Tathmini ya mapato ya kilimo cha michungwa 1000 baada ya miaka 3

nimekujbu lkua sina utaalamu wa kujua maeneo ila nimeona katika mkoa wa pwani,dar, tanga na morogoro nimesikia sasa maeneo mengine waulize wataalamu wa climate
 

mkuu ... ni hatari sana kufanya kilimo katika mazingira yetu kwa kutumia google

swali moja tuu kwako ..... hichi unachotuambia ni idea tu au umeshakifanya kwa kiwango fulani hata kama ni kidogo,

pia nina mashaka na bei ya kuuzia machungwa .... hapa dar wakati wa msimu machungwa sokoni huuzwa hadi sh.50 bei ya reja reja .... je bei yako ya kuuzia uliyotoa ina uhalisia?
 
nimekujbu lkua sina utaalamu wa kujua maeneo ila nimeona katika mkoa wa pwani,dar, tanga na morogoro nimesikia sasa maeneo mengine waulize wataalamu wa climate

Mkuu ni ukubwa gani wa Shamba unahitajika? vipi mtu akiwa na heakari kama Tano zinatosha? na vipi bei ya Mche mmoja wa hiyo aina unayo sema,
 
sikiliza machungwa aina hii ni makubwa na matamu ndio yale unayouziwa 300 mjini kwa matenga na kwa quality yake waweza kuuza hata super market na aliekua na muda aje nimpeleke akaone nilipofikia nimeanza na miche 300 ila sasa nina michungwa 21000 na sina eneo kubwa ila ningepanda hata kama ni michungwa milioni na nia na madhumuni ya kukupeni wazo hili nataka kuwauzia miche ili na nyinyi mufaidike bado nazalisha miche na shamba langu limejaa hapa natafuta soko la miche
 
kwa heka tano ni miche makadirio ni kama miche 350 zinatosha na tadhmini ya miche 350 kila mwaka unaweza kuingiza 400,000,000
 
ila ni baada ya miaka mitatu miche huanza kuzaa na pia inahitaji ushughulikiaji na katika miezi 14 ya mwanzo kila siku kila mche umwagiliziwe liter mbili
 

Usichukue muda mrefu mkuu tafadhali urudi kutoa uzoefu
 
dah .... ndugu yangu

Mkuu vp mbona unashtuka mashetani yako hayapendi kuwa milionea nini? Mi bado nawaza huo mchungwa wenyew uwezo wa kubeba machungwa elfu nne ambayo uzito wake unakaribia tani moja labda huo mchungwa unazaa mara tatu kwa mwaka ukijumlisha uzao wote ndo unatapata hiyo idadi ya machungwa au wenyewe unazaa non stop kila mwezi unavuna hauna msimu mleta mada tafadhali fafanua it's too good to be true
 

Weka picha basi mkuu tuone ulivyo fanya mbona maneno mengi???
 
jamani mm nipo dar hapa hayo mashamba yako tanga nikifika nitawatumia sasa hivi sina picha hapa yaliyopo hapa dar bado ni miaka miwili huko tanga nina michungwa 2000 nitawaonyesha nikifika!
 

Aweke picha tuuone ukiwa shambani kwake maana nahisi huu mchungwa utakua mkubwa kama mkaratusi!machungwa 4000 tena kwa mbwembwe anasema ni makubwa!Ni mchungwa wa bustani ya EDEN au?!
 
jamani mm nipo dar hapa hayo mashamba yako tanga nikifika nitawatumia sasa hivi sina picha hapa yaliyopo hapa dar bado ni miaka miwili huko tanga nina michungwa 2000 nitawaonyesha nikifika!
Hata huo wa Dar tupia tu sio mbaya kwa kuazia then ukifika huko Tanga tupia wala haitobadili maana...
 
Mkuu Kahtan Ahmed naomba jina la hayo machungwa itakuwa rahisi kwangu kuelewa.Unajua Brasil wanalima machungwa ya aina nyingi kama ilivyo Tanzania.

 
Last edited by a moderator:
Niliwahi kununua chungwa fulani hivi pale MSAMVU katikati ya mwaka jana na niliuziwa kwa tsh300 per pc,bila shaka ndio machungwa hayo na kama ndiyo yenyewe basi this is a big deal maana ni matamu sana.
Mkuu:Kahtan Ahmed"Ebu tupe jina la huo mchungwa ili tu google tupate some more details.
But hongera kwa kazi nzuri na ntakutafuta kwa msaada zaidi.
 
sasa hii ni biashara mm nauza wazo la biashara sasa kama nikikutajia na jina si biashara ndio imekufa kama unahitaji tukae kwenye meza tuongee biashara!
 
mm hapa nafanya biashara kama kuna yoyote aliekua intrest na kilimo hiki tukae mezeni tuongee biashara
 
kama unajiona una ardhi maeneo hayo nilisema na una nia ya kilimo hiki na pesa unayo kwa ajili ya gharama na kunilipa mm nitafute tuake mezani ww unataka jina kwani mm nilietafuta hizi details na kuzifanyia kazi nimepoteza muda wangu na gharama zangu wacha kung'ang'ania jina siwezi kuwapa jina hata siku moja na nikifika tanga nitawapa picha za hiyo michungwa
 

mkuu ... kwa mchanganuo huu wa mapato .... ukipeleka business plan banki wataita polisi
 

Ni vizuri ukaendelea na udalali wa ile gari Tarios kwenye thread yako nyingine kuliko kuleta porojo kwenye kilimo. Nikuelimishe kuwa machungwa na jamii nyingi za citrus family unapofanya 'budding' ni kweli kuwa unapunguza muda wa kuanza kuzaa matunda. Lakini kwa miaka michache ya mwanzo matunda huwa ni kidogo, kwa vile mti unajaribu kuzaa kulingana na uwezo wake in terms of strength, ndio maana ukiwa mkulima mzuri unashauriwa kupunguza baadhi ya maua au later matunda ili mti usielemewe na kuvunjika. Sasa kimantiki si kweli mchungwa wa miaka mitatu kubeba machungwa 4000, labda machungwa hayo yawe na saizi kama karanga....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…