Nimejarubu Ku google kwenye Nchi zinazo ongoza kwa kilimo Cha Machungwa bado sijapata mchungwa wa Kubeba hayo machungwa, Inaonekana itaanzia Tanzania kwa mara ya kwanza
kama wapata burudani lipia kabisa ,halafu unasema nimetukana? nimemtukana nani? nimejibishana na unanilaumu mm je umeangalia huyo anekiuliza kauliza nn mpaka tukabishana wacha mambo yenu hayo hamutaki kufanya kazi kisha mnasingizia serikali hakuna serkali hata moja duniani inayogawa fedha! fanyeni kazi nyinyi!
Halafu inaonyesha hata shule hamna kunaserikali nyingi tu duniani zinatoa hela za bure kwa wananchi wake (Unemployment Benefits) na hata Africa Gadafi alikuwa anatoa kwa wananchi wake na acha kuwaambia watu hawataki kazi kisa wamekuchallenge kidogo tu unawajua hao watu humu unaosema hawataki kazi? au kazi ni kulima michungwa yenye uwezo wa kubeba machungwa mengi kuliko uzito wa mti wenyewe? Jipange dogo
Kaka huyu dogo ni Pimbi sana ana majibu ya hovyo sijawahi ona na bado anatoa ideas za Kitapeli humu eti mchungwa unaweza kubeba machungwa makubwa 4000
Ndugu yangu Forum ya Ujasiria mali huwa inawatu wastaarabu kabisa huku watu hubadilishana mawazo kwa ukarimu na upendo wa ajabu, hii forum ilishanisisimua sana jinsi watu wanavyosimuliana matatizo na kupeana mawazo ya ufumbuzi, kamwe sikumbuki kusoma mtu akimdhihaki au kukebehi mwingine kama kwenye viwanja vingine huko! Lakini naona taratibu virusi wameanza kuingia huku naomba muweze kutambua mapema virusi kama hiki ili tusipotezeane channel!
kwa sasa wananitosha maana hiyo miche 5700 wameshaimaliza kwa bei ya 3000 na hakuna hata mche mmoja mpaka msimu mwingine nyinyi endeleeni kupiga soga! hao jamaa baada ya miaka mitatu watakua wamewapiga gap la ajabu ninachopokea kutoka sasa ni order tu basi!
,ghrama
ekari 1 = michungwa 76
michungwa 1000 = ekari 13.1
mwaka wa kwanza
miche 1000 kila mche tsh 1500 -- 1500*1000 =tsh 1,500,000/=
kutayarisha shamba ekari moja tsh 30000 -- 30000*13 =tsh 390,000/=
kuchimba mashimo kila shimo tsh 300 -- 300*1000 = tsh 300,000/=
kupanda kila kupanda mche mmoja tsh 200 -- 200*1000 = tsh tsh 200,000/=
mbolea samadi kila ekari tsh 20000 -- 20000*13 = tsh 260,000/=
dap(50 kg) kila ekari tsh 40000 -- 40000*13 = tsh 520,000/=
can(50 kg) kila ekari tsh 36000 --36000*13 = tsh 468,000/=
dawa kila ekari tsh 20000 -- 20000*13 = tsh 260,000/=
kupalilia kila ekari tsh 40000 -- 40000*13 = tsh 520,000/=
mwaka wa kwanza =4418,000/=
mwaka wa pili ni kupalilia tu 520000/= 520,000/=
mwaka wa tatu ni kupalilia na kuvuna
kupalilia 520,000
kuvuna 1,400,000
mwaka wa tatu = 1920,000/=
gharazama ya kumwagilizia kwa muda wa miezi 14
kisima kuchimba 3500,000
tank za maji 1200,000
irrigation system pipe 700,000 = 5400,000/=
total 12,258,000/=
kilimo cha umwagiliziaji ni bora kwasababu ukishapanda kila mche kwa kila siku unahitaji kumwagiliziwa lita mbili za maji kwa muda wa miezi 14 na kwa uhakika utavuna kile unachokihitaji
madesa yameshaaaaanza sasa....cost benefit analysis sijaiona hapa mkuu,wazo ni zuri,ingia chimbo vzuri ili na mm mwenye kishamba changu kokadenguno,katesh nifaidike,nakusubiria mkuu
Mkuu kahtan Ahamed heshim sana,
Nimepitia bandiko lako nikaona yapo baadhi ya mambo yanahitaji kuboreshwa kidogo.
Kwanza hakuna mchungwa unaweza kuzaa chungwa 4,000.Uzoefu wangu wa kulima machungwa wa zaidi ya miaka mitano mti mmoja ni kati ya chungwa 600 - 800 katika msimu mmoja.
Kuna aina nyingi za chungwa zinazolimwa Tanzania hasa mikoa ya ukanda wa Pwani ie Tanga,Pwani,Dar na Morogoro.
[1] Msasa (Kubwa na Ndogo) hii ni aina nzuri ya chungwa,inaweza kusafirishwa umbali mrefu bila kuharibika.Soko lake kubwa ni Kenya na miji ya Dar,Arusha,Kilimanjaro ....
[2] Valensia ni aina ya chungwa linaloweza kusafirishwa mbali.Aina hii ya Chungwa ipo kwa wingi Muheza na kidogo limeanza kulimwa maeneo ya Korogwe na Handeni (Michungwani,Kwedi Zinga na Kabuku) Uzuri wa Valensia msimu wake mara nyngi unatokea wakati msimu wa chungwa umekwisha au machungwa yanakuwa hayapo sokoni kwa wingi.Wakulima wengi wanapendelea kulima aina hii ya chungwa kwasababu za kibiashara zaidi.
[3] Jaffar ni aina ya chungwa kubwa zinazozaa sana mara nyingi msimu wake wa mavuno unagongana na Msasa.Jaffa ni kubwa,lina maji mengi,ni tamu sana,linaweza kuliwa hata kama halijaiva vizuri.Ubaya pekee wa Jaffa ni kuharibika kwa wingi linaposafirishwa mbali.wafanyabiashara wengi hawapendi kuyanunua kwa wingi kwa kuhofia kuharibika yanapofika sokoni.Jaffa si chungwa zuri kwa biashara lakini si vibaya ukayachanganya kidogo shambani let say katika eka 13 ukaweka eka 1.
Nitarejea baadae kukupatia uzoefu wangu wa namna bora ya kuanzisha shamba la michungwa,miembe na minanasi ukipenda stay tune.
sikilizeni kama mnataka kujua waulizeni wataalamu wenu juu ya machungwa aina ya ventore kisha mpate details mana naonekana kama nadanganya na hiyo miche ya pichani ni machungwa yaliyopewa na sikusema kama ni ya miaka mitatu ila nimetoa kwa uthibitisho
Mh, kwani kwenye red hapo si ndo aina yenyewe ya machungwa yanayonadiwa au...!!!? Mbona mleta mada kashayataja halafu akasema hayataji ng'oooo eti ni bidzshnesh...mh..! tusije tukawa tushavurugwa hapa...mwe...!!!
Tatizo uki google hiyo Ventore,huipati hata kwa bahti mbaya:confused2::confused2: