Uchaguzi 2020 Tathmini yangu juu ya Uchaguzi Mkuu 2020: Hakuna sababu nzuri ya kukataa kuteua wabunge wa Viti Maalum CHADEMA

1. Asilimia 88 ya mawakala wa CHADEMA walizuiwa/ kutolewa vituoni kabla na baada ya zoezi la kupiga kura.

2. CHADEMA nchi nzima hawakupata nakala za matokeo ya uchaguzi kutokana na mawakala kukatazwa kuingia vituoni au kufukuzwa vituoni hivyo hizo kura X/Y or Z hazifahamiki zipi ni halali na zipi si halali.

3. Wakati wa kuhesabu kura vituo vilivamiwa na maafisa wa polisi kwa kujaza kura zilizokuwa kwenye mabegi na sehemu zingine fomu za matokeo zilijazwa namba tu bila kuzingatia idadi hata ya wapiga kura kwenye kituo husika.

4. Wasimamizi wa uchaguzi kwenye vituo kadhaa waliingia na kura kwenye mabegi zikiwa zimejazwa kwa mgombea wa chama tawala.

5. CHADEMA wanahoji uhalali wa kura zilizotangazwa kwa kuzingatia swali kuwa ni zipi kati ya zilizokuwa kwenye mabegi ya wasimamizi wa uchaguzi au zilizopigwa na wananchi ?

6. Kama CHADEMA hawakuwa na wakala vituoni wakati wa kuhesabu kura je kura halali za kwao ni zipi alizopata mgombea wa ccm au walizopewa wao na tume nani anauthibitisho kuwa ni za kwao wakati hawakuwa na mtazamaji vituoni ?

Kwa kuzingatia kuwa uchaguzi ni mchakato na unahalalishwa na uwazi na haki katika hatua zote msingi wa CHADEMA kukataa kuchagua wabunge wa viti maalumu ni " Mchakato mzima wa kupiga kura na kuhesabu kura" kuwa haukufuata sheria na uligubikwa na mambo ambayo yaliondoa uhalali wa mchakato wenyewe na matokeo ya mchakato.
Hoja ya CHADEMA siyo idadi ya kura ila ni mchakato mzima wa upigaji kura.
Hoja ya mleta mada imefia hapa. Ngoja niendelee kupata [emoji485] wine yangu.
 
Ndg Kasenene,

Asante kwa maswali yaliyonyooka. Najibu kawa mtindo wa bandika bandua kama ifuatavyo:

1. Endapo CHADEMA wakakukubali kuteua wabunge wa viti maalum, Je? hii itakuwa imesaidia nini katika kujenga Demokrasia huru na utawala wa haki nchini?

Jawabu: Uwepo wa wabunge wa viti maalum bungeni kutoka Chadema kutaimarisha mfumo wa demokrasia ya Kibunge. Kamati za Bunge zinazopaswa kuongozwa na wapinzani zitapata wenyeviti. Pia, Mawaziri kivuli wanaweza kuwepo kwa ajili ya kuandaa bajeti vivuli zenye maudhui boreshi. Kwa sasa, bunge limenasa katika kipingele hiki, ama kwa kujua au kwa kutojua.

2. Je unadhani nani atakuwa mnufaika mkubwa wa hayo maamuzi endapo yatafanyika kati ya "waliyotengeneza hayo mazingira" au Demokrasia ya nchi yetu.

Jawabu: Watu "waliyotengeneza hayo mazingira" ya kamati kadhaa kuongozwa na wapinzani ni Bunge zima lililotunga kanuni za kudumu za Bunge. Bunge ni chombo cha Taifa. Kwa hiyo, Taifa litanufaika na uamuzi wa Chadema kupeleka wabunge wa viti maalum. Pia Chadema watanufaika kwa njia ya kupata mgao kutoka kwenye posho za wabunge kwa mujibu wa kanuni za Chama.

