Wee jamaa kama una sikio la kusikia nisikilize! Pamoja na ukweli ya kwamba uliyoyasema ni kweli, lakini Yesu alijitofautisha na kuwa mtu wa ajabu kuwahi kutokea kwa miujiza, busara, maarifa, unyenyekevu, huruma, n.k. kuliko binadamu yeyote aliyewahi kuishi! Alithibitisha torati ya Musa ya kuwa yule aliyetabiriwa kwa torati na manabii ndiye na kitendo cha kutomwamini kinawatia hatiani ya kwanini hawakumwamini! Baadhi ya miujiza aliyoitenda kuthibitisha Ndiye ni pamoja na:
1. Kufufua mtu aliyekufa siku 3 kaburini (lazaro),
2. Kutembea juu ya maji,
3. Kulisha mamillioni ya watu kwa mkate mmoja na samaki wawili,
4. Kujua maandiko yote ya torati bila kufundishwa,
5. kuponya viwete, vipofu, ukoma, nk, n.k, n.k; kwa ushahidi huu pamoja na unyenyekevu wa kukaa na watu waliotengwa na jamii kwa kuonekana hawafai sijui wana dhambi; vilimtofautisha na binadamu yeyote na hawakuwa na udhuru kwanini hawakumwamini?
Sababu nyingine kubwa ni kufufuka katika wafu na kuwatokea watu wengi pia mwili wake kutoonekana kaburini licha ya kuweka walinzi kulilinda kaburi. Sababu nyingine ni hile hali ya kustahimili mateso kwa masaa zaidi ya tisa ya kupigwa mijeredi na kujeruhiwa kuliko binadamu yeyote aliyewahi kuishi kwa kuchubuliwa na kubeba msalaba mzito! Hapakuwahi kutokea binadamu wa kuteswa kama Yesu alafu asife!
Binadamu wa kawaida ndani ya dakika au saa moja lazima ufe! Yesu alistahimili mateso ya kila namna ili binadamu tunapopitia magumu tusiwe na sababu ya kupinga wokovu! Naishia hapa kwa ujasiri mkubwa ya kwamba maisha ya Yesu hayakuwa maisha ya binadamu wa kawaida. By the way!
Akirudi atarudi kama mfalme na wala hatakanyaga ardhi na walokole atawanyakua juu na kukutana nao mawinguni! Hata hivyo nguvu za kuwezesha walokole kupaa na kunyakuliwa zitakuwa ndani yao kutokana na kazi za utumishi alizowapa wamtumikie!
Kuna walokole watashindwa kupaa na kubaki hapa duniani na kupitia mateso kama wale ambao hapo mwanzo walibeza maandiko!
Maisha ya sasa duniani walokole bado ni wachache! Wengi ni mapandikizi ya mpinga Kristo! Hata hivyo wanayohubiri ni kweli ya neno la Mungu! Mungu anaangalia Neno bila kujali linahubiriwa na nani?