hilo litaokoa uhai wa wananchi ambao kwa muda mrefu wamekua wakipata changamoto ya kivuko kwani Mto huu una mamba ambao wamekua wakisababisha Vifo vya wananchi wetu," Amesema Kunambi.

WhatsApp%2BImage%2B2021-07-29%2Bat%2B9.44.28%2BPM.jpeg
Mbunge wa Jimbo la Mlimba Morogoro, Godwin Kunambi (wa pili kutoka kushoto) akiwa kwenye Mtumbwi akivuka Mto Mngeta Februari mwaka huu ambapo aliitembelea Mto huo ukiwa hauna kivuko

WhatsApp%2BImage%2B2021-07-29%2Bat%2B9.46.38%2BPM.jpeg
Picha zikimuonesha Mbunge Jimbo la Mlimba Morogoro, Godwin Kunambi akipita juu ya daraja la muda ambalo amefanikisha ujenzi wake. Daraja hili litakua na uwezo wa kupitisha Tani 10 na litadumu kwa muda wa miaka 10 hadi 15.

WhatsApp%2BImage%2B2021-07-29%2Bat%2B9.46.40%2BPM.jpeg
Ndio tunakatwa tozo kubwa hivi ili kujenga hayo madaraja ya miti?
 
Tena wanaokata ni wafungwa.

Serikali kuna michezo ya kishenzi sana, vidaraja kama hivi ni vya kupigia hela. Miaka mitatu ijayo, watasema mbap zimeoza, na italetwa habari mwananchi mmoja kaliwa na mamba, basi madiwani watalambishwa laki laki, na kupitisha hoja, daraja jipya lijengwe. Procurement Officer na team yake wanalamba hata 15 Mil, maisha yanasonga.
Wabongo kwa upigaji Wana PhD.
 
Mil 31 kidogo sana, nikajua Mil 310 hivi.

Si Tozo lipo...atumie tozo vizuri bana, alaah
 
Huu ujanja ujanja wa kupiga ulioletwa na ile awamu ya tano, sasa imetosha...
Hatuwezi kuendelea kufanywa wajinga kiasi hiki..na hivi vimiradi vya mihemko
Hiki kidaraja kimetengenezwa na mafundi seremala, mungu anawaona nyie....
 
Ela zimeishia kulipa perfdiem ya staff wa TARURA walioenda hapo kusimamia ujenzi
 
Haya madaraja zamani Moshi yalikua yanajengwa bure na wanakijiji na yalikua mazuri zaidi ya hili na yenye kingo kusaidia watembea kwa miguu kujishika, sijui nini kilikuja kuikumba Tanzania, hakuna ujamaa tena wala huruma kwenye hela za umma.
 
Back
Top Bottom