3. Je umewahi kujiuliza imekuwakuwaje Chadema wakapata kiti kimoja cha ubunge wa kuchaguliwa (kupitia mwanamke) na kuachiwa hivyo viti maalum. Unahisi hii ilikuwa ni bahati mbaya? Kwamba haukuwa mpgango maalum? na kama ni mpango maalum nini lilikuwa lengo lao waliofanya hivi?

Jawabu: Sio kwamba nimewahi kufikiria. Najua kila kilichotokea kwenye kila hatua ya mchakato wa uchaguzi. Najua malalamiko ya Chadema. Najua matokeo yaliyotangazwa na NEC. Najua kwamba mgombea ubunge wa kwanza kutangazwa ni Mbowe, kwamba ameshindwa, And a lot more. Lakini, haya yote sio hoja yangu katika uzi huu. Hapa naongelea zile kura chache zilizotangazwa na NEC, na ambazo kwa mujibu wa udadavuzi wangu ni kura halali za Chadema. Na kwa hiyo, tunao wabunge halali wa viti maalum waliotokana na kura hizo. Natamani waende Bungeni leo ili kutekeleza majukumu yao, hala chama kiendelee kushughulikia masuala hayo mengine kuhusu kura zinazodaiwa kuibwa na watu wasiojulikana!

4.Je unadhani Chadema wakikubali huo "mtego" ulioandaliwa mahususi baina ya Chama tawala,Tume ya uchaguzi na vyombo vya usalama, Je haka kamchezo ka "kudidimiza" upinzani katakuwa kamepata dawa kuelekea demokrasia makini?

Jawabu: Mtego gani unaongelea? Utaratibu wa kupeleka wabunge wa viti maalumu Bungeni sio mtego kwa Chadema. Ni matakwa ya Kikatiba. Mtego ambao nauona mimi ni huu wa kuwa na Tume ya Uchaguzi ambaye ni Mtumwa wa serikali na chama tawala. Lakini, hiyo ni hoja tofauti na kinachojadiliwa katika bandiko langu.

5. Mwisho kabisa japo sio kwa umuhimu. Chadema wakikubali haka kamtego. Wahisani pamoja na marafiki wa dunia watakuwa na sababu tena ya kutunyooshea mkono juu ya uminywaji wa Demokrasia katika nchi yetu? Namalizia kwa mfano wa mwisho. Ikatokea ukamfumania mkeo na mwanaume mwingine kitandani kwako (kama umeoa), arafu akaanzisha ugonvi na bado kama haitoshi akatumia na vyombo vya dola kukukandamiza ili uonekana wewe ndio mshari na unayeleta chokochoko kwenye ndoa, Je utakubali ushauri wa kurudi mezani myamalize kundelea kukaa naye nyumba moja kwa sharti kwamba ukubali kuwa yeye ndiye mshindi? ila wewe ndio ulitaka kuleta chokochoko na kuharibu amani ya ndoa yenu na pengine unatumika na Mabeberu (watu wenye lengo baya dhidi ya ndoa yenu ndio maana ya neno beberu kwa mfano huu pekee)

Jawabu: Tatizo lako inashindwa kunyoosha maneno. "Haka kamtego" wahisani wanakajua. Lakini, pia wahisani wanapaswa kupigwa shule juu ya mienendo ya siasa za ndani ya Tanzania kwa kuzingatia kanuni za ukweli na uwazi. Hoja yangu hapa, yenye kutofautisha uhalali wa kura zilizozalisha wabunge wa viti maalum wa Chadema, na kura zinazodaiwa kuibwa kwa faida ya CCM, ni hoja inayoeleweka, na inayoweza, na inayopaswa kukubalika kwa wahisani wenye akili timamu.

Karibu kwa swali la nyingeza.
Wewe sii miongoni mwa mnaosema wanachelewesha maendeleo, sasa mnahangaika nao wanini, je nyie hamyataki maendeleo, au ndio mnazuia maendeleo kwa kuweka vigingi?
 
Najua mengi kati ya haya uliyoyaandika.

Lakini, nashauri kutofautisha maembe na machungwa.

Pia nashauri kujiepusha na mantiki ya samaki mmoja akioza wote wameoza.

