Tathmini fupi mechi ya mc Alger Vs Yanga

Tathmini fupi mechi ya mc Alger Vs Yanga

Gari imewaka...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Sindano fc.
 
Mchezo ulikuwa mzuri timu zote zilicheza Kwa mipango mizuri
Coach Saed umekuja Kipindi kigumu, nashauri upweke muda

Nampongeza coach Saed Ramovic ameingia na mbinu nzuri kiufundi

Tatizo la coach anakosa mamlaka hajiamini kabisa

Nimeshangaa sub ya Aziz ki kutoka mapema vile

Coach Saed anisikilize Duke Abuya siyo namba 6 Haiwezi, kila akicheza Yanga itafungwa tu
Yaani coach Saed ana copy team iliyomfunga Namungo ndo anaipeleka CAFCL, umeniboa sana

Mechi ijayo mpe Mkude acheze acha ubishi, Mkude alicheza vizuri mechi zote za Mamelod na team haikufungwa kabisa

Kibabage huyu yumo uwanjani kutimiza idadi ya wachezaji, yaani ni kama under 17 anacheza kwenye senior team, hakabi, hashambulii Kwa kifupi kibabage hana hata hadhi ya kucheza Yanga Princess

Pacome amecheza ovyo sana.
Huyu kijana pombe na maisha yake Masaki yameua kipaji chake, hana fitness kabisa
Coach Saed mpige bench Pacome hana fitness japo ana talent kubwa mpo nafasi Farid au Shekhan

Max, Muda, Yao mmeonyesha game nzuri mno

Musonda ni mchezaji wa kawaida mno , hachezi kama striker anazulula tu, hasimami mbele, coach Saed mpe nafasi Baleke au alikuchukulia mke

Coach Saed jitahiti iwe na Mamlaka Pacome na Kibabage waweke bench Bora tucheze pungufu

Usajili leteni beki wa kushoto na huyo Boka na mambio yake kama farasi ana miguu ya vioo, mchezaji Gani anavunjika kama glass pia kiungo mkabaji
Sitaki kumwona Kibabage Yanga

Mwisho nasema Bado points 12 zipo mbele Nina Imani Yanga tunaenda Quarter finai

Yanga bingwa
Lakini unakumbuka kuwa Yanga inafungwaje?😂😂😂
 
Attachments

  • Screenshot_20241116-181034_1.jpg
    Screenshot_20241116-181034_1.jpg
    193.7 KB · Views: 4
  • Screenshot_20241203-221155_1.jpg
    Screenshot_20241203-221155_1.jpg
    270.1 KB · Views: 2
Si vibaya mkishindwa huko mrudi kwenye kombe letu la shirikisho [emoji1787][emoji1787][emoji1787].
huko Kuna wenyewe
Wakishindwa wanarudi ligi kuu, hakuna Best loser safari hii.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
IMG-20241207-WA0005.jpg

Kumeanza kuchangamka!!
All the best kibonde w kundi
 
Ata kama Hersi asimpende Kibabage Bado Hersi sio Kocha, lakini kama iyo namba Kibabage Haifanyi vizuri na Boka anauguza Maumivu ulitaka nani acheze nafasi iyo!!
Kumbuka Gamondi hakua anautumia mawinga Asilia, yeye Mabeki wa pembeni ndio Ma winga wake na Kocha wa Sasa Mpaka Sasa anautumia mfumo uo.

Haiwezekani mfumo umtake Ki babage awe kama beki /winga alafu kwenye Counter za Mpinzani awe kwenye nafasi yake ya kuzuia.
Kumbuka Counter Attack zote ni pasi Chache za Mpinzani ili kwenda kushambulia eneo la wazi la timu inayo shambulia.
Kinacho tokea kwenye mfumo ni yule namba 6 anaye takiwa kuzuia Counter attack kwenye eneo ambalo mfumo ume mtaka beki wake kua katika eneo la ushambuliaji yeye kuchelewa kufika ili kuziba eneo ilo.

