Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Mama Amon, natumaini umesimama kwenye uaminifu (honesty) unapotoa hilo pendekezo.
Umeainisha sentenso ya muamala kama wa kibiashara vile kuonyesha faida watakayopata CHADEMA kwa kupeleka wabunge wa viti maalum. Kwamba watakuwa nyenzo ya kudai kura zilizoibiwa!
Naamini unao uelewa mkubwa kuweza kutambua kuwa alichofanya Mwenyekiti wa CCM ni kufifisha nguvu ya CHADEMA kwa kuwapoka ushindi wao kwenye urais na kwenye majimbo na kuhakikisha wabunge wake maarufu hawarudi bungeni.
Kisha kawapa mbunge mmoja tu wa jimbo asiye na historia ya “kutikisa” sana. Sasa anachotaka ni CHADEMA kuwa na uwakilishi dhaifu wa viti maalum kuhalalisha dhulma kubwa iliyofanywa kwa chama hicho na kwa Watanzania kwa ujumla.
Aidha, wewe kama ni mama (ke) kweli umeshasikia kejeli inayoshamirishwa na wabunge wanawake wa CCM wakishangiliwa na spika kuwa wanaopata viti maalum CHADEMA sharti “wadhalilishwe” na mwenyekiti wa chama hicho!
Halafu kweli unaamini hao viti maalum wataweza kudai kura za CHADEMA zilizoibwa?
Usishangae ukiona wadau hapa JF wakikutilia mashaka makubwa kuhusu nia yako halisi (real motive) ya kuleta bandiko hili.