Turudi kwenye hoja yetu:

Kura za Chadema zilizotangazwa na NEC ni kidogo kuliko uhalisia au ni nyingi zaidi ya uhalisia?

Kama ni kidogo kuliko uhalisia, ni kura halali au kura haramu?

Kama ni kura halali, kwa nini wabunge wa viti maalum wanaotokana na kura hizo wawe haramu?

Nashauri tupeleke wabunge, halafu tuendelee kupigania masuala mengine.

Hakuna athari.

Mtazamo wako hizo kura zinazodaiwa walipata CDM na ACT ni zile ambazo walizopigiwa. Unasahau kuwa mojawapo ya madai ya CDM ni kuwa kura ama hazikuhesabiwa kabisa au zilipuuzwa na zikajazwa namba ambazo wasimamizi wenye ndio wanajua walizitoa wapi. Kwa sbabu hii basi hata hizo kura zinazosemekana ni za vyama vya upinzani ni haramu kwa sababu hakuna uhakika kuwa zilitokana na zile zilizopigwa kwenye vituo. Ndio maana wanakataa kutambua zoezi zima na kukataa hesabu zote zilizotokana na huu uchaguzi ( ikiwa pamoja na zile wanazoambiwa walipata). Ukitaka kutenda haki ungewashupalia NEC wapitie upya hesabu zao na kura zilizopigwa mbele ya mawakala wa pande zote husika pamoja na namna wagombea walivyopatikana. Pale ambapo itaonekana dhahiri kuwa kuna kamchezo, uchaguzi ufutwe na urudiwe upya. Hiyo itasaidia kupunguza presha.

Amandla...
 
Hoja ya mleta mada imefia hapa. Ngoja niendelee kupata
emoji485.png
wine yangu.
Mimejibu kila kitu.
Hakuna pointi hapa.
MIe naongelea maembe, yeye anaongelea machungwa.
 
Tusome pamoja:

"When one wants to bring down a dictatorship most effectively and with the least cost then one has four immediate tasks: One must strengthen the oppressed population themselves in their determination, self-confidence, and resistance skills; One must strengthen the independent social groups and institutions of the oppressed people; One must create a powerful internal resistance force; One must develop a wise grand strategic plan for liberation and implement it skillfully." (tazama attachment, sura ya kwanza, chini ya sub-heading hii: "Facing the hard truth ")
Sijui kiingeleza vizuri, Ila swala la mabadiriko huwa halizuiriki labda kuchelewesha tu.... Mabadiriko huwa yanakuja kwa either kuratibiwa/organized and coordinated au mapunduzi/uprise revolutions.. Mara zote aina ya pili huwa na madhara ya kudi stabilize nchi/taifa mfano ya hivi karibuni Misri,Libya.. pia Kuna ileya Kati ya hizo mbili SEMI organized and coordinated revolutions eg Tunisia, Jordan, Zimbabwe

It's certain oppression and injustice entually turn into a revolution. Kwa hiyo kazi kwetu kuchagua tunataka aina ipi hapa Tz,

Note; siwapendi ccm kwa kui masikinisha hii nchi, lakini kwa katiba tuliyonayo God forbid ikatokea ccm ikapoteza uchaguzi kwa ngazi Rais(na lazima itakuja tolewa/poteza Tena siyo miaka mingi ijayo) taifa lipaitia kipindi kigumu/distabilize kwa muda (mfupi,Kati, au mrefu)... Because ccm hii Ni mfumo (mahakimu Kama wote, majenerali wajeshi na usalama, wakuu wa juu/Kati wa Kila Kona ya serikali Ni ccm,dc,rc,ded.... Sasa u can image kuwabadirisha hawa wote kwa muda mfupi chame a kingine kikichuwa madaraka Tena kwa katiba hii ilivyotoa nguvu na madaraka makubwa kwa rais
 