Kinacho tokea Beki wa kati lazima atoke kati aende kuzuia shambulizi ambalo namba sita na beki wa pembeni lime wapita.
Sasa washambuliaji wa counter wakiwa na namba nzuri Wana u shift mpira eneo Lingine inafanya Diffence kukatika na Goli kufungwa.

Kinacho hitajika si ku mlaumu ki babage au Hersi , kwakua tayari timu ipo kwenye mashindano na Ina majeruhi.
Inatakiwa Kibabage aongeze ufanisi akilikaribia lango la mpinzani au Kocha aje na mfumo utakao Fanya mabeki wote wawepo nyuma muda wote wa mchezo stail inayobtumiwa Ugenini.
Magoli tuliyofungwa Jana hasa la kwanza, timu yote ilikua inazuia kwaiyo ni Goli la timu.

Goli la pili Sina wa ku mlaumu kwakua Kibabage alizidiwa maarifa ,Mwam nyeto alizidiwa kasi kama alivyozidiwa baka na Hilal Dar, Kipa Diara asingeweza ku weka mikono kwenye mpira ambao mshambuliaji ameingiza mguu.
Ni kuweka Afya Yako rehani kwa kuikubali Ajali mbaya.
Kwanini yanga wana namba 6 moja.ndiyo maana tunasema yanga hawakujipanga
 
Mchezo ulikuwa mzuri timu zote zilicheza Kwa mipango mizuri
Coach Saed umekuja Kipindi kigumu, nashauri upweke muda

Nampongeza coach Saed Ramovic ameingia na mbinu nzuri kiufundi

Tatizo la coach anakosa mamlaka hajiamini kabisa

Nimeshangaa sub ya Aziz ki kutoka mapema vile

Coach Saed anisikilize Duke Abuya siyo namba 6 Haiwezi, kila akicheza Yanga itafungwa tu
Yaani coach Saed ana copy team iliyomfunga Namungo ndo anaipeleka CAFCL, umeniboa sana

Mechi ijayo mpe Mkude acheze acha ubishi, Mkude alicheza vizuri mechi zote za Mamelod na team haikufungwa kabisa

Kibabage huyu yumo uwanjani kutimiza idadi ya wachezaji, yaani ni kama under 17 anacheza kwenye senior team, hakabi, hashambulii Kwa kifupi kibabage hana hata hadhi ya kucheza Yanga Princess

Pacome amecheza ovyo sana.
Huyu kijana pombe na maisha yake Masaki yameua kipaji chake, hana fitness kabisa
Coach Saed mpige bench Pacome hana fitness japo ana talent kubwa mpo nafasi Farid au Shekhan

Max, Muda, Yao mmeonyesha game nzuri mno

Musonda ni mchezaji wa kawaida mno , hachezi kama striker anazulula tu, hasimami mbele, coach Saed mpe nafasi Baleke au alikuchukulia mke

Coach Saed jitahiti iwe na Mamlaka Pacome na Kibabage waweke bench Bora tucheze pungufu

Usajili leteni beki wa kushoto na huyo Boka na mambio yake kama farasi ana miguu ya vioo, mchezaji Gani anavunjika kama glass pia kiungo mkabaji
Sitaki kumwona Kibabage Yanga

Mwisho nasema Bado points 12 zipo mbele Nina Imani Yanga tunaenda Quarter finai

Yanga bingwa
Huwezi ukawa bingwa wa Mchongo ukafanya vzr champions League naiona YANGA ikimaliza mechi ikiwa mkiani na ikiturudisha kwenye Timu moja kweli hii ni aibu ya Karne
 
Tatizo Utopolo FC mmekariri matukio,,, mlisema hata msimu uliopita mlianza kwa kufungwa, haya mechi ya pili hiyo 🤣🤣
Mmekariri eti Mkude aliwaweza Mamelodi bora angecheza yeye badala ya Abuya..🤣🤣, kwamba mnafananisha ushambuliaji wa MC ALGER na Mamelodi,,,
 
