Taswira ya Yesu anayehubiriwa ni tofauti na Yesu halisi

Taswira ya Yesu anayehubiriwa ni tofauti na Yesu halisi

Ukisoma na kutafakari kwa umakini kuhusu Yesu unagundua kwamba alikuwa ni wale watu ambao jamii inawachukulia kwamba wamepinda yani outcast...
Wee jamaa kama una sikio la kusikia nisikilize! Pamoja na ukweli ya kwamba uliyoyasema ni kweli, lakini Yesu alijitofautisha na kuwa mtu wa ajabu kuwahi kutokea kwa miujiza, busara, maarifa, unyenyekevu, huruma, n.k. kuliko binadamu yeyote aliyewahi kuishi! Alithibitisha torati ya Musa ya kuwa yule aliyetabiriwa kwa torati na manabii ndiye na kitendo cha kutomwamini kinawatia hatiani ya kwanini hawakumwamini! Baadhi ya miujiza aliyoitenda kuthibitisha Ndiye ni pamoja na:

1. Kufufua mtu aliyekufa siku 3 kaburini (lazaro),

2. Kutembea juu ya maji,

3. Kulisha mamillioni ya watu kwa mkate mmoja na samaki wawili,

4. Kujua maandiko yote ya torati bila kufundishwa,

5. kuponya viwete, vipofu, ukoma, nk, n.k, n.k; kwa ushahidi huu pamoja na unyenyekevu wa kukaa na watu waliotengwa na jamii kwa kuonekana hawafai sijui wana dhambi; vilimtofautisha na binadamu yeyote na hawakuwa na udhuru kwanini hawakumwamini?

Sababu nyingine kubwa ni kufufuka katika wafu na kuwatokea watu wengi pia mwili wake kutoonekana kaburini licha ya kuweka walinzi kulilinda kaburi. Sababu nyingine ni hile hali ya kustahimili mateso kwa masaa zaidi ya tisa ya kupigwa mijeredi na kujeruhiwa kuliko binadamu yeyote aliyewahi kuishi kwa kuchubuliwa na kubeba msalaba mzito! Hapakuwahi kutokea binadamu wa kuteswa kama Yesu alafu asife!

Binadamu wa kawaida ndani ya dakika au saa moja lazima ufe! Yesu alistahimili mateso ya kila namna ili binadamu tunapopitia magumu tusiwe na sababu ya kupinga wokovu! Naishia hapa kwa ujasiri mkubwa ya kwamba maisha ya Yesu hayakuwa maisha ya binadamu wa kawaida. By the way!

Akirudi atarudi kama mfalme na wala hatakanyaga ardhi na walokole atawanyakua juu na kukutana nao mawinguni! Hata hivyo nguvu za kuwezesha walokole kupaa na kunyakuliwa zitakuwa ndani yao kutokana na kazi za utumishi alizowapa wamtumikie!

Kuna walokole watashindwa kupaa na kubaki hapa duniani na kupitia mateso kama wale ambao hapo mwanzo walibeza maandiko!

Maisha ya sasa duniani walokole bado ni wachache! Wengi ni mapandikizi ya mpinga Kristo! Hata hivyo wanayohubiri ni kweli ya neno la Mungu! Mungu anaangalia Neno bila kujali linahubiriwa na nani?
 
Qur'an na YESU wapi na wapi?
Mtu Muhammad amezaliwa mwaka 570 AD, yaani zaidi ya miaka 537 baada ya YESU...
Wala hujakosea, upo sahihi kabisa, Qur'an ni "criterion" imekuja kubainisha ukweli.

Kama kuna agano la kale na agano jipya basi Qur'an ndiyo agano la Mwisho.

Mbona huulizi hilo baina ya agano la kale na jipya miaka mingapi imepita baina yake?
 
Hivi mkuu unajua Marko, Luka hawakuwepo wakati yesu yuko hai? Ajabu Maria Magdalena aliyekuwepo kitabu chake walikiondoa kwenye list ya vitabu vya biblia.
Walikuwepo akiwa hai.

LUKA aliongozana na PAULO katika safari mbalimbali.

