Tatizo kubwa la kitochi 4G za tigo ni anaganda baada ya matumizi. Nimeambatanisha picha

Kwa ninavyoelewa simu za mitandao ya simu line ya kwanza wanaweka line yao ama wana activate yako ya mtandao wao, mpaka iwepo hio line ndio unatumia na line ya pili, kukiwa hakuna line yao haipigi kazi mpaka uitoe lock.

Ulipewa GB 24?

Shukran pia kwa feedback,
 
mkuu nilifanya hivyohivyo kama ulivyosema hapo juu kuhusu laini lakini wapi, kuhusu gb 24 walinipa maelekezo ya kupata hiyo ofa ya GB &dakika, unaandika neno "ZAWADI" kwenda namba 15300 kupata ofa, nilijaribu kufanya hivyo kwa simu nyingine ninayoitumia kwa sasa kwakua kisimu chao kiligoma kusoma line wakaniju " simu yako haipo kwenye utaratibu wa ofa" hivyo sikupa ofa yao hio. Nadhani kupata ofa ni mpaka utume ujumbe huo kwakutumia kisimu husika
 
Kama hautojali tunaomba mrejesho mkuu! Maana Jumatatu ni leo
Kiongoz hiki kisimu kwa ufupi kinamapungu yake na maboresho yake kutoka toleo la kitochi lilipita; MAPUNGUFU 1.Kama wewe ni kazi yako niyakufanya miamala ya simu kama wakala wa m-pesa au tigo pesa hii simu sikushauri ununue inasumbua sana unapotaka kuswitch kati ya input mode “abc“, “ABC“ Au “123“. Itakulazimu ukikate hiki kiinterface hapo chini katikati ya transaction kama input mode awali ilikua kwenye “abc“ au “ABC“

ili urudi tena huku Ili kuipata hiyo input mode ya “123“ uweze kufanya miamala, simu hii haikuruhusu kubadili input mode unayoitaka katikati ya muamala. 2.Kinasauti ndogo wakati wa mazungumzo itakubidi kama upo kwenye kelele uweke loudspeaker ili muweze kusikiliza vizuri 3.Kinapata joto kias4 unapokichaji ukiwa haujakizima japo sio kila wakati au unapostream videos kwa mda mrefu,juzi kilipata joto kiasi nilipostream videos instagram kwa zaidi ya masaa 2 mfululizo. 4.Line namba moja inakupa machaguo yakutumia 4G,3G AU 2G kwenye settings wakati line namba mbili inakupa option moja tu yakuchagua mtandao wa 2G pekee nasio vinginevyo 5.Settings za simu hazikuruhusu kutumia laini namba 2 kwenye internet,kuna option yakutumia line 2 kwenye kupiga simu na kutuma sms pekee, 6.Screen resolution ni ndogo japo sio sana kwaupande wangu i can live with it,sijui kwa watu wengine. 7.Hiki kisimu kinakuja na app ya aptoide kama app store kina apps nyingi zipo zakununua na za free,ila apps nyingi za free kwa upande wangu zimenigomea kufanya kazi na nyingine kama vile sofascore ilicrash upon downloading mara kadhaa kwa ufupi hayo ndio mapungufu niliyoyagundua kwa upande wangu ndani ya huu md mfupi wakukitumia hiki kisimu.
 
Ila kama we ni mzee wakuperuzi sana mitandao ya kijamii kama tiktok, instagram, facebook na youtube kinafanya kazi vizuri mno Kuhusu whatsapp sina chakukomenti kwakuwa huwa siutumii kabisa huo mtandao ukilinganisha na smart vitochi toleo la kwanza kwenye upande wa social media hakuna kinachokifikia hiki kisimu to be honest, pia speed yake iko vizuri na kinafungua website zote nzitonzito ambazo sikuweza kuzifungua kwa smart kitochi toleo lililopita bila shida yeyote ,pia opera mini app inapiga kazi perfectly,
 
Umefafanua vizuri sana mkuu, tunashukuru sana kwa mrejesho!
Kitu ambacho haujagusia ni ukaaji wa chaji, kikoje upande huo?
 
upande wa battery kutunza chaji i give it 8/10, upande wa camera mimi sio mpenzi kabisa wakupiga picha so no comment,
Asante sana mkuu! Maswali mengine watauliza wengine kama yapo, ila mimi naona umemaliza Karibia kila kitu
 
Ila huo ni mtazamo wangu labda labda kuna baadhi ya mapungufu niliyoyaeleza hapo juu kuna namna yanaweza kusolviwa kwenye i don‘t know! Kikubwa endelea kutafuta details zaidi na zaidi kwa watu wengine before making a move
 
Asante sana mkuu! Maswali mengine watauliza wengine kama yapo, ila mimi naona umemaliza Karibia kila kitu
Pia kaBla sijasahau walinipatia na ofa yao ya GB 1 kwa matumizi tofautitofauti, GB 3 kuperuzi facebook Tu, dk 100 mitandao yote na sms sikumbuki ni ngapi kwa mwezi wa kwanza, sijajua sasa kama wataendelea kunipatia tena kwa miezi mingine mitano iliyobaki au la.
 
Kama hautojali tunaomba mrejesho mkuu! Maana Jumatatu ni leo
Chief kuhusu lile tatizo la “input mode“ kama upo katikati ya muamala problem solved kiasi chake , unafanya tu kupress&hold button ya namba husika unayoitaka. Kuhususu apps nyingi za aptoide kugoma kufanya kazi nimedownload app ya “9APP“ KUtoka kwenye aptoide store kama alternative yakupata apps zilizonigomea awali, nitarudi na mrejesho wa kama apps from 9apps zinawork vizuri au la
 
Mkuu hivi zinauwezo wa kutumia VPN (ha tunnel na http custom)[emoji848][emoji848]
 
Mkuu hivi zinauwezo wa kutumia VPN (ha tunnel na http custom)[emoji848][emoji848]
Ni android hio, app itakataa kama
1. Inategemea play services sababu hamna playstore ila hili linaweza kuwa solved.
2. App imetengenezwa kurun kwenye resolutions kubwa.

Otherwise app nyingi za Android zina run humo.
 
je na telegram pamoja na jamiiforum kanaingia mkuu.
 
Ni android hio, app itakataa kama
1. Inategemea play services sababu hamna playstore ila hili linaweza kuwa solved.
2. App imetengenezwa kurun kwenye resolutions kubwa.

Otherwise app nyingi za Android zina run humo.
Kwa upande wangu toleo la kwanza nilichoka kwa maana ilikuwa haingii kwenye website kubwa kama sportpesa na galsport na ilekubonyeza bonyeza ..ilibidi niiuze ..tu..
 
Kwa upande wangu toleo la kwanza nilichoka kwa maana ilikuwa haingii kwenye website kubwa kama sportpesa na galsport na ilekubonyeza bonyeza ..ilibidi niiuze ..tu..
To leo la kwanza ni Kai os, hii ni android, hii ni simu ya android kama simu nyengine kasoro tu umbo.
 
Kwa upande wangu toleo la kwanza nilichoka kwa maana ilikuwa haingii kwenye website kubwa kama sportpesa na galsport na ilekubonyeza bonyeza ..ilibidi niiuze ..tu..
Haka kanafungua vizuri tu websites zote za betting tena na aviator unacheza vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…