Uchaguzi 2020 Tathmini yangu juu ya Uchaguzi Mkuu 2020: Hakuna sababu nzuri ya kukataa kuteua wabunge wa Viti Maalum CHADEMA

Tabia ya kushindwa kutofautisha hoja na mleta hoja ni dalili kwamba Watanzania wenye elimu iliyo chini ya kidato cha nne wanafikia 90%, na wewe ni miongoni mwao.

Sio lazima uandike chochote. Ukimya nao unakubalika.
Pole sana! Kuna nyakati elimu inaweza kushindwa kukusaidia hata wewe mleta mada pale unaposhindwa kutofautisha ushabiki na uhalisia baki na ujinga wako! Kaa ukijua hakuna coalition yoyote itasafisha huu uchafuzi mkuu
 
Ndiyo maana polepole aliwaita cjadema Malaghai wakubwa.
 
Hivi nyinyi watu was CCM si mlipiga kampeni nchi nzima na mwenyekiti wenu akawaambia Nileteeni Gwjimaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa . Sasa mnataka nini tena wakati wapinzani wanakwamisha maendeleo ya nchi kwa mtazamo wa dark ages wa chairman wenu . Sasa hivi nyinyi maccm mfocus vitu viwili , mosi andaeni utetezi wa mashtaka yanayowakabili ICC ambao hata hivyo hamna kwa video zilizotumwa huko , pili andaeni mipango ya kupandisha kodi nyingi sana kwenye bidhaa mbalimbali mwakamue raia mpaka damu , maana mabeberu hawatoi hata mia . Yaani wawasaidie halafu mje na kauli za kishamba na kilimbukeni za palamihogo wenu huyo .
 

Kwanza, sijui umeielewaje hoja ya mdau Tindo kwamba Bunge letu halina meno. Hata wewe unajua kuwa Bunge linaendeshwa kwa maagizo. Kama ilivyo kwa taasisi nyingine za umma, haliko huru.

Pili, unaeleza kama vile CHADEMA “wamezuia” wabunge wa viti maalum kwenda bungeni. Kama vile unataka kudai kuwa CHADEMA wamekiuka misingi ya demokrasia. Sivyo? Sijui kama una habari za ndani za mchakato wa CHADEMA wa maamuzi kuhusu kupeleka hao viti maalum bungeni. Wewe unajua kama vikao rasmi havijakaa na kuamua wasiwe na wabunge wa viti maalum safari hii? Mimi sijui.

LAKINI, all in all, hiyo hoja kwamba wabunge wa viti maalum watakuwa na sauti ya kudai kura zilizoibiwa na kuwasilisha/kusimamia hoja nyingine muhimu za CHADEMA kwangu mimi ina kila dalili ya “mzaha mbaya”. Maelezo yako hayatoi ushawishi wa kuridhisha. Dikteta aliyepo madarakani safari hii ameweka dhahiri kuwa lengo lake katika awamu yake ni kuufuta upinzani kikamilifu. Na haendekezi mijadala. Hata wanawake mahiri wa CHADEMA kahakikisha wanaporwa ushindi majimboni. It’s a terribly desperate situation.
 
S
Hakuna kiti cha ubunge maalum kinapatikana kwa fadhila.
Ila inawezekana upande wa pili hali ikawa hivyo.
Kwa Chadema hakuna uwezekano huo.
Kwa hiyo neno "fadhila" futa kwenye maelezo yako.
Mkuu Kama MUNGU haishivyo sifuti nakwambia, bila uchuguzi kuvurugwa, hao unaosema kuwa bit mahalum walikua na uwezekano wa kushinda si chini ya asilimia 87,7777 kwa ridhaa ya wenye nchi, I mean wananchi, Sasa vya bure vya nini futeni uchaguzi turudi field ,vinginevyo itakua ni fadhila ,
Usipende kuchukulia mzigo aliobeba mwenzio kuuna rahisi ,Kama Wana nchi ni walewale twende field ,sidhani Kama Kuna mwanamama, wa chadema anapenda kua viti mahalum, tofauti na wale waliokua wamepita viti mahalum mkuu,ila pamoja na hayo wabunge wapo, so acha waendelee achana na vyama vya upinzani
 
Uko sahihi sana, hata Mwl. Nyerere aliukubali uwaziri mkuu kisha ndio akaendelea kupambania kusaka uhuru....kabla ya jambo kubwa kupewa, MUNGU huanza na dogo kwanza...
 
Tafadhali Chadema huyu mama ametumwa na KIM wa bongo mwangalieni kwa jicho la saba
 
Ukiangalia ni kwamba hatujawahi kuwa na uchaguzi halali na wa haki,sasa hiki wanachofanya sasa chadema nacho pia si sawa na kuhalalisha uharamu wa chaguzi zilizopita?
 
Mama Amon
Naomba kukumbusha jambo moja kupitia mfano wako wa kwanza.
Kupokea mil.3 kama sehemu ya malipo ya fidia iliyoamriwa ambayo ni mil.10 inabadilisha kesi ya msingi kutoka kumlalamikia mwajiri wako kwa kukufukuza kazi hadi kudai kumaliziwa deni la fidia.
Uzito wa kesi hizi mbili ni tofauti sana.

Tukija kwenue hoja ya msingi, inawezekana ni kweli upinzani hasa CHADEMA unahitaji uwakilishi katika nyanja zote kuanzia Bungeni hadi kwenye mabaraza ya Halmashauri. Lakini uwakilishi huu unaweza usisaidie hata kidogo kumaliza matatizo ya upinzani zaidi labda kuugawa zaidi.

Itoshe tu kusema kuna haja kubwa ya kila upande kulegeza msimamo ili kupata suluhu inayoimarisha Umoja & Mshikamano (ndani ya miaka hii5) bila kujali mkwamo wa kisiasa ulipo sasa.
 
Mie niliyoyaona nitasimulia vizazi vyangu vyote nyaani nitamsimulia mwanangu siku zote ajue kuwa mwaka 2020 kulitokea tukio la kuumiza ,kufedhehesha na kudharaulisha nalo ni uchaguzi mkuu.Nitaandika hata nukuu vizazi vyangu vitasoma kitabu changu kuonesha nilivyoumia

Sent from my TECNO CF8 using JamiiForums mobile app
 
Bro tumekusoma vema tulichokiona ni kile kinachopinga ukweli kuwa hupaswi kukubali kuunga mkono kudhulumiwa wakati una nafasi ya kureact kwa migomo nk
Wao walioharibu uchaguzi wajenge walipobomoa

Sent from my TECNO CF8 using JamiiForums mobile app
 
Zikadaiwe wapi wakati hata fomu mawakala walinyimwa?

Sent from my TECNO CF8 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…