Mmekaa mkiani mwa kundi, nakuambia Yanga haiwezi kupata zaidi ya points 3 kwenye hili kundi acha matarajio yasiyo na miguu wala kichwa.
Msimu uliopita hadi raundi ya pili Yanga alikuwa mkiani akiwa na point moja tu lakini mwisho wa siku alifuzu
 
Imepita miaka mingi sana sijawahi kuona Yanga mbovu, iliyocheza hovyo kama jana. Kimsingi Yanga ilifia mikononi kwa Ramovic.

Je Ramovic alifeli wapi?

Yanga ilicheza vizuri maeneo mawili tu; Eneo
la beki, na la kati - Abuya na Max walifanya vizuri. Eneo la ushambulizi walikua vibogoyo - Musonda, Mudathir, Pacome, na Aziz walikua hawana meno. Kwanini?

Mfumo ulikua 4-2-3-1

Abuya na Max walianza kama 6 na 8, Mudathiri namba 10, Musonda winga ya kushoto na Pacome kulia, Juu kabisa alianza Aziz Ki kama mshambuliaji kiongozi. Je Aziz Ki ana sifa za kucheza hapo? Jibu ni hapana. Hana sifa ya kuwa mshambuliaji wa kati kama majukumu yalivyohitaji acheze hapo jana

Aziz Ki kama mshambuliaji wa kati lilikua kosa la kwanza. Sio mchezaji ambae ataweza kupambana kwenye 1 vs 1 na beki wa kati kwenye mipira ya vichwa, kutunza mipira kama streka. Aziz sio mchezaji anaetakiwa kuwa limited kucheza jukumu fulani pekee, ni aina ya mchezaji anaetaka uhuru.

Aziz Ki akianza kama streka wako, unawapa unafuu mabeki wa upinzani kwa kutengeza mashambulizi kwa uhuru maana wanakosa presha yoyote. Mc Alger walikua na advantage ya wachezaji wengi zaidi katika build-up yao

Kosa la pili ilikua kuanza na Musonda.

Musonda ni mchezaji mpambanaji, ila sio mfanisi sana anapokua na mpira. Anakua bora akiwa eneo la karibu na box, ila sio mbali na hapo. Musonda kama winga ya kushoto, labda alipangwa pembeni kusaidia kuzuia mashambizi ya Mc Alger. Lakini haukua mpango sahihi. Kushoto kwa Yanga hawakua na madhara

Mudathir kucheza namba 10 lilikua kosa la tatu. Hilo ni eneo linalohitaji mchezaji mwenye akili za ziada za kutengeneza nafasi. Muda hana sifa hizo.

Yanga ilibadilika kuanzia dk ya 83. Kwanini?

Aliingia Dube kama Streka, Chama alirudi namba 10 ambapo alipokua anacheza Mudathir aliyetoka. Kuanzia dk ya 83 Yanga ilishambulia, ilicheza katika mfumo sahihi na wachezaji kuwepo katika maeneo sahihi.

Mfumo wa Ramovic ulifanya Yanga ishindwe kuwajaribu Mc Alger. Mm naamini kama Yanga ingepanga kikosi vizuri, mechi isingeisha kama ilivyoisha. Kifo cha Yanga, Muuaji ni Ramovic.

Na huu ndiyo ukweli🦾🦾🦾
 
Huwezi ukawa bingwa wa Mchongo ukafanya vzr champions League naiona YANGA ikimaliza mechi ikiwa mkiani na ikiturudisha kwenye Timu moja kweli hii ni aibu ya Karne
Duh umewahi hata kucheza cha ndimu? Hivi upo sawa kichwani mpaka useme eti yanga alikuwa bingwa wa mchongo? Kwahiyo nani alistahili kuwa bingwa msimu uliopita?
 
Back
Top Bottom