Na pia habari za waandishi hao hazitofautiani na habari iliyoandikwa na MATHAYO( mwanafunzi wa YESU).

Maria Magdalena, pengine taarifa zake hazikujitosheleza au zilisimulia matukio fulani tu, halafu matukio muhimu akayapiga chini, na hiyo kitabu chake kilitumika kama taarifa ya ziada).
 
Wee jamaa kama una sikio la kusikia nisikilize! Pamoja na ukweli ya kwamba uliyoyasema ni kweli, lakini Yesu alijitofautisha na kuwa mtu wa ajabu kuwahi kutokea kwa miujiza...
Nahisi hata hukuelewa my point.

My point ni kwamba, lifestyle yake kwa jamii ile ilikuwa ni kama outcast. Kuanzia watu aliokuwa anaongozana nao, misimamo yake iliyokuwa dhidi ya kanuni na maisha ya watu wa kipindi kile.

Hata angelikuja leo bado angeonekana outcast.

Ni ngumu kwa mfano kumwmaini mtu anayeongozana na walevi na wazinzi kila mara na jibu lake awe anakwambia hao ndio watu anaowalenga kuwabadilisha. Mtu anayepinga sheria ambazo ni tamaduni za miaka na miaka.

Mtu ambaye anaongozana na masela halafu anajiita mfalme. Katika hali ya kawaida utasema huyu bangi inamsumbua.
 
Walikuwepo akiwa hai.
LUKA aliongozana na PAULO katika safari mbalimbali...
Luke hakuwahi kumfahamu Yesu wala kumwona. Alifundishwa Gospel na Paul. Kati ya hao waandishi wa gospel ya Yesu wawili kati yao hawakumfahamu Yesu personally labda mathew. Unless kama unaweza kunipa source inayosema otherwise mkuu
 
Nahisi hata hukuelewa my point.
My point ni kwamba, lifestyle yake kwa jamii ile ilikuwa ni kama outcast. Kuanzia watu aliokuwa anaongozana nao, misimamo yake iliyokuwa dhidi ya kanuni na maisha ya watu wa kipindi kile...
Bado uelewi! Kuongozana na walevi yeye alikuwa analewa? Kuongozana na makahaba yeye alikuwa kahaba? Kuongozana na majobless, je! yeye alikuwa ni jobless? Aliwapa ajira, chakula, uponyaji, n.k! Kijana okoka!
 
YESU alikuwa anafanya ISHARA na MIUJIZA mbalimbali.
Kama: kuponya viwete, kuponya vipofu, kufufua wafu, kutoa Pepo wachafu, Kuamuru dhoruba, kuongeza vyakula, kutakasa wakoma, n.k...
Wewe naye umepuyanga
Kilichokuwa kinaponya ni IMANI ya wahusika

Imani yako itakuponya au itakuangamiza.
 
Hata mimi niliwahi kuwaza hilo mkuu, kwa watu wa kipindi kile ilikua ni ngumu kuamini tofauti na sisi.
Hata sasa bado sana! Hizi dini zinamwamini Yesu lakini hazimtegemei na hivyo kuwadisqualify! Unatakiwa umwamini na umtegemee! Wengi yakiwakuta ya kuwakuta wanaenda kutambika na waganga wa kienyeji ndani ya dini hizo hizo!
 
Bado uelewi! Kuongozana na walevi yeye alikuwa analewa? Kuongozana na makahaba yeye alikuwa kahaba? Kuongozana na majobless, je! yeye alikuwa ni jobless? Aliwapa ajira, chakula, uponyaji, n.k! Kijana okoka!
Wewe ndiye huelewi sasa.

Jamii ya kipindi hicho ilikuwa inajitenga na watu wa namna fulani ambao yeye ndio alikuwa anazunguka nao. Haijalishi alikuwa hafanyi wanachofanya lakini ndio ilikuwa kampani yale.

So machoni mwao alikuwa kama outcast ndio maana hata walikuwa wanamshangaa inakuwaje anazunguka na watu kama wale.

Ingekuwa zama hizi angeonekana msela tu akiwa na masela wake
 
Kwamba alikuwa kama mtu aliyepinda halafu hapo hapo unamfananisha na mtu mwenye heshima zake anayeshangawa na wengine kwa kula na wenye dhambi!!!!embu nawa maji uso kwanza.


Kwa taarifa yako,Yesu alikuja kutengua dhana ya uyahudi kwamba Mungu ni wa sheria na masharti yasiyosameheka yakivunjwa,waliomuelewa walimuelewa kweli kweli,na waliompuuza walimchukulia kama mwenye kukufuru,mwenye kutengua kanuni za waheshimiwa makuhani na wafalme,ndio sababu ya pazia la hekalu kupasuka kati.

Alikuja kuwa jamaa wa usawa na haki kwa wote,masikini na matajiri,kwa vitendo na njia sahihi.
 
Kwamba alikuwa kama mtu aliyepinda halafu hapo hapo unamfananisha na mtu mwenye heshima zake anayeshangawa na wengine kwa kula na wenye dhambi!!!!embu nawa maji uso kwanza...
Kuna waliomkubali ndio baadhi wakawa bado wanashangaa mbona jamaa huyu bado anazunguka na hawa watu waliopinda?

Ndio maana mpaka leo hao Wayahudi ambao alijitambulisha kuwa mfalme wao hawamfuati wala kumkubali. Nasikia wanaamini bado hajaja. Huenda taswira waliokuwa nayo juu ya ujio wake ilikuwa tofauti.

Hebu na wewe fikiria, anatokea mtu anatembea na wavuta bangi na walevi, halafu anakwambia yeye ndiye masiah. Itakuwa vigumu kuamini hata kama yeye si mvuta bangi wala mlevi.
 
Kuna waliomkubali ndio baadhi wakawa bado wanashangaa mbona jamaa huyu bado anazunguka na hawa watu waliopinda?
Ndio maana mpaka leo hao Wayahudi ambao alijitambulisha kuwa mfalme wao hawamfuati wala kumkubali. Nasikia wanaamini bado hajaja. Huenda taswira waliokuwa nayo juu ya ujio wake ilikuwa tofauti.
Hebu na wewe fikiria, anatokea mtu anatembea na wavuta bangi na walevi, halafu anakwambia yeye ndiye masiah. Itakuwa vigumu kuamini hata kama yeye si mvuta bangi wala mlevi.

Wayahundi bado wanasumbuliwa na egoes.na hiki ndicho kilimleta Yesu.kuna mapimbi hata leo hapa duniani wanajipa ubora na ndio hawa wana ajenda zao kuhusu NWO,hawataki kabisa watu wamjue Yesu ndio sababu zikazaliwa dini za mchongo ili kumfanya aonekane alikuwa wa kawaida na ni mtu kama wengine tu.


Leo hii ukianza kampeni ya kuwathaminisha masikini,wanaoishi masaki na mbezi watakuona mfitini unawaharibia loyalty yao,watakuchukia na kukukwamisha kwa namna yyote watakayoona inafaa.
 
Bado uelewi! Kuongozana na walevi yeye alikuwa analewa? Kuongozana na makahaba yeye alikuwa kahaba? Kuongozana na majobless, je! yeye alikuwa ni jobless? Aliwapa ajira, chakula, uponyaji, n.k! Kijana okoka!
Nafikiri wewe ndo hujamuelewa jamaa. Anachomaanisha ni kuwa Yesu kwa hadhi yake na jinsi jamii ilivokua inamchukulia na kutarajia aweje kwenye jamii yeye tena watu aliokua ana interact nao walikua sio jamii ilitarajia. Mafarisayo waliamini ukiwa unasali basi hutakiwi kupishana hata na kahaba sasa kwa Yesu ikawa tofauti thus why iliwashangaza watu na ndiyo mana ilikua vigumu kwa wayahudi kuamini kua ndiye Masihi muhubiriwa na ndivyo hivyo hivyo inaweza kua vigumu kwa jamii ya leo. Isipo kuwa His second coming itakua in different fashion. This time there will never be Mercy.
 
Back
Top Bottom