Mtazamo wako hizo kura zinazodaiwa walipata CDM na ACT ni zile ambazo walizopigiwa. Unasahau kuwa mojawapo ya madai ya CDM ni kuwa kura ama hazikuhesabiwa kabisa au zilipuuzwa na zikajazwa namba ambazo wasimamizi wenye ndio wanajua walizitoa wapi. Kwa sbabu hii basi hata hizo kura zinazosemekana ni za vyama vya upinzani ni haramu kwa sababu hakuna uhakika kuwa zilitokana na zile zilizopigwa kwenye vituo. Ndio maana wanakataa kutambua zoezi zima na kukataa hesabu zote zilizotokana na huu uchaguzi ( ikiwa pamoja na zile wanazoambiwa walipata). Ukitaka kutenda haki ungewashupalia NEC wapitie upya hesabu zao na kura zilizopigwa mbele ya mawakala wa pande zote husika pamoja na namna wagombea walivyopatikana. Pale ambapo itaonekana dhahiri kuwa kuna kamchezo, uchaguzi ufutwe na urudiwe upya. Hiyo itasaidia kupunguza presha.

Amandla...

Ndugu, ukiwa na bahati ya kuhudhuria mahakamani utasikia mawakili wanasema:

Your honor, this is vexatious, yaani, Mhe, huu ni utukutu mahakamani.
Your honor, this frivolous, yaani, Mhe, huu ni utundu mahakamani.

Maana yake ni kwamba, kuna mtu anajifanya kujenga hoja, hana ushahidi, lakini anaing'ang'ania kiasi cha kuifanya mahakama ishindwe kutekeleza majukumu yake.

Ushauri wangu kwako: waulize hao wanaoyasema hayo maneno maswali haya:

  • Kama kura hazikuhesabiwa kabisa, zile zilizotangazwa zilitoka wapi? Kama wanajua zilikotoka wanaweza kuweka ushahidi mbele ya mahakama na kuthibitisha kauli hizo?
  • Katika vile vituo ambako Chadema wanakiri kwamba waliweka mawakala, nako kura hazikuhesabiwa? Kama zilihesabiwa mawakala wanazo takwimu tofauti?
Haya ni baadhi ya maswali, napenda yakusaidie kufikiri kama mtu mzima.

Ukiacha mlango wazi, mwizi akaiba, halafu ukaenda polisi kusema mwizi kavunja mlango, polisi wakija na kukuta mlango uko salama, wanakwambia wewe umeshirikiana na mwizi kujiibia! Hakuna mazingira kama haya kwenye maeneo mengi nchini?

Tuzidi kutafakari pamoja.
 
Ndg Kasenene,

Asante kwa maswali yaliyonyooka. Najibu kawa mtindo wa bandika bandua kama ifuatavyo:

1. Endapo CHADEMA wakakukubali kuteua wabunge wa viti maalum, Je? hii itakuwa imesaidia nini katika kujenga Demokrasia huru na utawala wa haki nchini?

Jawabu: Uwepo wa wabunge wa viti maalum bungeni kutoka Chadema kutaimarisha mfumo wa demokrasia ya Kibunge. Kamati za Bunge zinazopaswa kuongozwa na wapinzani zitapata wenyeviti. Pia, Mawaziri kivuli wanaweza kuwepo kwa ajili ya kuandaa bajeti vivuli zenye maudhui boreshi. Kwa sasa, bunge limenasa katika kipingele hiki, ama kwa kujua au kwa kutojua.

2. Je unadhani nani atakuwa mnufaika mkubwa wa hayo maamuzi endapo yatafanyika kati ya "waliyotengeneza hayo mazingira" au Demokrasia ya nchi yetu.

Jawabu: Watu "waliyotengeneza hayo mazingira" ya kamati kadhaa kuongozwa na wapinzani ni Bunge zima lililotunga kanuni za kudumu za Bunge. Bunge ni chombo cha Taifa. Kwa hiyo, Taifa litanufaika na uamuzi wa Chadema kupeleka wabunge wa viti maalum. Pia Chadema watanufaika kwa njia ya kupata mgao kutoka kwenye posho za wabunge kwa mujibu wa kanuni za Chama.

3. Je umewahi kujiuliza imekuwakuwaje Chadema wakapata kiti kimoja cha ubunge wa kuchaguliwa (kupitia mwanamke) na kuachiwa hivyo viti maalum. Unahisi hii ilikuwa ni bahati mbaya? Kwamba haukuwa mpgango maalum? na kama ni mpango maalum nini lilikuwa lengo lao waliofanya hivi?

Jawabu: Sio kwamba nimewahi kufikiria. Najua kila kilichotokea kwenye kila hatua ya mchakato wa uchaguzi. Najua malalamiko ya Chadema. Najua matokeo yaliyotangazwa na NEC. Najua kwamba mgombea ubunge wa kwanza kutangazwa ni Mbowe, kwamba ameshindwa, And a lot more. Lakini, haya yote sio hoja yangu katika uzi huu. Hapa naongelea zile kura chache zilizotangazwa na NEC, na ambazo kwa mujibu wa udadavuzi wangu ni kura halali za Chadema. Na kwa hiyo, tunao wabunge halali wa viti maalum waliotokana na kura hizo. Natamani waende Bungeni leo ili kutekeleza majukumu yao, halafu chama kiendelee kushughulikia masuala hayo mengine kuhusu kura zinazodaiwa kuibwa na watu wasiojulikana!

4.Je unadhani Chadema wakikubali huo "mtego" ulioandaliwa mahususi baina ya Chama tawala,Tume ya uchaguzi na vyombo vya usalama, Je haka kamchezo ka "kudidimiza" upinzani katakuwa kamepata dawa kuelekea demokrasia makini?

Jawabu: Mtego gani unaongelea? Utaratibu wa kupeleka wabunge wa viti maalumu Bungeni sio mtego kwa Chadema. Ni matakwa ya Kikatiba. Mtego ambao nauona mimi ni huu wa kuwa na Tume ya Uchaguzi ambaye ni Mtumwa wa serikali na chama tawala. Lakini, hiyo ni hoja tofauti na kinachojadiliwa katika bandiko langu.

5. Mwisho kabisa japo sio kwa umuhimu. Chadema wakikubali haka kamtego. Wahisani pamoja na marafiki wa dunia watakuwa na sababu tena ya kutunyooshea mkono juu ya uminywaji wa Demokrasia katika nchi yetu? Namalizia kwa mfano wa mwisho. Ikatokea ukamfumania mkeo na mwanaume mwingine kitandani kwako (kama umeoa), arafu akaanzisha ugonvi na bado kama haitoshi akatumia na vyombo vya dola kukukandamiza ili uonekana wewe ndio mshari na unayeleta chokochoko kwenye ndoa, Je utakubali ushauri wa kurudi mezani myamalize kundelea kukaa naye nyumba moja kwa sharti kwamba ukubali kuwa yeye ndiye mshindi? ila wewe ndio ulitaka kuleta chokochoko na kuharibu amani ya ndoa yenu na pengine unatumika na Mabeberu (watu wenye lengo baya dhidi ya ndoa yenu ndio maana ya neno beberu kwa mfano huu pekee)

Jawabu: "Haka kamtego" ka NEC ambayo imewekwa kwapani na serikali wahisani wanakajua vizuri kuliko wewe. Lakini, pia wahisani wanapaswa kupigwa shule juu ya mienendo ya siasa za ndani ya Tanzania kwa kuzingatia kanuni za ukweli na uwazi. Hoja yangu hapa, yenye kutofautisha uhalali wa kura zilizozalisha wabunge wa viti maalum wa Chadema, na kura zinazodaiwa kuibwa kwa faida ya CCM, ni hoja inayoeleweka, na inayoweza, na inayopaswa kukubalika kwa wahisani wenye akili timamu.

