Tathmini ya mapato ya kilimo cha michungwa 1000 baada ya miaka 3

Tathmini ya mapato ya kilimo cha michungwa 1000 baada ya miaka 3

sikilizeni kama mnataka kujua waulizeni wataalamu wenu juu ya machungwa aina ya ventore kisha mpate details mana naonekana kama nadanganya na hiyo miche ya pichani ni machungwa yaliyopewa na sikusema kama ni ya miaka mitatu ila nimetoa kwa uthibitisho
 
kwa kiukweli kaka sina utaalamu wa kujua ni maeneo gani ila maeneo ambayo nina ushahidi nayo ndio hayo niliokwambia na kuhusu mkoa wako kaka bado sijajua mana mm si mtu wa climate
 
mm nina uhakika na niliyokwambia kua mche mmoja unazaa mpaka 4000 na isipokua wakulima waliowengi hata hao wanaopanda valencia hawafuati masharti ya kilimo cha machungwa michungwa ya aina ninayokwambia ni kwamba inauwezo wa kuzaliasha 4000 ikiwa utafuata masharti niliyokueleza katika gharama hasa katika umwagiliziaji
 
maendeleo hayaji kwa ubishi na kama umeamua kukaidi mm wala hinizidishii wala kunipunguzia bali nafurahi kuona kuna watanzania wanahitahi kuelewa niacho waeleza kwa mafanikio kama ww upo shambani tangu kipindi cha ukoloni hiyo ni juu yako
 
sikusema kama hii picha ni ya michungwa ya umri wa miaka 3
 
sikiliza bluetooth
gharama zake zinamtiririko wa maelezo kweli ndio mana sikupata muda wa
kuandika hapa ila nitakuandikieni!

cost benefit analysis sijaiona hapa mkuu,wazo ni zuri,ingia chimbo vzuri ili na mm mwenye kishamba changu kokadenguno,katesh nifaidike,nakusubiria mkuu
 
siki mm si mtaalamu sana wa kuandaa report mzazi ila wazo ninalo na limekamilika!
 
Kijana hujanijibu swali langu kuhusu irrigation
 
Hongera sana kwa taarifa. Swali langu ni kuhusu aina ya mchungwa, na jina lake kitaalamu? Je soko la haya machungwa baada ya kuvuna utauza wapi yote uweze maliza shambani bila kuharibika?
 
mm si mtaalaam wa irrigation ila rabda nikupeleke sehemu ukaone jamaa walivyofanya irrigation yao nzuri na ni ya kieconimic
 
aina hii ya michungwa mjomba ni magumu makubwa na matamu suala la soko ondoa shaka mm nadhani ningewaonjesha aina hiyo ya machungwa subiri niagizie halafu nitawaambia muje muchukue moja moja kwa ushahidi kisha mtanambia wenyewe!
 
mm sina utaalamu na irrigation ila nikupeleke shambani kwa rafiki yangu halafu uone jinsi alivofanya very intresting na economic
 
songea sina ushahidi kama aina hii ya michungwa itakubali!
 
Nimekukubali mkuu Kahtan Ahmed kwa kuwa muwazi(honest enough) na pia kua tayari kuwasaidia na wengine! Swali langu kwako ni je michungwa hiyo inamea sehemu ya pwani peke yake?
 
Last edited by a moderator:
yoyote anaehitaji miche anipe order then nitawataarifu bei mana sasa imekua adimu!
 
Mkuu kahtan Ahamed heshim sana,

Nimepitia bandiko lako nikaona yapo baadhi ya mambo yanahitaji kuboreshwa kidogo.

Kwanza hakuna mchungwa unaweza kuzaa chungwa 4,000.Uzoefu wangu wa kulima machungwa wa zaidi ya miaka mitano mti mmoja ni kati ya chungwa 600 - 800 katika msimu mmoja.

Kuna aina nyingi za chungwa zinazolimwa Tanzania hasa mikoa ya ukanda wa Pwani ie Tanga,Pwani,Dar na Morogoro.

[1] Msasa (Kubwa na Ndogo) hii ni aina nzuri ya chungwa,inaweza kusafirishwa umbali mrefu bila kuharibika.Soko lake kubwa ni Kenya na miji ya Dar,Arusha,Kilimanjaro ....

[2] Valensia ni aina ya chungwa linaloweza kusafirishwa mbali.Aina hii ya Chungwa ipo kwa wingi Muheza na kidogo limeanza kulimwa maeneo ya Korogwe na Handeni (Michungwani,Kwedi Zinga na Kabuku) Uzuri wa Valensia msimu wake mara nyngi unatokea wakati msimu wa chungwa umekwisha au machungwa yanakuwa hayapo sokoni kwa wingi.Wakulima wengi wanapendelea kulima aina hii ya chungwa kwasababu za kibiashara zaidi.

[3] Jaffar ni aina ya chungwa kubwa zinazozaa sana mara nyingi msimu wake wa mavuno unagongana na Msasa.Jaffa ni kubwa,lina maji mengi,ni tamu sana,linaweza kuliwa hata kama halijaiva vizuri.Ubaya pekee wa Jaffa ni kuharibika kwa wingi linaposafirishwa mbali.wafanyabiashara wengi hawapendi kuyanunua kwa wingi kwa kuhofia kuharibika yanapofika sokoni.Jaffa si chungwa zuri kwa biashara lakini si vibaya ukayachanganya kidogo shambani let say katika eka 13 ukaweka eka 1.

Nitarejea baadae kukupatia uzoefu wangu wa namna bora ya kuanzisha shamba la michungwa,miembe na minanasi ukipenda stay tune.
 
Last edited by a moderator:
nashkuru sana kwa maelezo yako ila nakuomba nikwambie kitu kwamba usikatae mm nina baba angu tangu enzi za ukoloni ishu zake ni michungwa ila sasa ameng'oa michungwa ya aina zote ikiwemo valencia,jaffer na msasa na amepanda aina hii ya michungwa ninayokueleza hemu google machungwa toka brazil then angalia idadi kuna michungwa inazaa mpaka 16000 kwa kila mchungwa jaribu kufuatilitilia kilimo vizuri wacha kukurupuka
 
Back
Top Bottom