Ndugu, ukiwa na bahati ya kuhudhuria mahakamani utasikia mawakili wanasema:
Your honor, this is vexatious, yaani, Mhe, huu ni utukutu mahakamani.
Your honor, this frivolous, yaani, Mhe, huu ni utundu mahakamani.
Maana yake ni kwamba, kuna mtu anajifanya kujenga hoja, hana ushahidi, lakini anaing'ang'ania kiasi cha kuifanya mahakama ishindwe kutekeleza majukumu yake.
Ushauri wangu kwako: waulize hao wanaoyasema hayo maneno maswali haya:
- Kama kura hazikuhesabiwa kabisa, zile zilizotangazwa zilitoka wapi? Kama wanajua zilikotoka wanaweza kuweka ushahidi mbele ya mahakama na kuthibitisha kauli hizo?
- Katika vile vituo ambako Chadema wanakiri kwamba waliweka mawakala, nako kura hazikuhesabiwa? Kama zilihesabiwa mawakala wanazo takwimu tofauti?
Haya ni baadhi ya maswali, napenda yakusaidie kufikiri kama mtu mzima.
Ukiacha mlango wazi, mwizi akaiba, halafu ukaenda polisi kusema mwizi kavunja mlango, polisi wakija na kukuta mlango uko salama, wanakwambia wewe umeshirikiana na mwizi kujiibia! Hakuna mazingira kama haya kwenye maeneo mengi nchini?
Tuzidi kutafakari pamoja.