Karibu kwa swali la nyongeza.
Safi saana kwa majibu mazuri swali la mwisho. Umesema "alafu chama kiendelee kushughulikia masuala hayo mengine kuhusu kura zinazodaiwa kuibwa na watu wasiojulikana!" Kushughulikia wapi? kivipi? nani atakuwa tayari kuwasikiliza? (unapeleka kesi ya Chui kumla mnyama swala kwa mzee wa nyika Simba!?). Nadhani ni bora kuendelea kushughulikia hili tatizo kwa style hii watumiayo sasa kwani hii ndiyo pia imekusukuma wewe na wengine wengi duniani kulipigia kelele swala hili, vinginevyo wangefuata ushauri wako hii habari ingekuwa ni historia na watu (walioko madarakani) wangeendelea kujipanga na style nyingine mpya ya kufanya maangamizi makubwa zaidi katika uchaguzi ujao wa 2025. Acha Chadema waendelee na wanachokifanya kwa sasa kwani wanaoumia zaidi ni hao walioko madarakani kuliko wao Chadema. Kwani hata kwenye ndoa hakuna kitu kinauma kama kumfanyia ubaya mkeo, akaondoka nyumbani kwako arafu ukawa unambembeleza arudi home bila mafanikio huku yeye anapiga mark time aisee usithubutu mwanaume utakonda mpaka utaisha.... lakini akirudi kirahisi kirahisi hata wewe usahau yoote yaliyotokea kirahis rahisi na anayeishia kujuta ni mwanamke na ikitokea tatizo ilo ilo mara ya pili mwanamke akajaribu njia hiyo ya hapo mwanzo huishia kupoteza sijui kwanini? nadhani hii inatokana na ile theory ya "marginal utility of wants"
 
Ndugu, ukiwa na bahati ya kuhudhuria mahakamani utasikia mawakili wanasema:

Your honor, this is vexatious, yaani, Mhe, huu ni utukutu mahakamani.
Your honor, this frivolous, yaani, Mhe, huu ni utundu mahakamani.

Maana yake ni kwamba, kuna mtu anajifanya kujenga hoja, hana ushahidi, lakini anaing'ang'ania kiasi cha kuifanya mahakama ishindwe kutekeleza majukumu yake.

Ushauri wangu kwako: waulize hao wanaoyasema hayo maneno maswali haya:

  • Kama kura hazikuhesabiwa kabisa, zile zilizotangazwa zilitoka wapi? Kama wanajua zilikotoka wanaweza kuweka ushahidi mbele ya mahakama na kuthibitisha kauli hizo?
  • Katika vile vituo ambako Chadema wanakiri kwamba waliweka mawakala, nako kura hazikuhesabiwa? Kama zilihesabiwa mawakala wanazo takwimu tofauti?
Haya ni baadhi ya maswali, napenda yakusaidie kufikiri kama mtu mzima.

Ukiacha mlango wazi, mwizi akaiba, halafu ukaenda polisi kusema mwizi kavunja mlango, polisi wakija na kukuta mlango uko salama, wanakwambia wewe umeshirikiana na mwizi kujiibia! Hakuna mazingira kama haya kwenye maeneo mengi nchini?

Tuzidi kutafakari pamoja.
Yafaa tuwaulize walioyaratibu,tukiwauliza wengine tunawaonea.
 
Hilo ndilo neno kwani uchaguzi umekwisha na waliochaguliwa wameapa wakiendelea kuwajibika kwa wapiga kura. Kinachohitajika ni kwa viongozi wa upinzani, nanyi wafuasi, kutathmini, kwa kina, makosa yaliyofanyika kiasi cha kufanya vibaya SANA kweye Uchaguzi uliomalizika.

Kadiri viongozi wa upinzani, hasa CHADEMA, nanyi wafuasi, mnavyoendelea kulalamikia matokeo na kuilamu NEC, ndivyo mnavyowapa morali viongozi wa CCM kuisimamia vizuri Serikali yake ili Ilani ya Uchaguzi itekelezwe ipasavyo. Na utekelezaji ukifanikiwa, ni wazi Uchaguzi Mkuu, 2025, upinzani usahau kupata hata kata moja.
Hilo si ndo litakua bora zaidi kwa CCM, kwa sababu wapinzani wanachelewesha maendeleo.
 
