Taswira ya Yesu anayehubiriwa ni tofauti na Yesu halisi

Taswira ya Yesu anayehubiriwa ni tofauti na Yesu halisi

leoleo-tu

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2018
Posts
2,224
Reaction score
6,784
Ukisoma na kutafakari kwa umakini kuhusu Yesu unagundua kwamba alikuwa ni wale watu ambao jamii inawachukulia kwamba wamepinda yani outcast.

Hata wale wanafunzi wake aliokuwa akiongozana nao jamii inaonekaan ilikuwa inawachukulia kama watu wasiokuwa na maadili waliopotoka yani waliopinda.

Ndio maana kuna sehemu hadi anaulizwa, inakuaje anakula na kunywa na wenye dhambi? Hii bila shaka haina tofauti na sasa unamuuliza, we jamaa unaonekana ni mwenye ehshima inakuaje unashinda na wazinzi na walevi?

Hebu fikiria mtu unayemheshimu sana anakuja kahaba analia miguuni mwake anampangusa kwa nywele anambusu miguu, assume huyo jamaa anayefanyiwa hivyo ni hakimu na huyo kahaba ana kesi. Halafu baada ya kufanyiwa hivyo hakimu anamwambia kesi yako utashinda!

Bila shaka utasema hakimu kasema hayo kwa sababu kahaba kamtamanisha kwa kumshika shika na kumbusu miguu huenda watamalizana huko mebeleni. Hiki ndicho kilichotokea kwa yule kahaba na bila shaka wale jamaa walisema moyoni huyu jamaa amelegea kwa kahaba atakuwa msela tu anatuigizia.

Ukichukulia hali hii kwakweli hata angekuja leo hapa TZ bado watu wangemkataa. Wangemwona msela Fulani hivi mwenye group la watu waliopinda. Yani kipindi anajiita kwamba yeye ni mfalme wa Wayahudi, huenda wale viongozi walikuwa wanamchukulia kama Ney wa Mitego anavyojiita raisi wa masela au Madee anayejiita rais wa Manzese hawakuwa wakimchukulia serious kihivyo mpaka alipoanza wazingua.

Kama akirudi kwa style hiyo hiyo sijui ni wangapi wataamini kuwa ni Yesu.
 
Ukiweza kuangalia vitu kwa jicho la rohoni, utabadili mawazo yako.
Hapana mkuu mimi nimeongelea maisha yake. Hebu fikiria jinsi alivyokuwa anapingana na sheria zao. Ni sawa leo uje uanze pingana na kanuni na sheria kibao za serikali.

Kuna watakaosema wewe chizi, vyombi vya dola vitakuita muasi au hata gaidi. Wengine watasema bangi inamsumbua huoni hata watu anaoongozana nao
 
Ukitaka kumfahamu Yesu wa kweli isome Qur'an.

Au tuulize tunaoisoma tukufahamishe.
Kwenye quran, visa ama matukio ya yesu yameandikwa kama matukio ya ajabu ajabu sana. Matukio yasiyo na kichwa wala miguu. Childish ambayo hata mtoto mdogo asingeweza kuyafikiria akiachilia mbali kuandikw akwenye kitabu cha watoto lakini yameandikwa kwenye kutabu cha Allah SAW. Ni vituko.
 

Luka 5:31-32 BHN​

31. Yesu akawajibu, “Wenye afya hawamhitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa.

32. Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi, wapate kutubu.”
Ndicho hiki nachosema mkuu. Yote alikuwa na majibu yake lakini kwenye jamii alikuwa anaonekana kama outcast.
 
Ukisoma na kutafakari kwa umakini kuhusu Yesu unagundua kwamba alikuwa ni wale watu ambao jamii inawachukulia kwamba wamepinda yani outcast...
YESU alikuwa anafanya ISHARA na MIUJIZA mbalimbali.

Kama: kuponya viwete, kuponya vipofu, kufufua wafu, kutoa Pepo wachafu, Kuamuru dhoruba, kuongeza vyakula, kutakasa wakoma, n.k.

Masuala ambayo yanafanywa na watu wa MUNGU PEKEE YAO. ISSUE ya mwanamke KAHABA ni issue ya kujinyenyekeza na kuomba msamaha kutokana na dhambi za huyo KAHABA.

LAKINI, lengo la YESU kuja ni kukomboa watu kutokana na utumwa wa dhambi, na watu hao ni lazima wajinyenyekeze na kujishusha.

KIFUPI: YESU angekuja TANZANIA watu wengi wangemwamini kutokana na ishara na MIUJIZA ambayo angeifanya.

FIKIRIA jinsi watu wanavyowafuata mitume na manabii ambao hawajafanya ishara yoyote zaidi ya kusababisha vifo vya watu na umasikini pamoja na kuwapiga fedha ndefu( halafu atokee mtu anayefufua wafu na kuponya viwete, vipofu, nk. Asifuatwe?, Nani kasema?)
 
Ndicho hiki nachosema mkuu. Yote alikuwa na majibu yake lakini kwenye jamii alikuwa anaonekana kama outcast.
Kuna wakati majIbu ya Yesu usipokuwa makini unaweza kuhisi jamaa alikuwa michosho sana, lakini alikuwa sahihi Mafarisayo walikuwa na maswali ya kiwaki sana ya kinafiki, kumjaribu na kejeli

Yesu ni mtu mmoja alikuwa mwana sana ila alikuwa straightforward
 
Ukitaka kumfahamu Yesu wa kweli isome Qur'an.

Au tuulize tunaoisoma tukufahamishe.
Qur'an na YESU wapi na wapi?

Mtume Muhammad amezaliwa mwaka 570 AD, yaani zaidi ya miaka 537 baada ya YESU.

KIFUPI: Mtume Muhammad hajui hata SURA ya YESU inafananaje.

Ni kichekesho kumuuliza mtu aliyeota ndoto juu ya YESU, ukamwacha yule aliyemwona YESU.

Kwahiyo, Qur'an haina uwezo wa kumwelezea YESU Kwasababu waandishi wake hawakuwahi kumshuhudia YESU kwa namna yoyote Ile( SAUTI yake au SURA yake). Hivyo hawana EYE WITNESS TO JESUS hivyo hata mahakamani Hawa hawawezi kuwa mashahidi.
 
Back
Top Bottom