Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,089
- 2,725
- Thread starter
- #21
Kukubali kuteua viti maalumu ni kukubali uhalamia na ufedhuli uliofanywa na tume kwa maelekezo ya CCM. Mimi nilishiriki kusimamia uchaguzi huu, niliyoyaona yanatisha. Nimeeleza kidogo tu kuwa kwenye kituo changu nilichosimamia Tundu Antipas Lissu alipata kura 79 na Magufuli alipata kura 31 lakini Lissu akandikiwa kura 6 na Magufuli kura 379 sasa hapo unakubali vipi? Ni bora kuacha tu.
Umetoa mfano mzuri unaoimarisha hoja yangu.
Ni hivi:
Kwenye kituo ulichosimamia Tundu Antipas Lissu alipata kura 79 na Magufuli akapata kura 31.
Lakini Lissu alindikiwa kura 6 na Magufuli kura 379.
Kisha unauliza, "sasa hapo unakubali vipi?"
Majibu yangu:
Kama ni kweli, kura 6 alizoandikiwa Lissu ni sehemu ya kura zake halali 79 ulizozishuhudia.
Kwa hiyo, kwa mujibu wa maelezo yako, Lissu aliibiwa kura 73.
Hivyo basi, tunapaswa kukubali kwamba kura 6 ni kura halali, na kuendelea kudai kura 73 kwa kuweka vielelezo mezani.
Hizo kura 6 ambazo tunajua kwamba ni halali ni sehemu ya kura ambazo zimetangazwa na NEC na kuzaa wabunge wa viti maalum 19.
Kwa hiyo, viti maalum 19 vya Chadema ni halali.
Katika kituo chako ulichosimamia, ambacho sio halali, kama kikitibitika, ni kutotangazwa kwa kura 73.
Hizi kura 73 ziendelee kudaiwa bila kuharamisha kura 6 ambazo ni halali.
Wanasheria wote wa Chadema wanaujua ukweli huu.
Tafuta yeyote umwulize na atakwambia ninachokwambia.