Sijui kiingeleza vizuri, Ila swala la mabadiriko huwa halizuiriki labda kuchelewesha tu.... Mabadiriko huwa yanakuja kwa either kuratibiwa/organized and coordinated au mapunduzi/uprise revolutions.. Mara zote aina ya pili huwa na madhara ya kudi stabilize nchi/taifa mfano ya hivi karibuni Misri,Libya.. pia Kuna ileya Kati ya hizo mbili SEMI organized and coordinated revolutions eg Tunisia, Jordan, Zimbabwe

It's certain oppression and injustice entually turn into a revolution. Kwa hiyo kazi kwetu kuchagua tunataka aina ipi hapa Tz,

Note; siwapendi ccm kwa kui masikinisha hii nchi, lakini kwa katiba tuliyonayo God forbid ikatokea ccm ikapoteza uchaguzi kwa ngazi Rais(na lazima itakuja tolewa/poteza Tena siyo miaka mingi ijayo) taifa lipaitia kipindi kigumu/distabilize kwa muda (mfupi,Kati, au mrefu)... Because ccm hii Ni mfumo (mahakimu Kama wote, majenerali wajeshi na usalama, wakuu wa juu/Kati wa Kila Kona ya serikali Ni ccm,dc,rc,ded.... Sasa u can image kuwabadirisha hawa wote kwa muda mfupi chame a kingine kikichuwa madaraka Tena kwa katiba hii ilivyotoa nguvu na madaraka makubwa kwa rais

NImekuelewa. Kitabu hicho nilichokinukuu nitakitafsiri kwa kiswahili na kukiweka hapa katika siku za karibuni ili kila mtu asome na kuelimika.
 
Kama mnaona CDM wanachelewa jipitisheni nyie muongeze idadi si mlisema 28 walipita bila kupingwa na hakuna mgombea wa CCM alienguliwa na tume kwenye mchakato!
 
Nikupongeze kwa kuweza kuweka hicho kitabu hapa. Wale tusiotaka kuijua siasa wala kuifuatilia tuwapongeze kwa moyo mliokuwa nao
 
Ndugu, ukiwa na bahati ya kuhudhuria mahakamani utasikia mawakili wanasema:

Your honor, this is vexatious, yaani, Mhe, huu ni utukutu mahakamani.
Your honor, this frivolous, yaani, Mhe, huu ni utundu mahakamani.

Maana yake ni kwamba, kuna mtu anajifanya kujenga hoja, hana ushahidi, lakini anaing'ang'ania kiasi cha kuifanya mahakama ishindwe kutekeleza majukumu yake.

Ushauri wangu kwako: waulize hao wanaoyasema hayo maneno maswali haya:

  • Kama kura hazikuhesabiwa kabisa, zile zilizotangazwa zilitoka wapi? Kama wanajua zilikotoka wanaweza kuweka ushahidi mbele ya mahakama na kuthibitisha kauli hizo?
  • Katika vile vituo ambako Chadema wanakiri kwamba waliweka mawakala, nako kura hazikuhesabiwa? Kama zilihesabiwa mawakala wanazo takwimu tofauti?
Haya ni baadhi ya maswali, napenda yakusaidie kufikiri kama mtu mzima.

Ukiacha mlango wazi, mwizi akaiba, halafu ukaenda polisi kusema mwizi kavunja mlango, polisi wakija na kukuta mlango uko salama, wanakwambia wewe umeshirikiana na mwizi kujiibia? Hakuna mazingira kama haya kwenye maeneo mengi nchini?

Tuzidi kutafakari pamoja.
Mimi napenda mnavyopenda kuwatukana watu ili mjione kuwa ni werevu zaidi. Maneno vexatious na frivolous ni maneno ya kawaida tu ingawa labda wanasheria wetu wanapenda kuyatumia ili watu kama nyie muone kuwa kweli wamesoma.
Madai ya wapinzani ni kuwa sehemu nyingine wasimamizi walijiandikia matokeo waliyoyataka wenyewe. Mfano ni vituo ambako kura za wagombea zilifanana kiasi cha kutia shaka. Malalamiko mengine ni kuwa hata hizo sehemu chache ambako wakala wao walikuwepo, hawakupewa nakala ya matokeo kama ilivyokuwa kawaida. Ndio maana kama kweli figisu hazijafanyika, NEC wangeweka wazi hesabu zao na kuwakaribisha watu wakague na wawasimamie watakavyohesabu upya kura zinazotiliwa shaka. Wanaogopa nini kufanya hivyo?
Mimi sio mwanasheria lakini najua huwezi kujitetea kuwa niliingia kwenye chumba kisichokuwa changu na kuchukua luninga kwa sababu mlango ulikuwa wazi. Na ninavyojua, breaking and entering haina lazima uvunje mlango. Hata ukiusukuma mlango ambao ulikuwa haujafungwa inahesabiwa kuwa ume break na kuingia. Aidha, kutokuwa na dalili yeyote ya kuvunjwa mlango hamna maana kuwa mwenye chumba alishirikiana na mwizi maana mwizi anaweza kuwa amechongesha ufunguo wake. Polisi wakimsumbua aliyeshitaki watakuwa hawajatenda haki.

Amandla...
 
Kama mnaona CDM wanachelewa jipitisheni nyie muongeze idadi si mlisema 28 walipita bila kupingwa na hakuna mgombea wa CCM alienguliwa na tume kwenye mchakato!
Tabia ya kushindwa kutofautisha hoja na mleta hoja ni dalili kwamba Watanzania wenye elimu iliyo chini ya kidato cha nne wanafikia 90%, na wewe ni miongoni mwao.

Sio lazima uandike chochote. Ukimya nao unakubalika.
 
Ndugu, ukiwa na bahati ya kuhudhuria mahakamani utasikia mawakili wanasema:

Your honor, this is vexatious, yaani, Mhe, huu ni utukutu mahakamani.
Your honor, this frivolous, yaani, Mhe, huu ni utundu mahakamani.

Maana yake ni kwamba, kuna mtu anajifanya kujenga hoja, hana ushahidi, lakini anaing'ang'ania kiasi cha kuifanya mahakama ishindwe kutekeleza majukumu yake.

Ushauri wangu kwako: waulize hao wanaoyasema hayo maneno maswali haya:

  • Kama kura hazikuhesabiwa kabisa, zile zilizotangazwa zilitoka wapi? Kama wanajua zilikotoka wanaweza kuweka ushahidi mbele ya mahakama na kuthibitisha kauli hizo?
  • Katika vile vituo ambako Chadema wanakiri kwamba waliweka mawakala, nako kura hazikuhesabiwa? Kama zilihesabiwa mawakala wanazo takwimu tofauti?
Haya ni baadhi ya maswali, napenda yakusaidie kufikiri kama mtu mzima.

Ukiacha mlango wazi, mwizi akaiba, halafu ukaenda polisi kusema mwizi kavunja mlango, polisi wakija na kukuta mlango uko salama, wanakwambia wewe umeshirikiana na mwizi kujiibia! Hakuna mazingira kama haya kwenye maeneo mengi nchini?

Tuzidi kutafakari pamoja.
Katika mawakala 80000+ ambao CHADEMA waliweka.

Mpaka kufikia muda wa kuhesabu kura walikuwa wamebaki 10000 tu vituoni huku wengine walitolewa na wengine kukamatwa.

Hao 10000 wenyewe waliobaki vituoni hawakupewa nakala za matokeo hivyo hata matokeo ya uchaguzi CHADEMA hawana.

Sasa tuseme kuwa hao 10000 waliweza kusimamia kura za chama chao je kura walizopata CHADEMA zinaweza kuwa zimetoka kwenye vituo hivyo 10000 tu ?

Ndiyo maana nimesema hoja ya CHADEMA siyo wingi wa kura zinazowapa nafasi za viti maalumu bali ni uhalali wa kura zao zote walizopewa.
 
Kwa utawala huuu,,waache wajiendeshe wenyewe,, nafikiri sasa Tunduru itakuwa kama New York
 
Back
Top Bottom